
pamoja na kutosajiliwa msimu huu na timu yake ya yanga ama timu ingine beki wa kimataifa wa burundi ramadhani wasso hajamwaga manyanga. kila siku anajifua peke yake lidaz klabu na kisha huelekea gym kujifua zaidi. wadau wengi wanabashiri kutokea ya nonda shabani ambapo yanga walimlia kobisi naye baada ya kujifua kivyake akaibukia sauzi kabla ya kuelekea ughaibuni ambako kama wanavyosema, yalobaki ni historia na yanga kuishia oooohh nonda kacheza jangwani wakati ukweli ni kwamba 'alipita' tu. hahahaa ....waswahili bwana!


Bora uwaambie wewe Bro Michuzi maana tukisema sisi tulio ughaibuni watasema tunajidai, Yanga Simba,majungu uswahili vimezidi sana!! Soka hakuna, ndio maana watu si ku hizi tunashabikia timu za Uingereza ukiwemo na wewe!!
ReplyDeleteDuh Michuzi huu ni mfano mzuri sana wa msukumo binafsi.
ReplyDeleteHebu tudadafulie huwa anasukuma gozi peke yake kwa masaa mangapi kabla ya kwenda gym?