wadau nimepokea dongo hili sasa hivi...
Hi! Mr Michuzi,
Nimefurahi saaana nilipo ona mail yako hii imenithibitishia nijinsigani unavyo tujali WADAU wako!
Mr.Michuzi kwanza naomba nianze kwa kusema samahani sana kwa haya ntakayo yaongea kwa sababu nadhani yatawagusa wengi! Nimeona ni vyema niliongee hivi hivi bado la moto kwa sababu tumefika wakati wakusema enough is enough! kamani mpira sasa umeshavutwa umebaki kakipande kadogo sana ukatike!
Ndugu yangu Mr Michuzi mimi napenda kuongelea kulala kwa waandishi wahabari watanzania, sasa this is too much! yaani wewe Mr. Michuzi kweli inakuingia akilini kusema Kijana wamiaka 26 afe kwakisukari na Maralia kweli?!!!?
Hebu jaribu kunisaidia hata wewe binafsi katika uzoefu wako wa kimaisha umeshasikia kijana wa umri huo anakufa kwa kisukari? SASA kwanini nasema waandishi wahabari wamelala Bongo; Sijaona wala kusikia waandishi wame mfata huyo daktari aliyekua anamtibu Amina kujua zaidi, maelezo, kwa sababu hayo maelezo yanayotoka yanaonekana yametoka kwenye familia yake na sio kwa dakari! ni maelezo ambayo wameambiwa na daktari yes, lakini kumbuka wale wana uchungu kwa hiyo wasingeweza kuuliza manenomengi! nakumbuka wawle sio profetionals, waandishi ndio mnatakiwa kuwafumbua macho jamii nzima ya Tanzani pamoja na familia ya Hayati.
Hili swala ni zito sana lakini naona waandishi wamelepa kisogo,saahivi tutasahau, alafu mtumwingine litamtokea sisi kila siku ni kukaa kimya tu, watu tegemezi la Taifa, wanakufa watu tuko kimya tu hatufanyi lolote, ni Watanzania wangapi wamepoteza maisha yao kwasababu tu wanataka au wanasemaukweli? na waandishi wamekaakimya????
Hivi waandishi wa habari Tanzania wanajua kweli nini maana ya kua muandishi? Ukiwa muandishi wa habari wewe ndio macho ya watanzania wote wewe ndio unatakiwa usilale ujue nini kinachofanyika serikalini!
Amina aliposema anawajua watu wanaoHusika na madawa ya kulevya sikuona any press confrence iliyo itishwa kujua undani waswala hilo, na kama alikua anahitaji protection au la! au security. Haya yote yalikua yanahitajika kuulizwa na waandishi wa habari! hebu jamani tukae tufikirie ni wapi tunapelekwa kama wahusika wa haya mambo wasipo kamatwa, waandishi ndio watu wenye kazi ngumu na yakutishia maisha kupita kazi zote duniani,lakini sijui kama waandishi wa tanzania wanalijua hili.
Waandishi ndio watu wanao wachokonoa wanasiasa ili kufumbua maovu yao, lakini sioni kama waandishi wa Tanzani wanafanya hivyo.
Vyama vya upinzani Tanzania vinaonekana havina nguvu, kwanini!.....................Ni kwasababu tu waandishi wamelala je mnadhani waandishi msipoyafichua hayo maovu vyama vitapata wapi ya kuongea, vyama vitapata wapi ya kuonya serikali?
Sasa hivi kulikua kuna mswaada bungeni kwamba wabunge wanaokaa viti vya nyuma bungeni hawasikilizwi, kwa sababu wanachukuliwa"hamnazo" na sijaona muandishi yoyote aliyemfata kujua undani wahili jambo? Jamani, Je mnajua kwamba waandishi ndio macho ya jamii ya watanzania???
Mimi ntaendelea kuwalaumu waandishi kwa sababu hamtakiwi kua waoga! kama kweli mnatakiwa kusaidia watanzania na kama kweli mnauchungu na taifa lenu na kama kweli mna wapenda hao wanaopoteza maisha kwa ajili ya kutetea haki za wanyonge na wasiojua wanaathirika!
Please it is time we wake- up!
Kuna mambo mengi Bungeni yanaongelewa kwa mfano swala la migodi? waandishi mnalio ngelea juujuu tu,swala zima la ubinafsishaji, swala la AIR TANZANIA. Hivi kama waandishi mkiwa hamchokonoi haya maneno kiundani zaidi mnadhani watanzania wataamka?!!!? Watanzania ndio wanaojulikana kua politicaly dormant, dunia nzima, kwa sababu gani, kwa sababu wale wanaojaribu kuliongea wananyamazishwa, na waandishi hawasimami nao kidete katika kupigainia haki hizo!

Huu ni ujumbe kwa waandishi wote wa Tanzania!
MDAU ERIC

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 47 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 29, 2007

    we erick alokwambia tanzania kuna waandishi wa habari nani?kuna waandishi nchi hii?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 29, 2007

    kwa kweli ni wakati sasa umefika waandishi mnatakiwa kuwa wazi na kufatilia mambo mpaka muone mwisho wake.habari nyingi mnaandika tunona tu zinazimika tu ghafla bila kuwa na suluhisho lolote, u guyz u have 2talk anything mnachokijua jamani na sio wakati wa kuzibwa mdomo sa hizi tumieni uhuru wenu kikatiba.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 29, 2007

    barua yako nimeipenda sana.aminia eric.Sema tu sasa hapo shida sijui wahariri wa habari au waandishi wa habari.

    Ila nawapongeza waandishi kwa kuandika issue ya BoT na mbunge Mzindakaya.Keep it up.Sasa tunataka maneno ya JK kwenye hili swala.Muwekeni kiti moto.Tumechoka anavyowabeba watu.

    Hii itazaa VITA mbaya Tanzania siku moja.Mungu tuepushe.Ila ni vema JK ukaepusha VITA kabla ya kumuomba Mungu.Mungu alisema"Jisaidie nami nitakusaidi"

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 29, 2007

    JAMANI KISUKARI WATU HAWAFI KAMA ALIVYOKUFA AMINA CHIFUPA.COMPLICATIONS ZA KISUKARI NDIO ZINAUA.AMINA ALIPATA COMPLICATIONS GANI(DIABETIC COMA,DIABETIC FOOT,DIABETIC RETINOPATHY-ANGEACHA KUONA).

    WAANDISHI MKAONGEE NA DOCTOR ALIYEHAKIKISHA KIFO CHA AMINA NA CHETI CHA KIFO KIMEANDIKWA KAFA NA NINI?TUNA HAKI YA KUJUA KAMA WATANZANIA TUNAOWASHUKU WATU,NA SI KUSEMA KAZI YA MUNGU.KUMBE KAZI YA CHAMA AU WAUZA UNGA WANAOBEBWA NA CHAMA.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 29, 2007

    Eric check hapa http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=223

    Sababu ya kifo cha Amina imeshaanza kutafutwa, na kwa sababu alikuwa kipenzi wa magazeti najua kila gazeti linajua stori ya kifo cha Amina itauza kupita kiasi.

    So stay tuned, naamini kuna gazeti litairusha tu, hasa jamaa zetu wa Udaku.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 29, 2007

    Tanzania hakuna waandishi kuna waganga njaa. Mtu akiona stori inagusa masilahi yake haitoi, kwa ujumla ukishaingia ndani ya TZ uandishi wako unauacha kwenye seatbelt ya ndege uliyokuja nayo. Tanzania kuna "Wadaku" wengi sana yaani, waandishi wanaogopa kufanyiwa mbaya au kulazwa njaa. Hebu fikirieni japo mtasema oooh wenzetu wameendelea, Nchi za magharibi waandishi wamekuwa chanzo cha discipline kwa watendaji mbalimbali, ukiandikwa una kashfa lazima uachie ngazi mapema ili uheshimike.

    Mfano mzuri wa hivi karibuni ni aliyekuwa "Rais wa Benk ya Dunia" Paul Wolfowitz, Imembidi aachie ulaji bila kuwa kashiba Hapo Bongo Kuna Vigogo wangapi wanatuhuma nzito kuliko za huyu bwana lakini waandishi wameshanyamazishwa mdomo wasipigie kelele na watu wanaendelea kupeta tu.

    Mi ninauhakika kwamba tungekuwa na waandishi makini na wenye kujua maana ya uandishi TZ kweli nchi ingeendelea sana kwa kuwapigia kelele tu kila siku hata kama miaka 10 kila siku tunasema watu wangejifunza kuwajibishwa.

    Nakulilia Tanzania Yangu kwa kukosa watu muhimu wa kukusemea na badala yake wanasemea matumbo yao.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 29, 2007

    Ndugu yangu Eric,hakuna waandishi wa habari nchi hii,labda wapo wachache tu ambao pengine hata wamesomea fani hii.

    Ikitokea kuwauliza waandishi wa habari tanzania juu ya elimu yao, naamini kabisa aslimia 99 walipata division IV au zero!!!!!!!!!!!kidato cha nne, achilia mbali kidato cha sita,kwani wengi hawakufika huko, unategemea mtu wa jinsi hiyo akuletee kitu kizuri?mpaka kesho hawataweza kufanya hivyo!!!!
    Achana nao Erik!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 29, 2007

    Hao waandishi wanukuu wanaogopa nao kukolimbwa!! Uliza uliza uone cha mtema kuni!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 29, 2007

    Na kweli naungana na wewe, labda waandishi wa udaku na waoga ndio wamejazana

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 29, 2007

    TANZANIA NATIONAL MAIN STADIUM

    WADAU NAJUA HAPA SI SI MAHALI PAKE LAKINI NAOMBA TUFUNGUE TENA MJADALA HUU. INGAWA NA MIMI PIA INGLISH IZ NOT RICHABO LAKINI NAONA JINA LA UWANJA MPYA LIMECHEMSHA LUGHA KIMANTIKI NA LINATIA AIBU. HIVI TANZANIA NATIONAL MAIN STADIUM NI KIINGEREZA SAHIHI KWELI? KWANINI ISIWE MOJA KATI YA YAFUATAYO?
    1. NATIONAL STADIUM
    2. TANZANIA MAIN STADIUM
    3. TANZANIA STADIUM
    4. NATIONAL STADIUM,
    TANZANIA

    HIYO "MAIN" HAIINGII KABISA KICHWANI KWENYE MAANDISHI YAO YALIYOBANDIKWA TAYARI. ITAKUWA AIBU KUBWA KAMA HAIPO SAHIHI NA WATANI WETU WA JADI WATAZIDI KUTUCHORA KWA SWAHNGLISH YETU
    WATAALAMU WA INGLISHI TUSAIDIENI MAONI MAANA WENGINE MADARASA YETU SABA TU.
    MZALENDO HALISI

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 29, 2007

    Unajua Bwana Michuzi sisi Watanzania tutakuwa nyuma siku zote yaani fikra zetu ziko kwenye kila kitu kinachotokea lazima kuna nguvu za giza, na shangaa kwanini hawakubali kuwa Amina amefariki kwa malaria na kisukali, Nina sababu kama mbili hivi na hoja moja

    1 Watanzania tukumbuke kuwa malaria inauwa watu dunia hasa afrika kuliko ugonjwa wowote ule
    mnaoujua

    2 Ni watanzania wangapi huwa wanaokwenda kwa daktari kupima hafya zao mara kwa mara nasema hivi sababu watanzania walio wengi ni mpaka asikie kichwa kinamuuma au viungo vimeshikwa na uchovu na dalili za mdomo unapoteza radha ndiyo anakwenda kwa daktari na hata hajapimwa tayari keshamwambia daktari kuwa anahisi ana malaria

    3 Ukumbuke kuna habari zilisema kuwa AC amelazwa na amepandwa na ukichaa hii inaweza kuwa cerebral malaria ambayo ni hatari sana

    4 Kisukari ni gonjwa linaloweza kuwa kwenye mwili wa mwanadamu bila kugundulika kwa haraka na ikatokea siku likipata upenyo linakupeleka kwenye coma basi tena hii ni point of no return tunakuwa tumeshakukosa

    5 Nahisi kutokana na imani zetu za mambo ya miujiza na nguvu za giza Amina alicheleweshwa kupelekwa hospital kupata huduma za kitaalam zaidi sababu kutokana na maelezo ya baba yake mzazi Amina alianza kusumbuliwa na malazi ya ajabu kama vyanzo vya habari vinavyosema tangu tarehe 08/05/2007 kwanini hakupelekwa hospitali muda wote huo mpaka last stage ndiyo wakate shauri la kumpeleka hospitali.

    USHAURI TU WA BURE KWA WALE WATANZANIA WENYE IMANI POTOFU KWANINI MSIMSHAURI RAISI JK AWAANZISHIENI WIZARA YENU YA MAMBO YA MIUJIZA NA NGUVU ZA GIZA ili huyo waziri awe anafatilia mambo kama haya mnayoona yana utata.

    Lini tutajifunza jamani na kuacha mambo ya kuongea saaana utumbo na bila kuwa na fact hatutaendelea namna hii uchawi uchawi uchawi kila kitu, cammon Tanzanians wake-up this is 2007 for GOd sake

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 29, 2007

    WAANDISHI WA HABARI WALIISHIA KUULIZA HIVI, "ndugu/mheshimiwa umepokeaje kifo cha mh Amina Chifupa"?

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 29, 2007

    We Ganai hawajasema malaria kumbuka baba yake alivyosema ni homa yaani joto halishuki, na sio malaria. Wee ndio mchawi mwenyewe nini?

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 29, 2007

    Sasa hivi waandishi wengi wa habari hapa Bongo wanawafuata wanasiasa au wafanyabiashara wawape pesa ili waandike habari zao, ndio maana unakuta vyombo vingi vya habari vimeandika au kutangaza habari inayofanana baaada ya kukatiwa kitu kidogo. Waandishi wa habari wanatakiwa wabadilike na wafahamu ya kwamba wateja wao ni wasomaji yaani jamii yote ya watanzania na sio wanasiasa au wafanyabishara tu.
    Kuhusu suala la kisukari, ni nchi yetu pekee au na baadhi ya nchi za kiafrika zinazochukua muda kumgundua mgonjwa wa kisukari. Kwa nchi nyingine, mgonjwa yeyote anapofika hospitali anapimwa "full vital signs: blood pressure, temperature, pulses, respiration & blood sugar". Ni vipimo ambavyo havina gharama kubwa na vinarahisisha sana kutambua hali ya mgonjwa. Ugonjwa wa kisukari unaweza kuwapata hata watoto wadogo ila mgonjwa akizingatia madawa na aina ya vyakula atakavyoshauriwa na daktari ataishi maisha ya kawaida kama wengine.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 29, 2007

    Hii bwana iko wazi, tusidanganyane kabisa, Mh. Amina Chifupa ameuliwa na serikali na viongozi wake wote wanajua kuhusu suala hili, serikali yetu ni katili na inaabudu mauaji, mtu akiwa na muelekeo wa kuikomboa jamii basi hachukui muda anaaga dunia, tutakwenda hivi mpaka lini, wangapi mshawaondoa duniani kwa kutandaza ukweli hadharani, nyinyi wakubwa wa serikali ndio mnahusika na kila la kharamu nchini, ndio maana mkiona mnaadhirishwa mnaamua kumkatia mtu maisha yake. Mungu awalaani wote walioshiriki kufanya ukatili huu. Tusidanganyane kabisa ukweli ndio huo na nyote mnaujua.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 29, 2007

    Nani hajui kuwa waandishi ni sehemu ya jamii na wanavyofanya kazi ni kielelezo cha jamii ambako wanaishi...kama wamelala ujue wanajamii ndo wako totoro kwa usingizi. mara ngapi waandishi wameibua maovu ambayo kwa jamii zilizo makini zinazojua kuwajibisha viongozi wao wanaowachagua, zinawapatilisha hadi kuwalazimisha kujiuzulu ama kuwajibika kwa madhambi yao,na kweli wanafanya hivyo...lakini Tanzania watu wako usingizi totoro.Kwa hiyo wa kuwalaumu ni wananchi wenyewe wanaokubali kuhongwa kanga kuwachagua viongozi mamluki, mafisadi na wanaotoa kipaumbele maslahi binafsi kuliko ya taifa. Hali hiyo itakoma tu iwapo jamii itasema sasa basi...na kuchukua hatua za kweli.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 29, 2007

    Nakubaliana na Erik. Tujiulize namna alivyokufa Yaser Arafat baada ya kukubali kulegeza masharti kwa Wayahudi. Yuko wapi sasa!!! Baada ya Amina kutaka kupambana na madawa ya kulevya, mtandao wao umeona hii ni Nomaa. Hawa ni wamafia wameona bora tumalizeee kazi.Kazi kwenu waandishii.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 29, 2007

    Mimi mchango wangu ni kwamba tusiwalaumu waandishi wa habari wa Tanzania. Hili ni tatizo kubwa kwa nchi zinazoendelea au kuelekea kwenye demokrasia. Tunapenda sana kujilinganisha na nchi za Ulaya na Amerika ya Kaskazini (USA/Canada), lakini wenzetu wameishafikia kwenye demokrasia ya kweli. Sisi bado sana. Nasikia waandishi wa habari kwa nchi za Marekani ya Kusini na Kati wanapata taabu sana kuandika habari za wauza madawa ya kulevya na wengi wanauawa. Hata hakimu anayehukumu kesi ya madawa ya kulevya anasoma hukumu kwenye tape, anakuwa hayupo in person mahakamani.

    Hata hivyo tusikae kimya tuna haki ya kuhoji na kupata ukweli. Lakini tumepata ukweli gani kuhusu Marehemu Kolimba, Kombe na wengineo?

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 29, 2007

    Mh Ganai naona umeongea kwa jazba na lugha ya kejeri as if wenzako hawakuyaona yote hayo. Kinachoweka ukungu kwenye hili swala ni circumstances za tukio zima kuanzia siku alipotaka kulipua bomu Idara ya Habari Maelezo mpaka alivyokuja kupelekwa hospitali kisirisiri na kukawa na ulinzi mkali kiasi kwamba ni wauguzi na madakatari wanaomhudumia tu ndiyo waliokuwa wanaruhusiwa kumuona pamoja na ndugu zake. Magazeti yaliyoenda kutafuta habari hayakufanikiwa kumuona na wafanyakazi wa Lugalo Military Hosp walikuwa wanasema ugonjwa alio nao ni siri!!! Kwanini iwe siri???

    Kuna mambo yafuatayo ambayo yanaongeza mashaka makubwa kwenye hiyo issue:

    Moja, baadhi ya ndugu wamekana kwamba marehemu hajafa kwa hayo magonjwa yaliyotajwa na pia kuna magazeti yamesema kwamba madaktari walishangaa kiwango kikubwa cha sukari walichokikuta kwenye damu yake, wakasema kwamba hawajawahi kuona mgonjwa ana sukari nyingi kiasi hicho (abnormal)! Hilo pekee lazima likupe mashaka kwamba hapa kuna kitu kingine tofauti.

    Swala la pili ni kwanini marehemu akiwa hospitalini watu hawakutakiwa kumuona? Na je hiyo ilikuwa ni amri ya nani? Baba Mzazi? Ndugu zake? Au mtu gani? Nini kilichokuwa kinafichwa? Ni nani aliyewafunga midomo madaktari na wauguzi wasiseme maradhi ya marehemu? Hapo lazima kuna maswali mengi ya kujiuliza ambayo hayana majibu na ndiyo maana watu wanahisi kuna watu wamecheza rafu.

    Swala la tatu kwa uelewa wangu Baba mzazi wa marehemu ni mtu mwelewa sana, asingeweza kukaa na mgonjwa wa malaria nyumbani akisubiri malaria ikolee ndipo ampeleke mgonjwa hospitalini. Nina uhakika utata ulikuwepo tangu mwanzo na ndiyo maana ilikuwa ni confusion na walishindwa wafanye nini na mwishoni wakaamua kumpeleka huko walikompleka ili wajiridhishe kwamba siyo ugonjwa wa kawaida, ila ni ugonjwa usio wa kawaida na ndiyo tumeletewa majibu mengi tofauti kwamba amefariki kwa mchanganyiko wa maradhi.

    Mh. Ganai naomba ukumbuke kwamba rafu siyo lazima ichezwe kwa kutumia nguvu za giza, kuna watu wengi sana wameondoka kwa njia za kisayansi na wakalala salama. Kwa hiyo hapo issue siyo nguvu za giza pekee, kuna njia nyingi za ku-eliminate watu na zinaweza kutumiwa na watu wakanyamazishwa. Kuliwahi kutokea kesi ya kuagiza mchele mbovu ambao haufai kwa matumizi ya binadam, mashahidi 5 wa kesi hiyo kuanzia Mkemia Mkuu wa serikali waliondoka mmoja baada ya mwingine na kesi ikaisha maana mashahidi wote hawapo. Mazingira kama hayo hayasemi kuna nguvu za giza, bali watu wanaweza ku-suspect mchezo mchafu kwa kutumia sayansi ya kisasa. Kulikuwa na Mwandishi Stan Katabalo alihangaika na Loliondogate Scandal baadaye alikuja kuondoka yeye na wahusika wa Loliondo mpaka leo hii wapo. Kwa hiyo ninakuomba usiwe na mtazamo wa farasi wa kulenga kwenye nguvu za giza peke yake. Njia za ku-eliminate watu kwa njia za kisayansi zipo nyingi sana na sasa hivi zinatumika sana, siyo kwa nchi zilizoendelea pekee bali hata huku kwetu Bongo zipo.

    Mwisho kabisa, siamini katika ushirikina lakini inawezekana kukawa na mchezo mchafu uliofanyika na ndiyo maana watu wana mashaka. Na hilo la mashaka ndilo lilipompelekea Bwana Eric kuandika hiyo e-mail yake akiwataka waandishi wa habari watupe news zilizokamili. Mgonjwa aliyekaa hospitali kwa zaidi ya wiki lazima kutakuwa na vielelezo vingi ambavyo vilikusanywa ikiwa ni pamoja joto, BP, sukari, na hata dawa alizokuwa anatumia. Zikipatikana hizo documents hapo ndipo watu wataweza kuchambua na kujiridhisha kwamba hakukuwa na mchezo mchafu.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 29, 2007

    Nakuunga mkono mdau,Tanzania tuna reporters tu, waandishi ni wachache sana!.Ila na wewe umenishangaza, barua yako imekuwa upande mmoja, kuamini kuwa Amina amekufa kifo kisicho cha kawaida.Ugonjwa uliomuua Amina unafahamika kwa familia yake, they just want to fool us kwa kuogopa stigma tu!Kama waandishi watalazimisha kiujanja watolewe copy ya file lake wataona, maana hata certificate of death imeandikwa uongo nadhani.Hii inatokana na culture yetu ya ajabu tuliyojiwekea wabongo siku hizi.Ukweli ungewekwa wazi nadhani ingesaidia sana kuokoa vijana ambao wako mashuleni na vyuoni, wajue kuna bright future kama hawataharibu katika ujana

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 29, 2007

    Swali langu ni: Kwa nini Amina Chifupa alilazwa hospitali uchwara ya Lugalo. Kwa nini asingepelekwa Muhimbili ambako kuna madaktari mabingwa wa kila aina ya magonjwa. Je, ni wabunge wangapi wamewahi kulazwa hospitali ya Lugalo walipougua? Ina maana hakuwa na pesa ya kupelekwa hospitali ya maana zaidi?

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 29, 2007

    Anony hapo juu una maana indirectly Amina amekufa kwa ngoma!
    Lakini i want to tell you kama Ugonjwa haueleweki sio lazima iwe ngoma.Maana siku hizi Bongo ukifa isipokuwa ajali basi ngoma ,hata ikiwa ajali watu watasema ah hata hivyo angekufa tu soon maana alikuwa ameukwaa,mtu akijinyonga alikuwa na ngoma pia.
    Kwa kweli tumezidi wabongo Amina marehemu anaweza akawa kweli ametutoka kwa malaria ,na may be other things!Asante

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 29, 2007

    Pamoja na kwamba Tanzania kuna "waandishi" wa habari feki, tusiwalaumu sana katika kuandika kuhusu suala zima la ugonjwa na mauti ya Amina.

    Kwanza kabisa ugonjwa wa malaria au kisukari kinaweza kumuua mtu yoyote na wa umri wowote awe mtoto, kijana au mzee.
    Yote inategemea jinsi gani huyo mtu anatibiwa. Kwa wale wanaoamini nguvu za giza ndio hivyo tena wengi huwa wanakufa kwani by the time wanatambua kuwa ni malaria au kisukari inakuwa too late hata wakimpeleka hospitali inakuwa kazi bure.

    Pili, kwa ufahamu wangu mtu mwenye HIV/AIDS hafi kwa hilo bali kwa magonjwa mengine yanayomshambulia kama vile homa, kisukari etc. Kwa vile mwili unakuwa hauna kinga basi inakuwa rahisi kufa. Marehemu aliyekufa kwa magonjwa haya ambae pia alikuwa na HIV/AIDS sidhani kama cheti chake kitaandika kuwa kafa kwa HIV/AIDS ila nadhani wataandika hayo magonjwa mengine.

    Kuna kitu kinaitwa "Doctor-Patient Confidentiality". Maana yake ni kuwa Daktari haruhusiwi kumwambia mtu yoyote habari yoyote ambayo atakuwa ameambiwa na mgonjwa wake au atakuwa amegundua kutokana na vipimo ambavyo atakuwa amevichukuwa kwa mgonjwa. Daktari ataweza tu kumwambia mtu mwingine ikiwa atapewa ruhusa na mgonjwa mwenyewe au by implication, yaani kwa mfano mgonjwa mahututi akipelekwa hospitali na mtu basi huyo aliyempeleka ataweza kuambiwa habari za mgonjwa. Kwa swala la Amina, naamini kuwa wazazi wake wameambiwa maradhi yaliyomuua na ndio hayo waliyotuambia watanzania. Sijui Eric ulitaka waandishi wa habari waambiwe maradhi hayo wao kama nani?

    Kama kuna sehemu nimekosea basi nitaomba nisahihishwe.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 29, 2007

    Wadau naomba muelewe haki Tz itapatikana pale tu serikali itakaporuhusu raia mbili. Hebu pata picha kama Amina angekuwa anahold uraia wa pili wa nchi babe duniani je unafkiri mambo yangefanyikla kienyeji hivyo? mi naona sisi wenye mikoba miwili tukipewa chance tuwe tayari kuibana serikali ambayo inaongozwa kimasikini kwa kila kitu hadi mawazo. Hatuna njia ya kuikomboa bongo zaidi ya sote tulibahatika kuhakikisha tunakuwa kitu kimoja.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 29, 2007

    KIFO CHA AMINA KINA MAANA KWAMBA WENGINE WOTE MNAOTAKA PIGANIA UKOMBOZI MNYAMAZE!!!

    ReplyDelete
  26. Eric,

    Nijuavyo mimi ni kuwa daktari hawezi kuelezea habari za mgonjwa bila idhini ya mgonjwa mwenyewe au familia yake. Kama hawatoi ruksa ndo basi tena tulie tu, tubaki na speculations zetu. Ila death certificate ni public. Tuone itasema nini.

    Kwa hapa USA, wanaokufa na kisukari ni hao wagonjwa wa siku nyingi ambao imekwisha tafuna miili yao, nervous system, figo, moyo, miguu imeoza, etc. Kwa kweli siku hizi ni manageable disease, watu wengi wanaishi nayo.

    Lakini kama kweli alikufa na ugonjwa huo, huenda hawakujua na alipata diabetic coma. Mimi siyo mtaalamu na sijui details za ugonjwa wake.

    Ukweli investigative journalist wa kweli saa hizi ni lazima anafanya uchunguzi wake chini chini, anahoji hata wahudumu, na wafafiagi, hata wauza matunda au watu waliona nani anaingia hapo hopsitalini kumtembelea. Ataenda hata sokoni kujua familia yake walinunua vyakula vya aina gani.

    Kuna trend Bongo. Waandishi wa habari wazuri hawakai kwenye fani hiyo. Wengi wanaacha na wanakuwa wanasheria, wana Public Relations, na hata wafanya biashara.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 29, 2007

    Tanzania hamna freedom of speech. bado sana tuna mwendo wa kwenda. Wewe humu kwa michuzi ni comments ngapi ambazo hazina matusi kabisa wala nini. Ila kwa vile zinaukweli ndani yake. Na yeye kama mwandishi wa habari anajua ni kweli. Haziweki kabisa. Kwa hiyo mjue hapa mtasema lakini still demokrasia ya nchi inayosemwa haipo kabisa. Ni kudanganyana na kuambiwa wanachotaka msikie. Na wanafanyaga hivyo mkishaambiawa ni kisukari basi mfunge midomo kabisa. No more questions.

    Waandishi wahabari TZ ni watu na wanafamilia wanataka wawalishe. Ukifuatilia sana ndio hivyo kesho huka kazi. Nchi ni ya wachache hii.

    Well, tutabakia Tanzania yetu haina noma wala nini....ha ha hah aha ni kweli.....???????

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 29, 2007

    Mimi nashangaa kwanini alipofika hospital walificha faili lake?hapo kuna kitu,na kwanini faili liliandikwa kwajina la myu mwingine?kwahiyo kuna ugonjwa alikuwa nao lakini hawakutaka watu wajue,kwa umri wake kisukari nakataa,kwahiyo kama ni magonjwa ya kisasa si ijulikane wazi ili wengine wapate fundisho wajichunge,sio kuficha itasaidia nini?

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 29, 2007

    Kuna the so calles "doctor of Lugalo or Young doctors" Ameacha hii comment Nyie ma anon mnaosema eti tuanzishe uchunguzi kwa watu wanaokufa ghafla,nani kakwambia hicho ni kifo cha ghafla??!Hospitali ya Lugalo na jamii ya Young doctors TZ wote tunajua sababu ya kifo,post morterm ya nn sasa!? Mungu amlaze Amina mahali pema peponi, Amen

    Kama doctor mzima naona shule alienda kwa bure tu na anawaangusha wenzake. hao ndio madoctor wa bongo.

    1.A doctor must always maintain the highest standards of professional conduct. Where is yours

    2. A doctor should certify or testify only to that which he has personally verified. Wewe huku kwenye blog unakuja kueleza nini

    3. A doctor shall preserve absolute secrecy on all he knows about his patient because of the confidence entrusted in him wewe unasema haya yote ya nini? Tutajua wote hamko loyal sio wote mliomtibu amina kwanini mjue wote kilichomuua. Huyo aliyemtibu aliwaeleza ya nini au ni speculation zenu kwa vile na nyie ni madocto wa hapo.

    Do your job doc

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 29, 2007

    huyu aliandika barua hii, mimi sijaisoma yote lakini kipande nilichosoma mwanzo kuwa eti toka lini mtoto mdogo miaka 26 akafariki kwa sukari, siku nyingine usirudie kuandika kitu usichokuwa na uhakika, fanya utafiti ndo uropoke. Mi sifungamani na upande wowote, AC nilimuenvy lakini amefariki kama ilivyokawaida na wote tutafata. Kama kapigwa juju mi sijui. Lakini kama ni sukari, kwa taarifa yako mtu yoyote anapata sukari type 1, wengine wanazaliwa nayo, wengine wanapata wakiwa kuanzia umri wa miaka 12 - 14 na kuendelea. Maily hawa wanakuwa insulin dependent. Being african or Asian origin, middle age, overweight (obesed) of which Amina was not are likely to cause TYPE 2 DIABETIC. KWAHIYO USISEME MAMBO YA UZOEFU TOKA LINI MTU MDOGO AKAFARIKI NA SUKARI. SUKARI IPO PIA KATIKA UMRI MDOGO. SIKU NYINGINE CHUNGUZA NDO USEME.LA MSINGI NI LABDA KATIKA UTAFITI WAO WATAKE KUJUA TYPE GANI NA MENGINEYO.

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 29, 2007

    Sababu za kifo cha Amina Chifupa ziwekwe wazi (Maoni ya Mhariri)

    Bofya: http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=223

    ReplyDelete
  32. AnonymousJune 29, 2007

    Citizen journalism(blogs) ndio ufumbuzi.Ukiwa na blog yako unaandika with passion na sio anachotaka mhariri au mmiliki gazeti.Hivyo vyombo vya nje navyo vimekuwa biased sana tu.Kwa mfano FOX Channel Marekani hao ni pro Bush kwa kwenda mbele.CNN nao wazushi wa Democrat tu.Lakini guess what siku hizi hata wao wananywea mkia when it comes to blogs.Huko ndiko tunapotakiwa kuelekea.Ndio maana wanablog maarufu kama Michuzi,Ndesanjo Macha,jeff msangi,maggid mjengwa,Damija,Chemi na wengineo wamekuwa wakihubiri mara kwa mara kwamba lazima wananchi tuanze kuitumia silaha hii ya citizen journalism kuvumbua maovu.Hawa tunaowaita waandishi wa habari ni vihio.

    ReplyDelete
  33. AnonymousJune 29, 2007

    Kuhusu waandishi wa habari mi nadhani tunao ila tatizo kuu ni umaskini (rushwa) na ubabe. Nikisema umasikini nina maana ya uwezo wa kujua kinagaubaga cha jambo lakini kunyamazishwa kwa kupatika kidogodogo. Pili wenye nazo kutumia vyombo vya habari kujisafishia majina hivyo kutembeza mshiko. Ubabe wa nchi pia unachangia sana kwani ukilinganisha na nchi zingine za magharibi ambapo waandishi wana uhuru wa kutoa habari na pia nchi kuwalinda... hapo tz hatuna kabisa hiyo hivyo tunajikuta tunaburuzwa tuu angali tunajua ni makosa..mmmh ndio mzee!!!!


    Kuhusu vifo, mimi nadhani hakuna sababu ya kulalia upande mmoja, haswa kwenye kilichopelekea kifo cha Amina. Anything is possible, hivyo kama kweli wanafamilia wanataka kumaliza mzizi wa fitina basi waruhusu ukweli wa kifo uwekwe wazi. Kwani katika kila habari niliyoisoma, Shekhe Chifupa ambaye ni ndugu wa marehemu anadai kuwa hakuna sababu ya kutafuta mchawi na kuwa amina wakati wake wa kuondoka ulifika. Baba ya marehemu yeye alisema mwanae kafa na magonjwa mengi..in this case wao wanajua fika ni nini kimemuua marehemu. Sasa waandishi wahabari kama wanaweza waongee nae ila awape ukweli kabisaa na hii itafunga mjadala rasmi.

    Hivyo mi naona tusiwalaumu saana waandishi wa habari ila ni vizuri tujadili kwanza hali halisi ya nchi yetu ... wao wanatafuta unga wa watoto wao...

    ReplyDelete
  34. AnonymousJune 29, 2007

    Nilikua na angalia na kufuatilia habari za mheshimiwa mbunge wetu aliyetutoka, lakini cha ajabu waandishi au magazeti na site zote zilizoonyesha umri wake hamna ni mawili labda yaliweka umri sawa kila site ilikua inasema umri wake. Moja 23, mara 24, 25, 26, 27 nikawanawalaumu waandishi.

    Lakini at the same token nilivyokua naangalia sites zinazoonyesha ajira za kazi bongo. Nimeona zote zina mention age requirement. Kumbe Tanzania ina age discrimination????? Na hii ipo kwenye katiba au haipo kwenye katiba ya nchi au kwenye labor not kuwabagua watu kwa umri wao ? Ndio maana watu hawataki kuonyesha umri wao wa kweli kwa vile wanafikiri je kesho wakitafuta kazi mahali fulani wakionyesha umri mwingine na wengine walishaona atapata kazi?

    This is not nice...

    ReplyDelete
  35. AnonymousJune 30, 2007

    Ndugu zangu nami naomba nipewe nafasi nishiriki katika mjadala huu. Kwa maoni yangu kazi ya kukemea uozo unaondelea katika serikali ya CCM ni kubwa mno na waandishi wa habari pekee yao kamwe hawataiweza. Inabidi wananchi wote tuivalie njuga ya kukemea wizi wa mabilioni, rushwa za hali ya juu, ukosefu wa maadili ya uongozi katika serika ya CCM.

    Nasema waandishi wa habari pekee yao hawaiwezi kwa kutoa mifano hai. Mtakumbuka Mkapa aliwahi kuwasagia waandishi wa habari kwamba hawajui kuuliza maswali, na anapenda kuulizzwa maswali na waandishi toka CNN au BBC.

    Juzi juzi kulikuwa na tuhuma nzito dhidi ya Mkapa kufanya biashara akiwa IKULU. Pamoja na waandishi wa THIS DAY kumuomba kwa heshima na taadhima kujibu tuhuma hizo, aliamua kukaa kimya hadi hii leo hajasema chochote.

    BOT kuna upotevu mkubwa wa mamilioni ya fedha za kigeni. Wabunge wa upinzani na hata baadhi ya CCM wamelipigia kelele hili, lakni muhusika bado yuko kazini na wale wabunge wa CCM wamepewa onyo ili wasihoji uozo wowote unaondelea ndani ya Tanzania, kwa maana nyingine wayafumbie macho mabaya yote ndani ya Tanzania ili kufuata ilaniya uchaguzi ya CCM.

    Mikataba ya madini ambayo ni madini ya Watanzania wote mpaka leo bado ni siri, kama vile mikataba hiyo inawahusu watu wachache tu ndani ya Tanzania. Tuliobaki hatuna haki ya kujua details za mikataba hiyo.

    Kashfa ya Richmonduli ambayo mhindi na kampuni yake aliyedai ipo Houston, US na kulipwa $172 milioni ili kusambaza umeme miezi michache iliyopita kufuatia ukosefu mkubwa wa umeme, wabunge waliambiwa na kiongozi wa bunge Lowassa kwamba hakuna umuhimu wa kuijadili kwa kuwa umeme umesharudi!!! Pamoja na mhindi kulipwa mapesa chungu nzima wabunge waendelee kuwa mabubu.

    Kashfa ya Rada ambayo mhindi kalipwa $12 milioni mpaka leo haijulikani hatima yake, wamewaachia waingereza wachunguze wakati pesa ni ya Watanzania kwa mkopo tuliopewa wa milioni $40 na mhindi bado anapeta uraiani.

    Kwa kifupi waandishi wanaandika mengi sana lakini tusiwaache pekee yao wananchi pia popote walipo nje na ndani ya Tanzania inabidi washiriki katika kukemea uozo wa rushwa na wizi wa hali juu ndani ya sirikali.

    Kama kweli tunaipenda Tanzania basi popote pale tulipo tushiriki sambamba na waandishi wa habari katika kukemea maovu ndani ya serikali. Kamwe tusikubali tuwe mabubu kama ambavyo wanavyotakiwa wabunge wa CCM kugeuza vichwa vyao upande wa pili pale wanapoona uozo.

    Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  36. AnonymousJune 30, 2007

    jamani kisukari kinaua lakini once kikigunduliwa ni ugonjwa wakwaida. halley berry toka mdogo kila siku anainsulin yake.
    Sasa kwetu hatupimi na check up zenyewe ndio hizo mpaka uumwe. Huwezi jua ni homa ni kisukari kweli.


    Ila Raisi wetu aliwahimiza watu wapime ukimwi. Mimi ningeona wabunge na waheshimiwa wetu wote kabla ya kuanza kazi wafanyiwe physical check up. Na iwe annual routine baada ya hapo. na hiyo check up waangaliwe pressure, kisukari, ukimwi, ukimwi na uzito.
    Marehemu alikua mzuri sana lakini nikiwaambia watu alikua ni overwieight mtaanza kunisuta huku. Yule kweli kwa unene ule na urefu wake ...kisukari ni rahisi...

    ReplyDelete
  37. AnonymousJune 30, 2007

    MESSAGE TO ERICK...!
    THANKS ERICK LAKINI UMESAHAU KAMA HATA WAANDISHI WENYEWE WENGI NI MBUMBUMBU,DAKTARI WENGI NI MBUMBUMBU,SERIKARI IMEJAA MAMBUMBUMBU,SAMAHANI MSINILAUMU KWA HII LUGHA, BUNGE LENYEWE LIMESHINDWA KUHOJI HII ISSUE YA MADAWA HUYU DADA ALIPOITOA,HUYO MBUMBUMBU DOCTOR AMERUHUSU MAZISHI YAFANYIKE BILA AUTOPSY, WAANDISHI WAMEKALIA KUSEMA AMINA KATUTOKA, OOH AMENA AMETUACHIA SIRI KUBWA SIJUI, UPUUZI MTUPU...KWANZA WAANDISHI WENGI WA HABARI TUKIACHA WEWE MICHUZI ULIYEJIAJIRI PIA NI WACHOVU SANA NJAA KALI SASA WAKIFUNGUA MIDOMO YAO WATAFANYWA KAMA MASUMBUKO LAMWAI AMA MREMA. BONGO KUNA UPUUZI MWINGI SIDHANI KAMA WAANDISHI WA HABARI WANAWEZA KUIBADILI TANZANIA BWANA ERICK, WEWE UKO UGHAIBUNI RUDI BONGO UONE ISSUE, KAMA UNABEBA BOX BWANA ERICK ENDELEZA KUBEBA NA KUJIWEKEA TUHAKIBA BONGO KUNA ISSUE NYINGI SAANAA MBOVU. RAIS WETU MWENYEWE MSANII, ANESEMA HILI ANAFANYA JINGINE HANA SELA, VIONGOZI WAKE MWENYEWE WANAUWA HADHALANI ANAWAKINGIA VIFUA, WALA RUSHWA ANAWAFICHA WASIHOJIWE MKAPA ALITAKIWA AHOJIWE KUHUSU LADA JAKAYA ANAMWEKEA KIFUA SASA HIYO JUSTICE ITAPATIKANA KWA AMINA? DITO SI NDIYO HUYO ANAFUTIWA MASHITAKA ANAAMBIWA ETI KAUA BILA KUKUSUDIA? WAKATI KATOA BASTOLA NA KUMCHAPA DEREVA MBELE YA ABIRIA WAKE..ERICK HUNA HAJA YA KUSIKITISHWA NA WAANDISHI SANA SANA UNATAKA NA WENYEWE WAFE KIFO CHA MENDE, NJOO BONGO UANZE KUDADISI MADUDU YA SERIKALI UONE UTAVYO FANYWA! WATU WANA FAMILIA ERICK.. HAWAWEZI KUFANYWA KAFARA KAMA KINA SOKOINE, CHIFUPA, MWAIKAMBO,KOLIMBA AMA MALIMA. WABONGO WAMELALA CCM INAPIGA MITI KILA ANAYEFUNGUA KINYWA SASA UNATAKA HATA MICHUZI APIGWE MARUFUKU KUENDESHA KABIASHARA KAKE KA PICHA NA BLOG? ETI KWA SABABU YA KUPIGANIA UHURU? KILA MTU ATAKUFA NA RWAKE NDIYO KAMSEMO KA BONGO SASA HIVI...ASANTE ERICK LAKINI COMMENTS ZAKO DO NOT MATERIALIZE IN BONGO. ENDELEZA BOX HUKO ULIPO UKICHOKA NJOO HAPA NYUMBANI NA WEWE UPIGWE MITI NA KINA DITO AMA MPAKANJIA!

    ReplyDelete
  38. AnonymousJune 30, 2007

    JAMANI TUNA HAMU YA KURUDI TZ MIMI NA FAMILIA YANGU, LAKINI SASA HAYO MAZINGIRA YA KUTOANA LIVE NAMNA HIYO YANANITIA WASIWASI, SIJUI ITAKUAJE, KWELI TZ INAOGOPWA SASA HIVI HASWA NA WATANZANIA WALIOKO NJE, KILA MTU SASA HIVI ANAJIULIZA ARUDI HALAFU IWEJE, MAANA KUNA UTATA MWINGI AMBAO WENGI HATUUJUI, HALAFU WATU HAWAWI OPEN, INATISHA, INASHTUSHA, BORA TUBAKI HUKU HUKU MWE!!!

    ReplyDelete
  39. AnonymousJune 30, 2007

    wewe Zhazhalatee (anon wa June 30, 2007 6:57:00 AM EAT) na wabeba mabox wote hebu acheni kelele zenu huko kuhusu Bongo.

    Mnachotakiwa kujua ni kwamba ni lazima ujifunze kuheshimu ulichokikuta ukitaka cha kwako kiheshimiwe.

    Kwa hiyo kama hamna muda wa kujifunza kuishi katika system ya Bongo ili muweze kupanda na baadae muwe na nafasi ya kuleta fikra zenu mpya kaeni huko huko muendelee kubeba mabox.

    Mimi niko hapa Bongo ninajifunza namna ya kucheza na system ya maisha hapa Bongo. Mambo yakienda safi inshallah nitafika juu.

    Tuachieni Bongo yetu jamani. Kama mnapenda maisha yenu ya kuwa second class citizens endeleeni nayo.

    ReplyDelete
  40. AnonymousJune 30, 2007

    Unamaanisha nini unaposema second class citizen? Anaponunua nyumba mzawa na wabongo kama wana ubavu wananunua, gari analoendesha kama una ubavu nawe unaendesha, unapiga kura kuchagua umtakaye. Kashfa zinashughulikwa kama kazi na unaona watu wanapoteza kazi kama kuna kashfa dhidi yao na hata kufikishwa mahakamani. Unalipa kodi na unaona umuhimu wake, maji belele, umeme 24 hours a day, bara bara bomba n.k.

    Acheni hizo wabongo wana akili zao wanafanya madudu majuu lakini kwa kuwa hamyajui basi mntaka kupakaza kwa kila aina mara wanabeba maboksi mara wanakuwa treated like 2nd class citizen!!!! Bongo mabilionia ndani ya CCM na serikali wanazidi kuongezeka kila kukicha wakati mamilioni ya wananchi hawajui hata mlo wao mwingine wataupata wapi!!!!

    Majuu huihitaji kupigiwa debe ni Kigod father ili mambo yako ya kunyookee kama unavyeti vya uhakika, mchapa kazi mzuri na unathamini kazi yako basi wewe unapeta tu na matunda yake unayaona!! Sio bongo unasota mpaka uwe na kijimungu mtu ukipe rushwa na kukisifia sifia kila unapokiona ili kikikupigie debe upate promotion!!!

    Endeleeni kukumbatia uozo mkija shtuka wajanja wamemaliza kila kitu mtabaki kujiuliza waliokuwa wanaiba na kuhamisha mali zetu tulikuwa wapi!!!?

    ReplyDelete
  41. AnonymousJune 30, 2007

    Anony 1.09 PM.. Utamu kulia mezani....hata kama mtu ni 2nd, 3rd or 4th citizen lakini watu wanalii jikoni huku wanakula mezani kwa raha zote. Wewe raha yako iko wapo.....??? Huna freedom yeyote, ukisema kitu unauliwa, wakubwa wanaua na kuendelea na life kama kawaida.....Kidogo shehe anasema hamna kujadili kifo chake maisha gani hayo...

    ReplyDelete
  42. AnonymousJuly 01, 2007

    simjui amina , achilia mbali umri hebu tupeni clue? alikuwa mnene?na kama ni kisukari ni type 11 or one?
    DOS

    ReplyDelete
  43. AnonymousJuly 01, 2007

    Huyo anayesema tutakalia kuwa second class citizen anajua maana ya hilo neno au anajisemea tu. Je siye ni 2nd class kwa vile ni weusi au kwa vile tuwahamiaji? usiseme kitu usichokijua maana yake.

    Naona wengine wameshakueleza lakini hapo bongo wote raia wao si 1st class citizen lakini tuonyeshe uhuru walionao uko wapo pamoja na kuwa ni hiyo title?

    Bongo hamna future dreams wala nini, ukiwa nayo ndio hiyo inakatizwa mapema mapema. Mwana hamna kitu kizuri kama freedom na usawa

    bwana wangu usiseme usilolijua

    ReplyDelete
  44. AnonymousJuly 01, 2007

    Types of journalisms

    Reporter, Editor, Visual, Photographer, Graphic artist, and Page designer

    The types of reporters

    News reporter
    Florescent reporter
    Sports reporter
    Science reporter
    Investigative reporter
    Celebrity reporter
    Convergence reporter

    Sasa bongo mareporter hamna anaye specialize kwenye career yake. Kila mmoja akiamka asubuhi anakwenda habari iliyopo ina maana wote ni ma news reporters.

    Nafikiri sasa hivi kwa vile tuna wengi wangejitahidi kuspecialize kidogo au vyombo vya habari vingenunua habari kutoka kwa freelance reporters wanaospecialize kwenye mambo yao. Kwa kufanya hivyo watapata habari zenye kutokana na ujuzi na upendo wa hiyo field na sio kurukia kila kitu na wakati mwingine mareporter hawfatilii jambo tena wakishaliandika basi ndio hivyo wanaliachia njiani linapotea na upepo.

    ReplyDelete
  45. AnonymousJuly 02, 2007

    44 comments..... yaani watu wanaomba uandishi wa uwazi na ukweli. Lakini kila mwandishi kwenye post hii, except Chemi Che Mponda, anaficha jina lake - hata mimi.

    Mbona tunaogopa kusema wazi?

    ReplyDelete
  46. AnonymousJuly 03, 2007

    Kifimbocheza what is your point? U kweli ni ukweli iwe unonyesha jina au la hamna nayemtukana mtu wameelezwa ukweli...

    ReplyDelete
  47. AnonymousJuly 03, 2007

    @4:52:00 am, I didn't make any point! Niliuliza swali. Si ndiyo?

    Nisichokoze. wananchi wa kawaida hawasemi wazi hata kwenye mtandao. Je, waandishi wa habari waandike wazi ya mambo makali hapa tanzania? wanaogopa kufukuzwa kazi!

    @chemi, wengi wanaacha kazi yao kwa sababu watapata mshahara kubwa zaidi sana wakifanya kazi kwa counter wa benki kuliko kuwa mwandishi wa habari.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...