Haya ni machweo mwanana ya jua katika mji usio maarufu wa Bukene na mdau alietuletea anahoji ni wadau wangapi wanaosoma mtandao huu hivi sasa wanatoka au wanaujua mji huu ulioko mkoani Tabora?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 05, 2007

    Mimi naitwa Peter Maige.Sasa naishi Austria.Mimi nimezaliwa Nzega lakini nilikuwa naishi Bukene.Watu wa zamani ninaowakumbuka ni kama yule Hamisi Ntaliwe,klabu ya mpira ya usagaji,kina Boy idd walicheza mpira pale bukene,wengine wengi nimewasahau .Nilisoma Kili primary school.Anyway nilizaliwa 1963.mara ya mwisho kwenda bukene ilikuwa 1979 au 1980.Michuzi asante kwa picha,wewe ni mtanzania halisi asiye na ubaguzi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 05, 2007

    Picha nzuri sana hii,kila kitu kiko mwanana,sioni kingine cha kukosoa ukiondolea mtu anayeonekana na shati hapo mbele. Ahsante sana kwa kutuwekea hapa kuiona.

    SteveD.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 05, 2007

    Kumbe tabora pia kuna minazi! mimi nilidhania Tabora kunatoka mkonge tuu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 05, 2007

    Brother Misupu, Naitwa Maselle P, kwa sasa naishi Seoul South Korea. Mimi ni mzaliwa wa hapo Bukene mtaa wa Iluluma, na mzazi wangu mpaka sasa anaishi hapo, japo kabla ya kuja Korea nilikuwa nikiishi Dar es salaam. Nimefurahi sana kuona picha ya home. Mr. Peter Maige natumaini tutakuwa tunafahamiana kabisa.Pia nawakumbuka akina Francis Babalo, Mzee Ally Ngando, nk

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 05, 2007

    miaka ya 1986-92 nilikuwa napita hapo kwa treni kuelekea au kutokea Mwanza! MER

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 05, 2007

    minazi na tabora wapi na wapi?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 05, 2007

    Kuna wakati mji huo uliitwa Dubai. Enzi za National Milling. Wachezaji wa Simba na Yanga walichezea timu ya NMC hapo

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 05, 2007

    Anon wa 2:43PM EAT Hivi somo la geographia darasa la nne ulilielewa kweli?,

    Aliyekuambia Tabora wanalima "Mkonge" nani?, Hebu tuwe tuna apply hata elimu zetu za msingi ambapo najua watanzania asilimia kubwa tunayo katika kujadili mambo.

    Mazao makuu ya Bishara Tabora ni, Tumbaku, Karanga na Ufungaji wa Nyuki Japo kuna baadhi ya wilaya wanajaribu zao la Pamba.

    Mkonge unapatikana Morogoro kidogo, pwani na kwa wingi ni Mkoa wa Tanga na Baadhi ya wilaya za Kilimanjaro. Hii ni kwa mujibu wa niliyosoma mwaka 1986 nikiwa darasa la nne.

    Mimi nilitembelea mkoa wa Tabora kama mwaka mmoja uliopita na sijasikia wamegundua kilimo cha zao jipya la"mkonge".

    Tabora minazi inastawi japo si sana, kuna mitende pia ila Miembe ndio kwao maana waarabu walipanda miembe mingi sana.

    Tatizo la Tabora mzunguuko wa fedha ni mdogo sana ila kwa vyakula ndio kwenyewe.

    Katika wiliya ya Bukene nafikiri kuna "Mihama" pia ambayo matunda yake hupendwa sana na Tembo Kokwa lake ni kama nazi laki kulivunja mpaka utumie Shoka kama unachanja kuni na ukilivunja mbagu yake inafanana na nazi ila ngoma ni kwamba halivunjiki kwa meno wala kutafunika.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 06, 2007

    Aksante sana kwa picha hii.
    Mimi wazazi wangu walitokea Sikonge. lakini nimeshasikia mahali hapo.Hivi sasa ninaishi Amerika.Please any more pic.from Tabora in general....

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 06, 2007

    Massele P, nafurahi kuona watu wa Bukene mpo tena nje ya nchi, wewe ukiwa Korea na Maige akiwa Austria, inapendeza kwa kweli. Kwakifupi akina Babalo wangalipo, lakini siku hizi naambiwa kawa mtu wa 'mitungi' sana na bila shaka ukimuona kazeeka! Mimi nimetoka huko hivi karibuni na hii picha imepigwa nikiwa sokoni kuelekea kwenye minazi ya karibu na Mwantoba. Iluluma kungali fresh, kuna watu wamejenga nyumba fresh. Kwa jina naitwa Abdallah, mtoto wa Mzee Mrisho Salawi, kwa sasa maskani ni Dar.Ni vizuri watu wa BNE tukajuana na kuwasilina(amsalawi@yahoo.com)

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 07, 2007

    Watu wa BNE deal, hapa hakuna suala la bukene ni watanzania. Bwana Abdallah unataka masele P akuvute Korea au Maige akuvute Australia. Ni pale utakapokuja shangaa mtakapo kutana Kariakoo Shimoni mkinunua Dagaa wa mwanza.

    Halafu mambo ya nani kawa "mitungi" huo ni umbea aliyekuambia blog yetu hii ni ya umbea nani??. Hayo si maisha yake yeye mwenyewe kachagua bwana, kikubwa haibi mazao ya watu kuuza na kununulia pombe.

    Ila safi pale watu mliopotezana mnapowasiliana kama hivi ni jambo zuri sana.

    Michuzi hongera kwa blog maana pia ni kiunganishi kizuri kwa watu waliopotezana zamani kama bwana abdallah hapo katoa mail hii ni nzuri zaidi katika kuonyesha umoja wetu wabongo.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 09, 2007

    naitwa fidel sasa naishi uingereza.wazazi wangu wametokea huko bukene .nashukuru sana kwa kutupatia picha ya hapo.mara ya mwisho kufika hapo ilikuwa ni 1988

    ReplyDelete
  13. Mimi ni Mwana wa Bukene, Munir. Nilicheza mpira kwenye timu ya Vijana na timu ya NMC.Bukene ni mji maarafu umetoa marubani kama Latif Omar ( mtoto wa marehemu Taji), Saleh Sahaag ( mjukuu wa marehemu Taji) na wataalam wengine. Mimi nipo Marekani kutokea mwaka 1985. Bado nakumbuka Bukene. Mara ya mwisho nilifika 1993.

    ReplyDelete
  14. Mimi mzaliwa wa Bukene,Naitwa Noorie mto wa Mzee Taji naishi Marekani toka 1994.Maisha nitakumbuka Bukene.Nategemea kuwapeleka watoto wangu mwaka huu wakaone nilikotoka.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 16, 2008

    Wadau,
    Mie natokea Sikonge pia. Mwezi wa tatu nilikuwa huko na kukaa kwa masaa tu. Minazi Tabora ipo. Mwenye kutaka picha za huko ninazo picha kadhaa. Anaweza niandikia kwa anwani hii hapa chini na ntamtumia baadhi. Sasa Sikonge wako mbioni kufungua NGO ya maendeleo ya Sikonge. Nategemea pia kuwalazimisha ili wawe na WWW na picha za mara kwa mara za huko Sikonge. Pia tembelea anwani hii hapo chini uone picha alizopiga huyu dada wa Kidenish ....
    http://ester.leweb.dk/main.php?g2_page=1
    anwani ni SIKONGE@TLEN.PL
    Siku njema. Sikonge.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...