

picha ya chini natia sahihi kitabu cha wageni kwenye banda la kampuni mpya ya vifaa vya usalama na mawasiliano ya comsec ambayo imejipatia umaarufu kwa muda mfupi kutokana na kuwa na vifaa vya kileo kama vile kamera za video za usalama pamoja na mawasiliano ya bila waya. juu mteja akielezwa aina ya vifaa ambavyo comsec iliyo navyo. wao wanalenga sana usalama wa majumbani na kwenye maduka kama ya supamaket ambapo mtu hawezi kudokoa kitu na kuondoka nacho kwani akivuka mlango tu king'ora kinalia.
tovuti yao ni www.comsec.co.tz
Safi sana. Hawa jamaa nadhani wanaingia kwenye soko wakati muafaka. Udokoaji usiokuwa wa msingi utapungua kukiwa na CCTV na sec. system kwenye maduka makubwa. Mabenki yote nayo yakanunue CCTV pamoja na Bureau De Change. Huwa napata taabu kubadilisha vidola vyangu nikija Bongo maana Mijambawazi inatisha!!!
ReplyDelete