MICHU,
NIMESOMA HABARI KATIKA GAZETI LA THE GUARDIN KUHUSU SHULE YA MKUGILO HUKO MKURANAGA AMBAPO KUNA MWALIM MMOJA TU.
KILICHONIDUNDUWAZA ZAIDI NI KUSOMA KUWA WAKATI MWALIMU MKUU [HEADMASTER] ANAPOSAFIRI KIRANJA MKUU a.k.a HEAD PREFECT ANAKAIMU NAFASI YAKE.
SIJUI WADAU WANASEMAJE KUHUSU HALI HII,NA KAMA UJENZI WA SHULE NDIO MAANA YAKE.NAJIULIZA MASWALI MENGI SANA LAKINI NIKIFIKIRIA KUWA VIJANA HAWA WENYE DAMU BAR BARU WANAPOACHWA WENYEWE KATIKA MAJENGO NA KAIMU MKUU WA SHULE KIRANJA X ,NINI KINATOKEA YARABI!
NAOMBA KUTOA HOJA
MDAUKIMITO.
Kinachohitajika ni good incentives kwa walimu. Benefits wacha mishaara yenyewe hamna. Mwalimu hapokei mshahara miezi sita kweli nani ataweza kufanya hiyo kazi? Lakini taifa linawafelisha watoto wa taifa la kesho. Hamna kitu kizuri kama msingi mzuri. Hizo kodi zinazokatwa zinaishia kwenye matwin towers na taa barabarani wamesahau shule za msingi na hospitali kwa watoto wadogo.
ReplyDeleteMkiongeza vyuo vikuu hao wanafunzi watatoka wapi kama shule za awali hamna. Au vyuo vikuu vyetu vitakua vya wanafunzi kutoka nchi za nje.
Mungu ibariki Tanzania
Ukisikia kila kata iwe na shule hayo ndiyo matunda yake. BORA SHULE NA SI SHULE BORA. Kila siku utasikia WAKUBWA, ndio WAKUBWA WA NCHI, wakisema kila kata iwe na shule. Swali ni maandalizi yapi wameyaweka ya kukidhi haja mahitaji ya shule hizo kuanzia walimu, vifaa vya kufundishia nikimaanisha vifaa kweli vya kufundishia, majengo (nyumba za walimu, madarasa n.k)? Ukiangalia hakuna la maana linatoka katika mpango huu mfu wa kila kata shule. Maokeo ni kupata wahitimu wa kidato cha nne wa kuhesabu vyumba na madawati waliyokalia badala ya UJUZI, UTAALAM, UELEWA NA UFAHAMU unaolingan na elimu ya kidato cha nne. Kilichoko hapa ni kuendelea kuzalisha wajinga wengi. Haki ya kupata elimu bora iko wapi? HAKI.
ReplyDeleteHii ni off topic lakini nadhani ina husu elimu hiyo hiyo tuliyo nayo.
ReplyDeleteNimekua nikisikiliza hizi TV station na kuwasikiliza wasanii wetu. Pia nimefuatia bongo celebrities an kusoma majibu yao.
Naelewa kutokana na elimu yetu au kukimbia umande ni aibu kuona wasanii majibu waliyo nayo sio mazuri kabisa. Au yanaonyesha kama hana akili au awareness ya kinachoendelea ulimwengu huu zaidi ya muziki ni ndogo sana.
Mimi kwa ushauri wangu kuinuka kwa hii bongo flava ikaongeza ajira kwa vijana ambao wengine ni wasomi au sio wasomi basi ajira iongezeke kwa waliosomea mambo ya communicatio, public communication au mass communication.
Wasanii wangine ulimwenguni sio wote wamesoma lakini kama hawana hela za kuwa na PR wana hire per hour au consult a PR firm all the time kabla hawajaenda kuongea hadharani. Wanawasaidia sana kuwaeleza nini cha kuongea au kujibu kuhusu topic watakayoiongelea. PR wanafanya research na mtu akiongea akionyesha hata data za kweli kuhusu jambo analo liongelea watu wanamuona ni msanii mwenye akili sana. Kumbe amelipa kufanyiwa research au kubrush brush.
Nilizania wasanii wengi wakitembea nje ya nchi aaaa aaa aaaa nyingi tu nikajua kingereza ni kigumu kwao kuongea lakini pia hata kwa kiswahili mtu akiulizwa swali ni aaa aaa aaaa.
Watu wakiwasikiliza maongezi ya msanii kama ni mazuri hata mtu anakua na hamu ya kusikiliza nyimbo zake. Lakini kama msanii akiongea au akijibu majibu anaonekana kama mtu asiye na akili au serious hata watu watakua hawaamini sana mziki wake au mambo anayoyafanya kiusanii.
Naomba kuwakilisha hili.
Aibu, tena aibu kubwa kwani inaonyesha jinsi gani hii serikali imeshindwa kazi na wala haina muelekeo.
ReplyDeleteWanajisifia kujenga shule nyingi katika kipindi kifupi lakini hawaandai waalimu, hakuna vifaa vya kufundishia, hakuna bajeti ya kutosha kwa mishahara ya waalimu. Lakini, kila mwaka utamsikia Waziri Mkuu anaomba Bunge lipitishe sh. bilioni tatu kwa ajili ya matengenezo ya nyumba na ofisi yake.
Haya ndiyo matekeo yake mtoto anawaongoza watoto wenzake kama vile kizazi chote kimepotea kwa ukimwi.
Tukiandika humu, maalim Michuzi anayaweka maoni yetu kapuni. Ok man, do the honor.
Jamani tusipoteze muda na kujadili suala hili, serikali kupitia waziri wa habari aliisha sema mwezi uliopita kuwa ni hatari kwa mustakabali wa taifa kuwa na watu wengi graduates. Ukiangalia juu juu utaona suala hili ni jepesi lakini watunga sera aliisha kaa wakagundua kuwa mara nyingi serikali hubadilishwa na wasomi, ukiwa na watu wengi wenye uwezo wa kuchambua mambo ni vigumu kuwadanganya ili wakupe kura.
ReplyDeleteKwa staili ya kujenga majengo ya elimu pasipo elimu ni moja ya janja za kupunguza threat hii. Sasa kinachoendelea ni kutufumba macho ili kwenye statistics tuambiwe kuna shule kadhaa lakini shule hizo ni sehemu za watoto kushinda jioni kurudi nyumbani.
Suala hili lilihitaji maandalizi ya kina hasa kwa upande wa kuwaandaa walimu bora si bora walimu. Kwa ninavyojua mimi mwalimu anatakiwa awe ni mtu aliyepata daraja la 1 au 2, lakini mimi kuna mdogo wangu alikuwa na daraja la 1 alipoomba mwaka jana wakamnyima eti anaweza kuwakimbia.
Swali linakuja unapomchukua mtu mwenye uwezo wa chini akafundishe wanafunzi unatarajia products zitakuwa nini kama sio CHINI ZAIDI.
Hizo shule mnazoziona maandalizi ya kupata kura kwa watunga sera lakini hakuna nia thabiti ya kukuza elimu.
Huyo kiranja anayekaimu ukuu wa shule anaqualification gani? na analipwa mshahara gani.
Kitu kikubwa ni kuweka incentives kwa walimu kuwa tayari kufanya kazi hata porini provided wanalipwa vizuri, kwa sasa mtu anaona bora akae mjini bila kazi kuliko kwenda kufanya kazi katika mazingira magumu ya kijijini.
"EDUCATION WITHOUT APPLICATION IS USELESS", Watunga sera wasiogope elimu kwani nao kama si elimu wasingefika hapo walipo wa apply elimu zao katika kutunga sera za maendeleo sio za kulinda hatma zao.
"KWA PAMOJA TANZANIA ITASONGA MBELE"
Acheni porojo tunapenda kusikia kuwa yuko mtu atakayem-sponsor mwalimu japo mmoja tu kwa kumlipa mshahara ktk kipindi cha mwaka mmoja wa Sh.300,000/- (dola 280 tu) kwa mwezi). Ni kweli serikali inastahili lawama kwa kutelekeza hiyo shule lakini wewe umechangia nini? Achane hizo bwana! Michuzi weka Acccount No. tuone kama hao wenye porojo watafanya kitu.
ReplyDeleteAnon. wa July 10, 2007 6:03:00 AM EAT kumbe hata hesabu ndogo kama hizi hujui. kwani Sh. 300,000/= ni sawa na US $240.00.
ReplyDeleteSUala sio kama wananchi wanaweza au hawawezi kuchangia sh. 300,000 kwa mwezi. Suala (issue) ni Serikali yetu kutimiza wajibu wake.
ReplyDeleteSerikali ndio inakusanya kodi na sio wananchi. Inatakiwa kutumia kodi hizo kulipa walimu na wafanyakazi wengine wa serikali. Kushindwa kuwalipa vizuri wafanyakazi wake ni kushindwa kutimiza wajibu wake. Ni sawa na mzazi anayeshindwa kuweka chakula mezani na kuwataka watoto wajitafutie chakula!
Tatizo kubwa letu watanzania ni kwamba tumezoeshwa kuwa ni wajibu wetu kujitolea hata katika maeneo ambayo ni jukumu la serikali. Mfano: Watu wanalipa ushuru wa kiwanja na jengo; ni wajibu wa serikali kuhakikisha huduma muhimu kwa mtu kuishi pale kama barabara, umeme na maji vipo pale. Otherwise, serilaki inachukua kodi hiyo kwa matumizi gani? Lakini Mtanzania utaambiwa mjitolee muisaidie serikali kujenga barabara yenu. Serikali hiyo hiyo inakusanya sh. 100 kwa kila kilometa ambayo gari inapita. Na kwa vile wadanganyika tunakaa kimya na kujichangisha visenti kidogo vilivyobaki kukwangua barabara, basi viongozi wa serikali wanatumbua kodi zetu zote kwa starehe.
Kwa suala hili la walimu serikali inaweza kuilitelekeza bila kuhitaji fedha za ziada nje ya budget yake kwa kufanya yafuatayo:
1: Kuuza nusu mashangingi yote yanayohudumiwa na serikali. Hii itarudisha gharama ya magari hayo, plus at least Tsh.1.5 billion za maintenance cost, kila mwezi.
2. Magari (mashangingi) yanayobaki, yawekwe chini ya kitengo maalum cha magari ya serikali. Mawaziri na maofisa wengine wa serikali waombe gari la kutumia kwa shughuli za serikali kwenye hiki kitengo, tofauti na sasa ambapo wanayatumia kwa matumizi binafsi. (Kagame wa Rwanda ameweza kufanya hili). Pia serikali iache kuwapa mafuta ya buree maafisa wake wote wa juu: Isipokuwa na Rais na Makamu wake, basi. Kama maafisa wenye mishahara midogo wanaweza kumaintain magari yao, kwa nini makatibu wakuu wa wizara na wakurugenzi watunzwe kama watu wasiojiweza?
3. Wabunge wachague wenyewe magari wanayotaka na wakopeshwe at market rate bila ruzuku yoyote toka serikalini wala maintenance assistance toka serikalini. Hii pia ita save some billions. Inabidi wabunge wetu waelewe maana ya budget ya kufunga mikanda in real sense. Naamini ni wachache wataagiza mashangingi.
Kwa kubana matumizi tuu kwenye magari na matumizi ya mafuta serikalini tunaweza kuwalipa walimu kima cha chini sh. 300,000 kwa mwezi na kuwa na walimu wa kutosha shule zetu zote. Kama serikali inashindwa jukumu hilo inapaswa kuadhibiwa kwenye uchaguzi kwa kunyimwa kula (kura). Full Stop!
unayesema tuchange hela tuchange kwa msingi gani? Kodi yangu haitoshi na kama haitoshi basi itafutwe njia ya kuziba hiyo bajeti. Sio shule ifunguliwe na mwalimua awe mmoja. Bunge limepitisha 18% kwa elimu na 16% kwa barabara. Yaani basi wangeweka 20% labda kila shule ingepata mwalimu mmoja zaidi.
ReplyDeleteViongozi wajiulize kama wao wangesoma shule zisizo na walimu wangekua hapo walipo? au kwa vile wao wanahela za kuwapeleka watoto wao medium english academy schools ndio maana hawajali? wangetakiwa wawe mfano bora na kuamini elimu ya nchi yetu na kuwasomesha watoto wao public schools toka darasa la kwanza mpaka form VI na hata vyuuo wasome vya Tanzania sio kuwapeleka watoto wao nje ya nchi
ReplyDeletewe are simply not serious!too much longo longo.
ReplyDelete