
huku lexus lake likiwa limebana pembeni babu njenje akiangalia ubomoaji wa majengo ya ambassador plaza ambako bendi yao ya kilimanjaro band 'wana-njenje' ilikuwa maskani yake kwa karibu muongo mmoja. hivi sasa njenje watakuwa wakiduarisha wadau kule bwalo la maafisa wa polisi kila ijumaa kuanzia ijumaa ya tarehe 27 mwezi huu pamoja na shughuli maalumu kama vile harusi na kadhalika. wakati huo huo juhudi za kupata maskani mpya zinaendlea kwa bendi hii ambayo imedumu kwa miongo takriban mitatu bila kusambaratika

waziri ally (shoto) na babu njenje pamaoja na wana-njenje wengine wakila stori nje ya ambasador plaza ambayo leo imeanza kupigwa nyundo rasmi kupisha ujenzi wa jumba litalokuwa makao makuu ya kampuni fulani ya simu za mkononi

baa ya ambassador plaza kabla haijala nyundo leo
I see bwana michuzi hebu niambie hao njenje watakuwa wanapiga wapi kila jmosi? Maana ushanichanganya hapa umesema watakuwa kila Ijumaa wanapiga bwalo la polisi na jmosi je? Sasa mbona pale njenje plaza ndio palikuwa pazuri na centre kwa kila mtu kuweza kufika.
ReplyDeletejamani huyo hapo pembeni ndo waziri wa bi nyota? mh! mbona afya inaonekana ina mgogogoro au picha tu?
ReplyDeletekuna mtuu yeyote anaweza kuniambia wapi nnaweza kusikiliza nyimbo za kilimanjaro band? any websites.
ReplyDeletemichuzi unaweza kuniambia wapi ntaweza kusikiliza nyimbo za njenje? yani any website that you might know of.! ntashukuru
ReplyDeleteHawa ndiyo "Legends" wa Tanzania. The group is more than a family coherent group.. they have been there for us the lovers of Njenje and for themselves as a Group.... They need to be commended fro all these and why not proposing them to be a National Band!!!! (aKd)
ReplyDeleteHao wana Njenje wengine hawana majina?
ReplyDeleteBwana we hawa jamaa ninavyowapenda halafu unaniambia tena watakuwa wanapiga bwalo la posili itakuaje mbali namna ile?
ReplyDeleteWaama...moja ya tofauti kubwa ya wenzetu na sisi watanzania ni kama ifuatavyo: Katika kila jamii muziki hutumika kuelezea hisia, mila na desturi za watu wake. muziki hutumika wakati wa vilio, dhifa za kitaifa, furaha,sherehe mbali mbali na kadhalika. Kwa muda mrefu sasa tumekuwa na fikra potofu ambayo inaashiria muziki si kazi au si kazi ya maana. Kwa wenzetu walioendelea, huwaenzi wanamuziki wakongwe na kuwalea wanamuziki wachanga kwa namna mbalimbali toka ukuzaji wa vipaji,mwanga wa kujulikana (exposure)na kadhalika. Waweza jiuliza kwa nini nataja mambo hayo! Binafsi nahisi hii ni dhulma kubwa kuwanyima nafasi katika jamii wanamuziki ambayo maisha yao yameegemeza kila walichonacho katika kuifurahisha jamii, kuielimisha kwa namna mbalimbali na kadhalika.Iweje leo makampuni ya ndani au ya nje kutaka kuchukuwa sehemu zilizo muhimu ambazo hutoa burdani kwa jamii na kugeuza ofisi za kazi. Jee!kipaumbele chetu kiko wapi? Ni bora kuwa na ofisi za kampuni kubwa yenye uwezo wa kifedha kuwaondoa wanyonge, wanamuziki watoao burdani kwa jamii kwa kisingizio cha biashara? Kwa kuwa wana uwezo kwa nini wasipeleke hizo ajira za ujenzi na kazi kwenye maeneo endelevu ambayo kwa kweli yanahitaji huduma za makampuni haya makubwa? Hainiingii akilini hata kidogo kuona Njenje wanaondolewa mahala ambapo palikuwa wanawapa watu wengi uwezo wa kufika kirahisi,mandhari mazuri na ya kuvutia ati kwa kisingizio cha uekezaji!!Niwazavyo mimi, kungepatikana njia mbadala ya kubadili mwenendo au mfumo mzima wa kiundeshaji wa biashara na kupabakiza hapo mahala kama sehemu ya starehe. Nikumbukavyo mimi hapo mahala watu walikuwa wakikutana kwa ajili ya mikutano, mipango ya harusi na kadhalika. Pia palitoa nafasi ya watu kukodi kwa sherehe zao binafsi kubwa na ndogo. Sasa watu hawa waende wapi? Hii kweli ni haki kwa wananchi?? Naomba kuhitimisha mada yangu kwa kuiomba manispaa ya Kinondoni na wengine wote wanaohusika nchi nzima kutunza sehemu muhimu kama hizi katika kuhifadhi mila, tamaduni na desturi za mtanzania. Yatengwe maeneo maalumu kwa miradi endelevu, biashara za kimataifa na ofisi za biashara za ndani.Sioni sababu hata moja ya maana kuvunja Njenje Plaza kuwapisha wawekezaji wageni. Ningeelewa vizuri kama hao wawekezaji wangekuja kutumia mapesa yao katika kuujenga upya ukumbi huo pamoja na hoteli na sehemu ya Bar na kuwaacha watu waduarike hapo hapo!toba!!
ReplyDelete