
Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mama Regina Lowassa ndiye atakayekuwa mgeni rasmi katika Kinyangang'anyiro cha kumsaka malkia wa Temeke kitakachofanyika Julai 14, mwaka huu katika ukumbi wa PTA(Ndani ya viwanja vya Sabasaba).
Katika shindano hilo, ambalo Miss Temeke 2006 Jokate Mwegelo atakuwa akivua taji lake, BMP Promotions imekamilisha taratibu zote na uthibitisho kutoka kwa mama Lowassa wa kuhudhuria kama mgeni rasmi na hiyo ikiwa ni historia mpya kwa mashindano yetu ya kuwa na mgeni kama huyo.
Mrembo Jokate anayevua taji ametupa heshima kubwa manispaa ya temeke ya kutamka kwa kifua mbele kauli mbiu ya Mrembo mwenye malengo, hivyo BMP Promotions imeona ina kila sababu ya kuwepo kiongozi kama mzazi kushuhudia mrembo mwingine wa kauli mbiu hiyo akipatikana JUlai 14.
Wadhamini wakuu wa Miss Tanzania, Vodacom, Multichoice Tanzania, CXC Tours and Safaris, Redd's Premmium Cold, Fabak Fashion, Dollywood Fashion Photography, Screen Masters, Ako Catering, 88.4 Cloud's FM na mbunifu maarufu wa mavazi nchini Ally Rehmtullah hadi sasa ndiyo waliothibitha kudhamini mashindano ya Miss Temeke 2007.
Miss Temeke, mwaka huu itakuwa na aina za burudani ili tofauti ilikuwa picha isiyolingana na miaka ya nyuma jinsi tulivyokuwa tukifanya. Washiriki waliopo ni kutoka vitongoji vya vinne vya Kigamboni, Kurasini, Chang'ombe na Temeke South.
Wanaendelea kunolewa na wakufunzi Jokate Mwegelo, Devotha Chonya na katika shoo wakiwa na kiongozi wa safu ya wanenguaji wa Twanga Pepeta, Super Nyamwela katika klabu ya TCC Chang'ombe.
Warembo hao ni Baby Lema, Queen David, Caroline Msaki, Suraiya Mohamed, Linda Kaaya, Taji Simba, Monica John, Sophia Juma, Shani Cheni, Mercy Simba na Leotrocia.
imetolewa na: Benny Kisaka,
Mkurugenzi BMP Promotions (waandaaji wa miss tmk)
Jamani Watanzania hawa malkia, na uzuri umeshakuwa mwingi, tumeshachoka na vimbwanga vya umiss na umalkia, kili unapokatiza habari ndio hizo.
ReplyDeleteHivi watu hawana kazi ya kufanya, au kuvumbia vitu vyengine ama vipi ?
Mambo yakishakua mingi, hilo kwa hilo kwa hilo, inakua inakera.
Na wewe michuzi wacha kutuzingua, kila siku kutuwekea vichupi tu hapa.
TUMECHOKA! TUMECHOKA!.
Leteni Jipya..
Tafuteni kazi ya maana mukafanye!
ASANTS SANA MICHUZI KWA WALLPAPER NZURI SANA..
ReplyDeletehaya kila la kheri walimbwende lakini kwa sampuli ya hao hapo juu,miss world mtashika mkia wabongo.hao mbona wafupi alafu sura zao mhhhhhhhhhh .tafuteni walimbwende km wale wa mwaka 2005
ReplyDeletembona wana sugu za magoti?
ReplyDeleteha haaa wewe unayeongelea sugu za magoti wala hujakosea!unajuwa tatizo ni makrimu hayo na mikorogo wanayotumia. kila mtu anataka rangi ibadilike sasa kuna sehemu mwilini ambazo hata upake vipi mkorogo utadunda tuu hebu chunguza wanaotumia hayo madude utawajua tuu maana vidoleni(mikononi na miguuni) na visugudi vya mikono na magoti vinakuwa vyeusiiii!!
ReplyDeleteNaoana hakuna mtu mweupe hapa afadhali maana Tanzania tumesha kuwa kama Afrika ya Kusini zamani,weusi kuwabagua weupeNaona angeonekana mweupe hapa ingekuwa tabu,
ReplyDeleteWeusi wamejitokeza wame ambiwa wana sugu magotini wakijotekeza weupe wana ambiwa hawafai wahindi sijui nini kifanyike
Huu ndio uzuri wa Tanzania siku hizi.Tumesota sana.Wacha dada zetu wajirembue.Chakula cha vitamini kipo Bongo ndio maana watoto wanaanza kuwa na afya na uzuri kama huo.Enzi zetu sisi ilikuwa ni ugalu na msusa peke yake.Acha wewe tanzania sasa ni very international!.Keep on girls,dont watch dem bad mind!
ReplyDeleteWanatoka wapi kile leo?
ReplyDeleteJamani kumbe Tanzania ilikua imeficha warembo wakati ule ambao hatushiriki mashindano
God bless Tanzania na warembo wake