MATUMIZI YA TARAKIRISHI NA KUTOJUA SHERIA
(COMPUTER USE AND IGNORANCE OF LAW)

Kifungu cha 8 cha Sheria ya Makosa ya Jinai (Cap. 16 R. E 2002) kinasema kutokujua sheria hakumsaidii mtu kutotiwa hatiani kwa kosa alilofanya isipokuwa kama ufahamu ni sehemu muhimu ya kosa alilotenda.

Sheria ya Nembo za Taifa (The National Emblems Act Cap. 10 R.E 2002) katika kifungu cha 6 ni kosa la jinai kutumia Nembo za Taifa au mifanowe kama trade mark katika kutangazia bidhaa au kitu chochote kilichouzwa au kinachouzwa; kwenye matangazo ya biashara au katika MATUMIZI MENGINE YOYTE AMBAYO WAZIRI WA MAMBO YA NDANI HAJATOA RUHUSA YA KUTUMIA NEMBO HIZO. Nembo zenyewe ni BENDERA YA TAIFA, COAT OF ARMS (Wengi wanaiita Bibi na Bwana, sijui kama ndio jina rasmi la Kiswahili) na MIHURI YA TAIFA.

Ni Kosa la jinai kufanya vitendo vinavyotukana au kudharirisha Nembo za Taifa (kifungu cha 7)

Makosa hayo mawili mtu anaweza kukamatwa bila ya waranti (kifungu cha 14 cha Sheria ya Mwenendo wa Mashitaka ya Jinai, CPA, Cap. 20 R.E. 2002)

Adhabu ya faini ya Tshs. 20,000/= Kwa atayetiwa hatiani au aweza kuhukumiwa miaka miwili jela au vyote (faini na jela); adhabu hii ni kwa kosa lolote kati ya hayo mawili hapo juu.

Leo hii kuna blogu ngapi ambazo zimetumia Nembo hizo pasipo Ruhusa ya Waziri husika? Kuna blogu na websites ambazo zimewekwa pendera ya Taifa; kuna zingine zimewekwa Bendera na Coat of Arms; Ila walionifurahisha kuliko wote ni bloga mmoja ambaye sehemu ya kubandika picha yake, ndio kuna hii nembo ya Bibi na Bwana na mwingine aliiweka bendera ya taifa, vikatuni vilivyo uchi pamoja na maandishi yasemayo, “halalisha picha za ngono Tanzania”!

Kuna wengine huwa wanatutengenezea business cards na kutuwekea hizo nembo mbili (bendera na bibi na bwana); kweli Waziri wa mambo ya ndani anajua kuna watu wanatumia hizi ndembo watakavyo?

Wangapi huku kwenye mitandao ya kirafiki(hi5, face book, Graduate.com na mingine mingi) tumetumia nembo hizo kama picha zetu? Je tulikuwa tunajua kuwa tulikuwa tunatenda makosa ya jinai? IGNORANCE OF LAW IS NOT A DEFENCE!

Nilidhani niwashirikishe kwenye hili, au vipi.

Mdau mwenzenu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 09, 2007

    Very informative, thanks!

    SteveD.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 09, 2007

    I, personally thank you dearly for your message; a clarification on the usage of national symbols. While i applaud your clarification, i must say however that the whole law is futile is contemptible and full of shit. Infact Tanzania is the only country in the world that prohibits its people to own, express, flaunt, display or brandish their flag, let alone the national symbols. I always wonder "FOR WHAT REALLY AS SPECIAL"? if i cannot own or brandish my country's flag, how do you expect me to be proud of my country? I'm living in America now, and one of the things they always emphasize as patriotism is their FLAG, people buy them in the car-washing centres, hang them in their cars and everywhere. But you Tanzanians, it's the opposite. It seems as if, Tanzanians do things in reverse. What a nation! Maybe you can answer my simple question, What is special with our Tanzanian flag or national symbols?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 09, 2007

    Well hapo umesema kweli lakini pia jua kuwa kuweka bendera au kitu chochote ni kuwa na mapenzi na nchi yako na huku tayari kutetea nchi yako kwa mali na hali so ndio unaitwa uzalendo ila tu tusitumua kwa nia mbaya ...

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 09, 2007

    Hebu tutolee upumbavu wako huko, Nyambaaaf

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 09, 2007

    Unajua sheria zingine inafaa zibaki kwenye vitabu tu, au zifutwe kabisa.

    Leo tuko kwenye dunia ya ujasiriamali kwa hiyo vitu kama bendera ya taifa, ngao ya taifa, n.k. should be a fair game. Restriction pekee inayofaa ni kwamba hivyo vitu watumie raia wa Tanzania tu. Ninaamini wote wanaotumia wanatumia kwa ufahari wanaojisikia kutangaza nchi yao, na hawatakuwa na agenda za kupaka matope Tanzania.

    Mifano mizuri ni Jamaica, USA, na UK ambapo bendera zao tunazivaa kila siku, na zinatumika kwenye movies na blog na kila mahari ambapo wajasiriamali wanaona itafaa. It's sort of Patriotism so as to say.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 09, 2007

    Michuzi,nakupa honhera kwa kazi murua unayoifanya ya kuwahabarisha wapenda habari,halikadhalika nawapongeza wekundu wa Msimbazi kwa kuchukua ubingwa hapo jana. Wanajangwani wenzangu wasisikitike sana hiyo ndiyo mchezo wa soka,cha msingi tuajiandae kwa ajili ya michezo ya kimataifa neksti sizoni,pia kuhakikisha ikitoa wakati mwingine hatuwapi nafasi ya kwenda kwenye matuta maana wanangekewa nayo.
    Nelly

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 09, 2007

    Nyie wadau mnaojifanya kwamba mko US, kabla ya kulalamika mjaribu kufanya uchunguzi kwanza. Siku hizi bendera ya TZ zimezagaa kila kona na watu wanaziweka kwenye magari (ila uruhusiwi kupeperushs kama viongozi), hata wakati wa mechi za simba na yanga wengine utakuta wana vipeperushi vya bendera ya taifa. Sasa wewe unalaumu nini, inaonekana hujaja TZ kwa siku nyingi unasikia tu. Nyamaafuuuuuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 09, 2007

    Hii mada ni muafaka kabisa kujadiliwa. Huenda tu ningechangia kwa wale wanaoona kwamba siku hizi bendera na baadhi ya vitambulisho vya taifa vimezagaa na kuona kwamba hiyo si shida. Ukweli ni kwamba, kama sheria ya nchi haijabadilika, bado hilo ni kosa kisheria. Kwa hali ilivyo sasa,ni kawaida kuona wananchi wamebeba bendera, au wamevaa vitu vinavyofanana na hivyo. Tofauti na ilivyokuwa zamani kidogo ambapo ukionekana umevaa au kubeba kitu kama hicho basi unaweza hata kufungwa.
    Uweli wa sasa ni kwamba, kuna mambo ambayo hayana maana kuendelea kuyashikilia na tena katika ngazi ya sheria za nchi. Hili ni moja wapo. Nadhani hii sheria ni mojwapo ya mambo ambayo hayana budi kubadiliswa. Na kuruhusu wananshi kujidai na bendera, na vitambulisho mbalimbali vya utaifa wao. Ninakubaliana na hoja kwamba, kuna umuhimu wa kuratibu matumizi lakini uratibu uwe wa busara na hekima

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 09, 2007

    Hili suala la bendera mimi sioni kama ni vyema kuendelea kuwakataza wananchi wenye nchi kujivunia bendera yao. Kuna wakati fulani pale magomeni kwa wauza mitumba kulikuwa na bendera nyingi sana za mataifa ya nje kuliko bendera za Taifa la Tanzania. badala ya kuwapa wananchi bendera yao, mkuu mmoja wa wilaya akaamuru zile bendera ziondolewe. Hii ilikuwa kichekesho. nadhani hii ni mentality ya kikolono. Tanzania haina budi kubadilika. Mabadiliko haya chanya, lazima pia yapate baraka za kisheria kwa kufutwa kwa sheria kama hizi za kikoloni na ki mabavu.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 09, 2007

    Limradi sijaonyesha dharau, mimi kama mtanzania nitatakiwa kuwa na uhuru wa kupeperusha bendera ya nchi yangu jinsi ninvyotaka---hivyo we anon hapo juu unavyosema kama vyiongozi ndio maana yake nini. Mimi nipo nchi ya watu huku--gari yangu mbele inabendela ya Tanzania, PC yangu hapo job ina ngao ya bibi na bwana kama scree saver. Watu (fafanyakazi wenzangu) wakiniuliza ni nini hiyo, I proudly explain it to them. Nyumbani kwangu ndio kuwe na masharti?
    sheria za kibumbavu zote lazima :
    sheria ya raisi kuteuwa wabunge--hii lazima ifutwe,sheria inayozuia wagombea binafsi--hii lazima ifutwe, na zingine nyingi tuuuu---
    ndio maana kila siku mimi nasema watanzania tunadai kunauhuru tanzania wakati ukweli ni hakuna kitu--wengine tupo nje tunaishi kama wakimbizi.
    Na sio kwamba watanzania tulio nnje ndio tunaandika haya mambo tu--kuna wengine wapo hapo hapo bongo lakini wanaogopa, lakini wago unamwisho. JK naona anatuma mashushu wake hadi huku nnje sasa lakini kosa la vijana sikuihizi wanataka kazi wanazofanya. wengine tumesoma nao---majina yao tunayo--kazi wanafanya za kuzungia tunazijuwa--ati wanakuja kusoma--wengine wanajifanya watu wa watu--hatuogopi---wa UK baadhi majina tunayo--wa US ndio daa...
    Michuuzi nakuooooooomba usipigine chini hii kitu

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 09, 2007

    Kwani kwenye facebook au vitu kama hivyo mtu anauza kitu? Mimi nimeelewa ni kama unauza kitu ndio huruhusiwi kutumia nembo yao.

    Lakini wamesahau kuwa kuna website nyingi za kitalii pamoja na kuwa zinafanya biashara kutafuta watalii lakini pia zinaitangaza nchi.

    Itakua ujinga kuanza kutangaza nchi bila bendera ya nchi wakati kila nchi zinafanya hivyo ulimwenguni.

    Ni mwanzo wa kujiondoa ulimwenguni kimya kimya. Na wakianza kuwakamata watu wote wanaotumia nembo hiyo ili kuwatia sheriani, itakua ni ujinga, upotevu wa hela zetu na muda wa walipa kodi. Kuna mambo mengi ya muhimu ya kufuatilia na kuwatia sheriani zaidi ya hilo.

    Wangetakiwa washukuru raia wa nchi wanasaidia kuitangaza nchi amabayo imeshindwa kujitangaza yenyewe ulimwenguni.

    Mimi nikionaga bendera ya nchi nisiyoifahamu huwa naenda kuiangalia kwenye flags of the world na kusoma malekezo kuhusu hiyo nchi kidogo na natumaini kuna watu wengine wanafanya hivyo vivyo. Huwezi jua ni jambo gani litamvutia mtu kwenye hiyo nchi.

    Wanatakiwa ku update laws zao zingine zinapitwa na wakati.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 10, 2007

    Kesho ikija party ya east african comminity nyingine utaacha kuonyeshaflag yetu? Oh jamani???

    Hivi tunawalipa ya nini hao watengeneza law. Wamekalia kuendesha magari mazuri na kuishi nyumba nzuri. Kila siku asubuhi wanaenda kazini na kurudi jioni kwa nini hawa pitii laws zote na kuona ni zipi zimepitwa na wakati na zipi zinatakiwa kubadilishwa?

    Tuko bado la sheria zilizotungwa mwaka 1962 au 64. We need to catch up with the world if we want to get somewhere. Hata watu wasio watanzania wakisoma hii watatuona wajinga.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...