hii ni hoteli kongwe nchini ambayo siyo tu inapendeza kwa nje bali pia hata chakula, malazi na wahudumu ni bomba sana. nimejionea mwenyewe leo. ngoja niwasimulie...
mnamo saa saba hivi nilifika hapo nikiwa na mihadi ya kula dina la mchana na kocha wa timu ya taifa ya vijana bw. marcus tinocco ikiwa ni pamoja na kumuintavyuu. kwa bahati mbaya alichelewa kidogo hivyo nikabana lonji kumsubiri. alipofika nikainuka na kwenda ukumbi wa dina kujichana na kufanya naye intavyuu - unajua tena.
sasa bwana, kumbe pale lonji nilipoketi awali kamera yangu ya kiunoni ilinidondoka bila mimi kujua. niling'amua hilo nilipotaka kumpiga picha baada ya dina hevi la mchana na intavyuu. kwanza nikadhnai kamera niliiacha ofisini, nilipoenda kucheki na kukuta patupu nikarejea new africa na kuulizia wahudumu.
bila ajizi wakaniambia kamera ilokotwa na mteja mmoja ambaye aliikabidhi resepsheni. kuulizia na baada ya kuhojiwa hili na lile na kuthibitisha, nikakabidhiwa kamera yangu. yaani tayari nilikuwa nimeshaanza kupiga mahesabu ya kutembeza bakuli (huku nikitetemeka jinsi waosha vinywa watavyoninanga kama ndugu yangu nanihii...) maana kamera yenyewe ni ndogo lakini ya bei mbaya.
namshukuru mteja wa hoteli ya new africa kwa usamaria wake na pia wafanyakazi wote wa shifti ya mchana ambao walinipa faraja kubwa kwa kuweza kunihifadhia kitendea kazi changu kwa uaminifu.
NAWASHUKURU SANA WAFANYAKAZI WA NEW AFRICA KWA UPROFESHNO MLIONIONESHA SIO TU KWA KUWA KAMERA YANGU ILIPATIKANA BALI PIA KWA JINSI KILA MMOJA ALIVYOKUWA TAYARI KUNISAIDIA HATA KAMA ISINGEPATIKANA. ASANTENI SANA NEW AFRICA HOTEL KWA HILO NA KWA KUVUTIA WAGENI AMBAO HAWANA VIDOLE VYEPESI
Sasa Michuzi mbona hujatutajia beik ya hiyo dina ya lunch yao ilikuwa kiasi gani. Pili kwa kuwa ulifanikiwa kuipata kamera yako, hivyo unatushauri au unaipigia debe kiaina Africa Hotel ili twende hapo nasi.
ReplyDeleteHaaaah aaaa
SIO WOTE NI WABAYA BWANA MICHUZI KUMBUKA UMZANIE KUMBE SIO. UNGEKUWA WEWE NDIYE UMEIOKOTA HAPO NEW AFRIKA WAKATI UKIFANYA MAOJIANO NA HUYO KOCHA WA WATOTO
ReplyDeleteUNGEFANYAJE?? JIBU TAFADHARI
Pole kwa kupata kiroho kaka Michuzi.Lakini siku hizi naona wabongo (customer care) ktk biashara kubwa wanabadilika taratibu na kurudia ule utanzania wetu wa miongo kadhaa nyuma;UAMINIFU.
ReplyDeleteNimeipenda sana hii picha mkubwa wangu.Nachukua fursa hii kukuomba ili nikaiweke Google Earth kama "nilivyoziiba" nyingine na kuzibandika; naomba unisamehe kwa hilo. Itabidi nirudi ili ni-edit kwamba mpiga picha ni Michuzi na sio Tanzanianboy.
Kazi njema bro. Michuzi
Naomba mnirekebishe iwapo slang za bongo zimeniacha traffic lights: Dina la mchana ndio LUNCH?
ReplyDeleteInamaana lanchi ya asubuhi ndo kifungua kinywa?
Najua kwetu kijiweni bagia (makande/ugali) vyaliwa mida yote.
Blackmpingo