katibu mkuu wa tff frederick mwakalebela akionge na waandishi wa habari. leo katangaza kwamba baada ya simba kuchomoa kombe la tusker linaloanza jumamosi hii uwanja wa ccm kitumba huko mwanza, nafasi yao inachukuliwa na prisons ya mbeya ambao wamekubali kujaza hilo pengo. mwenyekiti wa yanga mh. imani madega akiongea usiku huu kadai kwamba simba imewamicha...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 27, 2007

    sijui katumia vigezo gani,kwa mawazo yangu timu bora zingeteuliwa
    kati ya polisi morogoro au JKT Ruvu.Lakini sasa basi tena kama wameamua walivyoamua.
    mji kasolo bahari Morogoro

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 27, 2007

    Kaka Michuzi Kaduguda na Dalali wameshachungulia wakaona uso kwa uso na Yanga sasa wakaona safari hii kibao kimewalalia wao sasa wanaogopa kuchafua CV yako wanajua wakifungwa na Yanga kamati ya muda imeundwa wao wanamwaga unga wao sasa Kaka Michuzi madaraka matamu. Kadugunda na Dalali wamechemka kwa hilo!!!!!! bila ubishi wowote.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 27, 2007

    Bwana Michu,
    Hilo ni somo.Hao TFF bado hawajajipanga sawasawa ndio maana matatizo hayatokwisha ktk soka la Bongo. Timu zenye nguvu wanatumia uwezo wao kama Simba walivyofanya. Sasa JKT Ruvu, Polisi Moro nk hawana mtetezi. Ndani ya TFF kuna viongozi wanaoongoza vilabu na wanaitumia TFF kwa maslahi ya vilabu vyao. Tazama yaliyotokea kwa Simba vs Ashanti, Kesi ya Chuji,usajili wa Tusker na ligi inayofuata, nk. Ushauri wangu ni kwamba, TFF watafute wakala wa kufanya mambo yao makuu kama vile kuendesha ligi, mashindano mengine yaliyo ndani ya kalenda yao, chombo cha sheria kusimamia usajili na haki za vilabu na wachezaji, nk. Ili kupunguza mzigo kiutendaji, kwa kuwa baadhi yao hawajaiva kuendesha chombo cha kitaifa. Tukinyamaza wataturudisha nyuma.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 27, 2007

    Huyu bwana kaduguda na mwenzake kwa kweli wamechemka sanaa..sijui wanafikiria nini kwenye vichwa vyao..ilikuaje wakubali kwenda kuchukua jezi na vifaa alafu baadae wabadilishe mawazo?,huo si utapeli jamani.Haya matatizo ya kuwapa uongozi watu wasiokuwa na akili timamu.mimi ni simba na hichi kitendo kimenikasirisha sana.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 27, 2007

    I see Mwanza imeendelea kweli wanja jingine jipya la Kitumba?na ile Kirumba bado ipo vile vile au?nifahamishe ndugu yangu mambo mapya ya jiji la zoo.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 27, 2007

    kitendo cha bro kadu kuchomoa nasikia kimewaudhi kweli friends of simba maana walishapanga mashambulizi. looks like kaduguda nia yake hasa ni kuwa embarass friends of simba na kuwaonyesha nani ana power. kumbuka hata kambi bamba beach friends ndo walipeleka timu kila siku karibu laki tano wamelipa.nasikia leo movie pick friends of ssc wameitisha kikao cha nguvu,shuhudia fitna itakayotoka hapo,could be mwisho wa dalali &co?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 27, 2007

    Kaduguda yule ni M**n**! Kabisa,Mambo gani hayo ya kujitoa mashindanoni wakati wachezaji wako tayari kucheza,
    besides posho zingewasadia wachezaji na vile vile wangepata exposure kwa maximo!
    Hii ndio shida ya viongozi vishoka!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 27, 2007

    MI NAIUNGA MKONO SIMBA KWA KUCHOMOA KUSHIRIKI KOMBE LA TUSKER.
    NAJUA WENGI WATAONA KAMA NI KITU CHA KIJINGA, LAKINI KWA SISI TUNAOWAFAHAMU SANA TFF, UAMUZI WA SIMBA KUJITOA NA KUANGALIA MASLAHI YA TIMU NI SAWA KABISA.
    MIMI NI MPENZI WA YANGA NA NINAONA UCHUNGU SANA WAKATI TIMU HIZI ZINAZOTENGEZA MAMILIONI YA FEDHA KILA MWAKA, ZIMEKUWA ZIKIHANGAIKA KUIJIENDESHA KWA VILE KILA KITU HASA MAMBO YA FEDHA, YAPO CHINI YA TFF! MPAKA LINI.
    WATU WENGI WANADHANI SOKA HUENDESHWA KWA SENTI CHACHE LA HASHA. TFF IMEZOA FEDHA KIBAO NA KUJIFANYA WAO NDIYO WATOAJI WA FEDHA TOKA KWA WADHAMINI.
    KWA NINI TFF ISIKAE PEMBENI NA KUZIACHA KLABU KUZUNGUMZA NA WADHAMINI WENYEWE?
    KWA NINI TFF ISIJISHUGHULISHE NA USIMAMIAJI WA MECHI NA SIYO KUJIINGIZA KATIKA UGAWAJI WA VIFAA NA MAMBO MENGINE YASIYO NA MSINGI?
    SIMBA ILIPOPEWA POSHO NDOGO, TFF ILIIBUKA NA KUIONGEZA FEDHA HARAKA ILI KUIKOA TFF KUTOPATA MAPATO DUNI KWENYE MASHINDANO HAYO. NDIYO...FEDHA ZA NYONGEZA ZILIPATIKANA WAPI WAKATI KILA KITU KILISHAPANGWA TOKA MWANZO?
    SIMBA INGETAKA KUFANYA UHUNI INGEIINGIA KATIKA MASHINDANO HAYO NA KUFUNGWA MECHI ZAKE ZOTE KATIKA KUNDI LAKE NA KUINGIA MITINI NA FEDHA. TFF AU WADHAMINI WANGEFANYA NINI?
    WATU WENGI WANAOJIFANYA WANAJUA SOKA HAWAELEWI NI JINSI GANI KLABU ZINAVYONYONYWA NA TFF KWA KILE WANACHOKIITA USIMAMIAJI NA UENDESHAJI WA LIGI AU MASHINDANO FULANI.
    KLABU HAZINA HAKI YA KUUZA TIKETI NA NDIYO MAANA KILA SIKU TIKETI ZITAUZWA MLANGONI TENA SIKU YA MECHI WAKATI MAMBO KAMA HAYO YANGEFANYIKA HATA KABLA YA MSIMU WA LIGI AU MASHINDANO YOYOTE YALE KUANZA.
    KWA MFANO HADI SASA TIKETI ZA STARS NA MSUMBUJI HAZIJAUZWA LICHA YA KWAMBA MECHI HIYO ITACHEZWA KWENYE UWANJA MPYA SEPTEMBA 9. TFF WANASUBIRI NINI KAMA SIYO KUTAKA KUUZA MECHI KWA MTU NA FEDHA KUTIA NDANI.
    TFF WANAPOUZA MECHI NA KUCHUKUA FEDHA, HIZO FEDHA ZINAENDA WAPI WAKATI HATA ZA KUHUDUMIA STARS ZINATOKA KWA WADHAMINI?
    KUNA MAMBO MENGI YA KUJIULIZA NA HII TFF. ALIPOKUWA NDOLANGA, MWANAKATWE, RAHE NA AKINA AMIN BAKHRESA TULIJUA WANAKULA FEDHA NA HATA RAGE AKAFUNGWA JELA!
    SASA YUPO TENGA NA WENZAKE HALI NDIYO IMEIZIDI KUWA DUNI LICHA YA KWAMBA MIAKA HII LIGI YAO INAENDESHWA NA WADHAMINI KULIKO ENZI YA KINA NDOLANGA!
    WASHABIKI WA SOKA MMEKUWA MKIROPOKA TU BILA KUJIULIZA KWA NINI KLABU HASA SIMBA NA YANGA ZINAPOCHEZA NA KUINGIZA MILIONI 90 HUWA ZINAAMBULIA MILIONI 15 AU 20 TU KILA MOJA?
    HIZO FEDHA NYINGINE ZINAZODAIWA NA TFF ZA MAANDALIZI KAMA VILE WAAMUZI NA MAMBO MENGINE YA KIOFISI NDIYO HUGHARIMU MILIONI 50 AU 60? NA KLABU NAZO HAZIINGII GHARAMA ZAIDI HIZO?
    KWA NINAVYOFAHAMU MIMI KLABU NDIYO ZINAZOINGIA GHARAMA KUBWA KWA KUTAFUTA KAMBI NA KULIPIA BILI ZOTE ZA CHAKULA, MALAZI PAMOJA NA POSHO ZA WACHEZAJI.
    LAKINI BAADA YA MECHI TU HUONDOKA NA MILIONI 15 NA ZILIZOBAKI HUZAMA TFF. HAO TFF WALIZISAIDIA KLABU KULIPA GHARAMA ZA KAMBI?
    MFANO MZURI NI MECHI YA SIMBA NA YANGA ILIYOCHEZWA MWEZI ULIOPITA HUKO MORO AMBAYO ILIINGIZA KARIBU MILIONI 50.
    SIMBA NA YANGA ZIMEONDOKA NA MILIONI SI ZAIDI YA MILIONI 25 KWA JUMLA(12M KILA KLABU). ZILIZOBAKI NI TFF, POLISI, UWANJA NA MAMBO MENGINE. HAYO MAMBO MENGINE NI YAPI YASIYOISHA KILA MWAKA HUKU KLABU ZIKIENDELA KUWA DUNI?
    NAKUMBUKA MIAKA YA 90, AZIM DEWJI NA ABBAS GULAMALI LICHA YA KWAMBA WALIKUWA WAKINUFAIKA KWA KIASI FULANI, LAKINI WALISHINDWA KUJUA NI JINSI GANI FAT (WAKATI ULE) ILIVYOKUWA IKIIBUKA NA MAPATO MAKUBWA WAKATI YENYEWE HAITUMII SENTI TANO KUSAIDIA KLABU KATIKA MAANDALIZI ZAIDI YA KUUZA TIKETI.
    NA NYINGI KATI YA TIKETI ZAO ZILIKUWA ZINACHAPISHWA MARA MBILI ILI KUNUFAISHA HAO VIONGOZI WA FAT!
    KADUGUGA ALIKUWA FAT NDIYO MAANA ANAJUA SIRI NA JINSI MAMBO YANAVYOFANYWA KATIKA KUNEEMESHA MATUMBO YA WACHACHE WAKATI WATOKA JASHO (WACHEZAJI) WAKIHANGAIKA NA MABASI AU BAISKELI HUKU WENYEWE WAKIWA KWENYE BALOON NA MA VX-5.
    TUSIWE WAJINGA KILA KITU KUWA WEPESI WA KUKUBALI NA KUWAACHIA WAJANJA WAKILA JASHO LA WANYONGE. WATU WAMEELIMIKA SASA HIVI NA NDIYO MAANA TFF WAKAIOMBA PRISONS YA MBEYA NA SIYO ASHANTI AU JKT RUVU.
    HAMJIULIZI HIVI KWA NINI KLABU ZA BONGO HAZINA HAKI YA KUUZA TIKETI ZA MECHI ZAKE KAMA ZIFANYAVYO KLABU ZA NJE KAMA UK, MAREKANI NA HATA ASIA HIVI SASA?
    HIVI TUPO KARNE YA NGAPI TUSIONGALIA MASLAHI YA KLABU NA KUIPA MWANYA TFF KUCHUKUA KILA WANACHOONA KINA MANUFAA KWAO.
    KLABU HIVI SASA ZINGESTAHILI KUUZA TIKETI ZA MECHI ZAO TENA KWA MSIMU MZIMA NA TFF INGEUZA TIKETI ZA TAIFA STARS NA SIYO KUZIINGILIA KLABU.
    SOKA NI BIASHARA NA INAHITAJI FEDHA, TENA NYINGI MNO.KAMA HUNA ITAKUWA KAMA TIMU ZA MAJIMAJI AU PAN AFRICAN. ZIPO WAPI HIVI SASA!
    KUCHONGA TUU BILA MPANGO.
    SAWASAWA SIMBA TENA MMEFANYA JAMBO HILO WAKATI ZIMEBAKI SIKU MBILI. INGEKUWA SIKU YENYEWE YA JUMAMOSI...DAMN RIGHT...TFF, TFF WHO'S TFF IN THE WORLD OF SOCCER? WEZI WAKUBWA NYIEEEE

    KWAHERINI...DAIMA NITATETEA MASLAHI YA KLABU MPAKA KIELEWEKE.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 27, 2007

    NYIE waosha vinywa mnaomlaumu Kaduguda na Dalali kwanza mgejiuliza, hayo mashindano wadhamini ambao ni TUSKER wametoa kiasi gani katika kugharimu mashindano hayo?
    Pili, kila klabu inayoshiriki inatakiwa ipewe kiasi gani katika kujikumu na gharama za usafiri, malazi chakula na posho za wachezaji?
    Kwa nini TFF isiweke jambo hili wazi na badala yake ilidai kuiongezea Simba posho hadi kufikia milioni 10, je vipi Yanga na klabu nyingine zilipewa kiasi hicho cha nyongeza?
    Tatu; Kama TFF inatumia mashindano hayo kumsaidia MAXIMO kuchagua wachezaji wa Taifa Stars, je klabu za Kenya na Uganda zitakazoshiriki zina uhalali gani wa kuongeza nguvu za wachezaji wa Stars wakati wao ni wa nje ya Bongo?
    Kama TFF na MAXIMO wanataka kuchagua wachezaji wa STARS, kwa nini wasitumie mashindano yanayoshirikisha timu za BONGO TUPU ambazo zina wachezaji wote wa hapa na wenye uwezo wa kuichezea STARS?
    Vipi wachezaji wa RUVU JKT, MTIBWA, Coastal Union na nyingine ambazo hazishiriki kombe la TUSKER wachezaji wao wataonekana wapi kama siyo kwenye ligi ya Bara au LIGI KUU?
    Kitendo cha TFF kuficha mambo na kufanya kienyeji bila kuzijulisha klabu katika maamuzi mengine, ndiyo yanayochangia kushuka kwa soka na hata kuvuruga muundo wa soka nchini.
    Iweje TFF iseme mashindano yatafanyika Uwanja wa Taifa, Dar bila hata kuwasiliana na meneja wa uwanja, Massanja ili kujua hali ya uwanja huo kabla ya kutoa kauli yao?
    Iweje TFF iseme mashindano yatafanyika Moorogoro na baada ya siku mbili wabadilishe kauli na kuhamishia Mwanza huku wakijua walishapanga posho za kuhudumia timu Dar, halafu Moro na baadaye Mwanza?
    Kwa nijuavyo mimi, kitendo cha kuhamisha mashindano kutoka Dar kwenda Moro, tayari wadhamini watakuwa wameingia gharama za nyongeza kuzihudumia timu husika!
    Ghafla mashindano yahamishwe toka Moro hadi Mwanza, hao wadhamini watakuwa wajinga kiasi gani kuikubalia TFF kuhamisha mashindano kienyeji kama siyo kuna JAMBO NDANI YAKE?
    Hivi majuzi tu TFF imeichomolea VODACOM kusimamia LIGI KUU kwa kutaka ipewe milioni 600 badala milioni 358 ili iweze kudhamini ligi hiyo.
    Kama TFF imeona VODACOM haina fedha, kwa nini isiishauri TUSKER kuingia mkataba wa kutangaza LIGI KUU ambayo itafaidika zaidi na badala yake kung'ang'ania timu sita tu?
    TUSKER inafaidika na nini katika kutangaza kinywaji chake hapa BONGO wakati pombe hiyo ni maarufu hata Kenya na Uganda pia?
    Kwa nini hasa TFF iwe rahisi kukubali mashindano haya kila mwaka kufanyika BONGO. KWA NINI? KUNANI ndani yake? Vipi Uganda au Kenya hazina viwanja au vyama vyake vya soka vimeweka masharti ambayo TUSKER haiwezi kuyafikia katika kulinda maslahi ya klabu?
    Klabu ambazo ndizo zinazoingia gharama zitapewa kiasi gani au ndiyo kusubiri mapato ya mlangoni kwa kila mechi zitakazokuwa zinacheza?
    Haya mambo ya kuendeshana kienyeji na hasa hili la soka, lazima liangaliwe upya. Klabu hasa husika lazima zishirikishwe katika kila jambo na ziingie mkataba ambao zitasaidia kutoyumbishwa ama kuyumbisha mashindano yoyote yale.
    Lazima kuna kitu ndani yake ambacho sisi WAOSHA VINYWA hatujui. Wanaokataa wanafahamu sana hili na ndiyo maana TFF ilikuwa tayari kuipa Simba milioni 10 za gharama. Milioni kumi ni kitu gani? Kwa nini TFF wanaitaka VODACOM itoe milioni 600 toka milioni 350?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 27, 2007

    annon hapo juu maelezo marefu KUTETEA MSLAHI YAKO??au ya klabu???tatizo michezo bongo serikali imeipa kisogo inajitokeza pale wanaposhinda,hata TFF wakabidhi mapato au uuzaji tiketi kwa vilabu huko nako kuna walaji kibao mifano tunayo akina Rage, Castro,na wengineo wote walaji tuu.ufumbuzi ni mpaka serikali itakapo ingilia kwa undani na kucontrol kila kitu kwani michezo ni part and parcel ya economy ya nchi.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 30, 2007

    wee anony wa 8:32.unaeunga mkono simba kujitoa na kuanza kutuhubiria mengiii,inaonekana unamatatizo yako binafsi na TFF kwani jana wadhamini wa Tusker wenyewe wamesema kauli ya Kadu sio kweli.Kwa hiyo unaposema TFF imezoa fedha kibao kumbe na wewe inabidi ujiangalie kauli zako.Kwa kudhibitisha hilo the Guardian limeandika ivi 'The TFF and sponsors of Tusker Challenge Cup,East African Breweries Limited,have strongly refuted allegations made by Simba Secretary Genersl Mwina Kaduguda that the soccer body was paid 40m/- by the sponsor as administration costs for the ongoing tournament.This is a false statement.Unfortunately,it has been uttered by a top leader of one of the big clubs in the country.This may led some people to believe the story.It is very disapointing to hear such a bogus statement from a leader of a highly respected club like Simba.Funny enough,Kaduguda and his VC are the one who represented the club in our meeting.
    Under the contract,the sponsor paid TFF 13.5m/ for adminstration and not 40m/- as Kaduguda claimed.This 13.5m/- includes the payment for the seven referees".

    Mbona kama wewe ni mtetezi wa vilabu hukuitetea yanga wakati huyo Kaduguda anainyonga wakati akiwa katibu wa FAT/TFF,inabidi uwe fair na wala sio kupeleka malalamiko tu kwa TFF,mimi nadhani Simba wamejikwaa/wamekosea kwani soka letu bado sana chini na timu ya taifa inategemea baadhi ya wachezaji toka simba inaama kujiondoa kwa simba kwa madai yasiyo rasmi ni kuirudisha nyuma soka ya nchi.Tuwe na mtizamo mpana na wala sio simba na Yanga tu.TFF wanajitahidi japo inabidi ibadilishe baadhi ya mambo kama ilivyoshauriwa na baadhi ya wadau wenye constructive ideas na wala sio kuisaga tuu.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 30, 2007

    Simba wamechemsha sio soka hilo.kadu jiuzulu.unaua vipaji.Maximo wafundishe adabu hao simba huku mikoani kuna vipaji zaidi ya hao wasimba.

    ReplyDelete
  13. Amechemsha yeye Maximo na TFF yake eti wachezaji watachaguliwa kutoka kombe la Tusaker!!!!Je wachezaji wa Ruvu JKT,Polisi ambao ni wazuru watacheza Tusker au watatoka Yanga Mtibwa na Prisons.Hana ubavu wa kuacha wachezaji wa timu hizo wewe tulia tu utaona.Kwenye ligi ndogo ndio kulikuwa na timu nyingi kwanini wachezaji wasichaguliwe ktoka huko???Mantiko ipo wapi???

    ReplyDelete
  14. MAXIMO LEO KATKA MAHOJIANO AMESEMA HAWEZI KUCHAGUA WACHEZAJI KUTOKA KATIKA KOMBE LA tUSKER KWANI TIMU AMESHAICHAGUA WIKI MBILI ZILIZOPITA NA AMESHAWAKABIDHI TFF ILI WAOMBEWE VIZA WACHEZAJI 24.ALISEMA KWAMBA HAWEZI KWENDA KUCHAGUA WACHEZAJI WENGINE KWA KUTIMIZA MATAKWA YA WATU(SIJUI KINA NANI HAO KWENYE TFF).AMEONGEZA KUSEMA KIKOSI ALICHONACHO KINAMTOSHA .HIVYO WAOSHA VINYWA NA WAZUSHI ZUSHENI LINGINE HUYO KOCHA HABURUZWI KAMA WENGINE WALIOPITA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...