salam, hope upo ok .
nilikuwa nakuomba jambo moja naomba toa maelezo yoyote yanayohusu rais wetu wa tanzania kuwa hanywi pombe manake watu wabishi sana mimi nawaambia kuwa rais wetu hanywi pombe lakini watu wabishi kama fupa. please consider that na mimi nitawaonyesha ili wasome wadau hawa wanataka kumpakazia rais wetu mtukufu.
thanks.......aljabry
wadau salaam hizo zimeingia sasa hivi na kwa kumjibu mdau huyo aliyeko ughaibuni ni kwamba ninavyoelewa mimi sio kwamba jk hanywi wala havuti bali pia ni swala tano...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 06, 2007

    Yaani na huu nao utaikwa mjadala? Sasa raisi akunywa pombe na asinywe, asali sala tano au chahce, inahusianaje na kazi yake? Kama atakuwa mlevi kazini, au anatoa hotba amelewa hapo sawa. Sasa akijinywea ninyi mnapoteza muda kumjadili. Kweli watanzania umbea upo kwenye damu. Na huo muda ulio nao na hao watanzania wengine kwa nini msijadili nini cha maana cha kufanya kubadili maisha yenu binafsi, au ya ndugu, au ya Tanzania? Michu, ondoa hii hoja. La sivyo blog hii sasa itakuwa ya umbea...

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 06, 2007

    Hii haihusiani na habari ya hapo juu ila nadhani ni muhimu pia kwa nchi na jamii,nimeiiba kwa Saidi Yakubu (bloguni kwake):

    Baba wa mwandishi Alan Johnston alietekwa nyara kwa wiki kumi na sita huko Ukanda wa Gaza, Graham Johnston amesema kuwa mwanae huyo amezaliwa nchini Tanzania mkoani Lindi wakati mzazi huyo alipokuwa akifanya kazi kama ofisa wa wakala wa meli.

    Mzee Graham mwenyewe akizungumza na shirika la utangazaji la Uingereza BBC kwa lugha fasaha ya kiswahili alisema yeye pia ni mzaliwa wa Tanzania mkoani Dar es salaam na kuwa ameishi Tanzania miaka tisa ambapo aliishi mkoani Lindi na Dar es salaam kabla ya kuhamia Nairobi Kenya ambapo mwandishi alietekwa nyara huko Gaza aliendelea na masomo yake baada ya kuanza kusoma mjini Mombasa, Kenya.

    Wazazi hao wana mahusiano ya karibu zaidi na Afrika Mashariki kwa vile mama wa mwandishi huyo nae ni mzaliwa wa Kampala nchini Uganda.

    Kwa vile ''Baba Alan'' na Alan mwenyewe wamezaliwa Tanzania na kukaa sana huko, pengine si vibaya iwapo mamlaka husika nchini Tanzania au hapa UK wakamualika katika kipindi hiki cha kujiliwaza atembelee mbuga za wanyama Bongo ambapo atavutia pia watalii wengine na pengine akitunga kitabu atataja mbuga zetu...
    wadau mnaonaje?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 06, 2007

    Hongera zake.
    Kaka Michuzi hata mimi pia Sivuti wala Sinywi, lakini watu watusingizia na kuchonga sana eti tusiokunywa wala kuvuta eti tuna ULEVI wetu MWINGINE.
    Wananiudhi sana lakini basi tu, nifanyeje!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 06, 2007

    Michuzi
    Nafikiri Mheshimiwa Rais ingetosha na si Mtukufu Rais, kwa hiyo kwako wewe Michuzi na huyo aliyekutumia hii mada na wadau wengine naomba isomeke wanataka kumpakazia mheshimiwa rais na si (wanataka kumpakazia rais wetu mtukufu)
    Ahsanteni

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 06, 2007

    Huyo mdau aliyezungumzia swala la Aln Johnston kweli mimi nimemsikia babaake akihojiwa na BBC mzee anakitema pomaja na kuwa ameondoka huku longtime ila Alan akisimama kwa TV ya UK tu asema amezaliwa TZ au E.A tutaosha ile mbaya.J.Magembe angemleta huyo jamaa kwenye his birthplace kwa mapumziko.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 06, 2007

    NI KWELI KIKWETE HANYI WALA HAVUTI.

    KIKWETE ULEVI WAKE UNAFAHAMIKA. WALA HAKUNA ALIYEMSINGIZIA MAMBO YA POMBE NA SIGARA. YEYE ROHO YAKE IKO NAPENDA VITU VINGINE

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 06, 2007

    Kikwete ulevi wake sio Pombe wala Sigara.

    Kikwete ulevi wake unafahamika.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 06, 2007

    ni kweli nyie msiovuta wala kunywa mna ulevi wenu mbaya sana zaidi ya pombe na sigara!!mnaujuwa wenyewe sana tu na sina haja ya kuutaja wadau...

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 06, 2007

    Napenda kuliunga mkono wazo la Mtalii Bongo na kumshukuru kwa kutujulisha juu ya mahali alipozaliwa mwandishi wa habari Alan Johnston aliyekuwa ametekwa huko Gaza. Ni jambo la kusisimua kuwa mwandishi huyo alizaliwa hapa Tanzania. Wazo la Mtalii Bongo la kumualika kutembelea mbuga zetu za wanyama ni zuri na kweli linaweza kuvutia watalii wengi kuandamana na Alan.

    Hii mada ya kuwa JK anakunywa au hanywi pombe ni jambo very personal na nadhani si kitu cha kujadili hapa kwenye blog hii.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 06, 2007

    Tee hee tee heee, vijana bwana mnanifurahisha, inaonekana unanipenda rais wenu, itabidi nigombee mihura mitatu. Ni kweli mimi sinywi wala sivuti, hata mademi situmii, tee heee tee hee.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 06, 2007

    Michuzi naona umezanza kuwa msanii. Umeanza kuweka matangazo ya CRDB, hilo tangazo basi waambie walipunguze urefu maana linachukua nafasi kubwa.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 06, 2007

    Habari wananchi wangu asanteni kwa kutaka kujua mimi rais wenu napenda nini.ningependa kuyabainisha kama ifuatavyo:

    1.Sinywi pombe
    2.Sivuti sigara
    3.Napenda kuswali sana
    4.Cha nne ni kwamba napenda sana warembo msinielewe vibaya jamani napenda kuwatizama tu.Nadhani wananchi wangu wapendwa mtakuwa mmefaidika na kufurahia kujua mawili matatu niyapendayo.
    wabilah taufiq asalm alyekum
    JK.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 06, 2007

    du,kumbe alan mbongo!lakini na yeye hicho kimbele mbele kwenda nchi za watu aache,siku nyingine watam ninihii.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 06, 2007

    Kama Michuzi huyo kikwete anywe asinywe pombe sisi wananchi haituhusu hata kidogo kwani kama anafanya kazi zake vizuri bila kulewa hatuna shida naye. Halafu hiyo Ari Mpya nguvu Mpya naona ilikuwa tiketi ya kumwingiza yeye Ikulu na si kwa faida ya wananchi kwani hiyo ya maisha bora kwa kila mtanzania imekuwa ndoto naumia sana ninapokuta walinzi wa jiji wanawakamata kina mama wanaoza nyanya, vitunguu nk huko kariakoo wakati ndio wanategemea kulisha familia zao na kuwapeleka watoto shule. Je tutafika kweli??? Na wale wa vibaiskeli barabarani wanauza Ice cream za Bakresa mbona hawakamatwi????? au wenye navyo watazidi kuongezewa na wasionavyo daima watanyanganywa na walivyonavyo?????

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 06, 2007

    hi everyone
    can any one tell me who is this aljabry and where is he?or she?

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 06, 2007

    jamani muacheni rasi wetu akilewa halewi inahusu nini na wewe ulietoa hii mada upo wapi???????

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 07, 2007

    Haya niangalieni nikikamua Gin & Juice..Kama nipo Long Beach Vilee

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...