salam, hope upo ok .
nilikuwa nakuomba jambo moja naomba toa maelezo yoyote yanayohusu rais wetu wa tanzania kuwa hanywi pombe manake watu wabishi sana mimi nawaambia kuwa rais wetu hanywi pombe lakini watu wabishi kama fupa. please consider that na mimi nitawaonyesha ili wasome wadau hawa wanataka kumpakazia rais wetu mtukufu.
thanks.......aljabry
wadau salaam hizo zimeingia sasa hivi na kwa kumjibu mdau huyo aliyeko ughaibuni ni kwamba ninavyoelewa mimi sio kwamba jk hanywi wala havuti bali pia ni swala tano...


Yaani na huu nao utaikwa mjadala? Sasa raisi akunywa pombe na asinywe, asali sala tano au chahce, inahusianaje na kazi yake? Kama atakuwa mlevi kazini, au anatoa hotba amelewa hapo sawa. Sasa akijinywea ninyi mnapoteza muda kumjadili. Kweli watanzania umbea upo kwenye damu. Na huo muda ulio nao na hao watanzania wengine kwa nini msijadili nini cha maana cha kufanya kubadili maisha yenu binafsi, au ya ndugu, au ya Tanzania? Michu, ondoa hii hoja. La sivyo blog hii sasa itakuwa ya umbea...
ReplyDeleteHii haihusiani na habari ya hapo juu ila nadhani ni muhimu pia kwa nchi na jamii,nimeiiba kwa Saidi Yakubu (bloguni kwake):
ReplyDeleteBaba wa mwandishi Alan Johnston alietekwa nyara kwa wiki kumi na sita huko Ukanda wa Gaza, Graham Johnston amesema kuwa mwanae huyo amezaliwa nchini Tanzania mkoani Lindi wakati mzazi huyo alipokuwa akifanya kazi kama ofisa wa wakala wa meli.
Mzee Graham mwenyewe akizungumza na shirika la utangazaji la Uingereza BBC kwa lugha fasaha ya kiswahili alisema yeye pia ni mzaliwa wa Tanzania mkoani Dar es salaam na kuwa ameishi Tanzania miaka tisa ambapo aliishi mkoani Lindi na Dar es salaam kabla ya kuhamia Nairobi Kenya ambapo mwandishi alietekwa nyara huko Gaza aliendelea na masomo yake baada ya kuanza kusoma mjini Mombasa, Kenya.
Wazazi hao wana mahusiano ya karibu zaidi na Afrika Mashariki kwa vile mama wa mwandishi huyo nae ni mzaliwa wa Kampala nchini Uganda.
Kwa vile ''Baba Alan'' na Alan mwenyewe wamezaliwa Tanzania na kukaa sana huko, pengine si vibaya iwapo mamlaka husika nchini Tanzania au hapa UK wakamualika katika kipindi hiki cha kujiliwaza atembelee mbuga za wanyama Bongo ambapo atavutia pia watalii wengine na pengine akitunga kitabu atataja mbuga zetu...
wadau mnaonaje?
Hongera zake.
ReplyDeleteKaka Michuzi hata mimi pia Sivuti wala Sinywi, lakini watu watusingizia na kuchonga sana eti tusiokunywa wala kuvuta eti tuna ULEVI wetu MWINGINE.
Wananiudhi sana lakini basi tu, nifanyeje!
Michuzi
ReplyDeleteNafikiri Mheshimiwa Rais ingetosha na si Mtukufu Rais, kwa hiyo kwako wewe Michuzi na huyo aliyekutumia hii mada na wadau wengine naomba isomeke wanataka kumpakazia mheshimiwa rais na si (wanataka kumpakazia rais wetu mtukufu)
Ahsanteni
Huyo mdau aliyezungumzia swala la Aln Johnston kweli mimi nimemsikia babaake akihojiwa na BBC mzee anakitema pomaja na kuwa ameondoka huku longtime ila Alan akisimama kwa TV ya UK tu asema amezaliwa TZ au E.A tutaosha ile mbaya.J.Magembe angemleta huyo jamaa kwenye his birthplace kwa mapumziko.
ReplyDeleteNI KWELI KIKWETE HANYI WALA HAVUTI.
ReplyDeleteKIKWETE ULEVI WAKE UNAFAHAMIKA. WALA HAKUNA ALIYEMSINGIZIA MAMBO YA POMBE NA SIGARA. YEYE ROHO YAKE IKO NAPENDA VITU VINGINE
Kikwete ulevi wake sio Pombe wala Sigara.
ReplyDeleteKikwete ulevi wake unafahamika.
ni kweli nyie msiovuta wala kunywa mna ulevi wenu mbaya sana zaidi ya pombe na sigara!!mnaujuwa wenyewe sana tu na sina haja ya kuutaja wadau...
ReplyDeleteNapenda kuliunga mkono wazo la Mtalii Bongo na kumshukuru kwa kutujulisha juu ya mahali alipozaliwa mwandishi wa habari Alan Johnston aliyekuwa ametekwa huko Gaza. Ni jambo la kusisimua kuwa mwandishi huyo alizaliwa hapa Tanzania. Wazo la Mtalii Bongo la kumualika kutembelea mbuga zetu za wanyama ni zuri na kweli linaweza kuvutia watalii wengi kuandamana na Alan.
ReplyDeleteHii mada ya kuwa JK anakunywa au hanywi pombe ni jambo very personal na nadhani si kitu cha kujadili hapa kwenye blog hii.
Tee hee tee heee, vijana bwana mnanifurahisha, inaonekana unanipenda rais wenu, itabidi nigombee mihura mitatu. Ni kweli mimi sinywi wala sivuti, hata mademi situmii, tee heee tee hee.
ReplyDeleteMichuzi naona umezanza kuwa msanii. Umeanza kuweka matangazo ya CRDB, hilo tangazo basi waambie walipunguze urefu maana linachukua nafasi kubwa.
ReplyDeleteHabari wananchi wangu asanteni kwa kutaka kujua mimi rais wenu napenda nini.ningependa kuyabainisha kama ifuatavyo:
ReplyDelete1.Sinywi pombe
2.Sivuti sigara
3.Napenda kuswali sana
4.Cha nne ni kwamba napenda sana warembo msinielewe vibaya jamani napenda kuwatizama tu.Nadhani wananchi wangu wapendwa mtakuwa mmefaidika na kufurahia kujua mawili matatu niyapendayo.
wabilah taufiq asalm alyekum
JK.
du,kumbe alan mbongo!lakini na yeye hicho kimbele mbele kwenda nchi za watu aache,siku nyingine watam ninihii.
ReplyDeleteKama Michuzi huyo kikwete anywe asinywe pombe sisi wananchi haituhusu hata kidogo kwani kama anafanya kazi zake vizuri bila kulewa hatuna shida naye. Halafu hiyo Ari Mpya nguvu Mpya naona ilikuwa tiketi ya kumwingiza yeye Ikulu na si kwa faida ya wananchi kwani hiyo ya maisha bora kwa kila mtanzania imekuwa ndoto naumia sana ninapokuta walinzi wa jiji wanawakamata kina mama wanaoza nyanya, vitunguu nk huko kariakoo wakati ndio wanategemea kulisha familia zao na kuwapeleka watoto shule. Je tutafika kweli??? Na wale wa vibaiskeli barabarani wanauza Ice cream za Bakresa mbona hawakamatwi????? au wenye navyo watazidi kuongezewa na wasionavyo daima watanyanganywa na walivyonavyo?????
ReplyDeletehi everyone
ReplyDeletecan any one tell me who is this aljabry and where is he?or she?
jamani muacheni rasi wetu akilewa halewi inahusu nini na wewe ulietoa hii mada upo wapi???????
ReplyDeleteHaya niangalieni nikikamua Gin & Juice..Kama nipo Long Beach Vilee
ReplyDelete