Michuzi!
Nimeona michango ya wadau. Naomba utundike shukran na maelezo yangu ya ufafanuzi.
Shukran!Wadau,
Nimefuatilia michango ya mawazo yenye kunihusu kuhusiana na harambeealiyoitangaza Issa Michuzi na iliyotokana na wazo la Mwalimu Mazara .Inahusu kamera yangu iliyokufa. Kwanza kabisa, nianze kwa kumshukuru kwadhati kaka yangu Muhidin Issa Michuzi.
Kwa taarifa tu,nilipokutana na Michuzi pale Food World mwaka mmoja uliopita nilimwomba niwe namletea kwenye blogu yake picha za shamba kwa maana ya kwetu Iringa." Maggid, kwanini usifungue blogu yako mwenyewe!" Hivyo ndivyo alivyonijibuMichuzi na tangu hapo amekuwa akinipa support kubwa.
Mtu mwingine aliyenipana anayeendelea kunipa support ni MK wa Mahusino.
Hakika sikujiandaa kuwa mwanablogu nitakayekuwa na watembeleajiwanaofikia zaidi ya 500 kwa siku. Hata kamera yangu haikuzidi thamani yalaki 4 za Kitanzania. Ilikuwa ni kwa matumizi ya nyumbani tu.
Pili, nawashukuru nyote mlionyesha moyo wa kunisaidia hata kwakuandika tu kuwa mnathamini mchango wangu katika jamii. Nawashukuru piamliochangia maoni yenye kunishutumu kwa hatua yangu ya kuomba msaada wachochote ili niweze kununua kamera iliyo bora zaidi. Na wala sina kinyongohata kwa wale wachache mlioamua kunitukana na kunikashifu.
Bahati nzuri hadi sasa hakuna aliyenitukana ”matusi ya nguoni” au kuwahusisha ndugu,jamaa na marafiki wanaonihusu. Naamini, kuwa hata nyinyi mlionitukana na kunikashifu mna mioyo yaupendo, isipokuwa katika maisha binadamu tuna frustrations zetu.
Wakati mwingine tunamhitaji ”kondoo wa dhambi”, kwa maana ya mtu wa kumaliziafrustrations zetu. Kama bado kuna wenye hamu ya kunitukana na kunikashifunawapa ruksa mje hata kwenye blogu yangu mmalizie ”hasira” zenu. Maana,duniani hakuna aliye timilifu, sote tuna madhaifu yetu.
Mwisho. Hiyo kamera inayoombewa msaada hapa si kamera ya kutisha,isipokuwa kwa sasa nilihitaji, kwa hiyari, watu wa kuniongezea nguvu ilinikamilishe azma yangu ya kupata kamera iliyo bora kuliko ile ya awaliambayo sasa imekufa kabisa.
Juzi hapa nilipita duka la Murtaza pale Mtaa waJamhuri nikazikuta kamera aina kama tatu hivi. Zote hizo nisemi-proffesional, thamani yake kwa moja haizidi milioni mbili, lakinihicho ni kiasi kikubwa sana kwangu kwa muda huu. Nina matumaini, kuwawanaonichangia sasa nikichanganya na fedha zangu zitatosha kabisa kununuakamera ya aina hiyo. Na kama kuna ziada itasaidia kuchangia kazi yakuboresha blogu yetu.
Nimeshukuru na kujaribu kutoa maelezo ya ufafanuzi. Tukumbuke,kutofautiana kimawazo na kimtazamo siku zote kupo.
maggid
Pole kaka MAJID hata mimi sikufurahishwa na maoni ya baadhi ya watu hasa ya kukutukana bila sababu ya msingi sdhani kama uliomba msaada kwa kuwa una hali mbaya kiasi hicho bali uliwataka wale ambao wanakutakia mema wangekuchangia.LAKINI HAWA WENZETU (BAADHI)WANATABIA YA KUPONDA KILA KITUKINACHOKUJA MBELE YAO HAWANA JEMA KWAO.
ReplyDeleteswala sio kuponda, bali ni kuchanganua mada. Huu mtindo wa omba omba unaendekeza uzembe.
ReplyDeleteUnaona bwana Michuzi ameweka bango la Tanzanite hapo juu.......Camera yake ikiibiwa sitegemei kuwa atatuomba tumchangie. Mie nafikiri enzi za ujamaa zimekwisha, inabidi tuwe wabunifu-kuomba omba sio ubunifu jamani.......
Usiumie Roho, Maggid, hiyo ni mitihani inakuja katika kila form, lakini kaza moyo, kuwa na positive attitude kama unavyojieleza katika ripoti yako hapo juu.
ReplyDeleteTuko pamoja na wewe kwa hili. Ujue kwamba wengi tunakusupport, ni rare talent uliyokuwa nayo, kwa kutupa habari zaidi ya watanzania katika miji mbali mbali Tanzania na maisha yao kwa jumla ambayo tunayaona na kuyasoma katika picha unazotuwekea kwenye blog yako. HIYO NDIYO PICHA HALISI YA WATANZANIA HALISI..
Piga konde moyo, TUNAPENDA BLOG YAKO!
By Mchangiaji
Kwanini unataka kununua kamera kipindi hiki ambacho umekiri mwenye "lakinihicho ni kiasi kikubwa sana kwangu kwa muda huu." Kwanini usingojee hadi uwe na hela halafu ununue hiyo kamera unayoipenda? Hii ni tabia mbaya ambayo unaonyesha. Sasa ukipenda gari aina fulani , tuseme VX kwa ajili inakupeleka sehemu muhimu ambazo ndio unapiga picha unazoweka kwenye blogi yako utakuja tena kwetu ooh unajua VX ni milioni 20 sasa sina ina naomba wadau mnichangie kwa sababu natumia hiyo kwendea kijijini kupiga picha. Usiwe kama sio msomi. Acha mambo ya omba omba unaweza kubuni njia mbadala ambayo unaweza changisha hela ukapata zaidi ya hizo unazotaka uchangiwe. Watanzania hatuna creativity yaani tunapenda vya dezo tu. Je ungefanya kutengeneza juice ya machungwa na kuandaa kama kiharambee flani hivi watu wanakuja nunua juisi kwa $500 au vyovyote, sio kuja kujidhalilisha hapa. Amkeni watanzania, acheni kuwa wavivu wa fikra, manshindwa kufikiria kitu kidogo kukuingizia hela. Nchi nyingine watoto wadogo ni wabuni jinsi ya kupata pesa, wanaosha magari (CAR WASH), kuuza lemonade (Juisi za malimao) au kukata nyasi. Lakini hawawezi kuja kusema tu unajua nichangie hela nataka kununua kamera. Mie hata mtoto wangu simpatii hela tu inabidi afanye kazi kwanza halfu anapata allowance yake. Tuamke ndio maana bado tuwanawaza kuwa tunahitaji wafadhili kama IMF au benki ya dunia kutusadia. Wananchi tuanze kuonyesha mfano wenyewe.
ReplyDeleteNdio hivyo kaka maggid duniani ni kuvumiliana kwani kuna wa2 wa aina tofauti wanatukana hata wa2 waliokufa.
ReplyDeleteBwana Majjid pole ndugu yangu huko ndiko kukomaa ki-blog nafikiri michu ameshakuleza yanayomkuta"waswahili walisema kwenye kundi na mamba na kenge wamo" sasa mi najua wema ni wengi zaidi ya wabaya japo wabaya nao wana nafasi zao ndio maana hata mungu aliumba peponi na motoni(jehanam) kwani alijua kuwa binadamu si viumbe wa uhakika hivyo wapo wachache watakaomsaliti na ndio maana akawapa kipaumbele kwa kuwatayarishia makazi yao ya jehanan.
ReplyDeleteHukuomba mtu ila ni maoni ya wadau wenye kuona na kuthamini mchango wako ndio waliotoa pendekezo ambalo nafikiri hata wewe halikuwa mawazoni mwako. Ulikuwa unapiga mahesabu ya kusubiri labla mazao yatakuwa mazuri uuze upate kujinunulia Camera ingine, lakini mpaka mvua inyeshe na mazao yawe mazuri blog si itakuwa imesahaulika?.
Nafikiri kama mtu unaona huna cha kutoa basi hata pole ndio uungwana si matusi.
OMBAOMBA WEMGI BONGO.KILA KONA BAKULI
ReplyDeleteNaungana na Bw.Skraga kwamba Majjid hakuorijinate hilo wazo bali wadau wenye kuthamini mchango wake... labda kuanzia sasa muongee na Mwl Mazara aliyemshauri na kuanzisha wazo hilo kwani mnaonekana hamkomi kumsakama mwana wa watu.
ReplyDeleteKwenye Blog ya Maggid anatueleta picha na habari mbali mbali bureee!Anatamua muda wake mwingi kuihangaikia blog hii ili kuwapa wale wanayeitembelea blog wake waelimike,waburdike,wapara habari mbali mbali,leo maggid akaharibikiwa na camera hiyo camera ana itumia kwa ajili yetu jamani hivi tulimchania itakuwa amejidhalilisha?Maggid hakuomba pesa kula yeye na familia yake,hili ni wazo liliotooka kwa wadau wengine maggid akalipokea,
ReplyDeleteJamani tuache kumdalilisha Ndg yetu maggid
Bwana Mdogo naona bado hujapevuka kwenye masuala ya kidiplomasia na kijamii kwa ujumla.
ReplyDeleteKimisingi we ulitakiwa ukae kimya tu na wala sio kuanza kujibizana na hao watoa maoni humu.
Unaona mfano mzuri wa Rais mmoja mstaafu ambae ameandamwa na kusakamwa na suala la yeye kuanzisha kampuni akiwa madarakani.
Umeona amejibu au amesemezana nini na hao wanaoandika juu yake mpaka leo hii?
Kwa taarifa yako katika nyanja hizi za uandishi (mimi nimesomea fasihi), watu wengine huwa wanaandika maoni ili kuchokoza wachangiaji wengine watoe maoni zaidi na kufanya discussion iwe laiv zaidi, na sio lazima sana wamaanishe kile wanachokisema.
Hiyo ni mbinu mojawapo ya uandishi.
Kimsingi wanafanya hivyo ili ku-provoke watu wachangie zaidi, yaani una solisiti fo moa koments kwa mbinu hiyo.
Bwana Mdogo hiyo ni mbinu mojawapo tu ya uandishi na wala isikupandishe presha bure!
Ungekaa kimya tu. Nadhani umenielewa.
Kazi njema.
Maggid, hebu weka akaunti yako hapo (jina, tawi, namba), mie ntakudondoshea alfu 20. Nina Tanzanite account CRDB, nazitransfer hapa hapa via internet
ReplyDeleteMI NAFIKIRI MAJID INAFAA APATIWE MCHANGO WA MAWAZO YA JINSI GANI ANAWEZA KUTENGENEZA FEDHA KUPITIA BLOG YAKE.
ReplyDeleteMFANO:
1. KUMWIGA BWANA MICHUZI NA KUTAFUTA MDHAMINI
2. KUWEKA GOOGLE ADWORDS (MK MSAIDIE KWA HILO)
3. KUENDESHA MASHINDANO YANAYODHAMINIWA NA MAKAMPUNI MBALI MBALI AMBAPO WASOMAJI WA BLOG TUNAWEZA KUPATA FEDHA AU ZAWADI KUPITIA BLOG YAKE (Yaani promo ya aina fulani)
MAJID AMKA MWANANGU HII NI DUNIA YA UJASIRIAMALI, KINA MATONYA HATUWATAKI
Nimetoka kuangalia kuna mtangazaji anaitwa Jennifer Sumi? Yaani hawezi kusoma magazeti kabisa anajikwa kwa tu. Haleweki. Jamani TZ hakuna watangazaji wanaoweza kusoma habari vizuri? Aibu tupu!
ReplyDelete