kuna ubaya gani usafiri wa bodaboda ukatambulishwa bongo na kuwa mbadala wa daladala kama ilivyo kwa wenzetu wa kampala pichani?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Haufai kabisa uharibifu wa mazingira kwanza moshi pili kelele kibao angalia na msongamano fadhali sema usafiri wa baiskeli kuliko hivyo vidude

    ReplyDelete
  2. Hii kaka yangu wala siisupport. Ingekua baiskeli kweli lakini hizi ni pollution tu. Zinabeba watu wawili tu na moshi unaotoka ni sawa wa magari tu hapa. Nooo..mimi ningependa baiskeli kama australia, indonesia au japani vile hapo ningekusupport

    ReplyDelete
  3. kaka michu vp? bodaboda hata bongo zipo kimtindo, nenda kanda ya ziwa, mwanza na mkoa wa mara zipo kibao...bunda, msoma mjini,tarime na kwingeneko...hata bagamoyo zipo na hata bajaj zilizojazana dar si kama bodaboda ila wananchi wanaziogopa cz ajali njenje

    ReplyDelete
  4. mhh UMENIKUMBUSHA MBALI DEAR!ZINA RAHA SANA NA NI USAFARI WA HARAKA,ILA KWA HAPA BONGO WANENE(WAKUU) WATASEMA NI UCHAFU KAMA HIACE,MH WATU WATAGONGWA!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  5. Kwa bongo jinsi watu wanavyopenda Ulaka(Pombe)hao masuka wa hivyo vitu watakua wako ulaka mbaya muno kiasi kwamba watawabwaga wateja everyday,A.City suka wa takee(Dreva taxi)anasaga gomba na chupa ndogo ya konyagi and then anakuuliza wee kuma unazama maeneo gani?Jamani?Customer service hapa iko wapi

    ReplyDelete
  6. Sir Michuzi unatania au?hivi sasa pata shika nguo chanika kwa vurugu la daladala na taxi unataka tena kizaizai cha pikipiki lakini wapelekee hiyo suggestion wazanzibari na wapemba ni usafiri wao wa jadi.

    ReplyDelete
  7. NOOOOOOO kwa bongo no kwanza usalama uwizi wa wabongo pochi utaweka wapi au simu halafu msongamano utakuwa mkubwa sana sorry kaka michuzi kwa mtazamo wangu mimi

    ReplyDelete
  8. Yaani madhara ya hivi vipiki piki unaweza kuyaangalia kwenye miji mikubwa kama Lagos au Abuja. Hivyo vikija hapa kwetu ni ghasia tupu. Msongamano, uwizi/ujambazi, ajali, kelele na polution ni baadhi ya vitu vichache. Kwa kweli siuafiki kabisa.

    Mzee wa TBS

    ReplyDelete
  9. kaka michu mi nauliza hivi: kama hizi bodaboda zikiruhusiwa hapa bongo wakati barabara tayari hazipitiki zitapiata wapi mwanawane? Huu mradi labda ukaanzishwe mikoa mingine kama kagera ambapo kuna dhiki kubwa ya usafiri ila sidhani kama wananchi(vigogo) watakubali walalahoi(makabwela)wazitumie kwa kuwa wanaona zinawakela kwa sababu wao wanatumia shangingis.
    Ndimi tpaul(agent)

    ReplyDelete
  10. Hii sio nzuri hebu nenda kaangalie lagos ilivyoharibiwa na hivi vipikipiki hivi sasa nchi yetu nimsongamano mtu barabarani je ukiviongeza na hivi siitakuwa tabu tupu. tmk to kariakoo itakuwa sawa na dar to moro.

    ReplyDelete
  11. kaka issa mimi hilo siliafiki kwa mtazamo wa ajali...udereva wa public transport wameachiwa wa msuba na wa kustua na viglasi, most of them lack manners, ethics, proffesionalism...safety consiousness,ona madaladala yalivyojaa 'ngao' na mi bull bar...maybe if only a pikipiki would be fitted bullbars_ jetdriver

    ReplyDelete
  12. kwenye jiji letu la SONGEA wenye dala5 wanalia sababu ya hizo bodaboda!ila sio siri mi sipendi kuigaiga!
    kwani bajaj haziko tena?

    ReplyDelete
  13. Hawatafata sheria.Tazama hata huko Uganda hawajafaa helmets

    ReplyDelete
  14. nasupport usemi wa papaa..Muhimbili na MOI patakuwa hapatoshi kwa watu watakao vunjika migongo kwa ajali..kibaya zaidi pikipiki 30 ndiyo sawa na kipanya kimoja...mmmh mengine yatupite jamani..

    ReplyDelete
  15. MIE HUKO SONGEA UMENIKUMBUSHA SONGEA.MWAKA JANA NILIKUWA HUKO MAENEO SEED FARM NILIKUWA NAONA JINSI WAENDESHA BODABODA WANAVYO VUNJA SHERIA.WANAENDESHA PIKIPIKI ZINGINE HAZINA PLATE NUMBER,HAWAVAI KOFIA,WAKISABABISHA AJALI NA KUKIMBIA.NA HATA WAKIVAA ELEMENT ABIRIA NAKUWA AJAVA HIVYO NI HATARI.BODA BODA KWA SASA NOOOOOOOOOOOO.ILA BAISKERI NAZIKUBALI MAANA ZINATUNZA MAZINGIRA NA NI SALAMA ZAIDI YA PIKIPIKI.WASALIMIE BOMBA MBILI

    ReplyDelete
  16. AHHAA KAKA MICHUZI UNANIUWA MBAVU KWELI KWELI YAANI KWA KUJIFAGILIA UKWENU TU UNANIFURAHISHA ANYWAY TUNAWAHESHIMU WAKWE ZETU LAKINI USAFIRI HUU KWETU HAPANA

    ReplyDelete
  17. Lazima kaka michuzi afagilie ukweli kwa vile it is a dream come true. Wabongo wengi wanaoa au kuolewa na wakenya sasa yeye ameupgrade..hivyo lazima aongee kila siku habari za uganda kwa vile za wakenya tumeshazichoka.

    Kila siku mume wangu kaja nyumbani kalewa..kesho mume wangu kanipiga...mara waliooa wakenya kila siku wanalalamika mke wangu anakunywa pombe sana ...anamiss nyumbani kwao...kesho ah ... nimesikia anatembea na yule jirani yangu ..sasa hatujui ya waganda keep update us na tueleze vizuri wengine hatujaoa kaka yangu. Macho yetu yapo Uganda kwa sana..wabongo wanatukataa

    ReplyDelete
  18. Sisi wa BKB hatuna shida bali tunatumia kama kawa, si unajua tena tu karibu na huko. Kwa kweli ni usafiri mzuri ila kama umebeba kitu cha thamani kuwa makini sana maana ni rahisi kukwapuliwa. Uzuri wake ni kwamba unafika hadi mlangoni hata kama kwako ni madongo kwinama litafika tu.

    ReplyDelete
  19. Ni mbaya kwa sababu ni usafiri wa kichoyo, unabeba abiria mmoja tu kwa wakati na pia unamfanya abiria na dereva wake kuwa ndio bodi la chombo hicho, kwa hivyo ajali ikitokea ni hatari kwa kweli.

    Pia ulimwengu uko katika mapambano ya kulinda mazingira, hivyo moshi wa vyombo hivi, hasa vikiwa vingi ni mbaya sana.

    Mwisho makelele, itakuwa kero sana.

    Nadhani tunahitaji mabasi makubwa ili hata vipanya vitimuliwe.

    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  20. no no hii ni hatari sana manake mimi i would rather walk from mbezi to kimara kuliko kupanda hivi vindubwada anyws sasa serikali yetu ijitahidi inunue double deckers kama wenzetu wa ughaibuni na wapunguze kukunua pradoz na shangingis au mnaonaje?

    ReplyDelete
  21. BIG SUPPORT to Anonymous of 28th aug 5:36 EAT..

    It is right time for government to implement reliable means of transportation like ones in big sities like London,Uk..we had a starting point , the way UDA was operating is the same as metro caoch in UK...To date they Still have 'ikaruss kumbakumba' and really help in high density areas like Edmonton and Lewisham..taking as example double deckers are needed to operate in dense populated areas like mbagala, manzese, kimara etc.
    In futute the goverment should think in investing in Underground or tubes networks..everything can be done so far we have unlimited land resorce , funds and others can be attained by impossing strategic plans.
    Bro Issa if possible forward my comment to the Ministers who deals with matters.Thanks

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...