Swali - tafsiri kwa kiswahili:
"I am going to the internet cafe to check my emails and later on i have to make a questionnaire..."
Jumatatu njema,
lynn
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
nakwenda kwenye mgahawa wa wavuti kuangalia barua pepe zangu na baadaye nitengeneze dodoso
ReplyDeleteNaenda kwenye kibanda cha mtandao kuangalia barua pepe halafu baadae nitatengeneza dodoso.......good day wandugu
ReplyDeleteNaenda katika mtandao wa tovuli kuangalia barua pepe zangu na baadae nitatengeneza dodoso. jumatatu njema. lynn
ReplyDeletenaenda kwenye mgahawa wa mtandao kukagua barua pepe zangu na baadaye kuandaa dodoso.
ReplyDeletenimetoka kwetu mahengeeee nimekuja darisalama, KUCHEZA NGOMA.
ReplyDeletequestionnaire = Maswali AIRE
ReplyDeleteNinakwenda kwenye mgahawa wa midahalishi nikasome barua pepe zangu kisha baadaye niandike dodoso.
ReplyDeleteKama hakuna kubaniana basi mimi ndio nimewin.........hureeeeeeeeeeeeeeee
Ninaelekea kwenye mgahawa wa tovuti kusoma barua pepe zangu, na baadae inanibidi kutayarisha dodoso.
ReplyDeletebarua pepe,tovuti,mtandao,dodoso.........kiswahili kweli kinakua kwa kasi.nawapongeza wadau wote hapo juu kwa umahiri wenu wa kujua na kuenzi lugha yetu tukufu ambayo naamini iko siku itakuwa national language ya kontinenti la afrika.
ReplyDeleteNinaenda kwenye mgahawa wa mtandao kuangalia barua pepe zangu na baadaye nitaandaa dodoso.
ReplyDelete"NAKWENDA KWENYE MGAHAWA WA MDAHILISHI KUANGALIA BARUA PEPE ZANGU NA BAADAE INANIPASA NITENGEZE DODOSO..."
ReplyDeleteHAPPY MONDAY,
Lynn (sorry couldnt work out figure out a taranslation for this!!!)
Nakwenda chumba cha tovuti na baadae natakiwa kutengeneza Hojaji
ReplyDeleteWADAU SHUKRANI NYINGI SANA KWA KUNIFUMBUA TAFSIRI HII. NILIKWAMA KUMWELEZEA RAFIKI YANGU YA KIDHUNGU ALIYETAKA NIMWELEZE KWA LUGHA YA KWETU (KISWAHILI) LAKINI KILA NILIPOTAKA KUJARIBU KUTAFSIRI NIKASHINDWA NIANZE VIPI.
ReplyDeleteMANENO KAMA INTERNET NILIKUWA SIJUI MAANA YAKE KWA KISWAHILI; QUESTIONNAIRE NALO LILIKUWA LINANITATIZA. NENO CAFE NALIJUA NI MGAHAWA AMBAPO KWETU TUNATUMIA KAMA RESTAURANT. DUH AMA KWELI KISWAHILI KINATANUKA. LAKINI YOTE HAYO SINA BUDU KUWASHUKURU KWA JITIHADAZENU.
AHSANTENI; WENU LYNN
im not even going to tempt to try this maana tafsiri yangu itakuwa worse,good work ,nice answers ,na enjoy kusoma majibu yenu
ReplyDeletelynn
nakwenda kwenye ukumbi (maana cafe ya mgahawa differs from cafe ya internet) wa mtandao kuangalia barua pepe zangu kisha baadae...niandae nonino...lynn what is this, an exam?...
ReplyDeleteWaswahili hili ni fumbo.. nalo linatafsiriwa kama ifuatavyo..
ReplyDeleteNaenda kijijini kuchumbia, lakini kuna mengi ya kufanya/kujiuliza kabla ya siku ya ndoa.
lol..
By Mchangiaji.
Naenda katika mgahawa wa ingia nyavu kuangalia ebarua zangu na baadae nitatengeneza swalihewa.
ReplyDeleteKwako Sadikika
ReplyDeleteYaani jibu lako limeniacha hoi, hakika kama kuna zawadi yakupasa kuipata. Very funny indeed
MTANZANIA(MAJORITY)- KISWAHILI ANAKIJUA SANA CHA KUZUNGUMZA, CHA KUANDIKA MATATIZO
ReplyDeleteKIINGEREZA ANAKIJUA SANA CHA KUANDIKA, CHA KUZUNGUMZA MATATIZO
jamani flash disk kwa kiswahili inaitwaje?
ReplyDeleteflash disk?kwa kiswahili?mhh hebu tuone. kwanza flash ni nuru(kama flash ya kamera),disc ni kama kisahani,kwa hiyo flash disc ni 'nuru sahani' au vipi wadau?
ReplyDeleteWADAU MBONA HATUELEWANI. BASHUKURU SANA KWA MSAADA WENU. HII HOJA SASA NAIFUNGA NATAFUTA MANENO MENGINE. NIKIKWAMA NITARUDI TENA HAPA KWA MICHUZI ANISAIDIE KAMA ALIVYOFANYA HIVI. MIMI MWENZENU SHULE IMEINGIA UMANDE; AHSANTENI WENU LYNN.
ReplyDeletekuna mtu anayetumia jina langu kuacha comments plz naomba tuheshimiane....we anonymous 9.18pm 28th and 27th aug 9.58pm.
ReplyDeletelynn