makamu wa rais dk. mohamed ali shein akipozi na uongozi wa benki ya crdb jioni ya leo baada ya kufungua rasmi tawi jipya la benki hiyo mtaa wa lumumba. hili ni tawi la 38 la benki hiyo ambayo ina tawi katika kila mkoa na imeweka historia kuwa benki inayomilikiwa kwa asilimia 100 na wazalendo ambapo hadi kufikia juni mwaka huu imeweza kuongoza kwa kuwa na dipoziti za shilingi trilioni 1.1 wakati mikopo ilotolewa kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo imefikia shilingi bilioni 620 ambayo asilimia 24 yake ilotolewa mwaka jana imeenda kwenye sekta ya kilimo, na pia asasi mbalimbali zipatazo 272 zimekopeshwa shilingi bilioni 65

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Nimepata ile tembo Visa card yenye VISA electron, na PIN code yake, hebu wadau nielekezeni jinsi ya kuitumia. Nikiingiza kwa ATM huku mbona naambiwa ati card temporarily rejected. Please naomba maelezo nataka nichukue hela

    ReplyDelete
  2. Wewe inaelekea hiyo card umeiba kwa mtu...sasa unataka wasanii wakusaidie.....kama wewe siyo mhalifu si umcontact provider???

    ReplyDelete
  3. Ndiyo ni ukweli ulio wazi kwamba CRDB mambo ni supa....ila kuna dosari sijui ni kwenye hii picha au kwenye management kwa ujumla.....GENDER IMBALANCE.....TUMECHOKA NA HUU MFUMI DUME!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  4. Anonymous August 17,2007 8:56:00 AM EAT,

    GIVE ME FIVE! That is true the top management of many banks not only CRDB are Men, but the reality is for them to be "Boss" women must be involved iwe home au ofisini jamani tunaposema mfumo Dume msituelewe vibaya, TUNAWEZA TUKIPEWA NAFASI...

    PICHA HIYO INASEMA YOTE!
    DA TULLY NA HUYO MWINGINE SIJUI NANI NDO AKINA DADA HAPO.

    ReplyDelete
  5. matatizo makubwa mimi niliona kuhusu hizi bank za nyumbani ni charges zao kwani ni kubwa sana kila ukienda kwenye acc yako wamechukua hela wao inatia hasira sana

    ReplyDelete
  6. Mr. Clean yupo katikati hana makuu mzee huyu wala mbwembwe za kibabaishaji. Tulia mtu mzima.

    ReplyDelete
  7. Michu,

    Pliz usidanganye umma kwamba CRDB ina matawi mikoa yote, hiyo sio kweli kabisa. CRDB haina hata tawi moja katika mikoa mitano ya Zanzibar.
    Nilipata tabu sana nilivohamishiwa huku znz kikazi kwani ilinibidi nihamie Barclays coz nilikua nna account ya CRDB na huku ndio hawana tawi.

    ReplyDelete
  8. Asante Anoni wa Tarehe August 17, 2007 8:51:00 AM EAT, kwa kuniita mwizi baada ya kuuliza jinsi ya kutumia kadi. Kama hujapata kadi ya aina hii toka kwa CRDB wenyewe ni bora kukaa kimya. Wanasema unaweza chukua hela toka ATM yoyote hapa duniani yenye nembo VISA ELECTRON. Nimeenda, nimeweka PIN imekubali lakini hela hazitoki. Niliuliza kwa wadau kama wa experience, especially wa hapa europe. Sasa we anoni, nimeiba kadi na PIN code yake. Please, be polite to ther people especially those who are seeking knowledge. Kama kuna mdau amepata shida hiyo hiyo kama mie naombe anisaidie kujua alivyoisolve. Meanwhile namuandikia mail Jenipher Tondi, afisa mahusiano wa CRDB anipe maelezo. Hizi kadi hazina chip, ila zinaingia kwa ATM bila shida.

    ReplyDelete
  9. Ndugu yangu wasiliana na CRDB watakuwasaidia haraka. Hata mke wangu alipata tatizo kama hilo lakini walilirebisha haraka sana. Ozzie

    ReplyDelete
  10. Huyo mtoto mwingine wa kike aliyeshika hand luggage anaitwa Esta Kileo (From BOT).....mambo shosti.........!!!!!!

    ReplyDelete
  11. Ester hongera sana. Nimefurahi sana kukuona kwenye top management ya CRDB

    ReplyDelete
  12. Asante sana Tarehe August 17, 2007 11:49:00 AM EAT, comment yako imenipa moyo.

    ReplyDelete
  13. ee bana Michuzi ungetutajia Safu ya Hawa Wakurugenzi, Namuona Sioyi hapo. Hongera kijana, such a young Mkurugenzi

    ReplyDelete
  14. CRDB ndiyo benki iliyoniokoa takriban miaka 15 iliyopita baada ya sisi wateja wadogo-wadogo kutimuliwa pale NBC City Drive kwamba hatuna hadhi ya kuweka vijisenti vyetu pale.
    CRDB walinipokea kwa mikono miwili na kunisaidia hadi nikawa mteja mkubwa.
    Nikiwa kama mteja wa kawaida kabisa, nimesahakopa kwa ajili ya biashara na nimekuza mtaji wangu kupitia mkopo wa CRDB.
    Japo kuwa kwa sasa nipo Ughaibuni, lakini naweza kuwa kumbuka baahi ya watu katika picha hii.
    Katika picha namtambua kutoka kushoto kwenda kulia msitari wa nyuma:wa kwanza simjui;wa pili namfananisha na Anderson Mlabwa (huyu Mkurugenzi-anashughlikia mikopo, kama sijakosea);watatu Tully Mwambapa (Mkurugenzi??);wanne huyo mrefu mweupe simjui; wa tano John Baptist Rugambo (Mkurugenzi nadhani marketing???/ brilliant person nimewahi kukutana naye katika masuala ya kibiashara hapo CRDB);wa sita simjui;wa saba Joseph Witts (nadhani ni mkurugenzi retail banking kama sijakosea/ niliwahi kukutana nae pia na kufanya nae mazungumzo pale HQ ni msaidizi sana).
    Mstari wa mbele: wa kwanza simjui; wa pili Charles Kimei CRDB CEO, very hard working man na mpenda wateja; wa tatu simjui;wa nne Mh. Dk. Ali Mohammed Shein (Makamu wa Rais wa JMT);wa tano Mh Abbas Kandoro (Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam); wa sita Sekou-Toure Khalifa (Nadhani kwa wengi tuliowahi kukutana nae kwa mara ya kwanza, tunaamini kweli hili ni sikio la CRDB, the man that listens, huwezi kutoka kwa huyu ndugu umekasirika au hujaridhika, seems to be very inteligent); wa saba simjui.

    ReplyDelete
  15. Michu CRDB ndio wadahmini wa blog yetu/yako wawe wanatoa dondoo au tips of the day on how to xxxx. mimi niko kwa mzee bush ninapata tatizo kama wenzangu la tempory xxx na hadithi nyingine nyingi. nikienda madukani kwenye pos haina shida nikitaka kucheck balance ndio mbinde. basi watueleze watu wote wenye visa cards ya either tembo au hii mpya unafanyaje kucheck balance . vilevile kama unataka kucheck kwenye simu yako nilijaribi huku ninatumia t mobil sijajibiwa mpaka leo. wawe wanajibu basi hata kwa international queries through mobile phones si ndio benki yetu jamani? maana mimi wapangaji huniwekea rent kwenye account yangu bongo inanisukuma huku kwenye bill zisizo na simile

    ReplyDelete
  16. hata mimi niliangalia hii picha nikashangaa...kaa vile wanawake wao hawanaelimu vile. Yaani uongozi kwao ni mwanaume ahhhh jamani....hivi kweli tutafika....???

    ReplyDelete
  17. Tutafika tu usiwe na wasi, kuna ishu more importants than gender balance issues kama vile nchi kuuzwa na akina Karamagi na kuliwa na akina Balali, so usiwe na wasi tutafika tu anon 9:02.

    ReplyDelete
  18. Wanawake wakiwa wengi rushwa zitapungua give us a chance and see.... Mmeona maendeleo ya waliberia?
    tatizo letu wabongo au waafrica tunaogopa sana kuongozwa na mwnamke au tunafikiri watagundua madhambi yenu na kufanya the right things.
    Hiyo body ya o nadhani ukiomba kazi lazima uweke picha....lol kama weew ni mwanamke itaangaliwa mwishoni.........

    ReplyDelete
  19. Sio ukweli kuwa CRDB inamilikiwa na wazalendo 100%. Ukisoma kwenye mtandao wao www.crdbbank.com utaona kuwa:

    "CRDB BANK LIMITED is owned by over 11,000 shareholders under the following major groups (by value of shares):

    Private individuals 37%
    Co operatives 14%
    Companies %10.2
    DANIDA investment fund 30%
    Parastatals ( NIC & PPF )8.8% "

    Kuna fununu kuwa DANIDA wanataka kurudisha hiyo 30% yao kwa serikali na serikali itaziuza kwa wananchi.

    SAC

    ReplyDelete
  20. Jamani kwenye Management kinachoangaliwa ni Qualifications na sio gender, nyie wanawake mnalalamika kuwa hakuna gender equality. Sasa kama wanye qualifications zinazotakiwa hawapo wachukue vilaza eti wanafanya gender equality? Cha muhimu nyie piga shule za maana muone kama mtanyimwa hizo nafasi. Nadhani manakumbuka ile issue wachaga na TRA watu walipiga kilele sana kuwa TRA wamejaa wachaga lakini ukweli ndo walikuwa wamesoma mambo ya TAX.
    Kwa hiyo vitu vingine tuwe tunakubali ukweli.

    Nawakilisha.

    ReplyDelete
  21. oh pleae niambie ni viongozi walio simama hapo wangapi wana PHds? Kama ni masters wako wanawake wengi tu wanazo na wanabakia chini kuteller tu

    ReplyDelete
  22. Wee anony wa August 20, 2007 3:39:00 AM EAT hapa kinachotakiwa ni masters au PhD ya kitu fulani sio kwamba ukiwa na masters au PhD yoyote wanakuchagua kwenye management.

    ReplyDelete
  23. Bongo tukubali tu gender issue bado kubwa. Honesty simjui mwenye PhD lakini nawafahamu wanaofanya hapo na wenye masters. Na sio za marine biologist au medicine. Zote ni za finance, management, public relation, administration. lakini wako kwenye floor tu.na kama ni experience wanazo za miaka mingi tu lakini opportunity of growth for them is a dream in those big cooperation.

    ReplyDelete
  24. Kweli lazima tukubali kwa bongo , bado gender ni issue, na pia sisi ladies tujitume zaidi, kwa kazi, kusoma na kuwa na confidence etc. I know the lady from the 1st row Esther ,she is more .... so as the other one Tully. Big Up for them.Pamoja nakujituma pia bado tunatakiwa tupewe chance kwani hatupewi na tunanyimwa kutokana na mfumo dume.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...