mdau ana hasira na kina iddi janguo na ma-limo yao; kenda kubeba kitu hichi huko dumilla. kitashuka karibuni....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. Awe na kisima cha mafuta pia< hayo wanayaweza wamanga tu!

    ReplyDelete
  2. na ndala?

    ReplyDelete
  3. wapi na wapi hama na kandambili?

    ReplyDelete
  4. Sawa, halafu ataendeshea wapi? Labda afanye kuwa bus la kwenda mikoani!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  5. Yeah, Kamua dada kamua...sio kila siku tuone nyundo za makaratasi...hata hizi ni nyundo ...kamua.....

    Hizi ni changamoto...ukisoma ukimaliza shule ukipata kazi unafanya mavitu ya nguvu...

    Yeah watanzania mia tukiwa na hasira hizi tutafika mbali...

    Tunataka matendo maneno yametuchosa....

    ReplyDelete
  6. hilo hammer huyo dada kapewa na buzi la kizungu anitonye na mimi nikapate moja nitese nalo kule mbezi kwenye bara bara yetu nzuri ya lami!lol

    ReplyDelete
  7. ukitaka kujua wabongo wengi fikira duni, soma hizo comments eti "kandambili na hummer wapi na wapi".

    that's nonsense kwa kweli, kuna uhusiano gani?mtu kanunua gari, full stop.

    hao wenye hizo comments, usishangae hata blog ya michuzi wanaoiona kwa jirani.

    no wonder nchi inakuwa rahisi kuiongoza kisanii bila matatizo.mapimbi wengi sana.

    ReplyDelete
  8. Anoni aug 17 12:42 hapo juu sawa kabisa.... nashukuru kwamba umeona how shallow some people are..... i am flipping sick... inasikitisha lakini ndo mambo yalivyo!!!

    ReplyDelete
  9. Hongera! Lakini, tunapoingiza mavituz tukumbuke hakuna barabara, ni nani wa kulaumiwa???!! Ni kama jinsi ambavyo majumba makubwa ya biashara yanafunguliwa kariakoo na katikati ya miji mingi Tanzania wakati hakuna parking wala sehemu za mapumziko (bustani); kwani wafanya biashara hizo hawawezi kuwekewa sheria kujenga sehemu hizo? (Naomba ujumbe huu ufike kwa viongozi wahusika, President included).

    ReplyDelete
  10. Kachuna buzi la australia nini...manake wengine twawaona wanachuna mabuzi ya Uk na USa lakini shida kama zangu ..te te tthhhhhheeee

    Dada hongera lakini tuelezani siri ya hilo gari....

    ReplyDelete
  11. Mimi namuunga mkono huyo dada kwa asilimia mia. Unajua wabongo bado wako nyuma wao wanaona kandambili ni uchafu hebu wajaribu kwenda kidogo nchi za wenzetu huko watu wanavaa viatu vya wazi ambavyo ni salama kwa afya pia. Viatu vinatumika ofisini tu, tena sio lazima waende huko waangalie wazungu wanapokuja holiday hapa bongo wote wanavaa viatu vya wazi kwani unafikiri hawana pesa au sio matajiri?. Acheni ujinga na kuchunguza vitu vidogo ambavyo wala haviwezi kuwasaidia.

    ReplyDelete
  12. Picha tu hiyo jamani mbona macho yawatoka hivyo???? umekosea binti ungeomba funguo upose ktk steering ingesound much better

    ReplyDelete
  13. Cmjui huyo dada na wala sihitaji kumjua, kwa sababu na yeye hatataka kunijua. Ila amenifurahisha sana. Ninavyohisi si kwamba 'amenunua' (kama kweli) ili aje atese nalo kwenye barabara za Buza, Tandika, Gongo la mboto na Mbagala Rangi 3. Litakuwa likipita barabara za Dar es Salaam kaskazini na kati kidogo, na pia ujue huko ndio mambo makubwa hufanyika. Si tunaona ile benzi (cjui iko moja au la!!!) inavyoazimishwa na maharusi. Nenda kajaribishe kugusa usikie pesa zake. Sasa akiileta jijini, najua wale wenye pesa, watoto wa wakubwa litawakamua sana wanapotaka kujimuvuzisha kwa harusi za kuua na shoka. Leta dada na wewe ule pesa za wa Tanzania ambazo zinazoenda kwenye mifuko ya wachache. Litakurudishia pesa zako haraka sana.

    ReplyDelete
  14. jamani ku pose kwenye gari anyone can do that, kwa hiyo labda alisindikiza buzi akaamua amuingize town Michu.....

    ReplyDelete
  15. We binti unapenda makubwa uwezo huna shauri yako watakukandamiza hapa town km mpira wa kona... usione vyaelea mama we tafuta makuu tu utayapata

    ReplyDelete
  16. kama lake kweli hebu mwambie afungue mlango basi akae humo ndani apige picha

    ReplyDelete
  17. lololo ,Jamani wabongo tunatishaaaa.ninachoshangaa kwa nini picha ikitolewa hapa ya mmbongo na labda na gari la nguvu au jambo ambalo labda ndio investment yake, lazima apingwe eti anapozi tu.Huu ni wivu wa waziwazi ,dada wa watu kaona hilo gari litamuingiza pesa home,watu hatutakiii.Wat oh kavaa kandamili ,hivi hamjui nyie flat sandals kama hizo.Hao akina iddi Janguo na malimo yao mnawaponda kila siku .Mna nini waja wenye Roho ya kwa nini?Nakumbuka kuna kaka flani michu alipost hapa snap yake na bima siuji gari gani huku s Africa ,mkamponda kwamba eti alivyo hawezi kuown gari kama hilo.aibuuu.shoshti sikufahamu weye lakini nakufagiliaaaa waaa waa waaaa.Usiangalie makunyanzi.Michuzi sipendi tabia yako ya kubana comment flani flani ,afu nyingine za matusi unazipublish!!!! tunakushangaaaaa

    ReplyDelete
  18. jamani kandmbili mambo ya summer ulaya hayoo!!

    ReplyDelete
  19. SIKU ZOTE NITAWAPONGEZA WABUNIFU KWANI WAO NDIYO CHACHU YA MAENDELEO.
    KAMA MDAU AMEAMUA KULETA HAMMER, POA SANA, MTU MWINGINE ABUNI KITU KINGINE, KAMA UTASHINDWA NA KITU KIPYA BASI JAPO KIFANANE NA KILICHOPO.
    LETE HAMMER HILO UZUNGUSHE PESA YAKO.

    ReplyDelete
  20. Wabongo hawana dogo ...kandambili ziko in kwa summer hii kama hujui...

    Wabongo ipe roho inayotaka.. Amepiga picha hapo either ananunua, au atanunua in future ni yeye....bora anadream kuliko kutodream ...asiyedream hapati kitu kwavile hajui anachotaka..

    ReplyDelete
  21. Sister hongera lakini labda wewe sio mbongo watu milioni humu wanaingia kila siku hamna hata mmoja anayekutambua jamani dunia kubwa ulijifisha wapi? Au uli homeskulling?

    ReplyDelete
  22. Mtu yoyote anayekandia kandambili wakati hali ya hewa hapo iko wazi, jua mpaka mtu anafinya macho, mkandiaji yoyote, the chances are, exposure ndogo, tembea uone dunia.

    ReplyDelete
  23. huyu dada kapiga tu picha nadhani michuzi ndiye mwenye makosa kusema eti ana hasira na kina janguo! huyu dada hanunui wala nini kapiga picha tu. hili ndinga maji marefu unafikiri ni corolla hiyo? hakuna hata haja ya kupoteza muda kujadiri hii picha...wote mwisho tutakuwa na akiri kama ya huyu binti!

    ReplyDelete
  24. ukitaka kuponda andika kiswahili fasaha au kiingereza fasaha,akiri ndo nini ,wivuuu tu !Kinachokufanya ufikiri huyu dada hawezi kumiliki hili gari ni nini!Fyuuuuuuu(msonyo).mnakera.

    ReplyDelete
  25. mwenyewe kapozi kulia na kushoto kwa driver ana noma dada wa watu hammer ikapita akaomba kupiga picha poa tu

    ReplyDelete
  26. hama hama,hama hama,subirini na mimi niagize ungo wangu toka kibondo halafu tuone nani mjanja.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...