wapenzi wa hummer kazi kwenu... hii mdau kaleta akiuliza kama itafaa bongo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Jamani hizi picha za hammer zina kera sasa nyie mnao mtumia kaka michuzi mnauzi sasa

    ReplyDelete
  2. kama Hammer ipo hata dizaini hiyo ya kuburuza tumbo chini, basi nawa omba wapinganaji wetu wa kiwanda cha kuzalisha magari aina ya Nyumbu ya JWTZ waanzishe kitengo cha magari ya kibiashara, kwani dizaini zake nina uhakika ni kiboko, angalieni gari apandalo amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Mh. Raisi wa Tanzania akikagua gwaride kwa Nyumbu, je wadau mnasemaje?
    Mdau
    Londoni.

    ReplyDelete
  3. Ndugu yangu sio kila kitu kinachotokea hapa kitakuwa kinakufurahisha, hiyo itakuwa ngumu sana ndugu yangu.

    ReplyDelete
  4. jamani acheni ushamba..hilo gari linatumia air bag , limeshuka ili abiria wapande, wakati wa kuondoka linapanda juu kama prado..wabongo ng'azeni macho mambo ya teknolojia hayooo.

    ReplyDelete
  5. Kwa kweli ni ngoma mdundo, lakini swali ni je Bongo yetu litapita barabara gani. Maana si unajua tena hata pale barabara inapopitika basi utakuta tuta hilo! Hapa bwana we njoo na jeep tu, utapeta lakini ngoma hiyo ni kujisumbua tu.

    ReplyDelete
  6. Washikaji eeh,hiyo Hammer inafaa sana Tanzania hasa jijini Dar maeneo ya Mbagara rangi tatu.Na kama litafanya kazi kama daladala itakuwa bomba zaidi.
    Majita

    ReplyDelete
  7. Kwani hakuna mambo mengine ya kutamani yawe bongo ?kama barabara nzuri,huduma nzuri na maisha bora ?kuliko kila siku kuweka picha za magari na kujifanya tuko level ambayo hatujafikia? Infrastructure jamani ndio muhimu mengine yatafuata baadae.

    ReplyDelete
  8. gari zuri tatizo lina rangi za simba.

    ReplyDelete
  9. hilo linafaa kuwa kipanya,hasa kigoma kwetu pale,ujiji hadi stesheni,juu limepakia vitebo vya dagaa na mugebuka.

    ReplyDelete
  10. ANAYOTUMIA JM KIKWETE NI HAMMER KAMA ZA KULE GHUBA KWENYE VITA NA SI NYUMBU !

    Mzushi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...