
katibu mkuu wa simba mwina kaduguda 'simba wa yuda' leo amepuuza adhabu ya kufungiwa miezi sita na kamati ya michezo ya tff kwa kosa la kushindwa kutoa ushahidi juu ya madai yake dhidi ya shirikisho hilo wakati wa kombe la tusker na kuibeza samansi ya kwenda kujieleza. amesema ni kamati ya nidhamu pekee yenye mamlaka ya kumwita na kutoa adhabu, na si vinginevyo. amekazia kwamba yeye anaendelea na kazi zake za ukatibu simba kama kawa na katika kuthibitisha hilo leo alisimamia mkutano wa wanachama ambao kwa kauli moja wamepitisha rasimu ya katiba mpya ya simba.
kwa upande wao tff wameshikilia msimamo wa kumsimamisha kaduguda kwa miezi sita na kusema kupitia kwa katibu mkuu wa shirikisho frederick mwakalebela kwamba hawatatambua kazi yoyote itayofanywa na simba wa yuda hadi kipindi cha adhabu kiishe na pia kimesema kama anataka anaweza kukata rufaa kwenye kamati ya nidhamu.
ugomvi wa mwina kaduguda na tff ulianzaia pale alipotaka mkataba wa michuano ya kombe la tusker uwekwe mezani ili kila mhusika auone na kuuelewa jambo ambalo anadai tff hawajafanya
...nitafanya kila niwezalo, lazima nirudi TFF...millioni 40 hizi nitusker peke yake...no, haiwezekani!!!
ReplyDeleteHawa ndio viongozi wetu watakoarudisha hadhi ya mpira kweli au wanataka kuturudisha enzi za akina 'wajina wake' Michuzi.
I really admire this person ana misimamo ambayo napenda viongozi wpte wangekuwa nayo ndiyo maana haswa anastahili kuitwa simba wa Yuda.Kaduguda you are correct kwani chombo chenye mamlaka katika masuala yote ya soka ni kamati ya nidhamu na si vinginevyo.TFF wakubali kuwa wamakosea kanuni katika kukusimamisha na wameze maamuzi yao kwan its too late kurekebisha sasa hivi.
ReplyDeleteTFF inayoendeshwa kimajungu majungu badala ya kufuta taratibu haitatufikisha popote zaidi ya kufanya tuzidi kuonekana wabahatishaji.
Michuzi tatizo lako unabana sana comments kwani hata nikijitahidi kuandika very decent comments huzitoi sijui mpaka nijitambulishe niko ughaibuni ndo uzitoe!Jaribu kuwa fair kwenye kutoa comments za watu wenye mitazamo tofauti.
ReplyDeleteKadu kachemsha, kuna tofauti ya Legality na Legitimate, alichotakiwa kufanya ni kwenda na kuzungumza na kamati iliyomwita na kuthibitisha kauli yake. Tatizo la Kadu ni msomi wa uswahilini. Hajaweza kubadili lugha anayotumia kuwasiliana na watu. Akumbuke kwamba yeye ni Kiongozi wa Klabu kubwa asiwe anazungumza kama mtu wa kijiweni!
ReplyDeleteAnnoy wa hapo juu nakubaliana na wewe, Huyu Kaduguda ni msomi wa uswahilini. BTW hivi huyu bwana pale Udsm alisoma fine arts nini ?? Maana anavyolopoka ufafikili kaishia form two
ReplyDeleteAsante sana mtoa maoni wa August 27,2007 10:24:00 AM EAT. Kaduguda ni picha halisi ya wengi wa viongozi wetu wa vilabu (hasa Simba na Yanga)na michezo kwa ujumla! Namna hii sijui kama tutafika huko ambako tumelenga katika michezo! Hovyoooo kabisa Kaduguda!
ReplyDeleteHIVI KADUGUDA NI MZIMA KWELI!!! MSIMAMO WAKE UMENIPA MASWALI MENGI AMBAYO HAYANA MAJIBU.MWANZONI NILIDHANI NI KATI VIONGOZI MWENYE UPEO WA KUIPELEKA NCHI PAZURI KISOKA!! LAKINI NIMEGUNDUA KUWA UMZANIAYE KUMBE SIO.HARAFU ANAONYESHA DHARAHU KWA VIONGOZI WA TFF,UJUE HAO WAMEPEWA DHAMANA YA KUINGOZA SOKA NA WAKILISHI WA WATZ 35 MILLIONI,KUHESHIMIANA NI JAMBO LA MUHIMU.NAOMBA NIUNGANE NA ALIYESEMA "KADU NI USWAZI UNAMSUMBUA" SHULE YA EVENING CLASSES!!! TFF HOYEEEE!!!
ReplyDeletesimba wa yuda anaunguruma
ReplyDeleteWANAOMLAUMU KADU WAMUULIZE YALIYOWAKUTA YANGA HUKO MWANZA.
ReplyDeletePAMOJA NA KUTWAA KOMBE NA SH. MILIONI 25, JAMAA BADO WANADAIWA FEDHA ZA CHAKULA NA MALAZI HAPA MWANZA.
WAMEONDOKA NA KUAHIDI WATALIPA DENI MARA WATAKAPOPATA FEDHA ZA ZAWADI. AJABU NI KWAMBA WATAZITOA WAPI WAKATI WAMEAHIDI KUWAPA FEDHA ZOTE WACHEZAJI? KIVUMBI HICHO.
TFF NA TUSKER WALITOA SH. 20,000 KWA KILA MCHEZAJI KUJILIPIA CHUMBA WAKATI BEI YA CHUMBA WALIKOFIKIA YANGA 30,000. BADO MATUMIZI MENGINE. YANGA WAMERUDI WAMEDAI HALI YA KIFEDHA HAIKUANGALIA UHALISI WA GHARAMA WALIZOINGIA KWA HIVYO WAMEACHA DENI MWANZA! MPO HAPO?
MSIWE MNALOPOKA NA KUDAI ETI MWINA KASOMA USWAHILINI. KWANI UDSM IPO WAPI? HIVI UWASHILINI MAANA YAKE NINI?
KLABU YOYOTE KAMA INAONA MSHIKO UNAOTOLEWA NA WADHAMINI HAUTOSHI WANA HAKI YA KUKATAA KWANI JASHO LINALOTUMIKA KUTANGAZA BIASHARA YA MTU, ANAYEFAIDIKA NI MTANGAZIWA NA WATANGAZAJI WANALALA NJAA.
TENGA NA KUNDI LAKE TANGU ALIPOINGIA MADARAKANI AMEFANYA NINI CHA KUJIVUNIA NA KUMFANYA AWE NA NAFASI YA KUCHAGULIWA TENA UCHAGUZI MKUU UJAO?
AU MNATAKA KUTUMIA USHINDI WA STARS KAMA KIVULI? STARS INASIMAMIWA NA KAMATI MAALUMU AMBAYO HAIKUTELIWA NA KINA TENGA. NDIYO MAANA FEDHA ZA WACHEZAJI WALIZOCHANGIWA BUNGENI HAWAKUZIGUSA NA WALIAMBIWA WASIZIGUSE. KWA NINI? KWA SABABU TFF HAIAMINIKI KWENYE MASUALA YA FEDHA HATA KIDOGO.
HIZI KLABU ZA YANGA NA SIMBA ZITAENDELEA KUDHULUMIWA HADI HAPO SERIKALI ITAKAPOINGILIA KATI NA KUWAKAMATA VIONGOZI WABADHIRIFU WA TFF NA KLABU HUSIKA. VINGINEVYO WEZI WATAENDELEA KUTUMBUA FEDHA KILA KUKICHA. NDIYO MAANA WATU WANALILIA KUONGOZA KLABU NA TFF SIKU HIZI. KISA...FEDHA ZA BURE! WAJINGA WAJINGA KIBAO HAMJUI KIENDELEACHO NDANI YA BOX.
(PUNTO)
INAPASWA MFAHAMU KUWA TFF NDIO CCM YA MPIRA NA CCM NDIO TFF YA SIHASA.........Simba wa Yuda aweza ibuka kama zitto nini ?
ReplyDeleteMzushi
...bado tuna invest kwenye magomvi...too much technicalities...mwisho itaanzishwa mahakama ya michezo, wadau au ipo?...whats all this scat
ReplyDeleteCHA AJABU NI KWAMBA HUYU JAMAA NA YEYE ALISHAWAHI KUWA KATIBU MKUU WA FAT NA ALIKUWA AKITAFUNA FEDHA HAKUNA MFANO. SASA NDIO ANAONA MADHAMBI YA WENZAKE! ANAROPOKA TUU BILA USHAIDI, HAYO NDIO MAMBO YA KISWAHILI YANAYOSEMWA HAPA. JAMAA ANAROPOKA BILA KUWA NA VIGEZO NA USHAHIDI SASA MAMBO NDIO YANATAKA KUMTOKEA PUANI. KAZI KWAKE. HATA MUNGU ANASEMA TUHESHIMU MAMLAKA SIYO KUJIFANYA KWA SABABU ULISHAWAHI KUWA MADARAKANI BASI NDIO UNAJUA KILA KITU. USHAMBA TUU NA SIMBA MWAKA HUU MKIMSHABIKIA ATAWAWEKA PABAYA SANA.
ReplyDeletebabu kadu hoovyoooo!!
ReplyDeletekwanza kila cheo anataka yeye... mara ktk marefarii yupo mara katibu,mara kocha msaidizi mbona unakuwa sio systematic, huyu jamaa chinga nini?!!
Wacha ushamba wa kuongelea eti anapenda madaraka.Kadu kwa sasa ni kiongozi wa Simba tu basi.Mbona Madega yupo TFF humsemi au chongo kwa mnyamwezi???????Mswahili amri ya Mungu
ReplyDeleteano wa aug 27,10:11:00 mbona unamshindilia tenga nondo ya kichwa,mwakani unataka kugombea nafasi yake nini?sema tu bwana wapambe tupo tuanze kazi.
ReplyDeleteCome on Kadu, kuwa muungwana waombe msamaha TFF waambie ulimi uliteleza. Ulikuwa una hoja nzuri sana kuhusu maslahi duni yanayotolewa na wadhamini (Tusker) kwa timu ila ulivuka mipaka kusema mambo ambayo hauna uthibitisho nayo. Take care, kauli zako zitasababisha timu unayoongoza ionekane hampo serious hata kidogo. Jaribu kutumia kiswahili sanifu hasa unapozungumza na press, epuka maneno ya mitaani mfano " haiwezekani mtu ukaandaa maulid halafu ukatuambia sisi tuje na pilau" au "wao wakimwaga ugali mimi namwaga mboga".
ReplyDelete