
msanii wa reggae lucky dube toka sauzi amefanya onesho moja washington dc metro area usiku wa kuamkia leo na kwa mujibu wa wadau waliohudhuria lilikuwa ni kati ya maonesho bora kabisa kufanywa hapo. inasemekana hao kinamama anaoimba nao wamefanya uchezaji wa "kufa mtu" pale wanapochanganya midundo ya reggae na uchezaji wa muziki wa asili wa ki-afrika ambapo wimbo wao wa 'ding ding licky licky bong' ndio uliotia fora zaidi katika onesho lao ambalo lilidumu kwa takriban masaa mawili.
Waw, Lucky Dube! As a reggae fun; to me,you are the best musician. Reggae is really strong, keep it up the son of Africa!
ReplyDeleteWell.
ReplyDeleteNamshukuru almighty kuwa nimeweza kuhudhuria live concerts mbalimbali mwaka huu za watu wenye majina makubwa katika muziki huu wa Reggae, lakini hakuna ambaye aliweza kufanya onesho lililofikia japo nusu ya hili.Sikuamini kwa kuwa sikutegemea kama bado ana uwezo aliouonesha na ilifika wakati watu tukabaki kuangalia tuu badala ya kucheza maana kundi zima hasa kinamama hao walifanya show ya ajabu. Attention aliyoipata ilitokana na kazi alioionesha na si kutokana na mavazi ama vituko stejini kama wafanyavyo baadhi ya wasanii. Alionesha Heshima ya hali ya juu na kuwaimbisha watu lugha mbalimbali za kiafrika. Kwa ujumla jamaa alifanya kazi njema na nimesikia ataelekea Ujerumani. Mlioko huko nasema kama atafanya alichofanya hapa, si show ya kukosa.
Blessings
Dube anatisha Period!!
ReplyDeletewatu wa Arizona(Phoenix,Tempe,scottsdale na hata Tucson)kaeni mkao maana Luky Dude tarehe 7/9/07 atagonga show ya nguvu ndani Messa Convetion Center Main Hall.
ReplyDeleteInfo:480 619 1264
Anon wa hapo unatuchanganya na tarehe zako. Mbona Mwezi wa Saba umeshapita maana umeandika 7/9/07.
ReplyDeleteHaya waheshimiwa mlio USA hii ni ziara yake anayoendelea nayo. Si wa kukosa maana kila alikokuwa amefunika "vibaya-mbaya"
ReplyDeleteFuatilia ratiba yake kwa kugonga hapa http://www.luckydubemusic.com/tourdates.html
Huyo anon hapo juu alikua anamaanisha tarehe Saba mwezi wa tisa 07,hapo bado kuna utata jamani?Watu wa U.S.A ni september,seven,07 au 09/07/07 tuko pamoja?
ReplyDeleterege inatisha.hii iwe changamoto
ReplyDeletekwa wanarege wa bongo:innocent nganyagwa,jikoman,bmv etc.