Warembo watatu walikuwa wakisifia majina ya wapenzi wao, hususan jinsi ya kufupisha majina pindi wanapotaka kuwaita.
Wa kwanza alisema boyfriend wake anaitwaTusamale, hupenda kumuita Tusa au humuita Male kwa kifupi.
Wa pili alisema yeye wakwake anaitwa Rutatila, na kwamba anapendelea saaana kumuita Ruta lakini mara chachechache humuita Tila.
Ukapita ukimya kidogo, huku hawa wadada wawili wakimuangalia mwenzao. Wakamuuliza shosti mbona upo kimya ?
Kwa sauti ya upole sana akawajibu: "nilikuwa nafikiria...kwani boyfriend wangu anaitwa Mbwambo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Kibooooooooo!! Mwache binti achanganyikiwe maana hilo jina la Mtani wangu GUMU KWELI! Bora angemuita Mbwa

    ReplyDelete
  2. Aaah! Hiyo mbona Ize, kwa msaada tu huyo dada wala asikonde, anaweza kumuita MB! au WAMBO! tehetehete....!

    ReplyDelete
  3. kifupi cha mshikaji wa huyo dada wa tatu kingekuwa mbwa au mbo kulingana na wenzie walivyofupisha. kama angeona hiyo haipendezi angejaribu mb au wambo

    ReplyDelete
  4. Huyo angemuita jamaa yake ambo kwa kifupi kuepuka aibu.

    ReplyDelete
  5. Michuzi weka hii hewani acha kuibania...ICT


    Hoja Binafsi ya kuunda kamati teule ya Bunge kuchunguza mkataba mpya wa madini ambao Waziri wa Nishati na Madini Karamagi ameusaini bila kuzingatia maagizo ya Rais
    Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe (MB)
    MHESHIMIWA Spika, kwanza napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa kunipatia fursa ya kuleta hoja hii hapa kwenye Bunge lako tukufu kwa mujibu wa kanuni zetu za Bunge. Kuletwa kwa hoja hii, bila kujali maamuzi ya kuhusu hoja yenyewe, ni ishara tosha ya ukomavu wa demokrasia yetu ambayo inakuzwa na mijadala ya Bunge lako tukufu. Nakupongeza kwa dhati kabisa kwa juhudi zako za kuliimarisha Bunge letu na kujenga muhimili imara wa ulinzi wa demokrasia ya vyama vingi nchini kwetu.
    Mheshimiwa Spika, mnamo tarehe 16/7/2007 mara baada ya hoja ya Waziri wa Nishati na Madini kuamuliwa na Bunge lako tukufu, nilisimama mahala pangu na kutoa taarifa ya kukusudia kuleta hoja ya kuunda kamati teule ya Bunge. Nilisema kama ifuatavyo (kwa mujibu wa kumbukumbu sahihi za mijadala ya Bunge), ninanukuu ‘…naomba kutoa taarifa rasmi… kwamba nakusudia kuleta hoja ya kuunda kamati teule kuchunguza mkataba mpya wa madini ambao Waziri wa Nishati na Madini ameusaini bila kuzingatia maagizo ya rais (wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) ya kupitia mikataba ya madini aliyoyatoa mbele ya Bunge lako tukufu tarehe 30 Disemba, 2005.’ Mwisho wa kunukuu.
    Mheshimiwa Spika, nimeshawasilisha hoja yangu hii kwa maandishi kwa Katibu wa Bunge na sasa nawasilisha rasmi katika kikao hiki cha Bunge kwa uamuzi. Nimezingatia kanuni 104 (2) katika kuwasilisha hoja yangu.
    Mheshimiwa Spika, katika maelezo yangu niliyowasilisha bungeni wakati wa mjadala wa hotuba ya Waziri wa Nishati na Madini siku ya tarehe 16/7/2007, nilihitaji maelezo kutoka serikalini katika masuala makuu mawili yafuatayo:
    1. Kuondolewa kwa kipengele katika sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 1973 kuhusiana na asilimia 15% ya ‘capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure’ bila ya kibali cha Bunge lako tukufu.
    2. Kusainiwa kwa mkataba mpya wa madini wa mgodi (mradi) wa Buzwagi kati ya serikali na Kampuni ya Barrick na sababu za mkataba huo kusainiwa nje ya nchi, London, Uingereza, na vilevile kwa nini mkataba huo umesainiwa wakati bado serikali inafanya durusu (review) ya mikataba kufuatana na maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndugu Jakaya Mrisho Kikwete.
    Mheshimiwa Spika, wakati akijibu hoja zangu Waziri wa Nishati na Madini alijenga hoja zake kama ifuatavyo:
    a. Kuhusiana na asilimia 15% ya ‘capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure’
    Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini amenukuliwa na kumbukumbu za majadiliano ya Bunge akisema, ninanukuu: “…kwa hiyo pamoja na kwamba ninamheshimu sana Mheshimiwa Kabwe Zitto na sote tunamheshimu ni msomaji mzuri, lakini wakati mwingine lazima kuangalia vitu gani unasoma. Ni kwamba kipengele hiki cha sheria kililetwa hapa bungeni mwaka 2001 kwenye bajeti kikabadilishwa…” Mwisho wa kunukuu.
    Mheshimiwa Spika, katika kuandaa hoja yangu hii, ilinibidi kupitia upya kumbukumbu za majadiliano ya Bunge ili kujiridhisha na maelezo ya Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini, maelezo ambayo mimi nililitaarifu Bunge lako tukufu tarehe 16/7/2007 kuwa sio sahihi.
    Mheshimiwa Spika, Kumbukumbu hizo zinaonesha kwamba, sheria ya fedha ya mwaka 2001 (Finance Act. No.14 ya 2001) ilifanyiwa marekebisho kadhaa ikiwemo marekebisho ya sheria ya madini kifungu cha 87 ambapo kifungu kidogo cha (3) cha kifungu cha 87 kiliongezwa. Kifungu kidogo hicho kinasema, ninanukuu:
    ‘(3) The provisions of subsections (1) and (2) shall not apply to any person who, immediately before the first day of July, 2001 was not the holder of a mineral right granted under this Act.’
    Mheshimiwa Spika, kifungu cha 87 cha Sheria ya Madini ya mwaka 1998 (No.5/1998) kinazungumzia mrahaba wa madini (Remission and deferment of royalties). Hivyo, kama sheria ya fedha ya mwaka 2001 haikubadili kipenge hiki, Mheshimiwa Waziri ametoa wapi jibu aliloliambia Bunge?
    Mheshimiwa Spika, suala hili linahusu haki, kinga na madaraka ya Bunge kwa mujibu wa sheria namba 3 ya 1988.
    Mheshimiwa Spika, hata hivyo katika hotuba ya Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Basil Mramba, akiwasilisha hotuba ya Bajeti mwaka 2002, tarehe 13 mwezi Juni, alizungumzia kipengele hiki. Ninaomba kunukuu sehemu ya hotuba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Basili Mramba.
    “Amendment to the Income Tax structure, (44) Mr. Speaker, in this area I propose to take the following measures:
    (v) I propose to reinstate the additional 15 percent capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure as set out in the Mining Act. No. 5 of 1998.” Mwisho wa kunukuu.
    Mheshimiwa Spika, nilipopitia sheria ya fedha ya mwaka 2002, nimekuta sehemu ya 8 inazungumzia mabadiliko katika kodi ya mapato ya 1973. Na hata katika ukurasa wa kwanza wa sheria hii (Arrangement of Contents), sheria ya madini haitajwi.
    Mheshimiwa Spika, maelezo haya ya Waziri wa Fedha ya mwaka 2002 yanaonesha dhahiri utata wa kipengele hiki. Ni kwa vipi kifungu cha sheria ambacho hakijafutwa kirejeshwe?
    Mheshimiwa Spika, tuchukulie kuwa maneno ya waziri ni ya kweli. Je, kwa nini makampuni ya madini ambayo yameingia mkataba na serikali kuanzia Julai mosi 2001 hayajaanza kulipa kodi ya mapato?
    Mheshimiwa Spika, utata huu ambao umegubika sekta hii ya madini, unaweza kufafanuliwa na Bunge lako tukufu kupitia Kamati Teule. Kamati Teule ya Bunge ichunguze upitiaji wa mikataba hii na kuona kama kuna vitendo vyovyote vya uvunjifu wa sheria za nchi na kupotea kwa mapato ya serikali na ufisadi.
    b. Kusainiwa kwa Mkataba wa Mgodi (Mradi) wa Buzwagi.
    Mheshimiwa Spika, wakati akijibu hoja yangu kuhusiana na suala la mkataba mpya wa mgodi wa Buzwagi, Waziri wa Nishati na Madini amenukuliwa na kumbukumbu za majadiliano ya Bunge akisema kama ifuatavyo:
    Mheshimiwa Spika, katika tathmini ya migodi, mgodi wa Buzwagi ni marginal mine ambao uhai wake si wa muda mrefu. Bila ya kutumia fursa ya sasa ya bei ya dhahabu, uwekezaji wake usingeweza kuwa wa faida. Hata hivyo, mkataba wa Buzwagi hauna mapungufu yaliyokuwamo kwenye mikataba ya zamani.’ Mwisho wa kunukuu.
    Mheshimiwa Spika, mapitio ya mikataba ya madini ni mchakato ambao mwisho wake ni kuletwa kwa sheria ya madini hapa bungeni na kuifanyia marekebisho ili kuiboresha na kuondoa mapungufu. Hivyo, mpaka hapo sheria itakaporekebishwa, ndipo tutasema tumemaliza zoezi la kupitia mikataba ya madini na hivyo kusaini mikataba mipya na makampuni yote ya madini yaliyopo nchini na yatakayokuja kuwekeza.
    Mheshimiwa Spika, suala ambalo linanipelekea kuomba kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza mkataba huu mpya, ni kuhusu uharaka uliopelekea Waziri wa Nishati na Madini kusaini mkataba huu. Sheria ya Madini bado haijarekebishwa, je, waziri anatumia vigezo gani kusema mkataba mpya wa Buzwagi aliousaini London hauna mapungufu?
    Mheshimiwa Spika, Waziri wa Nishati na Madini aliliambia Bunge lako tukufu kuwa Buzwagi ni marginal mine. Vile vile waziri anasema kuwa Kampuni ya Barrick inamiliki migodi mitatu tu kupitia kampuni zake tanzu ambazo ni Bulyanhulu Gold Mine, North Mara Gold Mine na Pangea Minerals Limited Tulawaka. Kwa maelezo haya ya Waziri Karamagi, Buzwagi sio mgodi.
    Mheshimiwa Spika, hoja hii ya kuwa Buzwagi sio mgodi inashabihiana kabisa na hoja ya Kampuni ya Barrick kwamba Buzwagi ni Project. Taarifa ya kampuni hii ya Barrick Gold Corporation-Global operations-Africa- Buzwagi, inaonesha kuwa Buzwagi ni mradi. Taarifa hii ninaiambatanisha katika hoja hii.
    Mheshimiwa Spika, taarifa ya Barrick, Annual Review 2006 inasema ifuatavyo katika ukurasa wa 23, ninanukuu. ‘A major milestone was reached in February 2007 when we signed a mineral Development Agreement (MDA) with the Tanzanian government. In 2007, we expect to complete a detailed construction design and receive EIA approval.’
    Mheshimiwa Spika, suala ambalo vile vile linanisukuma kuomba Bunge lako tukufu kuunda Kamati Teule ni kwamba, iwapo Buzwagi sio mgodi bali ni mradi, ni kwa nini tumesaini Mineral Development Agreement (MDA) mpya? Kwa kuwa Pangea Minerals Tulawaka ndio inaonekana kumiliki mradi huu, je, serikali imefanya marekebisho tu ya MDA na Kampuni ya Barrick? Naomba Kamati Teule ichunguze ni nini kilichosainiwa, marekebisho ya mkataba wa Tulawaka au MDA mpya ya Buzwagi?
    Mheshimiwa Spika, Buzwagi inashika nafasi ya pili kwa uwekezaji wa Barrick katika migodi hapa nchini. Wakati kampuni hii inawekeza dola za Kimarekani 400 milioni katika Buzwagi, imewekeza dola za Kimarekani 600 katika Bulyanhulu. Je, ni kwa vipi Buzwagi iwe marginal mine wakati uwekezaji wake unashinda uwekezaji wa Tulawaka na North Mara?
    Mheshimiwa Spika, chini ya kifungu cha 47 cha Sheria ya Madini ya Mwaka 1998 (Na.5/98), pamoja na mambo mengine kinataka leseni yoyote isitolewe mpaka taarifa ya mazingira iwe imetolewa na kuruhusu mgodi kuendelea na kazi.
    Mheshimiwa Spika, wakati Waziri wa Nishati na Madini ameweka saini mkataba wa Buzwagi juma la mwisho la mwezi Februari 2007, Baraza la Mazingira nchini limetoa kibali (Environmental Impact Assessment- EIA approval) tarehe 11 mwezi Mei 2007. Ni kwa nini Waziri wa Nishati na Madini, Mheshimiwa Nazir Karamagi alisaini MDA ya Buzwagi na Kampuni ya Barrick kabla Baraza la Mazingira la Taifa (NEMC) halijatoa ruhusa?
    Mheshimiwa Spika, sheria ya madini, niliyoitaja hapo awali, imeunda Kamati ya Ushauri ya Madini (Mining advisory Committee). Kabla ya waziri kusaini mkataba wowote ni lazima apate ushauri kutoka kamati hii. Kwa taratibu za kiserikali, kama kamati ikimshauri waziri na waziri akakataa ushauri huo, inampasa waziri atoe sababu ni kwa nini anakataa ushauri. Je, waziri alifuata ushauri wa Kamati ya Ushauri ya Madini kuhusiana na wakati mwafaka wa kusaini mkataba huu?
    Mheshimiwa Spika, inawezekana kabisa MDA ya Buzwagi kusainiwa Uingereza sio tatizo. Kwa mfano, mwaka 2006 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilisaini mikataba kadhaa. Ni mingapi kati ya mikataba hii imesainiwa nje ya nchi? Nini madhara ya kisheria kwa mkataba kusaniwa Uingereza? Je, mkataba umeandikwa “signed in London...” au “signed in Dar es Salaam...? Kamati Teule ya Bunge ndio chombo pekee kitakachoweza kutoa majibu ya maswali haya.
    Mheshimiwa Spika, suala hili ni suala la kitaifa. Halina hata chembe ya itikadi za kivyama. Ninaamini wabunge wataamua kwa maslahi ya taifa letu. Uundwaji wa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza mapitio ya mikataba ya madini na mazingira ya kusainiwa kwa mkataba mpya wa Buzwagi yatatoa msaada mkubwa kwa azma ya Rais wetu ndugu Jakaya Mrisho Kikwete ya kuona rasilimali za madini zinafaidisha nchi yetu.
    Mheshimiwa Spika, ninaomba kutoa hoja.
    …………………………….
    KABWE ZUBERI ZITTO (MB)
    JIMBO LA KIGOMA KASKAZINI
    Wakati wa kukataa kuonewa umefika! Tulinyamaza wakati wa IPTL, RICHMOND mikataba mibovu ya madini, sasa kuna BOT, Mkataba wa madini kusainiwa London, Kiwira, wabunge wa CCM wakiuliza wanaitwa kuonywa, wapinzani wakiuliza wanafukuzwa bungeni. Wakati wa Bunge kuwajibika kwa wapiga kura wake umefika! Vijana tuamke na tutetea haki zetu !!! Tutaonewa mpaka lini????

    ReplyDelete
  6. Michuzi michuzi michuzi Kaka. Sijajua namna ambavyo waheshimiwa wanatuma maswali na mambo mengine lakini kwa muda mrefu umekuwa ukituwekea mambo murua na kutufanya kupaona hapa kama sehemu ya "latest news" kila wakati. Yaani binafsi nikitaka kujua nini na kipi kimeendelea home kwa muda mfupi basi najitoma humu, kisha nanyaka mambo mawili matatu. Nondoz za wapendwa wenzetu na hata maswali na habari mbalimbali toka kwa wadau mbalimbali zilikuwa zikipatikana. Ni blog ambayo naweza ifungua popote, mbeleye ya yeyote bila kuhofia chochote. Lakini kwa sasa naanza kuhisi kama tunaanza kupoteza mwelekeo vile. Angalia hili tafadhali ujue kuwa waasomaji wanaojiheshimu na kuheshimu HABARI ni wengi kuliko hao wanaotaka kutuma maswali "yenye utata na tafsiri zinazoweza kukupunguzia heshima" na ambao wanaweza kutaka kuja kwenye blog yako kwa kuwa tu "wameshaharibu" huko kwengine.
    Endelea kutupa Real News & Picture kama ilivyokuwa awali na usilete hawa wenye maswali kama haya wakupunguzie ama kupunguzia Blog yako heshima.
    Blessings

    ReplyDelete
  7. Kuweni macho, matapeli hawachoki kutuma hizi.....

    YOUR OVERDUE INHERITANCE CLAIM!!!!!‎
    From: JAMES IRABO (abujajesu12@hotmail.com)
    Medium risk You may not know this sender. Mark as safe | Mark as unsafe
    Sent: 17 August 2007 10:51:33 AM
    Reply-to: jirabo12@jmail.co.za


    FIRST BANK OF NIGERIA PLC
    MARINA-LAGOS-NIGERIA
    INTERNATIONAL TRANSFER.
    LEICESTER CURRENCY
    CHEQUE/DRAFT DEPARTMENT
    TELEHRAM: FBNFOREX
    EMAIL:jirabo101@excite.com

    ATTN:BENEFICIARY,

    I am Mr James Irabo, Director allocation department from the(First Bank of Nigeria plc,)lagos branch. My office monitors and controls the affairs of all banks and financial institutions in Nigeria concerned with foreign claim payments.

    I am the final signatory to any transfer or remittance of huge funds moving within banks both on the local and international levels in line with foreign claim settlement.I have before me list of funds, which could not be transferred to some nominated accounts as these accounts have been identified either as ghost accounts, unclaimed deposits and over-invoiced sum etc.

    Your Name was among the people expecting the funds to be transferred into their account, on this note; I wish to have a deal with you as regards to your unpaid funds.I have your file before me and hope your data's are correct and un-tampered unless you reconfirm it not correct.

    As it is my duty to recommend the transfer of these surplus funds to the Federal Government Treasury and Reserve Accounts as unclaimed deposits,I have the opportunity to write you based on the instructions I received two days ago from the Foreign Debts Reconciliation dept to submit the List of payment reports / expenditures and audited reports of revenues.
    Among several others, I have decided to remit your claim sum following my idea that we can have a deal/agreement and I am going to do this legally.
    My conditions:

    1... The sum of USD$9.7M only will be transfer into your account after the proccessing of all relevant legal documents with your name as the bonfide beneficary,the transfer will be made by Draft or telegraphic Transfer (T/T), confirmable in 3 working days.

    2... This deal must be kept secret forever, and all correspondence will be strictly by email / telephone, for security purposes.

    3... There should be no third parties as most problem associated with your fund release are caused by your agents or representative.

    If you AGREE with my conditions, l advise you on what to do immediately and the transfer will commence without delay as I will proceed to fix your name on the Payment schedule instantly to meet the three days mandate.
    I hope you don'treject this offer and have your funds transferred.

    Waiting for your reply soon.
    Yours Faithfully,
    Mr James Irabo

    ReplyDelete
  8. Hii ni sawa kabisa na kuwa na jamaa anaitwa NATO kisha ikatokea mbwa anamfukuza kwa nyuma kwenda kumdhuru sasa ungependa kumjulisha aidha kwa kushauti au taratibu ili ajue kuna mbwa nyuma yake.

    itakuwa Natooooo..#@%&$#.....nyuma.

    Hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  9. Hehehehehe !! Michuzi umepinda!! Lol!! Hayo majinaz la mwisho noma sana!!Hahahaha Sawa bwana Misupu!!

    ReplyDelete
  10. The top 10 US national universities were:

    1. Princeton University

    2. Harvard University

    3. Yale University

    4. Stanford University

    5. California Institute of Technology

    University of Pennsylvania (tie)

    7. Massachusetts Institute of Technology

    8. Duke University

    9. Columbia University

    University of Chicago (tie)

    Source: http://news.yahoo.com/s/ap/20070817/ap_on_re_us/college_rankings

    OYAA WABONGO MNAOKULA NONDO US HEBU NIAMBIENI WANGAPI MPO KWENYE VYUO HIVYO.. NAJUA ASILIMIA 99 YA WABONGO HUKO US MNAPIGA KTK 'MANZESE UNIVERSITY' ZA HUKO

    HAHAHAHAHAHAHAHAHHHHHHHHH

    ReplyDelete
  11. Maskini huyo dada yaani akimwita mbwa atapigwa huyooo umwiteje mpenzi wako mbwa? Akimwita mbo hasa wakiwa wawili tu mjamaa atadhani anadai....wamnanii sasa aache amwite darling!?

    ReplyDelete
  12. MR RAS TWIN CHILL OUT YOU SEEM TO TAKE THINGS TOO SERIOUS, LIFE IS SERIOUS ENOUGH AND WE NEED TO CALM OURSELVES DOWN IN ONE WAY OR THE OTHER & HERE IS WHERE PEOPLE LET OUT STEAM, GO FOR MEDITATION YOU MAY SEE THINGS DIFFERENTLY.

    ReplyDelete
  13. Hey wewe mimi nimesoma University of Penny na NYU na sioni it is a big deal. Havard, Stanford, MIT, Duke nawafahamu watanzania zaidi ya 20 combine kwenye hivi vyuo. Havard peke yake ni watanzania wangapi wapo hapo?

    Nyie wabongo mnachambua hivi vyuo lakini mjue wenzenu hata kama wanaenda vyuo unavyoviita mazense ukimaliza college degree ni toafauti sana kama unavyowaza wewe huko..

    Jitahidi upate elimu kidogo uache kupoteza muda on line kuchambua vyuo bora ni vipi. Huo mda ungejifunza jambo moja zuri....

    ReplyDelete
  14. Another job offer scam watch out for this one. The catch here is that when you accept this job offer in no time you will start to recive customers (fake customers) and they will send you these cashier checks you deposit on your account. You keep your 10% and send the reminder to them... The end of the story is the same. Watch out


    Dear Sir/Madam,
    My name is Chris Southurst.I am a freelance researcher.I would be
    very interested in offering you apart-time paying job in which you could earn alot.I just resigned my job as a research scientist for
    AFBI(Agri-Food Biosciences Institute) but i still work as a freelance consultant for the
    institute which gives me very much time to do my own work which is
    basically being afreelance researcher who could be employed by research institutes to do research projects anywhere in the world.
    WHAT YOU NEED TO DO FOR US.Presently, I have just been granted a funding to head a research project in the tropical regions of West Africa regarding
    rare and vulnerable plant species and this would be commencing very
    soon, However my fundings were by my American counter parts which sent me the bunch of payments mostly in US based Money orders or Cashier check. Getting
    an accountant in the states or opening an account would have been my best choice but I have a deadline to meet and taking any of those choices would cost me time and a whole lot of other equirements I am not ready to deal with as I would be traveling a lot in the meantime.So presently,
    assuming you would be able to deal with cash, I would be willing to employ you on contract basis to be my payment representative back in the states, this way they could issue out the payment on your behalf and mail to you,then cash
    the payment,and deduct 10% of the total amount on the payment as your commission and then send the rest back to where ever you are ask to send the funds to via Western Union money transfer.

    JOB DESCRIPTION?
    1. Recieve payment from Clients
    2. Cash Payments at your Bank
    3. Deduct 10% which will be your percentage/pay on Payment processed.
    4. Forward balance after deduction of your percentage which is 10% and pay to any of the offices you will be contactedto send payment to(Payment is to forwarded by (Western Union Money Transfer).
    5. recieve a letter from the companys and dispatch to other customer's in US.

    HOW MUCH WILL YOU EARN?10% from transaction! For instance: you receive 7000 USD via cheques or money orders on our behalf. You make the clearance for the payment and keep $700 (10% from $7000) for yourself! At the beginning your commission will equal 10%,though later it will increase up to 12%!
    ADVANTAGES.You do not have to go out as you will work as an independent

    contractor right from your home office. Your job is absolutely legal. You can earn up to $3000-4000 monthly depending on time you will spend for this job. You do not need any capital to start. The employees who make efforts and work hard have a strong possibility to become managers. Anyway our employees never leave us.
    MAIN REQUIREMENTS.
    22 years or older legally capable responsible ready to work 3-4 hours
    per week.with PC knowledge e-mail and internet experience (minimal).And please know that Everything is absolutely legal,that's why You have to fill a contract! I would be glad if you accept my offer and I intend to
    commence on the job as soon as you are ready. If you are interested, get back to me
    asap.

    Please note when replying fill the form below:
    Name:
    Full Address:(not p.o.box):
    City:
    State:
    Zip code:
    Age:
    Sex:
    Phone Number(s):
    Current job:
    Email:

    Thanks for your anticipated action.And i hope to hear back from you.
    Chris Southurst
    AFBI(Agri-Food Biosciences Institute)
    Ireland,Dublin.Hillsborough
    Southurstc1@yahoo.com.

    ReplyDelete
  15. Weeee anon with your top 10 universities Brown, Cornell, John Hopkins, NYU, Georgetown, Rutgers, Purdue. Iowa state ni manzese ya kwako...maaana sivioni hapo....

    Kwanza wewe umesoma wapi? Mimi college yangu haipo hata kwenye top 100 lakini na make good money zaidi ya ndugu na rafiki zako wote hapo kwa mwaka ukichanganya.

    ReplyDelete
  16. Wewe, Anonymous wa tarehe August 17, 2007 3:49:00 PM EAT, kuhusu top-rated US universities, kama unafahamu statistics, ungetueleza vipimo vya data walivyotumia (variables).

    Kati ya vyuo hivyo ni vile wanavyoita "Ivy League". Ukweli ni kwamba chuo kikuu kinaweza kuwa Ivy League kumbe the quality of education provided is mediocre compared to other non-Ivy League sister universities!

    Kuna chuo hapa New York, Baruch College, ambacho ni constituent college ya City University of New York. Chuo hiki kinasifika sana kwa mambo ya Business Studies!

    Kama unapenda kujua, it is not the name of the University! Cha maana ni unataka kujifunza nini (what course of study are you persuing leading towards a university degeree!

    Kwa mfano, University of Missouri ina course nzuri sana ya Journalism, pengine kushinda hata Columbia University!!!

    ReplyDelete
  17. Mara nyingi vyuo wanavigrade kwa kupublish paper na sio ubora wa course zake. Kwa hiyo chuo kinaweza kikawa kibovu kwa course zake lakini wanapublish sana basi hiyo inawapandisha moja kwa moja.

    Kwa hiyo ndugu zangu huyo jamaa asiwaumize vichwa, nyie kule nondo zenu halafu rudini nyumbani mjenge nchi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...