TAARIFA YA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KUHUSU MAZUNGUMZO YA MUAFAKA KATI YA CUF NA CCM

Tarehe 7 Agosti, 2007, Mwenyekiti wa Chama cha Civic United Front (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba alitoa tamko la kuelezea kukwama kwa mazungumzo ya muafaka kati ya Chama chake na Chama cha Mapinduzi (CCM). Katika tamko hilo, Profesa Lipumba alielezea nia yake na ya Chama chake ya kujiondoa katika mazungumzo hayo ifikapo tarehe 15 Agosti 2007.
Napenda kukumbusha kwamba chimbuko la mazungumzo yanayoendelea sasa ni ahadi niliyoitoa kwa Watanzania wakati nilipohutubia Bunge tarehe 30 Desemba, 2005. Niliahidi kuwa nitakuwa tayari kuchukua hatua za kutafuta ufumbuzi wa mpasuko wa kisiasa Zanzibar. Kwa ajili hiyo, nilielezea nia yangu ya kusaidia kuanzisha na kuwezesha mjadala juu ya mustakabali wa kisiasa Zanzibar.
Ahadi hiyo niliitoa kwa dhati ya moyo wangu nikiamini kwamba hakuna tofauti zozote za kisiasa na kijamii katika nchi yetu au baina yetu au katika jamii zetu ambazo haziwezi kumalizwa kwa njia ya mazungumzo. Imani hiyo bado ninayo leo na nitaendelea kuwa nayo daima.
Ilichukua muda kwa mazungumzo baina ya CCM na CUF kuanza. Hii ilisababishwa na haja ya kufanya mashauriano mapana baina na miongoni mwa wadau wa pande zote husika ndani ya Chama cha Mapinduzi na wenzetu wa CUF. Mashauriano haya yalichukua muda kidogo zaidi ndani ya CCM kwa sababu utamaduni na mfumo wetu wa demokrasia ndani ya Chama cha Mapinduzi unatuwajibisha kuwa na mashauriano mapana na ya kina katika ngazi mbalimbali za uongozi na vikao vya Chama. Nafurahi kuwa kazi hiyo ilikamilika vizuri na tukafikia maelewano ya dhati kuwa CCM ifanye mazungumzo na CUF.
Baada ya hapo, Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM ilimuagiza Katibu Mkuu wa CCM kuwasiliana na Katibu Mkuu wa CUF na kumuomba akubali kushiriki katika mazungumzo baina ya vyama vyetu. Tulifarijika sana kwamba baada ya maombi hayo ya CCM wenzetu wa CUF walikubali kukaa pamoja nasi katika meza ya mazungumzo.
Tarehe 17 Januari, 2007, Makatibu Wakuu wa vyama vya CUF na CCM wakakutana na mchakato wa mazungumzo ukaanza. Baada ya kikao hicho cha mwanzo, kila upande ukaunda timu yake ya kushiriki katika mazungumzo hayo. Tarehe 01 Februari, 2007 Kamati yetu ya Pamoja ilifanya mkutano wake wa kwanza ambapo walikubaliana kuwa jambo la mwanzo la kufanya ni kwa kila upande kutengeneza mapendekezo yake ya mambo unayotaka yazungumzwe, yaani yawe kwenye Ajenda ya Mazungumzo. Baada ya hapo yalifanyika majadiliano mazuri na katika mazingira ya kidugu, ajenda ya pamoja ya mazungumzo ikatengenezwa. Ajenda hiyo ilikuwa na mambo matano makubwa kama ifuatavyo:


1. Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa Oktoba 30, 2005 na taathira zake;
2. Usawa na haki katika kuendesha siasa;
3. Masuala ya utawala ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar;
4. Njia za kuimarisha mazingira ya maelewano ya kisiasa na uendeshaji wa uchaguzi huru na wa haki Zanzibar; na,
5. Utaratibu wa kutekeleza Programu ya Utekelezaji wa Makubaliano yatakayofikiwa katika mazungumzo haya.

Tangu mazungumzo haya yaanze mwezi Januari mwaka huu, Kamati yetu ya Pamoja imefanya vikao 12 na wametumia siku 43 za mazungumzo. Pia Makatibu Wakuu nao wamekutana mara mbili kutafuta ufumbuzi wa yale mambo yaliyohitaji kufanywa nao. Tulikubaliana kuwa mazungumzo ya msingi yatafanywa na Kamati lakini pale ambapo Kamati itakwama Makatibu Wakuu waingilie kati kutoa mwongozo. Ukweli kwamba wamekutana mara mbili tu ni dalili kwamba mambo yanakwenda vizuri.
Hatua kubwa imefikiwa na mafanikio ya kuridhisha yamepatikana. Kuna mambo kadhaa makubwa na ya msingi ambayo pande hizi mbili zimekwishakubaliana. Katika ajenda tano za mazungumzo, ajenda tatu, yaani ajenda ya Usawa na Haki katika Kuendesha Siasa, Masuala ya Utawala ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na Njia za Kuimarisha Mazingira ya Maelewano ya Kisiasa na Uendeshaji wa Uchaguzi Huru na wa Haki Zanzibar, zimejadiliwa na pande zote mbili zimefikia maelewano mazuri.
Kwa upande wa ajenda ya kwanza inayohusu Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa Oktoba 30, 2005 na Taathira Zake, mazungumzo yamefanyika na maelewano yamepatikana kwa mambo kadhaa. Yapo mambo mawili matatu ambayo bado maelewano hayajafikiwa. Hatuna budi tuendelee kuyazungumza mpaka tutakapopata maelewano ya pamoja.
Jambo moja kubwa ambalo wawakilishi wa vyama vyetu bado wanaendelea kujadiliana na ambalo bado halijakamilika ni lile linalohusu namna ya kutengeneza mazingira yatakayowezesha vyama vya siasa Zanzibar, hususan CUF na CCM, kuishi na kuendesha shughuli zao kwa pamoja katika hali ya maelewano na mazingira ya amani na utulivu.
Mazungumzo kuhusu kipengele hiki yamechukua muda na muafaka bado haujafikiwa. Kwa maoni yangu imekuwa hivyo kwa sababu ya umuhimu wake na umakini unaotakiwa katika uchambuzi wa hoja na kufikia uamuzi. Katika mazungumzo kuna mambo rahisi yanayochukua muda mfupi kujadiliwa na kufikiwa makubaliano na kuna mambo magumu yanayochukua muda mrefu. Huu ndiyo uzoefu wa vyama vyetu katika mazungumzo tuliyofanya huko nyuma na hata kwa mazungumzo haya.
Kwa sababu hiyo, sisi wa upande wa CCM, hatudhani kama tumefikia mahali pa kusema kuwa mambo yameshindikana na hivyo mazungumzo yavunjike. Hatujafikia hatua hiyo hata kidogo. Ni maoni yangu na ya Chama cha Mapinduzi kuwa tuendelee kuzungumza na kila upande uboreshe hoja zake za kuushawishi upande mwingine. Tupo kwenye mazungumzo kwa ajili hiyo. Tupo kufanya hivyo. Naamini kwamba, kama ambavyo tumepata maelewano katika maeneo mengine ambayo yalikuwa magumu, hata kwa haya yaliyobakia hatimaye tutaafikiana. Wahenga walisema: “Penye nia pana njia”. Maadam sote nia tunayo, jawabu muafaka kwetu sote na kwa nchi yetu tutalipata.
Nawasihi wenzetu wa CUF wasijiondoe kwenye mazungumzo haya na badala yake tuendelee kuzungumza. Tunazungumza kwa sababu tuna tatizo tunalolitafutia ufumbuzi. Kuacha kuzungumza si jawabu kwani tutakuwa tunaacha kulipatia ufumbuzi tatizo linalotusibu sote. Tutarudi kule tulikokuwa, yaani kwenye uhasama, shutuma zisizoisha, kubaguana, kutozikana na hata kutosalimiana au kuchekeana. Tutaendelea na utamaduni mbaya wa kuzifanya tofauti zetu za kisiasa kuwa ni chanzo cha uadui, chuki na hivyo kuhatarisha amani, utulivu na umoja wa taifa letu na watu wake.
Ni kweli, mazungumzo ni lazima yawe na ukomo. Na sisi wote tungependa yafikie mwisho wake mapema inavyowezekana. Lakini, ukomo wa mazungumzo ni lazima utokane na ridhaa ya pamoja ya pande zote na hasa kwamba ajenda zote zimepata nafasi ya kujadiliwa kwa kina na maelewano yamefikiwa. Ukomo wa mazungumzo usiotokana na hayo ni kuahirisha tatizo litakalokuja kujitokeza na kutudhuru wote siku za usoni. Shabaha yetu katika mazungumzo haya ni kupata ufumbuzi wa kudumu na endelevu kwa matatizo yanayotukabili katika uwanja wa kisiasa nchini. Tunafanya yote hayo ili kujihakikishia amani, utulivu, mshikamano na umoja wa taifa letu na watu wake vinaendelea kuwepo daima dumu.
Napenda kumaliza kama nilivyoanza kwa kukumbusha kwamba mazungumzo haya yametokana na ahadi yangu na ya CCM. Ahadi hiyo ni ya dhati na niliitoa kwa kujiamini na kwa kuamini kuwa hii ndiyo njia pekee iliyo bora kuliko zote ya kushughulikia tofauti zetu. Kwa msingi huo, ningependa na CCM ingependa kuona mazungumzo haya yanaendelea na yanazaa matunda tunayoyatarajia sote. Nawasihi wenzetu wa CUF tuungane kuhakikisha tunafanikiwa. Tusikubali mazungumzo yavunjike kwani gharama ya kuvunjika kwa mazungumzo haya ni mbaya na haina maslahi kwa taifa letu na watu wake. Itahatarisha amani na utulivu wa nchi yetu.

Ikulu,
Dar es Salaam.
14 Agosti, 2007

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Tunamshukuru Rais Kikwete kwa kuonyesha uungwana wa kutoa maelezo kwa wananchi kuhusu Maendeleo ya mwafaka. Tunaomba aendelee kuhakikisha mazungumzo hayo yanafanyika kindugu kama utamaduni wetu Watanzania ulivyo na asiruhusu ubinafsi au fitna kutoka upande wowote kuvuruga hatua iliyokwishafikiwa. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika. A.R.C

    ReplyDelete
  2. Mbona JMK hapa ananichanganya.
    Anasema kuwa 30 Desemba 2005 alitoa ahadi ya kuwa na mazungumzo ya kutafuta muafaka wa CCM/CUF.

    Hapo hapo anasema kuwa
    "Mashauriano haya yalichukua muda kidogo zaidi ndani ya CCM kwa sababu utamaduni na mfumo wetu wa demokrasia ndani ya Chama cha Mapinduzi unatuwajibisha kuwa na mashauriano mapana na ya kina katika ngazi mbalimbali za uongozi na vikao vya Chama. Nafurahi kuwa kazi hiyo ilikamilika vizuri na tukafikia maelewano ya dhati kuwa CCM ifanye mazungumzo na CUF."

    Ina maana alitoa ahadi KABLA hawajashauriana NDANI ya CCM? Je, hiyo ilikuwa demokrasia gani? Na kama NDANI ya CCM wangekataa, angetekeleza vipi ahadi yake hiyo ya 30 Desemba 2005?

    ReplyDelete
  3. Michuzi na wadau wengine

    Ama kweli, naona sasa yamefika yale ya Bubu atakakusema... kabla ya mstari wa kifo wa CUF wa tarehe 15. Sasa sisi kama watanzania tujiulize
    1. Hivi muafaka wa Zanzibar utapatikana kama kususiana/kutingishana kutaendelea?

    2.Nini matokeo ya CUF kujiondoa katika mazungumzo? Na mpango mkakati wa CUF unasemaje baada ya majadiliano ya mezani kuendelea kusuasua? Hapa hapajatulia

    3. Tutaendlelea kuzungumzia mpasuko wa Zanzibar hadi lini? Gharama jamani, ukisikia vikao vimekaa jua fweza zinaungua

    4. Hivi siasa za zanzibar ni CUF na CCM tu au? Maana hawa jamaa wakishapatana, watazuka wengine kama kawaida

    Baada ya kutafakari kwa kina naona kama vile suluhu ya mpasuko ikipatikana ajenda nyingi za uchaguzi zitakuwa si ajenda tena na hivyo kutazuka ajenda mpya. Hii itakuwa ni ipi? Ni vyema kutafakari na kuibaini mapema. Maana siasa ni wingi wa hoja za nguvu

    adagio

    ReplyDelete
  4. Wanacheka sana wananchi wanalia

    ReplyDelete
  5. Tatizo la mtawala wetu ni kwamba yuko too simplistic. Hana maamuzi yenye uzito. Amekaa chini wee...ameona CUF wamechoka na sanaa ndo anaamua kuja kuwapoza. Man, get life and do what we sent you to do in the state house.

    JK, I voted you into office in 2005, but Iam HIGHLY unlikely to give you my vote come 2010. You have been a disappointment-so far!

    Umeamua kutekwa na haya majangili yenye njaa na uroho (the so called mtandao) maisha bora uliyosema yamekuwa kwa watawala na familia zao the rest of wananchi ni maisha chakavu! Naamini, you are a good person, but you have made me believe, mazoea yana tabu, sidhani kama itatokea nidanganywe na kiongozi wa design yako tena!

    ReplyDelete
  6. Mlipochorwa mkimlamba miguu JK mlikuja juu.Lakini jamaa alichokuwa anakizungumzia ndio mambo kama haya.Wapi toleo rasmi ya Lipumba?Iweje uone hili la JK ni muhimu kuliko lile la Lipumba?Media of any kind is supposed to be balanced Michuzi.You know better than that.Tuwekee pia ripoti ya Lipumba na sio hizi siasa za JK.Mwambie JK kazi za nchi haziendi kwa kukimbilia kweny e vyombo vya habari.Atulie nyumbani asolve mambo kama haya na sio kukimbilia NYC kila kukicha.Nchi inapasuka hiyo..shauri yenu.

    ReplyDelete
  7. Pesa za posho za vikao vya muafaka zikiwa zimeisha kila mtu ana haki ya kuwa ngangari na kujitoa kwenye mazungumzo!

    Kikwete haki ya Mungu Kama hurudishi posho za vikao vya muafaka mimi sirudi kwenye kikao cha muafaka. Heri muafaka ufe.Muafaka gani mtaongea wakati mtu hujala! Si utaishia kupiga miayo tu! Mtu ukishiba ndio unajua uongelee nini!

    Halafu posho ziongezwe,na vikao viwe vingi na tuongee taratibu,kwa muda murefu zaidi.Haraka haraka haina baraka.

    Mtu utaongeaje mambo muhimu kama ya muafaka ukiwa na njaa? Kikwete usinitanie.Usicheke cheke wakati watu tuna njaa.Mtu utaendeleaje na muafaka wakati fungu la pesa za vikao limeisha.

    Rudishia fungu la pesa za vikao mimi nirudi tuongelee muafaka kati yangu,wewe na mama Kikwete na niende niitishe press conference niwaambie wananchi kuwa kutokana na umuhimu wa muafaka kwenye eneo letu tumeonelea ni busara sana turudi tuendelee na mazungumzo.

    ReplyDelete
  8. Michuzi, hatukufundishi kazi ila we real need balanced information. Ukiamua kuandika habari sensitive za kisiasa, jitahidi kutujulisha upande mmoja unasemaje na upande wapili unataka nini.
    Tunajua kuna issue nyingine sensitive ya kusimamishwa kujishughulisha na shughuli za bunge kwa Mhe. Zitto Kabwe, tuwekee hapa wananchi tujadili.

    ReplyDelete
  9. MICHUZI MBONA HUJATOA HABARI ZA KUSIMAMISHWA KWA ZITO KABWE?

    ReplyDelete
  10. KAKA MICHUZI UMENIKASIRISHA SANA, NAPENDA KUKUMBUSHA KUWA BLOG HII SI YAKO PEKEE BALINI YA WANABLOG WOTE NIKIWAMO MIMI, MBONA MABO YA KUKUSOA SEREKARI HUWEKI??? NA KAMA UKIEKA NI YALE YA KIAINA TU. KWA MFANO MWAZO MWA SAKATA LA MWAFAKA MBONA HUJAWEKA TAMKO LA LIPUMBA??? AU SI MUHIMU KWAKO??? ACHA UBINAFSI BLOG NIYETU SOTE. KWANGU MIMI INGEKUA VYEMA KAMA UNGEAANZA NA TAMKO LA LIPUMBA NA HATIMAE UKAMALIZIA NA KIKWETE. ACHA U CCM KAKA KUA NYUTRO

    hajilukamba@hotmail.com

    ReplyDelete
  11. BRAVO MICHU KWELI WEWE NI MATUNDA YA CARDIFF PIHA HIYO NI BAO LAKISIGINO MUAFAKA HAUWEZI KUPATIKANA BILA YA VYAMA HUSIKA KUWA NA DEMOKRASI NDANI YA CHAMA NA SIO MAWAZO AU MATAKWA YA MTU BINAFSI,HAO 2 NI WENYEVITI WASTAAFU CAF BADO WALEWALE,2004 MWENYEKITI ALIWAHI KUTAMKA KATIBU LAZIMA AGOMBEE ZANZIBAR LABDA MIMI NIFE AMAAA!!!!!!!WE MUNGU,MATATIZO YA ZANZIBAR HAYAWEZI KUPATIWA UFUMBUZI BILA CAF KUFANYA UCHAGUZI WA HAKI SAW KWA WOTE NDANI YA CHAMA ILI KUPATA VIONGOZI WAPYA WENYE MAWAZAO NA FIKRA MPYA KWA MASLAHI YA TAIFA,KUJITOA KATIKA MAZUNGUMZO NI HASIRA BAADA YA KAMBIWA UKWELI HAKUNA SERIKALI YA MSETO NA HILO HALIWEZEKANI NA SIO DAWA YA MATAIZO YA ZANZIBAR,KUNA VYAMA VINGI TU ZANZIBAR SIO CCM NA CAF,MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.

    ReplyDelete
  12. Baby M went into Chris Hani-Baragwanath Hospital for a life-saving stomach operation and came out with HIV, which now threatens his life.

    Now, desperately worried about their son's worsening health, Baby M's HIV-negative parents are suing Minister of Health Manto Tshabalala-Msimang, Bara, and the health and blood transfusion authorities for R49-million.

    The potentially landmark claim comes months after Western Cape health authorities reached an undisclosed out-of-court settlement with a couple whose baby daughter was infected with HIV after her stay at two state hospitals.

    She was apparently infected after she was given an HIV-positive woman's expressed breast milk.

    'That is when I knew there had been a f***up'
    The application also follows a report compiled for the Treatment Action Campaign (TAC), which found that infection control, particularly in state hospitals, was largely inadequate.

    Documents filed at the Johannesburg High Court reveal that Baby M was admitted to Bara to undergo surgery for hypertrophic pyloric stenosis, a common infant intestinal complaint, on January 27 2004. He was just four weeks old.


    Exactly six months after the surgery, during which Baby M received a blood transfusion, his father noticed that the infant was losing weight and that there was "lots of white stuff" coming out of his eyes.

    "The doctor gave him medicine and told us to come back if he wasn't better in three days. He didn't get better. Then the doctor said he suspected my son was HIV-positive and that he was showing all the signs of an HIV-positive person.

    "But I wasn't worried because I trust my wife, and I knew that none of us had HIV," the man told The Star on Tuesday.

    'My son is struggling'
    "The same day as the doctor took my son's blood samples, he called us and said my child was HIV-positive, and that my wife and I need to be tested. They tested us three times, but they found no infection.

    "That is when I knew there had been a f***up."

    The man said he was still struggling to cope with what had happened to his second oldest son, who "is sweet and looks just like me".

    "I'm still so angry. No one can know how bad I feel, because I have to be strong for my family, I can't be weak.

    "My son is struggling, especially with his eyes, ears and tonsils, the white stuff comes out of his eyes. I pray before I give him his medicine and I tell him 'You'll be okay, like all the other normal children'."

    Although Baby M's parents launched their legal action nearly a year ago, health authorities have not yet filed a response to the claim.

    The National Blood Transfusion Service on Tuesday successfully applied for the application to be reworded.

    Baby M's parents have until next week to submit the reworded application. Their attorneys have indicated that the couple may go to court to get the child's urgently needed medical care paid for by the state.

    ReplyDelete
  13. Mheshimiwa Rais, nakubaliana na wewe, hii ni nia yako thabiti tangu awali na kwamba "penye nia pana njia." Hivyo basi

    1. Acha kusisitiza sana mambo ya CCM hapa. This is a national, infact an INTERNATIONAL issue of peace to humanity. Any sensible person reading between the lines is inclined to think along those misconceptions of "Bila CCM" "Nia ya CCM" etc. This isnt helpful at this point, we are not singing compaign songs here.

    2. Ningekuwa natoa ushauri kwa nchi tofauti na Tanzania ningesema iundwe kamati independent, prefarably headed by a religious leader, a shaikh or a pastor and some members of the academia who can be fair and balanced. Kwanini nasema ingekuwa nchi tofauti na Tanzania? Soma namba 3

    3. We have no Desmond Tutus among us. Every Desmond Tutu trying to come up anaandamwa na vyombo vya dola mpaka ana surrender. Academia is also another disaster except ofcourse, the late Chachahage RIP who, unfortunately, has not been succeeded so far. Waliopo wote ni bendera fuata upepo and they will support the power that be, no matter what! And why not, kwani hawajifunzi kutokana na yaliyompata Lamwai karibu ageuke Machinga? (There are a few ofcourse who are good, extremely good in writing but only writing, in a foreign language even kwa hiyo kwa mkulima wa Isangya ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa)

    4. Kutokana na sababu 2 na 3 hapo juu, nashauri swala hili lipelekwe Jumuia ya Madola. Hakuna asiyejua utete wa siasa za Zanzibar. Jumuia ya madola ilisha toa tamko na huu ni wakati mzuri wa kuwaomba waingilie kati. I know it is costly but who says peace is cheap?

    5. Nia unayo Rais wangu, ONYESHA KWA VITENDO

    God Bless Tanzania, my beloved country!

    ReplyDelete
  14. Michuzi mie niko nje kidogo ya mada nina swali HIVI website ya IPPMEDIA:COM vipi? hawajaupdate tangia 13 Agosti kwema au mie nachemsha???

    ReplyDelete
  15. ACHA HIZO MICHUZI, NIMETUMA MAONI YANGU LEO SIJAYAONA MPAKA SASA AU NA WEWE NI WALE WALE WANAOSIGN MIKATABA BILA KUPITIWA. ASANTE SANA MKUU KWANI BLOG NI YAKO LAKINI TANZANIA NI YETU, IPO SIKU BUBU ATAONGEA NA MAWE YATATUTETEA. INSHALLAH.

    ReplyDelete
  16. SASA HIVI NAONA IPPMEDIA WANAPATIKANA NAFIKIRI NI MAKOSA YA KIUFUNDI NA UWAJIBIKAJI MBOVU.

    ReplyDelete
  17. Namuonea huruma sana rais wetu Kikwete, infact he is dealing with wrong people. Siasa za Zanzibar whether uwe CCM au CUF ni ngunguri tu, hakuna hata kimoja watakachokubaliana kitatekelezwa. Mimi naamini ili uweze kutatua mgogoro wa zanzibar inabidi uwe dictator sio mazungumzo.Nani kasema CCM Zanzibar wanaweza kushare madaraka na CUF, au nani kasema panaweza kuwa na uchaguzi huru zanzibar? Wenye nchi yao walishasema ''zanzibar ilipatikana kwa kumwaga damu na kamwe haitaondolewa kwa makaratasi'' Kinachonisikitisha ni imani ya rais wetu kwamba anaweza geuza mambo huko, thubutu! niko tayari kucheza kamali katika ilo,mwenye ela zake aweke. Nina uhakika kabisa watakaobadirisha Zanzibar si viongozi wa leo, bali kizazi kijacho ambacho kitaona yanayofanyika huko ni uwendawazimu. Mungu Ibariki Tanzania,

    ReplyDelete
  18. Michuzi nimefuatialia sana masuala ya muafaka na siasa za Zanzibar kwa muda mrefu, tatizo la Zanzibar sio muafaka baina ya CCM na CUF, la hasha, hicho ni kiini macho tu. Suala lililopo hapa ni historia iliyopo kabla na baada ya mapinduzi ya mwaka 1964.
    Hadi leo kuna kundi la watu ndani na nje ya Unguja na Pemba hawakubaliani na lolote, hilo kundi halitakuja kukubaliana hata na muafaka kama utafikiwa (angalia historia ya muafaka uliopita)
    Hili kundi halitaki kukubali kwamba liliondolewa madarakani mwaka 1964 katika mapinduzi.
    Hili kundi halitaki kusamehe licha ya kusahau yaliyopita.
    Hili kundi halijui utaifa maana yake nini zaidi ubinafsi.
    Leo hii wanaitumia CUF na baadhi ya viongozi wake kuendeleza dhamira yao.
    wako tayari kufanya lolote wawezalo kuhakikisha wanaleta hali ya kutoelewana ambayo wanadhani ndiyo itakuwa njia mufaka ya kuwafikisha kule wanakotaka kwenda.
    Uzoefu wangu nilionao juu ya Zanzibar, kabla ya mapinduzi ya Unguja na Pemba, kundi hili ambalo linadai uhalali wa kuwa wao ndio wenye Unguja na Pemba wamekuwa wakiwakandamiza walio wengi wakati huo na kuwaona wao silolote sichochote.
    Leo kama wewe ni GOLO zanzibar utabaki kuwa mtu duni na wakutumiwa na hao ambao sio ma-GOLO.
    Nini kifanyike:
    Hili kundi liendelee kubanwa kuacha mwenendo wao huu.
    Waache kuitumia CUF kama daraja la kuwavusha kwenda wanakotaka.
    Wasiitumie CUF kama chaka la kujifichia.
    Hili kundi ni lazima lifamu kuwa utaifa ndiyo nguzo ya umoja na wala si vinginevyo.
    Mwisho, tungependa ndani ya chama chetu kuwe nn mabadilko ya kweli na wala si ya kuogopana, maana leo hii ukisema ukweli ndani ya CUF unaonekana ni msaliti, ni vema demokrasia ya kweli ikaanzia ndani ya vyama vyetu wenyewe.
    CUF ina viongozi wengi wenye mitazamo itakayo kikwamua chama katika milolongo ya kushindwa na CCM. Na vilevile kuwatumikia wanazazibari wote bila ya ubaguzi.
    Wakatabau

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...