waziri mkuu mh. el akimpa pole waziri wa mawasiliano na uchukuzi wa zenj brigeria jenerali adam mwakanjuki aliyelazwa katika hospitali ya taifa ya muhimbili baada ya kujeruhiwa katika ajali ya gari wiki iliyopita

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. Du pole sana Agnes mwakanjuki kwa kumuuguza baba namtakia Afya njema
    Lizzie

    ReplyDelete
  2. lizzie hata mimi naumwa..uko wapi??ila lizzie wengi mapepe!na wewe pepe pia?lol

    ReplyDelete
  3. kaka Michuzi huyo mzee ni Mwakanjuki na si kama ulivyoandika hapo juu.pole mzee Mawakanjuki!!
    ahsante

    ReplyDelete
  4. Wewe anon wa 9.49 sasa umesahihisha nini? Huyo Mzee ni Adam Mwakanjuki na siyo Mawakanjuki kama ulivyosahihisha!
    Pole Mzee Mwakanjuki Mungu akusaidie upone haraka.

    ReplyDelete
  5. Poleni Mwakanjukis, mungu ampe nguvu baba...ila hizi ajali bongo jamani, mbona zinatisha, naona kila wiki kuna habari ya ajali,anyway, kuomba mungu tu, popote tulipo, ajali haina kinga.

    ReplyDelete
  6. Hapo MOI imani ishaanza kunitoka Regina Luhanga hawakumfanyia uchunguzi vizuri kumbe tumboni alikuwa amedhurika viabaya sana wameshtuka when it was too late. Wenzao ukipatwa na ajali mbaya kama ile wanakuscan kila kitu wajue wapi umedhurika. Pamoja na kuwa ilikuwa mpango wa mungu lakini binadamu wana accelerate mpango wake. RIP best of best

    ReplyDelete
  7. anon wa hapo juu, nakuunga mkono, hata mie sipaamini bwana hapo, ila hawa wakubwa bwana, kalazwa hapo sababu hali si mbaya sana, kesho asubuhi akiamka kazidiwa haongei tu, jioni utasikia keshafikishwa South Africa kwa matibabu....tunakuombea upone baba mzee Mwakanjuki.

    ReplyDelete
  8. Pole ZAZA na MWENZIO mungu awajalie mzee apone.

    ReplyDelete
  9. zaza na Mufinza poleni

    ReplyDelete
  10. Tanzania Shaggy sana...hamna cha mipango ya Mungu wala nini...saa nyingine wanamsaidia Mungu kupanag siku yako...kila siku wanagunduaga kitu late...oh....wakati mgonjwa akilazwa kwanza wangemfanyia Cascan kuangalia kama kuna kitu worng zaidi ya vinavyoonekana.

    Pia hata sijui kuna life support ngapi kwenye facilites zetu....au kila mtu "living will" zao ni do not resuscitate?

    We need to lean how to allocate our money and budgets sio tungojee mpaka watu watupe misaada ya hivyo vyombo.

    Hospital local na ndogo za wenzetu zina vitu vya maana kuliko hospital zetu kuu. Na wala hamna anayewapa misaada na ni vimiji vidogo tu. Inatia aibu...kodi zinaenda wapi

    ReplyDelete
  11. Pole Mzee!!!
    Wakomalie wakupeleke nje ukatibiwe vema.Hapo MOI kasheshe.Na umuombee na yule dada toka TABORA alievimba matende muende wote.Hana wa kumsaidia yule.

    ReplyDelete
  12. WEWE ANONY HAPO JUU UMEMUONGELEA REGINA LUHANGA,NAOMBA UNIJULISHE REGINA AMEKUMBWA NA MASWAIBU GANI MAANA ALIKUWA MSHIKAJI WANGU SANA,NI JIRANI YANGU PALE MBEZI SUPER MARKET,GLITA ROAD

    ReplyDelete
  13. Anony. wa hapo juu, tayali jamaa wameisha mpaisha yuko bondeni sasa hivi. Nyie wakina "Masalakulangwa" ndo mtabaki mnafia Muhimbili.

    ReplyDelete
  14. Pole AFANDE!! Kaka Michu huyu alikuwa mkuu wa kambi (CO) wangu pale Oljoro miaka ya sabini (Operation Usafi) mtu poa sana. Mungu atamsaidia, lakini kama alivyosema mdau mwingine hapo kama akiomba akatibiwe nje basi ampigie ndogo ndogo yule dada yetu wa Tabora mwenye matatizo ya miguu.. (aDk)

    ReplyDelete
  15. Madaktari wa bongo ni njaa zinawafanya wasifikirie vizuri wangelipwa vizuri wangekuwa makini na afya za watu. Nina rafiki yangu walisahau kichuma tumboni kwa miaka saba kimekuja kugundulika kwa mzee bush. alikuwa anaumwa tumbo sana baada ya kukitoa haumwi tena. Waliosahau walimfanyia ultra sound kumthibitishia hakipo kumbe kilikuwa kimejaa tele which means hata ultra sound kwenye hospitali kubwa haka hiyo ya private havifanyikazi. Imagine ni watu wangapi wamekufa kwa uzembe wa watu wengine na wale wasio na uwezo ndio kabisaaa

    ReplyDelete
  16. Pole sana Mzee Mwakyanjuki. Poleni sana Mufinza na Zaza.

    Lakini Mungu yupo, Mzee atapona na kuwa mchangamfu kama siku zote.

    ReplyDelete
  17. Pole Chegevara, Aliko, Agnes na Dada Reheman najua mna wakati mgumu kumuuguza Mzee. Niko nanyi katika maombi, I wish Mzee a quick recovery,
    Jirani wa zamani Mbeya,

    ReplyDelete
  18. anony unayeuliza kuhusu regina luhanga amezikwa jana baada ya kupata ajali ya gari baada ya 8 days ndio wakagundua utumbo ulipasuka mwenzake aliye kuwa naye alifariki palepale ester maruma mbona announcement ya msiba wake imeandikwa humuhumu mpendwa?

    ReplyDelete
  19. Nikiwa nampa pole Brigedia Jenerali Mwakanjuki, na kumuombea kwa Mungu apone haraka na kuendelea na kazi, natoa wito kwa Wadanganyika wenzangu, kuwa nasi tujenge hospitali yetu nzuri ama tuboreshe zilizopo ili tutoe hii aibu ya kupeleka wagonjwa wetu nje ya nchi hata kwa magonjwa yanayoweza kutibika hapa hapa nyumbani. Mjumbe hauwawi, nadhani tumeelewana, bila shaka ujumbe huu utamfikia Mzee wa mvi EL hapo juu. Mungu Ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  20. Hivi huu msemp "ajali haina kinga" bado unanafasi katika dunia ya sasa kweli??. Kila kitu bongo kina kinasababishwa ba kitu kimoja kikubwa "RUSHWA" nina sababu za kusema hivyo.
    1. Sheria za barabarani hazisimamiwi ipasavyo na hata mtu akivunja anakata kitu kidogo yanaisha.

    2. Ujenzi wa miundo mbinu umejaa utata, hela inatumika nyingi ila barabara hazina ubora unaotakiwa kwa usalama, Mfano siku hizi barabara nyingi kuu duniani ni "2-way, 2-lane", Nina maanisha 2 zinaenda upande huu 2 upande huu mfano Ubungo-Mlandizi. Ilitakiwa iwehivyo mpaka arusha, tanga, moro na kwingineko.

    3. Nimekaa hapa scotland barabara nyingi za mitaani ni finyu ila sijaona Pass wala kuchomekea hata siku moja, watu wanadiscipline, kwanini na sisi bongo tusianzishe usimamizi madhubuti wa sheria, hapo ni kitu sheria tu, overspeeding n.k.

    4. Tabia ya kuthamini maisha: Bongo watu hawathamini maisha unakuta mtu anamchomekea mwenzake kama ni mchezo mdogo tu. Mtu anaona mpita njia anavuka hachukui tahadhari hata kidogo kwa kisingizio "analiona".

    Ajali kwa kweli tunaweza kuzikinga na kuzipunguza kabisa, Mtu akivunja sheria ashughulikiwe na hakuna mtoto wa kigogo au wa kimara. Hivi serikali ingewekeza kwenye kufunga camera za barabarani hasa miji kama dar, na kufuatilia wale wote wanaovunja sheria na kuwanyang'anya leseni na kifungo watu wangejua umuhimu wa kudrive safely.

    Tatizo ya nchi zinazoendelea wanachukulia matatizo haya kama mtaji wa kupata hela toka kwa wahisani, accident rates kubwa tunaomba misaada ya kuboresha miundombinu, inaishia mifukoni mwa wajanja. Kweli mtu ukiwa huku kwa wengine wanaojua utawala wa sheria, hakuna la ziada ila ni kuwa-condition watu waone kuvunja sheria ni kama ukikutwa unajisaidia haja kubwa sokoni, yaani aibu.

    Niishie hapo ila inasikitisha sana basi tu sijui ndio umasikini, ila sidhani ni RUSHWA tu inawapa watu kiburi, kwamba nikaharibu ntatumia pesa kusawazisha

    ReplyDelete
  21. Mwakanjuki sent to South Africa for treatment
    ISSA YUSSUF, Zanzibar
    Daily News; Tuesday,August 14, 2007 @00:01
    ZANZIBAR’s Minister for Communications Brigadier (Retired) Adam Mwankanjuki, has been admitted to the Milpark Hospital here for further treatment.

    According to an official in the Chief Minister’s office, Mr Mwakanjuki, the Zanzibar Minister for Communications, was flown to South Africa on Saturday.

    The official said the Isles Chief Minister Mr Shamsi Vuai Nahodha and other leaders visited Mr Mwakanjuki at the Muhimbili National Hospital.

    Mr Mwakanjuki, accompanied by his son, was seriously injured when his car had a tyre burst and rolled over several times at Wami-Sokoine area, about 40-km from Morogoro, on his way from to Dar es Salaam from Dodoma.

    Mr Mwakanjuki’s son and the driver were also injured in the accident and are admitted to the MNH. Their condition is improving.

    Meanwhile, the Principal Secretary (PS), Ministry of Regional Administration and Isles Security Units, Mr Hassan Wambi has also been taken to India for further treatment.

    ReplyDelete
  22. Duh! Jamani kuna nini mwezi huu wa nane. Ehe! Mola tuepushie hizi ajali. Tulilalamikia mabasi sasa hata magari yetu binafsi yanatumaliza. Mungu awape nguvu majeruhi.

    ReplyDelete
  23. Mi sijui ni semeje, kwajinsi ninavyoumia roho kwa Nchi yangu Tanzania.
    Yahani hatupo serious hata kwa kitu kimoja.
    Ndio maana pesa yetu inashuka kila siku na uchumi kudidimia , inaniuma sana.
    Yahani hata kutibu wagonjwa tunashindwa , sasa tunaweza nini?.
    Tanzania Nchi yangu.
    Na hii usitoe.

    ReplyDelete
  24. REJEENI UJUMBE WANGU WA TAREHE AUGUST 12, 11:18 HAPO JUU, MI SI NILISEMA , MZEE AKIAMKA HALI IMEBADILIKA KIDOGO TU, MTASIKIA YUKO SOUTH AFRICA, SI MNAONA? HII BONGO HII BWANA,,,MI BORA NIBAKIE ULAYA NISAFISHE VYOO VYA WAZUNGU, JAPO NALIPWA PESA YANGU KWA HAKI NA KODI NAKATWA KWA HAKI, NA HUDUMA MUHIMU NAZIPATA..HAPANA JAMANI, YAANI KAMA VILE NILIOTEA, HAYA MZEE HUYO ANATIBIWA SOUTH,WENZANGU NA MIE TUNATESEKA NA TUNAFIA BONGO.

    ReplyDelete
  25. anony hapo juu ester maruma kafariki?????????????? ester yupi???wa moshi?? yule mwenye mdogo anaitwa malkia na elionora?? au ester yupi jamani???

    ReplyDelete
  26. anon wa hapo juu, Esher maruma wa arusha huko, babake ana law firm huko, yeye mwenyewe nahisi alisoma Law, walipata ajali mbaya, hemu search habari za Michuzi mwanzo wa mwezi huu, nadhani utaiona na photo yake, au muombea michuzi akutumie kama huipati.

    ReplyDelete
  27. Anonymous wa August 14,2007 10:48:00 PM EAT
    Ni kweli dear Ester huyo huyo. Amefariki tarehe 1 August na tumemzika tarehe 3 August. Inasikitisha sana kwani hata rafiki yake mpendwa Regina Luhanga waliokuwa wakisafiri pamoja kwenye gari yao binafsi naye amefariki. Ni ajali ya gari pale Mombo. Pole sana kwa kutopata taarifa mapema lakini Michuzi aliweka picha zao humu kwa taarifa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...