mbunifu wa mitindo ya mavazi hadija mwanamboka akiongelea leo kuhusu uzinduzi wa taasisi iitwayo 'tanzania mitindo house' ambayo itakuwa inashughulika na ukuzaji wa fani hiyo na kusaidia wenye shida kwa njia ya maonesho ya hisani. onesho la kwanza la taasisi hiyo itafanyika jumapili hii katika ukumbi wa coco beach ambapo wabunifu kadhaa wataonesha mitindo waliyobuni. wabunifu hao ni pamoja na jamila swai, haji mohamed, fatma amour, cynthia mosha, henry singano, masoud kipanya, francisca shirima na hadija mwenyewe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Great idea..keep it up guys

    ReplyDelete
  2. ohh i wish ningekuwepo jamani michuzi lol!!!,,, hao watu wanatisha ila kitu kimoja tukumbuke kupendana na kila mnachopanga mtafanikiwa.msije mkatoka hapo coco beach kisha mkaanza fitna maana wabongo ndo zetu hizo.ila mmejipanga fresh masoud big up brother luv ya.

    ReplyDelete
  3. Issa kwanini huyu dada haitwi Khadija washokera, au sababu baba yake mzee mwanamboka anapesa ndio kaolewa na jina lake?

    ReplyDelete
  4. Duh anony wa 8:52:00 kidogo inaonekana una mambo ya ki-longtime wangu. Umezoea mwanamke akiolewa basi mara moja na jina kabadili sio?? duh, pole ndugu yangu. siku hizi watu wamesoma na wanajulikana kimataifa na majina yao sasa leo wewe ulikuwa unaitwa Mwajuma Mwalufuruku eti umeolewa mumeo anaitwa Abdallah mpungudu eti na jina ubadili kesho yake, waaapi mpaka umalize lipia "deed poll" ya vyeti na kurudisha umaarufu wako sio muda mfupi....

    anyways, dada Mwanamboka ujiitege jina lolote dada yangu achana na msukutua kinywa mchovu wa kusema eti ubadili jina wewe tesaga ndugu yangu.....

    Mungu Ibariki Tanzania na watu wake....

    ReplyDelete
  5. Sio mimi niliyetuma hayo maoni ya Hadija Mwanamboka kuitwa Hadija Washokera lakini siamini kwamba kumpinga mtu hoja yake ni mpaka useme ana mambo ya kizamani au vipi. Mimi mke wangu anatumia la kwao kwa sababu hatujaona umuhimu wa kubadirisha. Lakini pia kubadirisha sio mbaya, na wala sio uzamani. Kama ni uzamani, basi tutasema Mellinda Gates bado ana uzamani, au Laura Bush, na yule anayejiandaa kugombea Urais Marekani Hillary Clinton, wote watakuwa washamba. Ni maamuzi tu ndugu zangu.Ozzie!

    ReplyDelete
  6. Laura Bush Hillary Clinton na wengio hapo juu waliolewa zamani.
    Hata hivyo kubadili jina la pili kutoka lile la usichana kwenda kwenye lile la mume ni maamuzi binafsi kwa baadhi ya nchi na kwa zingine ni muhimu.

    ReplyDelete
  7. Swali langu kwa Bi.Mwanamboka;je hata wabongo waishio nje wanaweza shiriki au ordha imejaa kwa sasa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...