Ndugu, karibu kwenye blogu yangu www.ngurumo.blogspot.com kuna maswali yako; nauliza kujibiwa. Kama utaona huko ni mbali, tafadhari yaone hapa chini.
Naomba ushiriki wako kwa kujibu maswali yafuatayo kwa kadiri unavyoona inafaa. Nakuhakikishia kwamba nitakapohitaji kutumia mawazo yako mahali popote, nitakunuu bila kuongeza chumvi. Asante.
1. Kama wewe ni mwanablogu, kwa nini unablogu? Kama si mwanablogu, kwanini unasoma blogu?
2. Je, ni vema wanablogu (na wachangiaji wa maoni) watumie majina yao halisi? Faida na hasara zake ni nini?
3. Je, matumizi makubwa ya blogu yanamaanisha enzi za vyombo vya habari vya kale (redio, magazeti na TV) vimepitwa na wakati?
4. Je, wanablogu wanawajibika kwa nani?
Ansbert Ngurumo
The University of Hull
Tel:+44 7828696142
United Kingdom


Mimi sikujibu NG'O kwani najua majibu unayo na unayafahamu na najua umejiandaa ku-challenge vipi.
ReplyDeleteMajita.
Hayo ndio majibu yangu
ReplyDelete1. Personal I used to blog lakini nimeacha siku hizi na niliblog as a school project. Ninasoma tu blog ya muchuzi kwa up to minute news za home.
2. Kuandika jina au kutoandika ni uamuzi wa mtu wengine wana prefer privacy lakini maoni atakayosema hayanatofauti sana kama angeandika akitumia jina lake kamili au la. Na pia mtu anaweza kufungua account na kusign in lakini ukweli hilo sio jina lake kamili.
3. Faida za kuwa anonymous ni kuwa mtu anaongea yote kutoka moyoni bila kuona aibu. Hamna hasara kwa vile mwenye blog ana last saying ya kuondoa maoni kama hayapendi na yenye matusi.
4. Matumizi ya blog hayamaanishi kabisa au hayatachukua nafasi ya habari kabisa kwa vile sio watu wote wana access ya internet. Na walionazo sio wengi wanapenda kusoma habari kupitia kwa PC. Na pia muda wa kusoma habari kupitia internet yaani blogs ni mwingi kuliko kusikiliza kwenye radio. Kwa hiyo watu wengi huwa wanatumia blog kusoma habari za kimataifa. Lakini local newa huwezi ukategemea blogs.
5. Kuwa na blog ni hobby tu hamna kinachowafanya kuwajibika zaidi ni kama vile ukiwa na mbwa au samaki. Jinsi ya kutunza vitu hivi nchi za nje ni gharama sana lakini kama ni hobby yako hutajali gharama yake. Kwa vile faida ni furaha yako. Huwa unazifanya kutokana na moyo wako na watu wakija nyumbani kwako wakiona fish tank lako au mbwa wako amependeza wakikusifia na kukupa hongera furaha unayoipata ndio hivyo kama ya wanablog. Na ndio maana kwa vile ni hobby unaona kila kukicha toka blog zilivyoanzaga ni ngapi zimeshapotea. Wasio na hobby hii uwe mwandishi wa habari au uwe unablog mambo mengine kama hupendi haitalast na utaiachia mbali hata ukisifiwa vipi.
6. Na sasa hivi popular things ni broadcasting au podcasting. Youtube ndio the next big thing kwa sasa. Kwa hiyo nayo kwa vile ni hobby hata hivyo watu wenye kupenda kukaa mbele ya kamera au wanaopenda kuongea tu ndio watafany ahivyo. Ndio maana sio wote wanaopenda kublog wameshift kwenye podcasting or youtube.
1.Binafsi ninablogu kwa sababu kuu tatu.Moja,napendea kuwasiliana na jamii kwa njia hiyo (blogging).Siwezi kutuma barua yenye mawazo au mtazamo wangu kwa kila mwanajamii ulimwenguni.Blogu yangu inanisaidia sana kurahisisha azma hiyo.Pia katika njia hiyo ya mawasiliano iliyorahisishwa na teknolojia ya mtandao,nanufaika na comments ambazo nyingi ni darasa kubwa pengine zaidi ya kuhudhuria taasisi ya elimu.Pili,napendelea kuandika (iwe e-mail,shairi,barua,nk).Kwa vile blogging inahusisha kuandika (japo si kwa mkono),moja kwa moja imetokea kuwa ni miongoni mwa hobbies/interests zangu.Tatu,ninaandika makala kwenye gazeti moja la huko nyumbani,na blogu yangi inatumika kama kumbukumbu (archive) ya makala zangu zinazotoka kwenye gazeti hilo.
ReplyDelete2.Nadhani ni vema,japo si lazima,kwa mwanablogu kutumia jina halisi.Nilisoma mahala flani ambapo jamaa mmoja alikuwa akiandika makala za "diary" ya Steve Job wa Apple,ilhali yeye sio Steve.Imechukua muda mrefu kwa jamaa huyu kubainika (hakuchukuliwa hatua) lakini kwa namna flani wapo waliomwona mtu huyo kama si mwadilifu japokuwa alichokuwa akiandika kilikuwa kikiwavutia wengi.Inapendeza kumjua mtenda kitu (hasa kikiwa cha manufaa),na inasaidia urahisi wa mawasiliano ya njia-mbili (interactivity) kati ya bloga na hadhira yake.Kwa mtoa maoni,kutumia jina halisi kunamwezesha bloga kuwasiliana nae (mtoa maoni) kirahisi.Kwa kutoweka jina lake,mtoa maoni anajinyima fursa ya kupewa majibu au feedback kuhusu maoni yake,japo bloga anaweza kufanya hivyo kwenye sehemu ya comments.Hata hivyo,kutoweka jina hakuathiri ubora wa maoni ya mtoaji alimradi kutoweka jina huko hakufanywi kwa sababu ya kutoa maoni yasiyofaa (eg matusi).
3.Kwa mtazamo wangu,blog ina nafasi ya pekee katika sekta ya mawasiliano lakini haifuti umuhimu na nafasi ya nyenzo nyingine za habari kama runinga,radio na magazeti.Nyingi ya nyezo hizo za "asili" zinaendeshwa kitaasisi zaidi tofauti na blogu nyingi zinazoendeshwa kibinafsi zaidi (kwa maana ya mtu mmoja mmoja),lakini hilo pia linaweza kuwa na faida hasa pale taasisi ya mawasiliano inapopandikiza matakwa yake watendaji wa taasisi husika.Ni kama barua pepe zisivyoweza kupoteza kabisa uuhimu na nafasi ya barua "za kawaida."Pia blogu zinaathiriwa zaidi na ukweli kwamba hadhira yake kubwa ni watu wenye kufahamu na/au wenye access ya teknolojia ya mtandao,na kwa hali hiyo inawatenga zaidi wale ambao hawana access kwenye teknolojia hiyo,mfano vijijini.Lakini radio,na runinga kwa kiasi flani,imeendelea kuwa nyenzo muhimu ya mawasiliano hata kwa wale wasiojua kusoma.Magazeti yana hadhira ya watu wanaojua kusoma lakini ukiachilia mbali suala la bei,yanapatikana kirahisi.Hata hivyo,blogu kwa mfano ile ya mjengwa,inaweza kuwa nyenzo muhimu katika maeneo ambayo radio zinasikika,runinga zinaonekana na magazeti yanafika,lakini nyenzo hizo tatu hazina makazi/kituo mahala husika.Ironically,wakati blogu inaweza kutoa habari ambazo pengine ni vigumu kupatikana kwa nyenzo "asilia" za habari,wadau wa eneo husika wanaweza kuwa hawanufaiki (kwa maana ya kuziona habari hizo) kutokana na kukosa teknolojia ya mtandao.Kingine ni athari za subjectivity ya bloga.Ni rahisi kwa umma usiokwenda mbali zaidi kuchungiza mantiki ya habari,kuamini gazeti,radio au tv kuliko blogu kutokana na imani (inayoweza kuwa sahihi) kuwa blogu ni mawazo na utashi wa bloga.Hilo linaweza kuepukwa kwa bloga kuwa objective katika anachokiweka humo japo sote twafahamu kwamba hakuna kitu kama absolute objectivity.
4.Bloga anawajibika zaidi kwa hadhira yake,maana kama ingekuwa ni suala la kujifurahisha yeye mwenyewe basi angejiandikia yeye mwenyewe.Ieleweke kuwa kuwajibika kwa hadhira hakumaanishi kuifanya blogu iwe ya kuridhisha tu ahadhira hata pale inapopaswa kukosolewa.Pia bloga anawajibika kwake mwenyewe kwani kwa kuwa na sense of responsibility,anajiongezea heshima na kuaminika machoni kwa hadhira yake.Tukiwajumuisha watoa maoni katika swali hili,nadhani wao wanawajibika kwao binafsi (eg pale wanapotoa comments zinazohitaji ufafanuzi) lakini pia wanawajibika kwa jamii.Ni kama vile kupata fursa ya kutoa maoni mkutanoni kisha kutoitumia vizuri fursa hiyo.
Naomba kusisitiza kuwa huo ni mtazamo wangu binafsi,na yeyote yuko huru kunikosoa.
Kabla sijakujibu maswali yako, kwanza niambie unasomea nini hapo Univesiti of Hal. IT?
ReplyDeleteKama ni IT sikujibu inawezekana unafanya unaandika risech pepa au dizatesheni, sasa sisi ndo unatufanya think tanks wako, wakati digrii unaipata wewe. Wacheni hizo! Mweeh!
Perez ama kweli una roho ya korosho.Kumsaidia mwenzako kimawazo tu unaonyesha uchoyo wa hali ya juu.Ni sawa na mbwa kumfukuza mbuzi kwenye majani na majani yenyewe hawezi kula.Acha roho mbaya.
ReplyDeleteperez ndio wale walikua hawatoi hata past papers wakijua utawashinda. hutaendelea ng'o wengine watakuacha hapo hapo....kiakili, mawazo na maisha....watch out my dear...kama bado wewe ni mtoto I hope utaweza kuchange hako katabia...kama wewe ni mtu mzima I feel so sorry for you
ReplyDeleteMa-anony wa 2 hapo juu.
ReplyDeleteHata mimi nilivyokuwa chuoni(sitakitaja) kulikuwa kuna KABILA fulani likisifika sana kwa kuunda grup diskashens za watu wa kabila lao tu (silitaji) ili wawanyime wenzao waiokuwa kabila hilo wasiweze kupata matirio wanaliyokuwa wana diskas.
Diskasheni yao ngoja niwamegee kidogo, ilikuwa kama hivi:-
"Nyerere na Marx wagamba the same, but Angels agamba critique".
Kwa hiyo kama niko hivyo kweli, mimi sio wa kwanza!