NIMEPATA MASWALI MENGI TOKA KWA WADAU DUNIA NZIMA WAKIULIZIA JUU YA MOHAMED MPAKANJIA, MGANE (MWANAMKE NI MJANE, UPO HAPO?) WA AMINA CHIFUPA ALIYEFARIKI JUNE 26 MWAKA HUU. NIMEONGEA NA MTU WA KARIBU WA MPAKANJIA, MH. KEPTENI JOHN KOMBA KIASI CHA NUSU SAA ILOPITA NA AMEKANUSHA UVUMI KWAMBA MEDI MPAKANJIA AMEFARIKI DUNIA.
"SI KWELI, NI UWONGO..." ALINIJIBU MH. KOMBA HATA KABLA YA KUMWAMBIA SHIDA YA KUMPIGIA, IKIASHIRIA HIYO HAIKUWA SIMU YA KWANZA KUPIGIWA.
"NI KWELI MEDI MPAKANJIA AMELAZWA HOSPITALI YA JESHI LUGALO LAKINI ANAENDELEA VIZURI NA MATIBABU NA SI KWELI KAMA AMEFARIKI DUNIA"' ALINIELEZA.
HAKUSEMA AMELAZWA ANAUMWA NINI, NA UVUMI HUU UMEENEA ZAIDI HASA BAAD YA GAZETI MOJA LA MCHANA KUNADI KWAMBA MPAKANJIA AMEPATWA NA UGONJWA ULIOMFIKA MAREHEMU AMINA.
WADAU MSIWE NA WASI, NAENDELEA KUFUATILIA KWA KARIBU HAYA NA MENGINEYO. KAMA KAWAIDA NYIE NDO MTAKUWA WA KWANZA KUJUA KATIKA MAMBO YA BREKING NYUUUUUUZZZZ

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. asante sana bwana michuzi wabongo kwa uzushi mshhhhhhhhhhhhhhi mimi nimeambiwa watu wameenda kwenye msiba northampron wa medi kumbe uongo mungu mpe maisha marefu baba wa watu

    ReplyDelete
  2. Michu huyo Komba si msemaji wa familia. Ok tusubiri update kutoka katika familia. Ila kama ni uongo namuombea ahueni mapema maana itakuwa hapatoshi na huzuni tele na mkanganyiko maana amina trh 26 june sasa yeye iwe 25Aug yaani miezi 2 tu kweli, mungu amuepushe na huu uvumi

    ReplyDelete
  3. michuzi unapofuatilia please fuatilia ni nini pia kilichowapata wenzetu hawa Amina na Meddy isije kuwa ni yula mzee wa kigamboni???(unaukumbuka mkwara wake baada ya kudai mwanae aliolewa na Meddy)

    ReplyDelete
  4. Namuunga mkono Anon wa pili. Kama Komba ni msemaji wa familia, wadau hatuna neno, kama sio basi Misupu utakuwa umechemsha kwa kwenda mbele. Inabidi umtafute ndugu wa karibu wa familia na kuulizia nyeti kama hizi na sio mtu wa karibu wa familia. Ikibidi uende pale Lugalo na kujionea mwenyewe, then utupe updates

    ReplyDelete
  5. Jamani mbona sisi nasi tumepata hizo hizo habari kuwa Mgane wa Amina Chifupa amefariki dunia! Hebu Michuzi fuatilia kwa makini hili swala kwa familia ya Mpakanjia, maana nasi hizo habari tumezipata toka Lugalo hospital! Then tujue ni nini jamani kinachowapeleka wenzetu haraka hivyo!!!

    ReplyDelete
  6. Is it serious? Jamani mbona inatisha sana hebu tusubiri ukweli toka kwa Michuzi!

    ReplyDelete
  7. Ah! ndala kasheba alishaimba zamani sana katika wimbo wake maarufu wa "Dunia msongamano kasema baba"

    ReplyDelete
  8. Mbona habari za magazeti zinapingana na za Komba


    http://www.ippmedia.com/ipp/alasiri/2007/08/25/97093.html

    http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/8/25/habari3.php

    ReplyDelete
  9. KAKA MICHUZI FANYA FASTA NDUGUYANGU FUATILIA MAANA NIMEPOKEA SMS KIBAO KWAMBA MEDI KATANGULIA MBELE YA HAKI.KAMA NI UZUSHI INSHAALAHA TUNAMUOMBEA UZIMA MWENYEZI MUNGU AMPATIE NGUVU AWEZE KUREJEA KATIKA MAJUKUMU YAKE.MZALENDO

    ReplyDelete
  10. KAKA MICHUZI FANYA FASTA NDUGUYANGU FUATILIA MAANA NIMEPOKEA SMS KIBAO KWAMBA MEDI KATANGULIA MBELE YA HAKI.KAMA NI UZUSHI INSHAALAHA TUNAMUOMBEA UZIMA MWENYEZI MUNGU AMPATIE NGUVU AWEZE KUREJEA KATIKA MAJUKUMU YAKE.MZALENDO

    ReplyDelete
  11. Wampeleke nje akatibiwe. Haya mambo ya kuamini ushirikina yatampoteza na baba wa watu. Hata kama ni miwaya ...USA watu wanakanya miwaya na wanaishi tu na hata maini wanapewa mapya.

    Kama anahela yake jamani ndugu zake mpelekeni nje akatibiwe..msimlaze tu hapo Lugalo halafu muanze kugombania mali yake.

    Kumbukeni ana mtoto mdogo na mtoto anahitaji baba yake jamani...mweee dunia hii...

    ReplyDelete
  12. amina wakati anafariki hakuwa na mume, so huyo mgane katokea wapi tena? acha uzushi michuzi, huyo bwana alimpa talaka mkewe

    ReplyDelete
  13. Hali ya afya ya Mpakanjia si shwari

    2007-08-25 19:21:22
    Na Mwandishi wetu, Jijini


    Kuna taarifa kuwa mfanyabiashara maarufu wa Jijini Dar es Salaam, Mohamed Mpakanjia amekumbwa na kile kile kilichomuua mkewe, marehemu Amina Chifupa.

    Baadhi ya watu walio karibu na familia hiyo wamelidokeza gazeti hili kwamba dalili alizokuwa nazo marehemu Amina siku za mwanzo za ugonjwa wake, tayari zimeanza kuonekana kwa mumewe.

    Baadhi ya watu wamedai kuwa kutokana na hali yake kutoridhisha, sasa Mpakanjia kalazwa katika Hospitali Kuu ya Jeshi iliyopo Lugalo Jijini.

    Amesema namna ya ugonjwa unaomsumbua Mpakanjia ulivyo ni fumbo linalowashangaza hata wao, hasa kutokana na ukweli kuwa dalili za ugonjwa wenyewe ni kama zile alizowahi kuwa nazo mkewe, marehemu Amina Chifupa.

    ``Hali yake si nzuri. Hivi sasa, hata anachokizungumza hakieleweki� amedhoofu mno na hata kusimama mwenyewe hawezi. Kwakweli anasikitisha sana,`` akasema ndugu huyo.

    Dalili kama hizo pia zililipotiwa kujitokeza kwa aliyekuwa mkewe, marehemu Amina Chifupa, ambaye alifariki dunia Juni 26 mwaka huu katika hospitali hiyo hiyo ya Lugalo.

    Kabla ya kifo chake, marehemu Amina aliripotiwa kuzungumza mambo yasiyoeleweka na mwili wake kudhoofu kiasi cha kushindwa kuinuka.

    Baadhi ya ndugu wa mfanyabiashara huyo wamedai Bw. Mpakanjia alilazwa hospitalini hapo mwanzoni mwa wiki hii.

    Akizungumzia kile kinachomsibu Mpakanjia, ndugu mmoja wa mfanyabiashara huyo amesema mgonjwa wao hivi sasa ana hali mbaya na kwamba hata kula kwa mikono yake hawezi.

    Amesema amewekewa mirija kwa ajili ya kumsaidia huku madakitari wakijitahidi kumhudumia.

    ReplyDelete
  14. Bro michu fatilia hizo habari kwa makini sababu zinatuchanganya vichwa...Hatuna la kufanya ni kumuomba mungu apitishe shani yake.lakini kama kuna mkono wa mtu nae ana hukumu kubwa mbele ya mola kulivyo alivyowahukumu Amina na Meddy..rabi mpe shufaa Inshaaalah

    ReplyDelete
  15. Ah midomo ya wabongo sio mizuri kabisa. Nakumbuka watu maarufu wote waliowahi kuzushiwa magazetini kuwa wamekufa hawakukaa sana wakaondoka kweli siku chache tu baadae.

    Ee Mola muepushia Mja wako hili balaa la midomo michafu. Mapenzi yako yatimizwe.

    ReplyDelete
  16. kaka michu mbona hizi habari zinatatanisha maana watu wamepata wapi kuwa meddy ameshavuta mungu amjalie apone kama ni uzushi

    ReplyDelete
  17. Wabongo nao yaani Who is Mpakanjia anyway? Yaani Michuzi ndo nimegundua IQ yako ni ndogo kabisa, vitu vya maana huwekagi kwenye blog lakini ikifika wakati wa udaku ndo namba moja. Nafikiri Mpakanjia is not much famous kama Michuzi unavyotaka kumfanya. Lete serious hoja watu wadiscuss sio udaku bro.

    ReplyDelete
  18. Issah isije ikawa taaaaaaaaaaaabu sana kuugua kwake, ukaacha na kutupa tori nyingine, kama anaumwa anaumwa tu na kama mzima poa tu kwani mwenyezi mungu ndo anapanga, watu tusije acha yetu tukaanza kwa sana kufuatilia ya Meddy ,ila mungu ampe ahueni na au la apone kabisa kama yu mgonjwa,

    ReplyDelete
  19. wadau, medy anaumwa lkn hajafa, kuweni wapole...na medy si mgane wa amina coz alimpa talaka 3...biashara iliisha kitambo kilichokuwa kinaendelea ni yale mambo ya mzazi mwenzangu..hatuombei medy afe japo kuna wa2 wanapakaza yeye ndie chanzo cha kifo cha ac...tutapata nini kwa maombezi yasiyo na faida kwa yeyote beside mzee gabriel chifupa amechukulia kama mipango ya mungu japo kuna kipindi walidata wa kasema amina alilogwa...siyo isue lkn

    ReplyDelete
  20. wewe anoni uliyetangulia unanishangaza kwa kweli hasa unaposema kufa kwa chifupa ni mipango ya mungu
    hivi ni kweli mungu huwa anafanya mipango ya kuua watu ?
    au unasema tuu bila kutafakari kwa kina kabla ya kusema

    ReplyDelete
  21. kuna mtu hapo juu amesema kua Michuzi ana IQ ndogo sana, sasa kama wewe una IQ nyingi sanaaaa unatafuta nini kwenye blog ya mtu mwenye IQ ndogo? kwani umelazimishwa kusoma hii blog? acha dharau, Michuzi anajitolea kuwaletea habari, wengine mnatukana bila sababu.
    Michuzi endelea na kuleta habari zote utakazozipata, usiwasikilize watu kama hao.

    ReplyDelete
  22. Dear Anna
    Asante kwa kumjibu huyo anoy anaye mwona Michuzi ana IQ ndogo. yeye binafsi mchango wake ni upi.Bro michuzi Mpumbavu ni mpumbavu haijalishi amepita darasani au la,darasani tunafuta ujinga .Kwa hiyo huyo annoy kama alipita darasani alichofuta ni ujinga hayamkini upumbavu bado anao. tunakushukuru kwa mchango wako tuletee na taarifa za Kabwe na Bwana Sitta.

    ReplyDelete
  23. michuzi achana na story za hao wapumbafu hapo juu mimi mbona mpakanjia alinirusha juzi juzi tu nilipotoka ughaibuni lakini nimepima ngoma sina kumbe ni stotry za wakosaji,wivu tu wanamwonea huyu baba!

    ReplyDelete
  24. Watanzania kwa umbea, hata wasomi, waandishi wetu wa habari, woooote. khaaa!. Mpakanjia awe mgonjwa au la linamhusu nani? yaani ili mradi watu waseme ahh kumbe kweli mkewe alikufa na ukimwi na kama ni hivyo ni watu wa kwanza? mbona hapa tulipo kila mmoja wetu kaguswa na kifo kwenye family via aids. Kifo cha mtu ni siri ya Mungu hata kama diagnostic inasema ...sijui nini kila mtu atakufa kwa njia yake na hakuna atakae chagua...(labda ujitundike)
    Tafuteni kujua mambo ya nchi lkn sio private life za watu.

    Watu mnaosha vinywa kiasi mambacho siku yanakupata wewe unaona haya unakufa kimyakimya

    Mungu ibariki tz hasa watu wake watoke kwenye umbea, wivu, woga, unafiki, nk

    ReplyDelete
  25. i fully support annon. wa 04:03...let us not discuss watu, let us discuss events...let us leave alone mpakanjia...kila mtu ana yake...mpakanjia wee mpakanjia

    ReplyDelete
  26. kwenye gazeti la SANI la jumamosi waliweka picha ya John Komba ana Mpakanjia. wameonesha Mpakanjia ameenda kumuomba msamaha baba mkwe wake wa Kiagamboni yule wa kiarabu. Ina maana ni kweli alimuoa yule binti wa kiarabu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...