
chama cha demokrasia na maendeleo a.k.a chadema mchana huu kimetoa tamko kupinga kufungiwa kwa mbunge wake mh. zitto kabwe kwa madai ya kukiuka kanuni za bunge kufuatia hoja yake binafsi kuhusu kusainiwa mkataba wa madini na waziri karamagi huko ughaibuni hivi karibuni. habari kamili za sakata la zitto kabwe linapatikana katika linki hizo hapo chini. wadau awali ya yote naomba radhi kwa kuchelewa kuipandisha topiki hii moto kutokana na kutingwa na shughuli za kikazi. hivyo nafungua mjadala....
tsn.com/habarileo/page.php?id=3432


Vipi sera za uwazi zimeishia wapi? Kama Bunge na serikali vinataka kuwa na ari, kasi na nguvu mpya lazima vikubali kukosolewa na sio kutumia ubabe wa kuwanyamanzisha wale wanaosema ukweli
ReplyDeletemichuzi ulitakiwa kututumia habari za tamko rasmi la chadema mara baada ya zito kusimamishwa na sio hizi za kusimamishwa sio breaking news tena hizo tunazo.
ReplyDeleteTuambie Chadema wamesema nini, basi
1. Nafikiri CHADEMA isingepinga uamuzi wa Spika, in any case, it is upon the parliament kutengua uamuzi wowote uliojiwekea. Doctrines of Separation of powers and independence of the legislator teaches us so. Siasa za vyama, kimsingi, havipaswi kuvuka mipaka na kuingilia maamuzi ya bunge. More importantly, CHADEMA should let the public sympathize with Kabwe. Wananchi wamuone akitumikia adhabu waone unyenyekevu wake, nao wataamua. CHADEMA isimnyime Kabwe fursa hii muhimu ya public concern and judgement.
ReplyDelete2. Kabwe has a clear point and it is unquestionably honest, straightfoward and unmistakably to the interest of the public at large. Kusema iundwe kamati kuchunguza jambo fulani is totally independent of kulidanganya bunge. Kama bunge ni fair basi iunde hiyo kamati (to find out the truth) hata kama kwa haraka haraka imemsimamisha Kabwe. The former canstill be done irrespective of the latter. These are two separate charges. Hata ingekuwa ni mbele ya hakimu au jaji, angetaka charge sheet irekebishwe ili haki itendeke.
3. Mambo yanayohusu mikataba ya madini ni agenda tete sana. This is, to the best of my knowlege, among what will make hard for KIKWETE to see Ikulu come 2010. Hali ni mbaya sana hivyo Sitta amsaidie Rais hoja hizi zinapokuja Bungeni, siyo kufunika mkaa wa moto kwa gunia, in the long run it isnt that helpful. Kuna wananchi wanaoendelea kusulubiwa na hata kupigwa risasi na wawekezaji wa sekta ya madini mfano ni kule Mirerani. Things are happening quit openly.
Michuzi, Nashukuru kuipandisha issue hii nikiwa bado na hasira, wadau mjadala wa jana umethibitisha kuwa system ya utawala wa nchi hii is almost spoiled na kama watu watasimama kidete, hatimaye watanzania wanyonge wataelewa uozo unaoendelea na nguvu ya umma itasimama kupinga uozo huo.
ReplyDeleteBig up sana Zitto, i liked the way ulivyokuwa courageous, Zitto has just started, ametikisa tu kidogo na tumeona wakubwa walivyobabaika. Nimekumbuka maneno ya mwanamapinduzi mmoja wa Burkina Faso (Thomas Isidore Sankara -December 21, 1949 – October 15, 1987) alisema:
"I would like to leave behind me the conviction that if we maintain a certain amount of caution and organization we deserve victory. You cannot carry out fundamental change without a certain amount of madness. In this case, it comes from nonconformity, the courage to turn your back on the old formulas, the courage to invent the future. It took the madmen of yesterday for us to be able to act with extreme clarity today. I want to be one of those madmen. We must dare to invent the future."
Usiogope mwanamapinduzi Zitto,tunawataka wanasiasa wa aina yako, wazalendo ambao ni free from umaarufu, itikadi, na rushwa, wenye mapenzi ya kweli na nchi yetu. Najua katika mfumo wa sasa hili haliwezekani lakini the time is coming,that time has started, watu watachoka, hawatamsikiliza mtu yeyote wala kutishiwa nyau na wataitafuta haki yao.
Hapa kuna ukweli kwamba Mh. Kabwe alikuwa hana data za kusupport hoja yake. Inakuwa vigumu sana kusema kwamba Bunge limemuonea, naamini sheria na taratibu za Bunge zipo huru na wazi kwa kila Mbunge bila kujali anatoka chama gani. Kwa maana hiyo ninaweza sema kupewa kwake hiyo Suspension ni sawa kama sheria na taratibu hizo zilifuatwa.
ReplyDeleteMzee wa TBS
CCM MTAWAONEA WANAOSEMA UKWELI MPAKA LINI?
ReplyDeleteKwanza naomba nitoe hoja zangu kuwa kumfungia bwana Zito Kabwe kujihusisha na masuala ya bunge si halali na imeniuma sana kwa kweli, sasa nyinyi wana ccm kama hamtaki kukosolewa mlikubali nini kuruhusu mfumo wa vyama vingi? Huu ni uonevu wa wazi kabisa we say our Tanzania ni nchi ya demokrasia sasa hiyo demokrasia ipo wapi? hebu acheni mambo yaubabaishaji jamani mkubali kukosolewa na wewe matilda Buriani ni dhahiri unachuki binafsi na Zito Kabwe acheni uonevu muongoze nchi laasivyo mnatuitafutia mambo kama ya congo na somalia huko maana mnapotupeleka wananchi so kwenyewe kabsaaa.
Go Zito wembe ni ule ule....
Nimekasirika sana
KWANZA SISITI KUKUITA WEWE NI SHUJAA WETU SISI WADANGANYIKA ! NA NI JASIRI ! NA SI MNAAFIKI KAMA WAWAKILISHI WETU WENGINE(anagalau kuwa shujaa gharama yake ni nzito lakini nakupa moyo ibebe kijana sababu hakuna tena na kama wapo ni wachache waliojaliwa hilo)UMEWEZA KUSIMAMA NDANI YA BUNGE AMBALO NATHUBUTU KULIITA NI LA MASLAHI YA WACHACHE SI LA MASLAHI YA WADANGANYIKA NA KUFUKUNYUWA JUU YA UFISADI WA MIKATABA YA MADINI ! PAMOJA NA KUJENGEWA HOJA TOKA KWA WAKUBWA NA UONEKANE KUWA WEWE NI MUONGO LAKINI WADANGANYIKA TUMEELEWA MENGINE AMBAYO TUSINGEYAJUA.HILI LA MIKATABA YA MADINI SASA NAONA RAIS AMEZE TU MANENO YAKE MAANA MAMBO YANAVYOENDA NI TOFAUTI NA AHADI ZAKE TENA NI BADO MAPEMA SANA SIJUI BAADA YA MIAKA 10 AU 5 YA UTAWALA WAKE ITAKUWAJE NA WAKUBWA WASICHUKIE KWA JINSI ZITTO NA WENGINE TUNAVYOSEMA JUU YA RASILIMALI ZA NCHI HII ! JAMAANI HIZI SI ZENU PEKEE KAMA MNAVYOZANI MMEPEWA ZAMANA TU YA KUSIMAMIA KAMA MNATUONA TUNA GUBU BASI KAPANDENI MASHAMBANI KWENU NA YAOTE NA HATUTAWAHOJI ASILANI HAYA NI YA WOTE MWENYE ENZI KATUPA.KWA HIYO NDUGU ZITTO NAKUPONGEZA SANA NA MUNGU AKUPE MOYO WA UJASIRI ZAIDI YA HAPO SAFARI BADO NI NDEFU .NA WADANGANYIKA NINGEOMBAA WAKUPOKEE KAMA SHUJAA SIKU YA KUREJEA TOKA DODOMA BILA KUJALI ITIKADI KAMA WAWAKILISHI WETU WALIVYOKUWA KWENYE HILI SAKATA.
ReplyDeleteALUTA CONTINUA !
Mzushi
Tatizo lako Kabwe ni ubishi, una ubishi mwingine hauna hata maana. Nasema hivi kwa sababu ninakufahamu fika kwa ubishi.
ReplyDeleteNina hakika hata mtu akikuuliza sasa hivi jina lako nani, sentensi ya kwanza itakuwa ni ya kubisha, labda 'unalitakia nini jina langu'
Sasa hivi umekuwa mbunge changa karata zako vizuri ili uwatumikie wananchi vizuri zaidi.
Najua wengi watakutumia kwa maslahi tofauti na huenda pengine bila ya wewe kujijua japo utajiona kuwa wewe ni mwerevu na hakuna anayeweza kukutumia. Kumbuka kuwa uko katika mchezo wa SI-HASA, wajanja zaidi yako wako wengi na wengine ndiyo viongozi ndani ya chama chako.
Hii ndio LAANA ya WANAFIKI, mtetea haki hatakiwi kwenye BUNGE la WAENDEKEZA MATUMBO YAO BINAFSI BADALA YA MASLAHI YA WANANCHI. Pitia blogu ya mwanafunzi uone mada inayotia AKILI hapa http://kamerayamwanafunzi.blogspot.com UONE KUNA JAMAA KAWEKA MADA BOMBA IHUSUYO NCHI NA URITHI WA MWALIMU NYERERE.
ReplyDeleteMECHI YA STARS NA MSUMBIJI TAYARI MATOKEO.
ReplyDeleteSTARS 0, MSUMBIJI 3.
SENEGAL 3, BKFASO 1
IMEDAIWA WACHEZAJI WA STARS WAMEFUNGWA KWA SABABU WALIKUWA WAKITUMIA MUDA MWINGI KUUANGALIA UWANJA MPYA AMBAO HAWAJAWAHI KUTEMBEZWA TANGU ULIPOJENGWA HADI KUMALIZIKA.
LINGINE IMEDAIWA KUWA HAWAJAWAHI KUCHEZA MBELE YA UMATI WA WATU 60,000 KWA HIYO KELELE ZA WASHABIKI WALIONA KAMA WANAFUKUZWA NA NYUKI.
LA KUSHANGAZA NI KWAMBA WENGI WAO WAMEZOEA TAA ZENYE MWANGA USIOZIDI WATI 100 (BALB), KWA HIYO MAKALI YA TAA YA UWANJA MPYA WALIONA KAMA WAMEINGIA PEPONI NA KUSAHAU WAPO MASHIDANONI DHIDI YA MSUMBIJI.
MWENYE KUPINGA AJITOKEZE!
Kabwe angalia utajikuta pabaya,anayozungumza ni mambo ya kweli kakini punguza kidogo speed.
ReplyDeleteNext time Kabwe jipange uje na data, bunge si mahala pakuleta ubishi wa wakaanga chipsi.
ReplyDeleteVilevile hoja zako zipige msasa; watanzania hatujali mikataba ilisainiwa wapi bali tunajali faida ipatikanayo na mikataba hiyo. Wala hatujali kama mikataba ilisainiwa kwa kasi ya mwale wa juwa au watochi, tunachojali na kupigia kelele ni faida ya mikataba.
Alafu, ikitokea tena unaiba mke wa mtu tafadhali hakikisha hauendi 'pure leather' kwani tunakuhitaji.
hii issue imetia doa serikali ya Kikwete. Kama kuna utaratibu ambao haukufuata kupitisha mikataba ya madini, kwa nini wasiunde tume kuangalia ukweli wa mambo?? Kusema kuwa Zitto amedangaya umma ni kupindisha vipengele vya kanuni za bunge ili kumnyamazisha bwa zito. Hii sio mara ya kwanza, sababu huyo spika bwana Sitta nafikiri amepewa kazi kumdhibiti huyu kijana. Kumbe demokrasia bado, jamani.......
ReplyDeleteZitto, kazi nzuri bwana, mie nafikiri unaitumia vizuri nguvu ya hoja, lakini wao wanatumia hoja ya nguvu.............
Bwana Mdogo Kabwe angalia sana sasa hivi wataku-kabwe baada ya hapo yatasemwa na kusahaulika kama mbunge mwenzio AC. huu ni Ushauri tu kama bado unaipenda Dunia
ReplyDeleteMzee wa TBS acha hizo. Wala usitake watu wasahau hoja ya msingi na kujadili kauli yako.
ReplyDeleteKinachoonekana wazi ni kuwa kijna Zitto amekamata nanihii... za wazee kama uswahilini tunavyosema. Na kila mara ndilo analofanya. BIG UP!!! Matokeo yake ni kumnyanyasa kwa kutumia wingi wa wabunge wa CCM ndani ya Bunge, wengi wao wakiwa hata hawajui wanachofanya.
Mimi namfahamu Zitto tangu akiwa sekondari. Ni kati ya watu wachache sana wanaoona mambo kwa darubini. Hii hoja ina ukweli, na utajulikana siku si nyingi.
CCM inamtaka sana Zitto ila ndo hivyo, mwali aliwahiwa na wenye sera zilizomvutia. Hii yote ni kuhakikisha inambana aone maisha ya siasa magumu na aamue kuvuka daraja. Wanasahau bila akina Zitto wengi, morARI MPYA hovyooooo tu na maendeleo ya waTZ yatabakia kuwa ndoto.
Tunaongozwa na viongozi wanaojifunika kwa ngumi. Wasiopenda kuhojiwa. Ila naamini yote haya yana mwisho na naomba uwe mwisho mzuri. Lakini mwisho mzuri utatoka wapi wakati amani inachezewa?
adagio
JAMANI ZITTO kaonewa akiwa anawakilisha watanzania wote, hivi demokrasia inamaanisha nini katika bunge la Tanzania. Je ina maana kunyamaza kimya ndio kuwa na nidhamu? imenisikitisha sana.
ReplyDeleteJamani mwenzenu naomba hii nchi iuzwe, na kama imeshauzwa kila mtu agawiwe kilicho chake, ili mimi nitumie nitakachogawiwa kutafutia visa niende kubeba mabox!
Zitto kaa chonjo kaka, kwa mtaji huo tusije ambiwa "ZITTO KABWE IS NO MORE" ibaki historia na watu kusema kuwa utakumbukwa daima kwa harakati zako.
Imenichukua saana muda hadi kuamua kuandika hapa, hii inatokana na ukweli kwamba sitaki kuamini hata kidogo kuwa tunayoyasema hapa yanawafikia walengwa. Na kwa mtazamo huu tunakuwa kama tunatwanga maji ndani ya kinu.
ReplyDeleteKwanza nimpe HONGERA saana ZITTO, huu ndio ushujaa. Mengi yamesemwa lakini ukisikia kuthubutu ndio huku sasa, yani hata kama mtu anasema jamaa hana DATA, lakini swali ni je, hao wenye data ni wangapi wamejitokeza na kuamua kusema hadharani pale bungeni kama ZITTO????
BIG TIME ZITTO, si unajua tatizo ni kitumbua cha watu unaweka mchanga?? Lazima hayo ndio matokeo, lakini mimi ombi langu ni moja, Umefika wakati watanzania sasa tuachane na uwoga!!
ZITTO awe chambo na sasa jamani inabidi umma uamke!! Kwa nini tusilalamike kama maliasili zetu ndio zinaliwa na wachache?? Tena kwa kutuona kama sisi ni mataahira???
Kama kasema uongo, kwa nini tume haiundwi??? ili tumfukuze kabisa ubunge na sio kumsimamisha??? inamaana wanajua nini kimo ndani.
naomba niishie hapa bwana michuzi mana sasa naweza kuta natukana bure halafu ukasita kuweka maoni yangu hapa. inatia uchungu kuona watu sasa wanasahau utaifa na wanaweka U-CCM mbele
zito angalia usije uwawa na wewe kama chifupa wazee wa siasa sio wa kuwachezea.
ReplyDeleteSiasa za bongo noma sana, yaani mtu anaonewa hivihivi. Sasa kama wanamsimamisha hawaoni kwamba hawajawatendea haki wananchi! Huyo Karamagi anajulikana ni mtu mjanjamjanja tu! Halafu eti wanapiga makofi bungeni ajabu ya mussa!
ReplyDeleteAnalyst,
ReplyDeleteYou are a true analyst. Bravo!
Walidhani wamemkomoa Shujaa wa Watanzania Zitto Kabwe kwa kukemea maovu ya mikataba ya madini na rushwa, kumbe wamempa umaarufu mkubwa kabisa nchi nzima. Usiogope baba sema tu na Watanzania ndani na nje ya nchi tunakuunga mkono kwa unayoyasema. Hongera sana Zitto tunataka Wabunge kama wewe ambao wataweka maslahi ya Tanzania mbele badala ya yale ya Chama.
ReplyDelete++++++++++++++++++++++++++++++
Wananchi wamlilia Kabwe, wadai haki haikutendeka
*Wakosoa jibu la Waziri kuondoa shutuma
*Wanasiasa wasema Zitto ameibuka shujaa
*Mwenye asema hatakubali, atakata rufaa
Na Waandishi Wetu
SIKU moja tu baada ya kukabiliwa na adhabu ya kusimamishwa kuhuduria vikao vya Bunge kwa takribani miezi mitano, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema) amejizolea umaarufu mkubwa na baadhi ya wasomi, wanasiasa na wananchi wa kawaifa wamemchukulia kama shujaa kutokana na msimamo wake.
Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti wananchi mbalimbali, mmoja mmoja, taasisi na vyama vya siasa, wameelezea kutoridhishwa na hatua iliyochukuliwa dhidi ya mbunge huyo na kusema hatua hiyo haikuwa ya haki na inakandamiza uhuru na demokrasia Tanzania.
Profesa Mwesiga Baregu, mhadhiri mwandamizi wa masuala ya siasa na ushirikiano wa kimataifa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema uamuzi wa Bunge kumsimamisha Kabwe kuhudhuria mikutano miwili ya Bunge haujamtendea haki.
Akizungumza na Mwananchi, ofisini kwake jana, Profesa Baregu alisema kwa kitendo hicho, Bunge halikumtendea haki Kabwe, halikutenda haki kwa demokrasia na pia halikutenda haki kwa wananchi.
Alisema kumwadhibu mbunge huyo hakujaweza kuondoa ukweli kwamba kuna mikataba mibovu inayoingiwa na serikali na suala la Buzwagi ni mfano tu kati ya mikataba mingi mibovu iliyoingiwa, hasa ya madini.
�Wabunge wengi wanaonyesha kuwa hawana utashi wa kulinda maslahi ya wananchi na ndiyo maana wakakataa kuunda kamati kujadili suala lile muhimu,� alisema Profesa Baregu.
Alisema kuzimwa kwa jambo lile bungeni si dawa na wala kumuadhibu Kabwe kwa kuonyesha uzalendo wake hakusaidii kuliziba tatizo bali kilichofanyika ni kudhihirisha tu kwamba Bunge limetumika kuisigina demokrasia.
Profesa Baregu alisema kimsingi maswali ya Kabwe hayajajibiwa kwani jibu la kuwa kulikuwa na ulazima wa kuharakisha mkataba si jibu lenye mantiki.
Naye Dk Mohamed Bakari wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Uongozi wa Umma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema alichofanya Kabwe ni kutoa shutuma na njia muafaka ni anayeshutumiwa kutoa hoja mbadala na kuonyesha kwamba shutuma zilizotolewa si za kweli.
Alisema hilo ni jambo la kawaida hata katika uvumbuzi wa kisayansi, kinachoanza ni kuwa na wasiwasi na kitu, dhana ndiyo huzaa ukweli, sasa hakukuwa na ubaya wowote kuiacha dhana kujadiliwa ili hatimaye ukweli upatikane.
�Jibu la Waziri peke yake halijatosha kuondoa shutuma na kwa kweli kilichotendeka ni sawa na kuwazuia watu kusema. Kitendo kilichotendwa dhidi ya Kabwe ni cha aibu kwa Spika na hata kwa Bunge,� alisema Dk Bakari.
Umoja wa vyama vya upinzani mkoa wa Arusha, umempongeza Kabwe kwa kutoa hoja binafsi ya kutaka kuundwa kamati ya kuchunguza kusainiwa mkataba wa mradi wa madini ya Buzwagi wilayani Kahama na umemkaribisha mkoani Arusha kuzungumza na wananchi.
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, amepinga hatua iliyochukuliwa na Bunge kumsimamisha Kabwe na kudai kuwa adhabu hiyo ni ya ukandamizaji wa demokrasia nchini.
Mbatia alisema pia kuwa hiyo ni picha halisi kuwa Bunge chini ya Spika Samwel Sitta, limekuwa ni la kuwaburuza wapinzani na pia kumlaumu Spika kwa kuruhusu kuingiza mjadala wa kiitikadi katika Bunge, suala ambalo alisema si sahihi.
"Zitto Kabwe ni shujaa, ninavyomjua mimi si mropokaji hata siku moja, lakini amedhihirisha pia ushujaa kwa kusimamia lile analoliamini mpaka dakika ya mwisho, adhabu aliyopewa haikufuata kanuni na misingi ya haki za binadamu kujitetea, ni maonevu ambayo yameweka kovu lisilofutika kwa makundi ya demokrasia," alisema.
Mwenyekiti wa Chama cha DP Mchungaji Christopher Mtikila pia ameungana na wenzake akisema Zitto hana kosa, adhabu aliyopewa ni uharamia wa demokrasia na suala ambalo kila Mtanzania anatakiwa kulitambua na kutotakubali kukaa kimya.
Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu kutokea Mwanza, Mchungaji Mtikila alisema tayari ameshazungumza na mwanasheria wake aliyeko Dar es Salaam ambaye anaandaa kusudio la kupinga adhabu hiyo ili kulifikisha Mahakama Kuu mapema iwezekanavyo.
Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) Wilaya ya Arusha, Calist Lazaro, alisema licha ya kumwalika Kabwe kwenda Arusha kuzungumza na wananchi, juu ya hoja hiyo na watamuandalia mapokezi makubwa. �Tayari tunajipanga kumpokea aje Arusha kwani wabunge wa CCM hawajamvua ubunge, sisi tutaendelea kumpa heshma yake.�
Kwa upande wa Asasi za kiraia zimesema utaratibu uliotumika kumwadhibu Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, ni batili kwa maelezo kuwa haukufuata maadili wala kanuni za Bunge.
Akizungumza kwa niaba ya viongozi wa taasisi hizo jana, Wakili wa Kujitegemea, Tundu Lissu, alisema adhabu iliyotolewa kwa Kabwe sio halali, huku akitaka mbunge huyo aruhusiwe kuendelea na vikao vyote vya Bunge.
Lissu alisema ni bora Bunge likaeleza mbunge huyo amepewa adhabu ya ngapi ili wananchi walinganishe na kufahamu adhabu ambayo ilikuwa inastahili kulingana na kosa, kama analo.
Naye Gema Akilimali wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), alisema Bunge sasa limegeuka kuwa serikali na siyo mhimili wa tatu wa serikali kama ilivyokuwa hapo mwanzo.
�Spika aueleze umma, je Bunge lipo au halipo kwani, linatetea serikali badala ya wananchi hii ni ajabu!� alisema Akilimali.
Pia alipendekeza Bunge lielewe kuwa adhabu ya Zitto ni dhidi ya wananchi wa Kigoma Kaskazini kwani, kutokuwa na mwakilishi katika vikao viwili vya bunge ni hasara kubwa kwao.
Mbali na mahojiano na makundi hayo ya wanazuoni na viongozi wa kisiasa, wananchi kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania, wametuma barua pepe na wengine kupiga simu chumba cha habari, wote wakilaani kusimamishwa kwa Mbunge huyo.
Wakati huo huo Kabwe ametangaza azma ya kukata rufaa Mahakama ya Rufaa kupinga adhabu ya kusimamishwa kujishughulisha na shughuli zote za Bunge hadi Januari mwakani kwa madai kwamba ameonewa.
Akizungumza na Mwananchi jana, Zitto alisema anawasiliana na mwanasheria wa chama chake, Tundu Lissu, pamoja na wanasheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kuiomba mahakama uwezekano wa kuipitia upya hukumu aliyopewa na Bunge.
Alisema adhabu aliyopewa ni ya uonevu kwa kuwa kanuni ya Bunge namba 59 iliyotumiwa kumpa adhabu hiyo, haihusiani na masuala ya adhabu, badala yake ilipindishwa makusudi ili kumkomoa.
Zitto alisema kanuni hiyo inahusu masuala ya amani na usalama bungeni tofauti na ilivyotumiwa na Bunge kumuadhibu.
"Walipindisha kanuni kunikomoa, wameshindwa kuthibitisha uongo wangu, najua nafsi zao zimejuta kwa sababu nimeibua uozo unaofanywa. Nitashtaki pia kwa wananchi, waamue la kufanya," alisema Zitto.
Alisema adhabu hiyo pia haikutokana na Spika bali na Bunge, kinyume na kanuni za Bunge.
Hata hivyo, Zitto alisema pamoja na adhabu aliyopewa, moyo wake ni mweupe kwa kuwa ametimiza wajibu wake wa kikatiba wa kuhakikisha analinda raslimali za nchi.
"Nimefanya kazi ambayo Mbunge anatakiwa kuifanya. Wengi walikuwa hawajui kama kuna mkataba uliosainiwa kimya kimya na serikali London. Hata wabunge walioshinikiza niadhibiwe pia walikuwa hawajui hilo," alisema Zitto.
Imeandikwa na Boniface Meena, Mussa Juma, Andrew Msechu, Hawra Shamte na Muhibu Saidi
Hongera Zitto sema kazi unayo tatizo ni kwamba asilimia kubwa ya wanasiasa, mawaziri,wabunge na viongozi wetu Tanzania wanaweka maslahi yao kwanza badala ya Taifa ndio maana kila siku watanzania wanazidi kuwa maskini wakati wao wanatajirika, tunarudi kule kule enzi za RUKHSA , Mungu Ibariki Tanzania Aluta Continua !!
ReplyDeleteWaungwana hii mikataba ya madini itaendelea kuwa siri hadi lini!? Mali ni ya Watanzania wote kwa nini waifanye siri ilhali mali ni kwetu sote. Tujikusanye ili tupeleke malalamiko yetu kama Watanzania kwa Global Witness ili watusaidie. Tutaendelea kudhulumiwa mali yetu hadi lini!?
ReplyDeletehttp://www.globalwitness.org
Global Witness exposes the corrupt exploitation of natural resources and international trade systems, to drive campaigns that end impunity, resource-linked conflict, and human rights and environmental abuses.
Global Witness was the first organisation that sought to break the links between the exploitation of natural resources, and conflict and corruption; and the results of our investigations and our powerful lobbying skills have been not only a catalyst, but a main driver behind most of the major international mechanisms and initiatives that have been established to address these issues; including the Kimberley Process and the Extractive Industries Transparency Initiative (EITI). Global Witness is largely responsible for natural resources occupying the prominent role in the international agenda that they currently do.
And away from the policy arena, Global Witness' hard-hitting investigations have had direct and major impacts, such as the IMF withdrawal from Cambodia in 1996 over corruption in the logging industry, the imposition of timber sanctions on Charles Taylor's Liberia in 2003, and the precedent-setting arrest and conviction of arms trafficker and timber baron Gus Kouwenhoven, in the Netherlands in 2006.
Despite the great strides made in the first decade of Global Witness' existence, the struggle to ensure that natural resource exploitation is equitable and sustainable is still in its early stages. Resource-fuelled wars such as those that shattered the DRC, Liberia, Angola and Cambodia could happen again tomorrow, and add to a death toll that has topped over six million since the late 1990's, because the international community has not addressed the trade in conflict resources.
The competition between the old and emerging powers to secure the world's remaining oil reserves is escalating, perhaps dangerously so. The scramble by extractive industries to secure exploitation rights over the world's mineral wealth, whilst at the same time resisting any kind of regulation that would enforce good practice, threatens some of the planet's poorest populations, whilst the world's dwindling forests, home to millions of people and reservoirs of biodiversity, continue to face an onslaught by some of the most corrupt regimes and companies, bent on satisfying an insatiable demand for timber regardless of cost.
Natural resources could be the key to ending Africa's poverty, and making it, and other areas of the developing world, the economic powerhouses they should be. But Global Witness believes that neither governments nor industry have shown the leadership or the vision to create the sea change in the international architecture that is necessary to make natural resources a benefit and not a curse. Global Witness also believes that this sea change is possible, and it is for this reason that we are continuing to deploy the accumulated thinking, experience and skill that we have developed over the past decade, to help bring about this change. There is no alternative.
Nasikia eti huko kwenye ASASI mbalimbali za serikali alikokuwa anakwenda kuchukua data, "watu wa system" walikuwa wameshakuwa-planted so data nyingi kama sio zote alizokuwa anapewa zilikuwa FEKI zikitolewa na hao watu wa system. Si mnakumbuka yalimtokeaga Mrema siku zile zake za 'ulipuaji wa mabomu?' Basi ndo na Kabwe walivyom-fix hivyo hivyo.
ReplyDeleteUsicheze na SYSTEM bwana!
Namna pekee ya kuondoa mambo kama haya ni kutenganisha mihimili mitatu Bunge, Serikali na Mahakama kwa maana hiyo wabunge wasiwe mawaziri maana wanakuwa sehemu ya serikali. Kinadharia wanasema wametenganisha ila kiutendaji wameunganisha, haya ya Kabwe yasingetokea kama mihimili ingetenganishwa na haya ya Kabwe yasingetokea maana wabunge hata wa CCM wangesimamia bunge.
ReplyDeleteFor this one I am dropping my ccm card, halafu bro! michu acha upendeleo tunataka tamko la chadema
ReplyDeleteMHESHIMIWA ISSA ASLAAM ALEIKUM....WAZIRI ANADAI MASHINE ZA KUTENGANISHA MADINI HALISI NA YA AINA "..NYINGINE.." NIGHARAMA KUBWAA KWAHIYO AFADHLI WAWEKEZAJI WABEBE UDONGO WAKAHCEKECHEE "..UGHAIBUNI KWAO.." "..$%^&#@#*&^UUZI MTUPU.."KWANINI BUNGE LISIPITISHE SHERIA YA KUWAPIMA "..AKILI VIONGOZI WETU.." MARA KWA MARA, HASWA PALE INAPOSEMEKANA KWAMBA MAAMUZI SIO SAHIHI.."..MEI BI SIO KOSA LAO NI MATATIZO/UGONJWA WA AKILI TU.."
ReplyDeleteDuh, kweli kasi mpya, nguvu mpya na ari mpya..... wahenga walisema "dua la kuku halimpati mwewe" hawakukosea...Sisi walalahoi kila siku tunasoma na kusikia mambo ya Richmond, Dowans, Radar, Magari ya jeshi, helicopter za jeshi, ndege ya raisi, BOT Twin towers, Kiwira na mengine meengi tuu...mwisho wa yote wenzangu mmeona, watu wanakata mbuga magazeti yanapata a habari nyingine na kisha TUNASAHAU!!! kama sijakosea wabunge vijana wenye nguvu na sauti ya kuongea ninaowakumbuka kwa umri wangu mdogo ni watu kama Sokoine (RIP)- wahujumu wa uchumi, Amina Chifupa (RIP) - Madawa ya kulevya na ujambazi, Horace Kolimba (RIP) - dhana na imani potofu za ujamaa na kujitegema, Kabwe Zittoz - mikataba hewa na utapeli wa mawaziri!! sasa jamani katika wote hao niliowataja mmeona ni kijana wetu Zitto tu ndiye hana kitu kwenye "mabano" manake waswahili wanasema "Mungu amependa akaaamua kumuita mbinguni" duh, ni kaazi kweli kweli manake Mungu anaangalia nani ni msumari zaidi kabla kisha aamue kumuita?? point yangu inarudi kwenye msemo wa wahenga hapo mwanzo nilivyoanza, " dua la kuku halimpati mwewe".
ReplyDeletekingine nawaomba wakubwa wanaotufanyia watufanyiayo,"mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni" na kama haki sitapata mwalimu Nyerere alisema "haki ni haki na kila mtu ni haki na jukumu lake kugombea haki yake kwa nguvu zote na ikiwezekana jasho lake lote", mimi naongeza kuwa ukishindwa kutumia U-Mahatma Ghandhi......... basi tutaangalia upande wa pili wa mapambano!!!
Mungu ibariki Tanzania na watu wake.....
Niliwai sema Tanzania ni tenga halibebewi maji. Zito kabwe ni very important role katika siasa ya Tanzania, however syestem doesnt support such kind of politics.
ReplyDeleteUshari kwa Zito kabwe, Tanzania inakufa taratibu kabisa na si jukumu lako wewe Zito wala mimi mlala hoi kuiokoa, wacha ife then tuzike.
Nchi imejaa rushwa, unyonyaji, siasa ya ubabe, wizi, geeeeeeessss, i cant talk about tanzania, short i hate it.
Mimi naona ZITTO his good but! anatakiwa akiwa anawasilisha hoja zake awe na data kamili zenye uhakika sio feki zitamtoa macho. Pili hawa wanajiita wanaharakati wanamdanganya wanaohonga vi- PS feki kwenye maofisi wape siri matokeo yake wanapewa siri feki wanakimbiza kwa wabunge kama akina ZITTO ambao wana ujasiri sasa wanamharibia kijana wa watu.
ReplyDeleteZITTO ongeza ujasiri lakini punguza JAZBA, umri wako na jazba ulizonazo hutafika mbali. Sio kwamba kuna mtu atatoa roho yako la! bali tutakuchoka kama tulivyomchoka Mrema. na usipoangalia papara zitakuponza nenda na DATA tafuta unayofanya ni mazuri kwa faida ya watanzania na wananchi wa jimbo lako wazidi kukupa ubunge ila dear check out!!
spika ateuliwe na rais badala ya kuteuliwa miongoni mwa wabunge,wakati hilo likiwa kwenye mjadala na siye ndugu wananchi bunge lijalo tusichague vyama tuchague wabunge makini ili kuleta uwiano hasa katika maamuzi yanayohusu maslahi ya nchi,kwa maamuzi haya iliyofikia bunge la safari hii limechemka kuliko mabunge mengine yote yaliyopita,ndio;Standard and speed tumeiona ila massage sent.
ReplyDeletekaka michuzi asante kwa habari hii. nilikuwa naisubiria kwa hamu tokea jana....najua umetingwa na kazi nyingi.. u're forgiven though.
ReplyDeletezitto represents vijana wasomi wa kitanzania wenye upeo mkubwa wa kuona and able to analysize society matters. for that he is a true chadema and intellectual. am happy kuwa hajaniangusha as i thought the moment alipochaguliwa kuwa mbunge ataweza kutatua matatizo ya tanzania na kuwakilisha wananchi..... bravo zitto and thank you for presenting us, just know we're behind you.
its high time now vijana wakitanzania tujumuike kutetea nchi yetu, its time to be critical and democratic. for this i'll join chadema kwani wameonyesha democrasia ya kweli na sio ubabe na kugombania mali za wananchi.
zitto waonyeshe mambo uliyafanya UDSM enzi zako. big up zitto, lets work on influencing more pple like you. remember to pray and u'll be safe and stand strong.
I think its high time for my fellow Tanzanians to wake up and fight against this!for he was there deffending our affairs and its our time now to fight for Kabwe.This is totally unfair to suspend him because such a harsh punishment was suppossed to start with Adam Malima who caused a loss of about 100m/= instead they say"Adam was new in the House".How about Kabwe?How long have he been in the house?But because he touched their point of interest then they fired him out so that they can eat our national cake without any reluctancy.How shame is such a decision!From that point of view"I SWEAR TO GOD THAT I WILL NEVER EVER VOTE FOR ANYONE BECAUSE THERE IS NO MEANING OF HAVING REPRESENTATIVES"Take a look at this SILLY decision a man with a sane mind and who love his country couldn't even dare to do such a thing!I URGE MY FELLOW TANZANIAN TO STAND STRONG AND FIGHT AGAINST THIS DUBIOUS PERSONS WHO ARE ALWAYS ABSENT IN THE HOUSE AND WHEN THEY ATTEND THEY JUST DECIDE ANYTHING THEY FEEL LIKE DOING AS FAR AS THEY SUPPORT THEIR FELLOW "CHUKUA CHAKO MAPEMA" CCM MEMBERS.IF POSSIBLE LETS MAKE A DEMO AGAINST THIS.SOLIDARITY FOREVER...!!!
ReplyDeleteMHESHIMIWA ZITTO KABWE ANATAFUTA UMAARUFU TU. MHESHIMIWA ZITTO ANANIKUMBUSHA MALALAMIKO YANAYOTOLEWAGA NA GRADUATES WA ENGINEERING TO UDSM PALE WANAPOKUWA WAMEFANYA KAZI KWA MWAKA MMOJA KATIKA MGODI HALAFU WANAANZA KULALAMIKA KUWA WAWEKEZAJI NI WEZI ILHALI HAWANA PICHA KAMILI YA PROCESS NZIMA YA MINING PROJECTS.
ReplyDeleteHEBU SOMA MAKALA HII YA MAHOJIANO NA MWANASHERIA WA BARRICK GOLD UPATE PICHA KIDOGO OF HOW COMPLEX THE INVESTMENTS ARE http://www.dailynews-tsn.com/page.php?id=2331
MR. PRESEDENT MOTO UNAWAKA KATIKA NCHI HALAFU WAZIRI WAKO ANAFUNIKA NA GUNIO, HAJUI KWAMBA NDIO KAHARIBU??? SPIKA WA BUNGE ANAONA KATOA UAMUZI IMARA LAKINI KWA NINI KAMATI ISIUNDWE KUCHUNGUZA MAYBE ZITTO NI MUONGO LAKINI MMEPROVE VIPI??? HAMUONI SASA NYIE NDIO MNAHAIBIKA, HUYO JAMAA SIO MTU SAFI KABISAAAAAAAAAAAAA, HIYO INAJULIKANA KABLA HATA HAJAWA MBUNGE KWANZA HANA UKABILA FUATILIENI KITENGO CHA CONTAINER MUONE JINSI WAHAYA WALIVYOJAA, DADA YAKE, KAKA ZAKE NA WATOTO WA KAKA ZAKE, YALE ULIYOSEMA MR. PRESIDENT
ReplyDeleteKila kilicho na mwanzo kina mwisho. Sasa hivi leo Malima alisema uongo katika bunge hilohilo akusimamishwa ubunge,Kabwe katoa tuuma zilizo na ukweli kasema uongo sasa hivi hii nchi inakwenda wapi bunge halina mwelekeo. Hivi spika wa bunge anafanya nini? kazi yake kukandamiza watu wakati yeye ndio kiongozi. Lakini kitaeleweka tu!!!! Mwisho wa siku.
ReplyDeleteKWANZA NAMPA POLE MH. ZITTO KABWE!
ReplyDeleteSASA TUNAPATA PICHA HALISI UOZO ULIOPO SERIKALINI:-
INAMAANA HAWA WATOTO NIKIWA NAMAANA KM VIJANA WADOGO WANAOINGIA BUNGENI KICHWA KICHWA KWENDA KUROPOKA DHAMBI ZA SERIKALI MFANO HAI KM MAREHEMU AMINA CHIFUPA... HIVYO KILE KIAPO UNACHOAPISHWA NIKULINDANA NA SI KUUMBUANA! HAPO TULITEGEMEA MH. KALAMAGI AJIBU TUUMA NA SIO BWANA MDOGO KUSIMAMISHWA BUNGENI. JAMANI TUMECHOKA NA MAOVU YA BAADHI YA VIONGOZI WALIOPO MADARAKANI KUTUMIA MADARAKA YAO VIBAYA KWA MANUFAA YAO BINAFSI NI UOZO MTUPU NA BADO MNAENDELEA KUMLINDA KALAMAGI..... MFANO HAI WALE VIONGOZI WENYE NIA YAKWELI WALIOTEMWA NA WENGINE KUFA KM MREMA, MAREHEMU CHIFUPA, KOLIMBA, SOKOINE NA HUYU ZITTO NAE TUNAMUONA... TUNASUBIRI MATOKEO HATUJUI HUKUMU YAKE NI KIFO AU KUPEWA UKICHAA. MIMI MKEREKETWA
kwetu kigoma akina kabwe wote ni wazaire(wabwali)huyu kawa mtanzania tangu lini????au kisa kazaliwa ujiji,
ReplyDeletePublic against Kabwe Zitto’s suspension
ReplyDeleteTHISDAY REPORTER
Dar es Salaam
MEMBERS of the public yesterday denounced the suspension of Kigoma North MP Zitto Kabwe from attending two consecutive parliamentary sessions, with some scholars terming it a mob justice.
Many Dar es Salaam residents called THISDAY newsroom to express their disapproval on the verdict, which they said was passed by the ruling party CCM against the youthful MP.
A lecturer with the University of Dar es Salaam, Dr Sengondo Mvungi said the suspension was a big blow to democratic rule, saying: ’’Watching that debate (on Tuesday) one gets convinced it was CCM MPs against the opposition�there was no public interest.’’
He said Mr Zitto followed all the rules to present his private motion and had the right to do so but it came as a big surprise to have himself punished.
The don warned all MPs, particularly those on opposition, with critical arguments against the government to prepare themselves for similar reprisal. ’’That stroke is there waiting for any other critical MP,’’ he said.
Dr Mvungi argued that the issue of truth or cheating couldn’t be established through voting but via adduced evidences.
’’What we have seen in parliament is mob justice�majority declared Mr Kabwe a liar and he was lynched without evidence,’’ he said.
Another city resident, Mr Zacharia Mtigwa, charged: ’’This is purely not a parliamentary decision�it is CCM’s.’’
He said CCM parliamentarians have shamed themselves by passing such an illogical decree.
Mr Constantine Akitanda, a resident of Mbezi on the outskirts of the city said the lawmaking House did injustice to Mr Kabwe whose argument was simple and sincere.
’’He merely asked for the formation of a probe team to examine the conduct of the minister (for energy and minerals Nazir Karamagi) in signing a mining contract with Barrick Gold Mine.’’
Mr Akitanda charged that contrary to the way parliaments operate all over the world, Tanzania’s had long ceased to serve the public and was working for the interest of the elite few. He particularly accused CCM MPs of putting party interests ahead of the country’s.
But, the chairman of Democratic Party, Rev. Christopher Mtikila, blamed the speaker of the National Assembly, Mr Samwel Sitta for allowing ’’such a nonsense decision in parliament.’’
’’The punishment is wrong and it is equally wrong for the speaker to want MPs in parliament to please him�that is not their job, theirs is to serve wananchi, their voters,’’ said Mtikila.
He said it was time wananchi woke up and proved that they are the ones who own the parliament, the executive and the judiciary as enshrined in the national Constitution and that whoever is serving in any of the institutions was a mere employee.
The deputy leader of opposition in parliament, Dr Wilbroad Slaa (Karatu�Chadema) described the suspension as a victory to the opposition and all democratic activists.
’’I’m glad that the public has got the message right�we are receiving windfall of congratulatory rather than consolation messages from all over the country. This is real victory,’’ he said.
Zitto Kabwe keep it up. Nakushauri uandike kitabu haraka iwezekanavyo ili jamii ya wapenda haki na usawa iwe na kumbu kumbu yako. Ni vizuri mawazo yako ukayaweka katika maandishi kama alivyofanya baba wa Taifa ili watanzania tuweze kukumbuka daima. Ujasiri ulio nao ni wa hali ya juu ambao umekujengea maadui wengi, jitahidi kuwa mwangalifu katika nyendo zako zote wasikutafutie sababu. Long Live Zitto Kabwe, Long Live Tanzania.
ReplyDeleteBaada ya kusoma maoni ya wachangiaji juu ya suspension ya Mh. Zitto, leo nimethibitisha mambo kadhaa muhimu kuhusu watanzania, watanzania wengi wako hivi:
ReplyDelete1.Hodari wa kulalamika pasipo kuchukua hatua,
2.Wanafiki na wenye wivu wa kushindwa,
3.Waoga, na Wabinafsi
4.Wanaofikiria leo na kesho tu!
Tatizo kubwa la nchi hii ni vita baina ya TABAKA KONGWE linalowakilishwa na wazee walioko madarakani na TABAKA JIPYA lenye vijana wanaopenda mabadiliko.
Sisi vijana wa nchi hii tukiweza kuacha niliyoyataja hapo juu, na kisha kumtambua hasa adui yetu ni nani, tutaibadilisha nchi hii.
Nidhahiri adui yetu si CCM!!! ni tabaka kongwe linalohodhi madaraka ya nchi nii!!!
Tuache kulalamika, tuache ubinafsi na wivu wa kijinga na tamaa za mali za haraka haraka, tupigane kuwaondoa wazee hawa kwenye system!!!!
Mh. Zito ni anawakilisha tabaka jipya la vijana wenye wepesi wa kufikiri na kuunda mikakati ya kujikwamua!!!!
Wakati tunamsupport Zitto tuamue kuchukua hatua. Siasa za leo kwenye mazingira haya ya utandawazi na ushindani si za WAZEE tena hasa kwa nchii maskini kama yetu, ni siasa za VIJANA!!! na tuingie sasa kupambana na tabaka kongwe TUSIMUACHIE ZITTO PEKE YAKE JUKUMU HILI!!!!!
katika bunge la ajabu duniani hili ndio la kwanza angalieni lina wabunge wangapi wa upinzani kutokabara!kwahiyo wache wafanye wanavyotaka kwa hao wadanganyika walio wachagua!jamani mkitaka kufanya mikataba hata mbiguni kwangu poa tu!au wezangu mnasemaje?
ReplyDeleteKwa kweli hii ni historia- wadau nielimisheni hivi kuna mbunge alishawahi kusimamishwa kwa sababu ya kudadisi jinsi serikali inavyofnaya kazi??...............
ReplyDeleteHivi kweli tunategemea kupata mchango wa wapinzani kama tunaendelea kuwaziba midomo??
AIBU KUBWA SANA , SHAME ON YOU WABUNGE WA CCM!! SITTA AFUKUZWE KAZI, NAONA KAZI IMMEMSHINDA. HUYO KARAMAGI NAYE ACHUNGUZWE, HATA KAMA KAMA hakupata 'DEAL' LAKINI INAWEZEKANA NI MZEMBE AU HAKUFUATA UTARATIBU UNAOTAKIWA KATIKA KUSAINI MIKATABA. TOKA LINI ISSUE YA MADINI IKAWA DHARULA -EMERGENCY-?? HAYA MAELEZO HAYAKUBALIKI KABISA.
nashangaaa hii topic haijapata maoni mengi kutoka kwa wadasu, kwa sababu ni topic nyeti sana (au bwana michuzi unayaficha nini??)
Je, kuadhibiwa kwa Kabwe ni Uadilifu wa Sheria, Siasa, Upinzani, Woga, au Chuki Binafsi?
ReplyDeleteTumuangalie Kabwe mwenyewe: Kabwe anatoka Chadema, si mwana-CCM.
Kabwe ni mbunge kijana sana na anayejiamini yeye mwenyewe anasema amekwenda shule. Kabwe alihusishwa kwa karibu sana na kashfa nzito ya uhusiano uliokuwa na mashaka na mbunge mwingine amabaye kwa sasa ni marehemu. Kabwe anaonekana kujiamini sana na anaweza kuwa mwiba kwenye maovu ya viongozi wabovu katika nchi hata kama nyakati zingine anajikwaa kwenye sheria fulani fulani katika kufuatilia aliyoyapanga.
Haya yote yanaweza kuwa chanzo cha kuminywa Kabwe kisiasa, kwa woga wa maovu yaliyoko ndani ya serikali au chuki binafsi.
Hebu tuwaangalie waliokuwa wakali sana na hii hoja: kwanza wengi wao ni wana-CCM, wengi wao wao wakiwa wazee wakongwe na baadhi yao ambao wamewahi kuwa katika serikali. Ni watu ambao kwa kiwango fulani wameliweka taifa letu hapa lilipo. Na wameishazoea uozo mwingi sana kiasi ambacho hawaoni kabisa hoja ya Kabwe isipokuwa pale alipojikwaa.
Katika swala hili jambo moja ni wazi sana na halina ubishi. Kwamba ni kweli yawezekana Kabwe alitumia neno ambalo asingekuwa na lazima ya kulitumia ingawa neno lenyewe sio kinyume cha sheria mpaka hapo waziri muhusika atakapotoa vielelezo vya wazi zaidi na bayana kudhihirisha kwamba aliyoyasema mbunge si kweli. Lakini hilo halikufanyika kwa kiwango cha kufuta mashaka badala yake Mbunge mmoja ambaye ameishawahi kuwa katika serikali hii ya CCM akatumia wasaa huo kufanya lile ambalo wengi tumekuwa tukilihofia la kuwapunguza makali wale wanaohoji uhalali wa yale yanayofanywa na hao tuliowapa dhamana ya kuongoza mambo yetu.
KUADHIBIWA KWA KABWE NI SAWA KUUA MBU KWA BUNDUKI.
Michuzi umebania comments za watu watu tumezungumza sana humu au Adam Kigoma Malima ni ndugu yako?? maana yeye amedanganya bunge lakini hakuchukuliwa hatua zozote weka maoni yote hadharani watu waone waliyozungumza na wengine maana katiba ya nchi inaruhusu bwana KILA MTU ANAO UHURU WA KUSELA ANALOLIONA.
ReplyDeleteYale ya Irene Sanga ndo haya jamani. Huko bungeni wao wanasubiri tu kuja kuuliza tena "TUNAVAA VIATU NAMBA NGAPI?" Zitto unafanya kazi yako vizuri, tuko pamoja na wewe, kwani wewe unajali ahadi zako kwa wananchi.
ReplyDeleteNa nyie mnaodai hakuwa na data, hivi hamuoni kama matokeo ya mikataba ya NJI hii ni data sahihi kwetu? Data sahihi za RICHMOND hazijapatikana mpaka leo machoni kwa wananchi, kama zipo basi ni kwa hao wenyenchi, mnategemea tutakaa kimya mpaka lini tukisubiri huo mnaoita ushahidi huku tukiwa tunateketea? Raisi Hami J mwenyewe alishaachisha watu kazi bila kusubiri ushahidi(alijieleza baada ya hapo kuwa alichemka, na maisha yakaendelea). mwalimu alishamweka ndani mgiriki kwa kuikashfu serikali yake bila hata kuhitaji milolongo mirefu ya kisheria (ushahidi na data sahihi vikiwa ndani). Hii ni kutokana na kujali heshima ya nchi na maslahi ya watanzania kwa kupinga adui rishwa. Hapa hakuna cha data wala nini, Zitto hajalopoka, ana uhakika na anachosema, na ndio maasa, Mungu si Athumani jamii ya wadanganyika iko pamoja na yeye. Unataka data zipi tena kwenye jambo hili? Hivi hata kwenye madini tumefikia hatua ya kubembeleza wawekezaji kiasi cha kuwafuata hukohuko uzunguni kusaini mikataba (tena inayodaiwa hatua zote za awali zilikamilika hapahapa nchini?)
ZITTO THANX A BIG TIME!!!!!
Hao wamechemsha tu. Jina lako linavuma tu. Haufi wala nini, mpaka Mungu atakapoamua.
NB: Analyst Nimekukubali.
From Serengeti Of Flowers
We anon wa August 16, 2007 1:47:00 PM EAT, kwenda zako mshamba wewe. Wenzako wanaongelea masuala ya manufaa ya taifa wewe unaleta mambo ya ukabila. Kajifunze kwanza kuandika - who cares about ubwali...shut up!
ReplyDeleteMabadiliko mazuri katika nchi yaweza letwa na raia wa nje pia wazawa kama wameshindwa mfano waganda walimshindwa Idd Amini watanzania wakamtoa waganda sasa wanaishi kwa Raha.Msumbiji,Angola n,k kote wamesaidiwa na wageni wa nchi zingine.
ReplyDeleteKama watanzania tumeshindwa kuwakabili wahuni wa ndani ya nchi wacha hao unaowatuhumu na kuwaita wabwali(WAKONGO) wakina Kabwe watusaidie.Hakuna ubaya.
Nadhani nchi hii tunahitaji wageni watusaidie naona kama wazawa tunashindwa.Na watakuja tu tutake tusitake.Kuna wenye huruma na nchio hii kama sisi tulivyokuwa tunawahurumia weusi wa Afrika ya kusini pia wako wanaoumia wa mataifa mengine kwa mambo yanayoendelea humu.Let them come.I don`t care.Wawe wabwali,wahutu,watusi,banyamlenge au njanjaweed n.k cha muhimu yaje mabadiliko mazuri kwa wananchi.
2008-ZITTO KABWE Cio Raia wa Tanzania kwani ana asili ya DRC Congo... Subirini
ReplyDeleteKUDADADEKI POLITICS!!!
NAMUHURUMIA SANA JK. HIVI MMEGUNDUA ILE SLOGAN YAKE YA ARI MPYA NGUVU MPYA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA HAIPO TENA. ILA ITSH HIGH TIME WATANZANIA TUNAHITAJI KUONGEA NA KUJADILI HIVI VITU.
ReplyDeleteWABUNGE WA CHAMA MASLAHI NI WAJINGA SANA.
Hii yote ni kwa sababu: -
ReplyDelete1. Mbunge - Mkuu wa Mkoa
2. Mbunge - Waziri
Saa ngapi atatumikia wananchi na saa ngapi ataitumikia serikali?
Niliwahi kushauri kwa kuandika kwenye blogu yangu mwaka jana kuwa, Wabunge wengi hawajui yanayotokea majimboni mwao kwa sababu kwanza hawaishi kwenye majimbo yao ya uchaguzi lakini pia inawawia ngumu kujua matatizo anuai ya majimbo yao kwa sababu wengi hawajui historia ya maeneo hayo.
Hongera Zitto - Ziiiiiiiiii kwa JK na timu yake!!
Hakika kesho nitakuwepo kukupokea!!!
Hivi mzee kama Malecela haoni aibu kumkandamiza kijana kama yule kwa kufichua uozo na upuuzi ulio ndani ya CCM na serikali yake. CCM acheni Unafiki. Tuweke mbele Maslahi ya Taifa na hususan kizazi kijacho.
ReplyDeleteMimi nawaambia JK saa hizi usingizi hapati, anajijutia nafsi yake kiherehere cha kugombea urais halali vizuri kama mimi na kibaya zaidi aliwaahidi watu mambo mengi ambayo hayatekelezeki.sikuona sababu ya kupangua safu ya mawaziri wakati alikuwa na uwezo wa kuwatimua waliochemsha bure ghali fadhila anazilipa anaungua huku anacheka
ReplyDeletewatanzania tulioko nje tuungane na kuipundua hiyo serikali ya ccm tumechoka tuseme basi .kama vijana wa mwaka 80 waliotaka kumpindua nyerere .
ReplyDeleteRobert shija, washington dc
ZITO NAKUPONGEZA KWA USHUJAA NA MSIMAMO ULIONAO.UMETUPA HABARI AMBAZO HATUKUZIJUA, CCM WAMEKUITA MWIBA, HAWANA MEMA JUU YAKO, MUNGU AKULINDE, TAIFA BADO LINAKUHITAJI.
ReplyDeleteNAKUPONGEZA ZITTO KWA USHUJAA WAKO, MUNGU AKULINDE, TANZANIA BADO INAKUHITAJI.
ReplyDeleteNia yao awapishe kidogo, maana anawasumbua sana. Akiwa Bungeni Lowassa hatulii. lakini wamemsaidia kisiasa. Maana wakati mwingine ni bora kukaa nje kuliko kuwa ndani unafanya madudu!
ReplyDeleteNadhani sasa wanajilaumu, maana hata wanukuu sheria gani, wananchi hawapo tayari kusikiliza lolote nje ya hapo.