TWANGA PEPETA WAMEAHIRISHA SAFARI YAO YA HOLLAND KUTOKANA NA UGUMU WA KUPATA VIZA KATIKA MUDA MUAFAKA. HIVYO LEO NA KESHO WANAMALIZIA KUSHUTI VIDEO LONDON KABLA YA KUKWAA PIPA LA QATAR AIRWAYS KUREJEA BONGO NA KUWAHI KUVUNJA JUNGU WIKIENDI HII.

MWENYEKITI WA ASET MH. BARAKA MSIILWA ANAWATAKA RADHI WADAU WOTE WA TWANGA WLIOJIANDAA KUPEPETA ROTTERDAM SIKU YA IJUMAA KWA USUMBUFU WOWOTE ULIOTOKANA NA AHIRISHO HILI AMBALO LIKO NJE YA UWEZO WAO

ASANTENI,
TARISHI HAUWAWI...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Michuzi Wadau wa Jiji lilio chini ya usawa wa bahari tuna machungu saaana. Mwambie Baraka kuwa amejidhalilisha na kudhalilisha kampuni yake ya ASET.
    1. Licha ya kero kwa wana UK kuweka mabango na picha ya Choki wakati yeye hayupo katika msafara kuonekana kuwa ni muendelezo wa mambo ya kiswahili swahili hivi sisi sasa huku tunapinga huu utapeli wa waziwazi!

    2. Michu kaa pembeni katika hili na wala wasikutumie kueleza upuuzi ambao kamwe haukubaliki (mpelekwa asiye hodari aweza kugharimika maisha kwa niaba ya Mpeleka mjanja. Yaani ina maana kuwa toka wanatoka TZ hawakuwa na visa ya NL? Je hii kampuni ina washauri kweli mwenye uzoefu katika mambo ya kibiashara na mahusiano ya Kimataifa? Je waliwahi Kusikia kuwa kutoka UK kuja NL unapewa visa kiulahisi tu ndani ya siku tatu hivi ili muradi uonyeshe kuwa mnajua kupinda mugongo au kukata kiuno au kurusha miguu juu kwa staili ya wizi toka kwa Wanaumeee! Sasa nawambieni kuwa hata wangekuwa wanatokea Ujerumani au nchi nyingine iliyo katika makubaliano (Schengen Treaty)huwezi kuingia tu hapa kama vile unatoka Ilala kwenda Leaders Club! Bado inastahili angalau upeleke maombi yako mapema na kuonyesha kuwa Wasanii wote hao wana Bima ya muda na mwenyeji wao au Twanga wenyewe wanafedha ya kutosha ya kuishi hapa kikamilifu na ratiba yao hapa inaeleweka na kuandaliwa vilivyo. Haya yote hayakuwa yameandaliwa na eti tangazo lao hapa Uholanzi lilikuwa ni tangazo la kutoka katika globu ya Michuzi!

    Michuzi hii hali ya kucheza na wateja kama vile hawajui haki zao sasa jiandae kumtaja waziwazi aliyeleta hilo tangazo na muandaaji wa utapeli huu ili awajibike mwenyewe. Yaani ukweli wa mambo ni kuwa safari ya Uholanzi haikuwepo ila walikuwa wanajaribu kutubipu watu wastaarabu tusiobipu wala kubipika kwa kurusha katangazo uchwara ili kuona reactions ya watu huku kama watashabikia sana basi waanze tafuta utaratibu wa safari kwa staili ya zima moto! Hilo haliwezekani huku na baya kabisa eti anakutuma wewe kuomba msamaha kwa niaba yao kwa nini wao wenyewe wasiseme? This barbaric action shall never be tolerated!!
    Hapa watu walisha ahirisha shughuli mbalimbali na kupanga ratiba yao ya ijumaa kuwapokea Watanzania wenzao kwa shangwe na kuburudika sasa hilo halipo na wengine hatuwezi kurejea kazini tena siku hiyo!! Fikiri tulikuwa tumewajulisha rafiki zetu Wabongo wa Ubelgiji na wakawa wemekodi Minvan kuja kuungana nasi na mambo kibao ambayo siwezi kuorodhesha hapa!! Damage tunayoongelea si tu ya kupoteza fedha bali zaidi kabisa ni maumivu ya pigo hili kisaikolojia.
    Michu kuwa mkweli waulize hata return ticket zao zilikuwa ni za kutokea UK na sio Schiphol sasa wangekuja huku na ungo??? na wala usije ukabana hii comment yangu maana utakuwa umezidisha hasira zetu kundi zima la Wazee wa Amsterdam, Denhaag, Rotterdam, Delft na Antwerp ambapo kesho kama hatujasikia neno la kuridhisha toka kwa Baraka au Asha basi tutakuwa na session na mshauri wetu wa masuala ya kisheria. Samahani sana kwa kuandika na hasira si kawaida yetu na hapa hatutowi vitisho na mtu yeyote asije akatulaumu baadaye (watch our words)!.

    Mdau
    Michael Mwaipopo

    ReplyDelete
  2. Mdau Mwaipopo tuliza hasira kidogo. Twanga hawana uzoefu na nchi za Ulaya. Wamezoea Uarabuni ambako mambo bado yanakwenda Kiswaziswazi. I am sure next time watapanga ziara kwa ufanisi zaidi.

    ReplyDelete
  3. I tottaly agree with bro Mwaipopo..you can not change plan as simple as kumsukuma mlevi huu si ustaarabu..once you put adverts you have to make sure all the plans settled in place .you can't say that blood rubbish..YOU CHEAT your wadaus ..they need to say sorry in big manner and explain much what was really happened.
    Poleni sana wadau wa huko najua watu walishajinoa kisasawa.kama namuona anti Sonny ...

    ReplyDelete
  4. Basi jamani kwani ni mambo yalitegemewa yawe hivyo lakini hayakuwa poleni sana ndugu zetu wako msichukue hasira sidhani kama twanga wange fanya hasira
    mdau england

    ReplyDelete
  5. Kaka Michuzi kwa kuwa umeamua kuandika heading zako katika KISWANGLISH basi mimi nashauri isomeke "Breking'i Nyuuuzzzzi" kwa uongeza alama ya mkato kama unapoandika neno Ng'ombe

    ReplyDelete
  6. We Maipopo si uchome nauli ukawaone twanga bongo?Au hawakawii kukuzuia usirudi holand?Zaidi ya Twanga you can do otherthings.
    Mdau.

    ReplyDelete
  7. Yaani mnataka kutudanganya sasa kwamba hao asset walikuwa hawajui kama visa ya NL ilikuwa nilazima waiombee nchini kwao? Toka lini mtu akapewa visa ya nchi nyingine juu kwa juu wakati ana tourist visa?

    ReplyDelete
  8. Looh! band kubwa kama Twanga Pepeta hawana washauri wa maana?

    Ilitakiwa wajue kwamba visa zote walitakiwa kuzitafuta wakiwa Tanzania. Ukiwa huku Ulaya huwezi kuomba visa ya nchi nyingine mpaka uwe na visa kwenye hiyo nchi unayoombea inayozidi miezi sita.

    Kuna haja ya kuwa na mahali pa kuwashauri wasanii wetu tena bure kwa faida yao maana wakifanikiwa na Tanzania inafanikiwa.

    Kama wanataka msaada wengine tuko tayari kuwasaidia bure kuelewa nini kinatakiwa wakitaka kufanya maonyesho nje.

    ReplyDelete
  9. Heeeeeee!!! jamani nyasi ni nyasi tu hata ukizitia chumvi na nyanya ziatabaki nyasi. Sasa kweli huyo ndugu wa holand ndo alijiandaa kiasi hicho, heeheee, ancha nicheke mie. Hata kazini haendi, jamani ushambenga huo. Sasa si apande ndege arudi nyumbani aje awaone twanga. Anawalazimisha mambo wasiyoyajua, Michuzi kashaeleza kuwa poleni kwa usumbufu utakaojitokeza, mtu lazima tu agombe. Mtajiju, rudini kwenu.

    ReplyDelete
  10. We mwaipopo.hayo yote uliyoandika naasira yote ya nini shukuru umejulishwa kuwa hawataweza kufika NL.ingekuwa imeahirishwa konset ya snoopy dog ungeridhika kwa kuwa ni mnyamwezi.ila unashindwa kueshimu bendera yako ambayo imekueshimu na kukujulisha kinachoendelea.toka umezaliwa na kufika hapo NL umewahi kusikia Mlimani park inakuja piga hapo?na wakapiga.Iheshimu twanga na na uongozi wake na pamoja na watu ambao wanajitahidi kuandaa matamasha haya ulaya.Kuweni wastaarabu kwani kwa juhudi zinazo fanyika.Kama unawahitaji twanga watumie mwaliko na uandae yote yanayohitajika halafu uone matokeo yake.Tuliza Ball umesha kuwa mtu mzima sasa mpaka umefika ulaya.
    Ni mimi
    Mkereketwa wa Twanga.
    Bagdad.Iraq

    ReplyDelete
  11. Wee anon usituzingue na maneno yako eti nyasi ni nyasi au wewe ni kibaraka wa ASHA BARAKA unajaribu kupoza haya mambo? anavyosema mwaipopo ni kweli tupo hata mimi nimeomba ruhusa kazini kwani nisingeweza kucheza dansi usiku wa ijumaa rotterdam na kuwahi kwenda kazini groningen jumamosi asubuhi kama uijui holland uliza sio unapayuka tu. watu kweli tumetiwa hasara.

    ReplyDelete
  12. Aisee wewe mkereketwa wa bagdad unaoneka ndio leo umeingia ktk hii blog yetu na ndio maana urukia vitu ambavyo uvijui basi taarifa yako sikinde ngoma ya ukae walikuwa hapa miezi miwili iliyopita na ungekuwa unaingia ktk blog hii Michu alikuwa anawarusha ebu mzee michu muwekee ile picha ya mlimani waliopiga na mwanamuziki maarufu wa kibongo hapa holland garinona aone. wewe kama unataka uweunaingizwa bure twanga tafuta njia nyingine sio hiyo uliokuja swala la kulalamika na bendera ni vitu tofauti wazee wa holland hasira zetu zipo pale pale twanga wametuuzi sana pamoja na promotor mchwara wa hapa holland.

    ReplyDelete
  13. Kama alivyoambiwa Jemedari Naaman,
    Mbona Mwaipopo hajasema jambo kubwa? Wanachokiomba wadau wa Netherlands ni Kiongozi wa bendi mwenyewe kutolichukulia suala hili mzaa, atoke hapa na kuomba msamaha tu mwenyewe kwa maelezo yanayojitosheleza yaishe(soma comments za watu wanaoelewa utaratibu wa upatikanaji wa visa walivyokata issue).
    Watu hawajafanya assignment zao na kupata kilichokuwa kinaendelea toka tangazo hilo litolewe hadi Onesho lilipoahirishwa.
    Aidha Kaka Michu kwa sababu jana umemtambulisha Lawyer wako kwetu basi muulize tu polepole implications za Tangazo kama hilo walilolitoa ugaibuni na apime sababu ya kuhairisha halafu usikie atakwambia nini.
    Tuwe waungwana hakuna cha snopy mbwa wala cha ukereketwa uchwara wa kuomba free pass kwenye gate la Leaders Club hapa, ukiteleza sema tu mapema ili upewe mkono unyanyuke na safari iendelee!!
    Mdau wa Antwerp

    ReplyDelete
  14. Halafu waambieni hao twanga waache ushamba UK si London tu, kuna miji mikubwa nako hawajaenda, kuna Birminghma, kuna Manchester. Vipi wana mpango wa kuja huku?

    Manchester City tunawakaribisha.

    ReplyDelete
  15. jamani yamekuwa haya tena
    someni

    http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=67238#post67238

    Mzee mzima Baraka Msiilwa ingilia kati omba msamaha yaishe maana hao jamaa naona wameshupalia hili suala.

    ReplyDelete
  16. Wadau mnaomponda Mwaipopo mnachemsha..yeye kuja bongo its something else it,s not a matter of travelling fro moro to dar, it involve alot..suala he was prepared and planned for Twanga in Holland!!mambo yanapangwa bwana kazini lazima u call sick, holiday whasoever na hulipwi siyo style za kibongo za ma ED tuu..Ukiwa bongo huwezi feel usumbufu anaousema kama wakiarisha Leaders utaenda TTC club..Mimi nafikiria nafsi yangu jinsi nilivyojiandaa mwezi na nusu je wasingekuja London? Duuh!!namuelewa Mwaipiopo so wasuuza vinywa tulieni msichanganye makali ya maisha na usongo wa ulaya kwenye concerns za watu wa holland..let them talk kama hamjui situation za majuu tuluieni wachamba vinywa.

    mdau, london

    ReplyDelete
  17. we unae mtetea mwaipopo kwa utumbo wake wote mnaonekana ni wakimbizi vumilieni mpate karatasi mrudi bongo ukaone mugongo mugongo.pigeni kelele hakuna anaye wajua.
    Bagdad

    ReplyDelete
  18. Wee mdau wa bagdad wacha kutuchengua fikiria kwanza hapo ulipo utatokaje. yote hiyo kwa sababu ya kutaka kuja ulaya kwa mguu ukajikuta umeingia bagdad achana mambo ya twanga tafuta njia utoke hapo kabla ujalipuliwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...