wadau uhondo wote huu ulikufa mara tu tv ilipoingia bongo. yaani majumba yote ya sinema yalifungwa na kuanza biashara zingine, ati kwa sababu kuna tv. hii imekaaje wadau?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Aah mi si nilishasema hao wahindi hawajui marketing bwana. Na sababu kubwa ni kwa vile hawataki kujichanganya na jamii ya weusi. Sasa wewe utamuuzia bidhaa mtu ambaye hata humjui vizuri? Mbona Marekani TV zilikuja na cinema zikaendelea kushamiri?? Angalia hata hii Dar Cinemas, bado haifanyi marketing za maana. Wao wanajidai wanafocus upper class, lakini wangekaa chini na kuisoma jamii kidogo wangeweza kuvuna pesa nyingi zaidi hata kwa middle and low classes.

    ReplyDelete
  2. Wamefanya maamuzi ya haraka kufunga maholi ya cinema mbona ulaya bado kuna theaters na watu wanakwenda? kuona movie chox au odeoni kuna raha yake bwana ..mmh bro umenikumbusha mbali enzi za 'disco dancer' ha ha haaa...kupata ticket ilikuwa big deal

    ReplyDelete
  3. Imekaa vibaya hii bado haijatulia..wenzetu wamekuwa na tv since way bak na hawaku get rid of the cinema hallz...lakini sisi sijui tuliona tumefika..na tv channel ilikuwa moja tuu CTN ambayo most of the the time ilikuwa inaonyesha CNN ..NINI HII!!!! Na jumba la sasa hivi ndio expensive sio kila mtu anaweza kwenda ..labda ndugu zake miss TZ hehe...mdau UK

    ReplyDelete
  4. Baba Muhdini, hiyo picha ya kipande cha gazeti imenifanya kushika machozi (hold back tears). Jamani, is this right? Miji yote? Nakumbuka nilivyoona picha ya Eek Baap Che Bete pale Empress, na picha ya Star pale Chox, na picha ya Titanic hapo Avalon: nilikuwa nimepania kuto-angalia Titanic ya video hadi niione kwenye big screen. OMG, I miss the rumbling steriophonic acoustics of Avalon Cinema!

    ReplyDelete
  5. MAJUMBA YA SINEMA YAMESHINDWA KUJIENDESHA KWA SABABU YALIKUWA YANATUTAPELI,HAWAKUWA NA SINEMA MPYA ON TIME.

    MIMI BINAFSI NIMESHAWAHI KWENDA SINEMA KUANGALIA MECHI YA SIMBA NA YANGA ILIYOCHEZWA NYAMAGANA MIAKA YA SABINI. KITU AMABCHO TAYARI KINGEKUWA KTK VDEO .

    ULAYA NA USA MAJUMBA YA SINEMA YAPO MPAKA LEO KWA SABABU WANAPATA MOVIES MPYA KABLA HAZIJAINGIA KWENYE VHS OR DVD .

    ReplyDelete
  6. Bro michu umenikumbusha enzi ya Drive -in cinema au Newchox,Odeon,Cameon na British Council kulikuwa na cinema! kwakweli cinema km hizi zina raha yake bwana asikuambie mtu. Tv nyumbani ni nyumbani ni sawa nakunywa lager home au kuangalia mpira au pambano la ngumi home kwenye luninga! Na lakwenda nje lina ladha tofauti! kila kitu kinahitaji wakati wake kwakweli wake za watu tulikuwa tunapata outing at least! sasa hivi outing uende bar ukanunuliwe mbuzi na bia kwanza kabla hamjaondoka ugomvi!Kwakweli inatukumbusha wengine wakati tunachumbiana yani michuzi umenigusa sana nataka hata kulia, hilo la mwenge lakupeleka watoto.

    ReplyDelete
  7. Hii haijakaa vizuri michuzi,sijui ni ushamba wetu wabongoooo,mbona nchi za wenzetu yaani ulaya na amerika wana matv majumbani kwao te nmakubwa ya kufa mtu na bado kuna majumba kibao ya sinema.unajua ku raha ya kuangalia sinema nyumbani kwenye tv na kwenda kwenye majumba yanayochezesha sinema.sisi bado tupo nyuma ingawa kuna majumba 2 ya cinema lile la mwenge na GAME

    ReplyDelete
  8. Enzi hizo kweli mambo yalikuwa Shega, Ingawa Sinema zilikuwa zinachelewa lakini tulikuwa nanazifaidi, Hata huko mikoani kulikuwa na majumba ya sinema...

    Nahisi Video (VHS)zile pirated ndizo zilichangia kufa kwa majumba ya sinema..

    ReplyDelete
  9. Issa Michuzi, Kuna kitabu nilisoma zamani sana sikikumbuki cha historia ya zanzibar, inaonesha zamani znz ndio kwenye tanzania ni ya kwanza kwa train ilikuwa inatoka forodhani mpaka bububu, na pia kwa traffic light za chini zile na pia LINDI ndio alikopatikana mnyama yule mrefu kuliko wote ambao wazungu wao wanasema amepatikana uzunguni mbona waafrica wakigunduwa kitu hatuthaminiwi wala hatusifiani?.

    ReplyDelete
  10. Michuzi: Majumba ya Cinema yalikufa lkn kwa sasa yamerudi na yanamilikiwa na Mtanzania mwenye asili ya Asia SABODO
    1.NEW WORLD CINEMA-MWENGE
    kuna kumbi tatu hapo!!

    2.CINEMARAX-MLIMANI CITY ambapo pia
    kuna kumbi tatu.
    Tatizo bei zake ni balaaa....

    ReplyDelete
  11. Raha ya kwenda kwenye juma la Cinema ni BIG SCREEN BIG SOUND, maana mtu unamwona kama alivyo na hata kikaratasi kikidondoka unakisikia, ndo maana wakabuni Home Theaters. Kaka umetukumbusha mbali sana. Hapo pembeni naona chata ya SilverSands inanikumbusha Disco la MThree chini ya DJ Eddy Sally. Yupo wapi siku hizi?

    ReplyDelete
  12. Umesahau siku za Drive In. Pale palikuwa penyewe. Kile kiti cha nyuma kwenye gari mmmmhhh!

    ReplyDelete
  13. Nakubaliana na mengi yaliyosemwa. Pia kuna kitu kingine:survival economy...rate of substitution is very high.

    ReplyDelete
  14. Mtanzania wa kawaida hata hela ya unga kilo moja hana je kwenye jumba la sinema la kisasa atakwenda?....Picha ya leo leo Ulaya au Marekani haiwezi kulipa ukiileta bongo!..Tuendelee na TV au DVD mbovu za wahindi!....Mungu ibariki Tanzania na watu wake!

    ReplyDelete
  15. Eeeh, wenyeweeee! Vijana wa siku nyingi naona kaka Michu kawakumbusha mbali kweli... baby boomers

    ReplyDelete
  16. Mimi nadhani kufungwa kwa majumba ya cinema kunatoka na nguvu za kiuchumi tu.
    Kwa mfano kama demand ya watu wa kwenda cinema ingekuwepo hayo majumba yasingefungwa hadi leo nani asiyetaka pesa?
    pili baada ya watu kuwa na TV na Video majumbani mwao, wengi walikuwa wanaangalia cinema kupitia kwenye video zao. Ikumbukwe kwamba Tanzania population yetu ni ndogo sana na haina nguvu za kiuchumi kama vile mataifa makubwa. Wengi wa waenda cinema kila mara ndio walikuwa wanjia mbadala ya kuangalia cinema hizo. Hebu jiulize ni mara ngapi ulikuwa unakwenda cinema?

    Kwa Sabodo sasa hivi kuendesha Cinema pale mwenge ni kwamba anafanya biashara katika mazingara tofauti na miaka ile ya nyuma. Ana changamoto nyingi zinazomkabili kama mtu aliyewekeza pesa zake ni lazima mradi wake uwe endelevu na urudishe gharama za uwekezaji.
    nadhani biashara inaweza kupanuka kadri ya watumiaji watakavyoongezeka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...