HABARI ZIMETUFIKIA PUNDE KWAMBA HUKO MBEYA SEHEMU ZA MBALALI KUMETOKEA AJALI MBAYA SANA YA BARABARANI NA WATU KADHAA WAMEPOTEZA MAISHA YAO HAPO HAPO ASUBUHI HII.
TUNAENDELEA KUFUATILIA NA MTAPASHWA KADRI HABARI ZITAVYOPATIKANA. WAHUSIKA WAMEELEKEA SEHEMU YA TUKIO NA WATATOA TAARIFA HARAKA IWEZEKANAVYO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Langu lakusema hapa nikwamba madereva wote waanze mitihani ya udereva upya bila kupita kwa rushwa, kwani madereva wengine wakijua kuendesha kidogo tu basi wananunua leseni kwa rushwa na matokeo yake ni kuua watu.
    Jingine inatakiwa hii serikali i-update hizi sheria za barabarani, madereva wazijue saini zinazosema hapa mwendo kiasi gani na hapa hutakiwi ku over take,
    Sio kuendelea na saini za miaka ile wakati Bongo ilikua na magari machache. Wakati huu ndio wakutakiwa madereva wazijue vizuri saini.
    Dereva asingetakiwa kufanya mtihani kwa vitendo bila kujua mtihani wa nadharia, kuzijua saini zote ndio aje afanye mtihani wa vitendo.
    Na wasimamizi wa mitihani wawe wametoka serikalini na wawe wanajulikana kitaifa sio kufanya mitihani vichochoroni kwa rushwa, matokeo yake itakua ndio kama hivyo watu kila mwaka wanauliwa kama mbuzi kwa ujinga wa wachache.
    RUSHWA ITATUMALIZA
    Kama sio rushwa basi mambo yote haya yangeangaliwa kwa undani bila kujali vipesa vya mtu.

    ReplyDelete
  2. Naskia hawa jamaa walikuwa wamekodi basi la sabco kuja dar kuangalia mechi ya leo ya Taifa stars..mbona hii game itaondoka na wengi

    ReplyDelete
  3. Video ya Taifa Stars..

    Taifa Stars Video.

    http://ie.youtube.com/watch?v=apTfdv5AcW8


    Embedded code, zipo kwenye link hiyo hapo juu, kama utapenda kuipa post nzima kwa ajili ya Taifa Stars


    By Mchangiaji

    ReplyDelete
  4. NI HABARI YA KUUMIZA SANA.

    MWENYEZI MUNGU AZIPUMZISHE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI.

    PIA TUNAWAOMBEA MAJERUHI WAPATE KUPONA HARAKA NA KUWAPA POLE WALE AMBAO KWA BAHATI MBAYA WAKAPATA VILEMA VYA MAISHA.

    MWISHO TAHADHARI::
    MADEREVA JAMANI,MADEREVA JAMANI MTATUMALIZA MAMBO MENGINE SIO KUMSINGIZIA MUNGU.

    SIJUI CHANZO CHA JALI ILA NAHISI KAMA KAWAIDA YAO UTAKUTA MWENDO KASI.

    PIA NI TABIA ILIYOZOELEKA KABISA TANZANIA WATU KUPENDA KUENDESHA MAGARI WAKIWA WAMESHALEWA POMBE AU WAMEKULA MAUNGA YAO.

    MFANO LEO HII TUKISHINDA HII MECHI WENGINE UTAWAKUTA WANASHEREKEA NA NA BIA MKONO MMOJA NA MKONO MWINGINE STERINGI.ZISI IS VERY PAINFULL

    TUWE MAKINI TUFUATE SHERIA ZA USALAMA BARABARANI.

    WAPUMBAVU WOOOTE MNAO LEWA NA KUENDESHA.WASHENZI WA TABIA MNANITIA MACHUNGU.

    NINGEKUWA LI POLICE TRAFFIC HAKUNA CHA FAINI.NIKIKUDAKA UMELEWA UNAENDESHA NAKUPIGA KWANZA NAKOZI,YAANI MAKONDE YA KUTOSHA NA UKICHUKULIA NINA BODE KUBWA.

    UKITAKA KULETA KIBESI NACHOMOA BASTOLA NAKU-DITOPILE.SHEEEZI TAIPU!! MNANITIA HASIRAA!!

    ReplyDelete
  5. Bw. Issa Michuzi na swali naomba utupe jibu humu je senegirls wanaanza mapema au wakianza wao na sie huku tutakuwa tushaanza ball, nabaazi ya timu kama uganda na eritrea na wengineo ambao tunaangaliana kwa point muhimu ila watanzania nawaomba hata tukifungwa au tusifike ghana tusivunjike moyo kwani maximo kwaiweka timu pazuri inshaallah tutafika south africa.

    ReplyDelete
  6. Kaka Michu,

    Mama yangu alikuwemo katika hao waliopata ajali, namshukuru Mungu yeye ameumia kidogo tu amesalimika alikuwa kwenye gari dogo, walikuwa wanapeleka mitihani ya darasa la saba, aliokuwa nao kwenye hilo gari wamefari kasoro yeye, ni vile tu kwasababu ameokoka (mlokole), shetani hampati tena, la sivyo tungekuwa tunaongea habari nyingine saa hizi.

    Mimi niko ughaibuni, naomba unipe habari zaidi na picha ikiwezekana.

    JJ.

    ReplyDelete
  7. Michuzi, tafadhali waambie wadau kuwa kwenye blogu ya Mjengwa kuna maelezo zaidi na picha za majeruhi wa ajali hiyo. http://mjengwa.blogspot.com

    ReplyDelete
  8. Poleni sana walioumia. Poleni sana wafiwa.

    Mungu awape nguvu ndugu wa marehemu katika kipindi hiki kigumu.

    Mungu awalaze mahali pema mbinguni. AMEN.

    ReplyDelete
  9. TFF ITAFANYA JAMBO LA BUSARA IWAPO WAWEKA KWENYE RATIBA YAO JAPO DAKIKA MOJA YA KUSIMAMA,KWA HESHIMA NA KUWAOMBEA NDUGU ZETU WALITUTANGULIA MBELE YA HAKI.

    MWENYEZI MUNGU AZIPUMZISHE ROHO ZA MAREHEMU MAREHEMU PEPONI.AMINA

    ReplyDelete
  10. MWENYEZI MUNGU AWALAZE MAHALI PEMA:AMIN

    ReplyDelete
  11. Dada Chemi Che-Mponda,

    Najua umesikitika sana sana kwa habari hii ya ajali, na unaungana na wafiwa wooote nchini na popote duniani.

    Ila Dada Chemi, waliokufa hawalazwi mbinguni, inategemea kama mtu akifa katika Kristo yaani ulikuwa unaambatana na Mungu basi utaenda peponi na kama ndio hao tena wakina "starehe nyingi za dunia" wakamsahau Mungu basi ndio hivyo tena "ngoma isambe".

    Dada Chemi, Mbinguni wako wazee 24, wenye uhai wanne, makerubi na maserafi tu na Mungu yuko kila mahali hana "permanent spot" maana hiyo mbingu unayoisema ambayo wewe huwezi kuifikia, kwake yeye ni ndio mavumbi ya miguu yake. Na paradiso (paradise) wamewekwa wale waliokufa katika Bwana ambao tutaungana nao tena siku hiyo ikifika na ukiwa kama ni mmoja wao basi Mungu akishamaliza kuhukumu ulimwengu ndio sasa "Anawamuvuzisha" peponi.

    Dada Chemi Ndio maana Yesu alisema "Tubuni kila inapoitwa leo ili mjiweke safi msije mkaachwa", Ndio maana walokole wengi kabla ya kuanza safari huwa wanaingia kwenye maombi kuomba wafike salama maana shetani anawatafuta sana walokole, lakini sisi tunawaona "wamechanganyikiwa", kama Mama wa huyo JJ hapo juu yeye ni mlokole, hajakufa wala kuumia sana maana malaika walikuwa wanamlinda, sema AMEN.

    Kazi kwako Dada Chemi jiweke tayari tengeneza njia yako mwanawani, Mungu akusaidie.

    BMW

    ReplyDelete
  12. Inasikitisha sana, Pole kwa wafiwa wote, na watanzania wote kwa ujumla, pia tunawaombea majeruhi wapone haraka.
    anon wa 3:31 hapo juu, sio kwa vile mamako kaokoka ndo maana hakufa, usiseme hivyo, sema siku yake ilikuwa haijafika..unaposema hivyo, unawaumiza wale ambao ndugu zao walifariki, kwani una uhakika gani kuwa wengineo walikuwa hawajaokoka na je waliookoka ndo hawatafuka kamwe? mshukuru mungu kwa kumuachia mamako uzima, na tuzidi kuwaombea wafiwa faraja ya mwenyezi mungu.

    ReplyDelete
  13. 1. anony mama yako alikua anapeleka mitihani na gari la mchanga? Habari ni kuwa basi limegongana na Lori la mchanga

    2.Na sio kwa vile mama yako ameokoka ndio maana amepona....if it is true alikua kwenye hiyo ajali, siku yake ilikua haijafika. Siku ikifika haina cha mlokole wala nini.

    3. Wee hapo juu mbona umemwamkia Dada Chemi hivyo? Usimhukumu mwenzio usije ukahukumiwa. Toa kwanza boriti kwenye jicho lako.

    All we need to remember is this tomorrow is not promised. So live each day as if it were your last...that is to say be nice to people, don't take people for granted and if you want to be a MOUTHWASHER be Listerine mouthwash. Don't just write crappy or make something up out of thin air about someone for the sake of the blogger. Matured people have feelings too

    May God continue to bless and comfort the family and friends of those who passed away at this difficult time

    ReplyDelete
  14. BMW thanks for making my day, nimecheka mpaka basi, anyways ni uchambuzi wa kweli na nimependa jinsi ulivyoweka humour ndani yake, kweli nilihitaji kitu kama hicho baada ya habari mbaya kama hizi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...