michu ee
hebu niwakilishie hii. Si mara moja wala mbili hawa jamaa unaowaona hapo ambao tumezoea kuwaita FFU siku hizi wanafanya kazi za askari wa usalama barabarani. Mi nataka kujua tu hivi hii imeanza lini? Maana mwanangu wanatisha na mijinguo na mijibunduki yao utafikiri tuko baghdad au kule ukanda wa gaza. Hivi askari wa usalama barabarani wako kisheria au mtu yeyote akiamua anaweza kusimamisha magari na kuhoji madereva ili mradi uvalie kijeshijeshi?
Mwanangu hata picha yenyewe nimeipiga kimachale machale kweli maana wangeniona sijui ingekuwaje. Hapa ilikuwa taa za kawawa na nyerere maarufu chang'ombe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. hiyo ndio bongo bwana,sasa wewe unafikiri hawo ffu watapata wapi rushwa?hao wanatuliza fujo na kukaa kambini sasa wewe siunawajua wafanyafujo watakupaje rushwa?wacha watafute rushwa waishi vizuri kidogo kama askari wengine na traffic mishaara yenyewe ndio hiyo.wabunge kazi yao kujiongezea posho hawakumbuki watu wengine.

    ReplyDelete
  2. Wewe acha ushamba na mambo ya ajabu.Askari wote wa jeshi la polisi wanasoma na kufahulu mambo ya kipolisi pamoja na kozi ni moja.Wote wanasoma masomo kama Traffic law,law of evidence,police duties,criminal law,first aid,Law of Investigation nk.Siku ya mwisho maarufu kama passing out,inatokea tu kama zali wengine wanapelekwa traffic,FFU,GD,Mbwa na Farasi,madawa naIB.Sasa wewe ukikamatwa na FFU wakati una makosa unataka kuleta ushamba gani hapa hapa kijijini?????FFFU amesoma traffic law na anajua kila kitu sasa wewe shida yako nini???Si umwambie mwende mahakamani.
    Watu wengine bwana!!!Kwa hiyo unataka tukuonee huruma au tuwaseme Polisi????Acha ushamba wewe na tii sheria za barabarani.Punguza hiyo mi-speed yako na kuendesha ukiwa umelewa.Unafikiri hatuji kuwa Bongo mnaendesha hata kama ukiwa bwakisi???HATUKUONEI HURUMA NG'OOOOOO.KOMA.
    Majita

    ReplyDelete
  3. Jamani mtarumbana buree kwa kitu msichokijua...

    Hao FFU mnao waona ni kikosi maalumu kwa ajili ya kuangalia usarama barabarani wakisaidiana na trafic, na hicho kikosi kiliundwa tangu mheshimiwa Jk aingie madarakani, kwa hiyo once mnapokutana nao hao jamaa msifikirie wapo kimakosa la hasha wapo kisheria kabisa na ndo mana unaona hata vihiace vimepunguza kutanua tanua barabarani maana wakikamatwa shughuli yake ni pevu.

    ReplyDelete
  4. bongo mshikaji wangu nuksi mi niliibuka na kamera yangu wakati wa holiday si nikapiga picha mara jamaa wakanidaka kisa eti siruhusiwi kupiga picha maeneo hayo nyeti, mi nashangaa maana sasa wazungu wanatulia kwao wanaelekeza satelaiti zao na kukuchungulia kupitia google, sasa hapo kuna haja ya kusema usipige picha, upungufu tu wa maarifa ndio uliojaa kwenye vichwa vyao hao.

    ReplyDelete
  5. Two words, martial law, whats next? A police state?

    ReplyDelete
  6. FFU ni polisi kama polisi wa kawaida, hicho ni kikosi maalum "Field Force Unit" ndani ya jeshi la polisi. Trafiki pia ni kikosi ndani ya jeshi, kuna CID na kuna general duties. Sasa kwa vila jeshi la polisi ni Usalama wa Raia hata nembo yao inasema hivyo, basi hakuna mipaka ya polisi yeyote kufanya kazi ambayo Wa-TZ tumezoea kuona inafanyika na polisi mwingi. Isipokuwa tu! Malindo ya Benki ndo yanafanywa na FFU. Pia hata trafik wa kawaida anaweza badilishwa kitengo na kuwa FFU pale inapobidi, huwa wana badilishwa sana vitengo kwa ajili ya kuboresha ufanisi. Ukiona Kamanda anawaacha hao jamaa kikosi kimoja muda mrefu basi ni uzembe tu.

    ReplyDelete
  7. na wangekuona ungewaeleza!...walianza vizuri SANA...sawa na counterparts wao wa "TZR"...but kama kawaida, ngoma zetu huwa hazikeshi!...hawana tofauti yoyote na wengine!...ni biashara tu!...nyie mlio huko nje hamuwezi kuelewa...wakiwa hawana kitu hawa hata uwe vipi hawakukosi kialfu japo tano kitakutoka tu...credibility yao ime fade completely...

    ReplyDelete
  8. Hao jamaa ni kweli walianza vyema sana na tuliwapenda na kujisikia tumepata ukombozi....hata hivyo siku zilivyokwenda c wao wala mabosi wao wanasikika tena...yaelekea walikuwa wanadanganya toto...sasa kuliko ukutane nao ni afadhali ukutane na hao wakora... jamaa hawa hawafai,,,na hata ukiwaambia twende kituoni watakupeleka na watakuchomoa hata pale kaunta....wamekosa aibu na maadili mbele yao wenyewe na mbele ya Mungu... Ole wao na familia zao kwa kula haram hizi....

    ReplyDelete
  9. naomba kukusaidia bwana kaka kuwa; who is a traffic officer? jibu any police officer in uniform when perfomming traffic duties. sheria hiyo haisemi white uniform. kwa hiyo ni any police uniform. utaratibu wa tofauti za unifomu ni kuwezesha utambuzi wa haraka. tena wote wanapata mafunzo yote ndio maana leo aweza kuwa traffiki, kesho ffu na keshokutwa cid.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...