sio kweli kwamba watunzi na waandishi wa vitabu hamna bongo. james bwana ni mmoja wapo ambapo juu anaonekana na watoto wa shule akiwasomea riwaya yake kwanza ya watoto iitwayo mganga pazi. kwa kuongezea mdau james ameshatoa kitabu kipya alichochapa mkuki na nota kiitwacho 'haramu' ambacho nimemaliza kukisoma na si mchezo. ukitaka nakala yake nao kupitia sales.mauzo@mkukinanyota.com ama wacheki www.mkukinanyota.com
james bwana pia ndiye loya wangu....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. hongera James Bwana!
    ILA MICHUZI BWANA, SASA KAMA HUYO NDIO LAWYER WAKO UNAMWAMBIA NANI? UMEULIZWA?

    ReplyDelete
  2. "james bwana pia ndiye loya wangu...."

    thanks for the disclaimer braza Michuzi. Maana nilikua najiuliza imekuwaje huyu bwana tunasoma habari zake kwenye globu hili tukufu, kumbe hiyo ndo sababu.... (i'm just kiding). But on a serious note, nampa 'ushavu' bw. james maana tunahitaji watunzi kama hawa.

    ReplyDelete
  3. MIMI BINAFSI NINA KUPONGEZA SANA BW. JAMES KWA KUWA NA KIPAJI, FURSA, NA MAPENZI YA KWELI KWA JAMII HASA WATOTO.
    SI WOTE AMBAO HUAMUA KUTUNGA VITABU KWA AJILI YA WATOTO, WACHACHE WA WAANDIKA VITABU WA KITANZANIA HUANDIKA JUU YA MAMBO MENGINE MBALIMBALI LAKINI SIYO MAHUSUSI KWA WATOTO.
    LEO HII TUNASHUHUDIA BAADHI YA WAZAZI WAKIPELEKEA WATOTO WAO MAGAZETI YA UDAKU NYUMBANI KWA AJILI YA KUSOMA, (NI MAPUNGUFU MAKUBWA)
    MAGAZETI HAYO YAMEZAGAA YANAUZWA KILA KONA BILA KIZUIZI KUACHIWA WATOTO KUYASOMA.
    HAKUNA BASI HATA TAASISI INAYOPIGIA KELELE JUU YA JAMBO HILI.
    HAKIELIMU? LABDA HALIKO KATIKA MASLAHI YAO? SIJUI TAASISI NYINGINE? KIMYA?

    NINAKUUNGA MKONO JAMES KWA KITENDO CHAKO CHA KUKAA NA WATOTO UKIWASOMEA KITABU, KWANI UNAWAPA HAMASA KWA WAO KUJISOMEA VITABU NA MAJARIDA MENGINE MENGI KADRI WANAVYOKUWA.
    KWA WENGI WATANZANIA, HATUNA UTAMADUNI WA KUJISOMEA NA HILI NI TATIZO HADI KATIKA SEHEMU ZA ELIMU KWA MAANA YA MASHULENI HADI VYUONI. NINA TOA MWITO KWA WAZAZI PAMOJA NA WALEZI WENGINE, TUJIZOESHE TABIA YA KUWASOMEA VITABU VYA HADITHI WATOTO HAWA AMBAO NI WADOGO KILA SIKU KABLA HAWAJAKWENDA KULALA. HII ITAWASAIDIA WAO KUWEZA KUPENDA KUSOMA VITABU KADRI UMRI WAO UNAVYOONGEZEKA NA WATAPATA MAARIFA MENGI KUPITIA KUSOMA.

    KWA MARA NYINGINE TENA NINAKUPONGEZA KWA MCHANGO WAKO MKUBWA AMBAO NI WACHACHE WANAWEZA KUUONA NA KUUTHAMINI.

    ReplyDelete
  4. big up James,kazi nzuri sana na vipi soccer bado unacheza..loooooong time sana mazee pale Mzumbe high school na hongera sana kwa kuoa na kuwa mwanasheria,nipo hapa Wall street NY (Dow Jones)...nitakutafuta najua pa kukupata

    ReplyDelete
  5. Nawewe anony wa kwanza kuna mtu alikushikia bunduki usome? na uliombwa umuulize michu? kuku weee!!!

    ReplyDelete
  6. Hongera JB! Unakumbuka Vitara:-)BOSTON

    ReplyDelete
  7. Bro James! Hongera sana, this is really impressing! Keep it up. Long time since za mzumbe - kilakala. Usisahau kutunga hadithi kuhusu dada wa kilakala that time, kwani itakuwa hadithi nzuri.

    Ciao! All the best,
    One of the sisters of Kilakala High School class of 1990!

    ReplyDelete
  8. Kaka James nafikiri unajuwa kuwa
    siwezi kunyamaza kwa hilo unalo lifanya kwani unafanya kitu cha maana katika kuwaelimisha, kuwafrahisha na kuwakanya vijana,kupitia katika kuandika vitabu.Hapa Marekani umri wa (young adult)wanasumbua sana sijuhi huko nyumbani vijana wa umri huu wana vitabu vinavyo walenga? au diyo wote wanawekwa kwenye kundi la watoto? natamani wapewe attension kwani hawa ndiyo wataitwa baba mda si mrefu. Nakutakia kila na kheri
    Projestus.

    ReplyDelete
  9. Jamaa nakumbuka Mzumbe alikuwa anasakata soka ile kishenzi---kona zake zilikuwa kama zinajichonga hivi--jamaa mtaratibu asie penda makuu kama group lake la mirambo---Hongera sana tunakufuata

    ReplyDelete
  10. Big hands to JB..our kids will have fun to read Mjomba's books..keep it up

    Chonde.R ,UK

    ReplyDelete
  11. Nakuona James, hongera kwa kazi nzuri.
    Tutafutane basi muda mrefu umepita

    Patrick Kamera

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...