kuna mdau kanitumia hii sasa hivi akijigamba kwamba yeye kapata kazi hapa, nchini ubejgiji...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. mzee mwenyewe kazi ni kazi tu ,cha muhimu pesa tu.tena huyo kwa ulaya ana kazi nzuri,kuna za kuosha wazee!!

    ReplyDelete
  2. kumbe hata ubelgiji wabeba maboksi..hee tena inaelekea ana degree ya kubeba maboksi..maana anaonekana ni expert...alivyoyapanga hayo maboksi..yamependeza...ajitahidi kuyapanga anaweza kupata scholarship (masters)..ya kufagia snow..au kuosha vyoo.

    ReplyDelete
  3. Usijali Mdau wa Michuzi.
    Bora mkono uwende kinywani, na pia upate safari za chooni. Mabox ndo yenyewe bwana. Kazi njema

    ReplyDelete
  4. Hongera sana mdau kupata kazi.Kazi ni kazi.Mradi huombi mtu wala kutapeli mtu.Dukani hakuna anayeuliza kama pesa umebeba box au umechokonoa choo.Hongera sana.

    Kama kuna nafasi za kazi kama hizo watafutie na watanzania wengine wawe nduguzo au rafiki.Tunao wengi tu nchini kwetu hawana ajira na waweza fanya kazi kama hizo.

    Tusaidiane watanzania kutafutiana ajira nje kama hizo ya nchi kwa ajili ya watu wetu wasio na ajira tukusanye pesa tuwekeze nchini kwetu.

    koloboi@yahoo.com

    ReplyDelete
  5. Mbeba maboksi mwingine huyo , anyway kazi ni kazi ilimradi mkono uingie kinywani, i guess someone has to do it.

    ReplyDelete
  6. watanzania ndo maana hamuendelai,kwani mi sioni shida ya kubeba hizo boksi za choclate.
    kama morgage anailipa kwa kazi hiyo,na analipwa pesa nzuri,si lazima ave tai,mambo ya kizamani kuvaa suti au tai na huna kitu.
    kula mzigo vijana,usisikilize majungu.

    ReplyDelete
  7. Hongera kwa kupata kazi ya heshima. Tatizo tulilonalo wanawake ni kutokukubaliwa kwenye mtulinga wa maboksi. Msiyaone hayo maboksi yalivyotulia hapo...tatizo lake linakuja kwenye muda utakaopewa kukamilisha hilo zoezi. Muda unakuwa kiduchu kwa kazi kubwa. Lakini still hiyo kazi ni nzuri kwa vile ubebaji ni kwa kutumia mashine. Tabu tunayo sisi wakina mama....jamani usije ukasikia kazi ya kuosha vizee.....NI KUCHEZEA MA*I KWA KWENDA MBELE. Hata kama unavaa gloves lakini what about pua na macho. Mbali na hapo eti kazi inatakiwa ifanywe kwa upendo na huku unasmile..." hellow darling, ohh good girl...turn this side dear".....NI BALAA TUPU!!!!

    ReplyDelete
  8. Ni kweli ukilipa dukani,usafiri nk hakuna anayeikataa pesa eti kwa hoja kuwa umebebe mabox.Ndio maana wabongo wenye maendeleo hapa ni wachache,tunabaki tukitumwa hovyo hovyo na wegeni ndani ya nchi yetu.
    Badala ya kufurahi kuona wabongo wenzetu huko nje wanaishi kwa hadhi hata kama wanabebea mabox, hawaombi,hawaibi wala hawaiharibu sifa ya Tanzania tuna kashfu.
    Inasikitisha sana.

    ReplyDelete
  9. mmh hiyo miGUYLLAN mi chocolate naitamani kweli..mi sifichi wala nini, maboksi na mimi nabeba,tena napenda kazi sehemu kama hizo hapo na maduka ya chakula, njaa ikikomaa unachomoa chocolate moja unamumunyuma,KASHESHE liko kwenye macamera ya hawa jamaa,yamejaa kila kona,,hata mengine huwezi yaona,, kesho yake watafutwa, ooh kazi basi, hee imekuwaje,,,jamaa wanakuita, then wanakuonyesha kwenye screen jinsi uliyokuwa unaimumunya michocolate yao,,lol!!MI MZOEFU,sometimes kama vipi, nikimaliza kubeba mibox na kusafisha, basi udenda unakutoka , njaa nachomoa huko store ambako hamna camera, then natumbukiza kwenye lifuko la mauchafu, nikifika nje wakati wa kutupa mauchafu, nafungua fuko, natoa vilivyo vyangu, then natupa miuchafu yao, then unaanza mbele,,,mmh lol..hiyo ilikuwa zamani, sikuhizi nimekuwa , mmh LAKINI NJAA YANGU HAIJAKUWA....LOL!!!

    ReplyDelete
  10. DU, MABOX KWENYE KIYOYOZI, WALETENI WAMACHINGA WA TANDALE WACHUKUE EURO HAPA WAACNHANE NA LUMBESA!

    ReplyDelete
  11. Mbona office yake nzuri tu. Bongo wamekalia mabox lakini ukifika hawana hata aibu kuomba hela. Kila siku twende tukupeleke kuna hii sehemu imefunguliwa hujaiona. Ukifika uwalipike kila kitu. Kama mabox mazito msiombe kata kipafyum basi.

    Mnashangaza sana mngejua tu wachache ndio wamebeba nchi the rest hata sina la kusema.

    Mimi ni painter lakini ninakula, nina kwangu na ninatunza familia yangu. Ni wangapi hapo bongo wanawake na watoto bado wanaishi kwa baba na mama? Ni wangapi hawajui kesho watoto watakula nini? Mimi napaka rangi, nina mke na watoto wawili na niko shule....

    ReplyDelete
  12. halafu uzuri wa kubeba maboksi mamtoni, unaheshimika tu kama kawaida,,kukitokea virupurupu kazini nawewe utapewa,,vitrip vya wafanyakazi kwenda kurelax labda na familia na wewe mbeba maboksi unahusishwa, party za christmas, na shughuli kibao,,tena majuzi tu, tumeenda trip ya boat,wafanyakazi wote, boat yazunguka tu masaa kama matano night kali, watu tunakula na kunywa,,yaani mimi na boss mkubwa kabisa wa hilo kampuni tumekaa meza moja, tunagonga cheers..inatia raha, na motisha.Bongo nimekaa miaka kibao, sura hata ya balozi wangu wa nyumba kumikumi, kuiona NO, eti naye kutwa kwenye gari, christmas ikifika, yeye anaaalikwa party kwa mkuu wa mkoa, akina sie hakuna kitu,,gari yake vioo tinted, humuoni kabisa.

    ReplyDelete
  13. MZEE WA UBELGIJI HAO JAMAA NA UHAKIKA WANAKUPA TUITION FEE NA INSUARENSE..KUSANYA EURO HIZO TUENDELEE KUWEKEZA BONGO.HAKIKISHA UNARITAYA VIZURI(IF U NO WAT I AM TOKING ABAUTI) ILI UKIWA BONGO ULIPWE KIINUA MGONGO KUTOKA HUKO..MAMBO TARATIIIBU.

    ReplyDelete
  14. MABOKSI SI MCHEZO!!!
    Wanakijiji wenzangu,hebu hapo ulipo sasa hivi jiangalie na ujiulize mwenyewe una Elimu gani,una mali kiasi gani,Familia yako inaishi vipi na inakutegemea kiasi gani na wewe una majukumu yapi katika famila yako na unaisaidiaje.Majibu ya maswali hayo USIYAANDIKE Hapa kijijini.Baki nayo.

    Mimi wajameni ni mpiga Maboksi mashuhuri hapa Marekani.Hata hivyo nimetoka mbali.Nimejisomesha mwenyewe kwa kazi ya uvuvi.(mkokosi) kuanzia sekondari hadi chuo.Na sasa hivi nalamba maboksi.Ukubwa wa familia yangu naijua mimi.Na jinsi ilivyobadilika na sasa ni kati ya familia bora huwezi amini.Kisa MABOKSI.

    Sasa wewe unayejifanya unaponda maboksi,Hebu fungueni macho wajameni,mnafikiri hilo boksi ni kilo ngapi?Halafu baada ya kupanga hayo maboksi unafikiri hiyo "pale"(sijui kiswahili chake ni chanja) yani hapo maboksi yalikopangwa inabebwa na nini,hivi hakuna msaada wa ka-mashine kwenye kazi hii ya boksi na haya ma tekenolojia ya wazungu,Mmmm mie sina majibu.Swali la msingi kabisa unafikiri huyo mdau kwa kazi hiyo analipwa dola ngapi kwa saa????na je kwa uchungu huo (kama kweli anao),unafikiri kwa siku anafanya masaa mangapi???Nabashiri,anapiga si chini ya masaa 16.Sasa mtu kama huyo kwa wiki analipwa kiasi gani wajameni.
    Kazi kwenu.Mimi aaaah,kutoka uvuvi wa dagaa na sangara hadi kupiga boksi kwa hawa makitimoto?Tena umande sikuukimbia!!Shida nini bwn.Najaribu kuwapa challenge wadanganyika wenzangu.Acheni hulka ya kutaka kazi za mkono mfukoni na ki-degree chako huku unalipwa kimshahara utafikiri huujui mti aina ya "mdigrii" au hukukata "kiu" kwa wale wa mzumbe.Ughaibuni kimsingi ni pagumu ila kila mtu ana mitazamo yake.Kama wewe ni mtu wa kutaka ukirudi dar nzima wanyamaze kazi huna.Watapigwa viboko hao wadanganyika hadi wakuite mkuu kila wakati.Ila kama wewe ni mkokosi mwenzangu na unataka kubadili familia yako kutoka hali iliyonayo hadi sehemu fulani ya maendeleo kazi unayo.Utalamna boksi hadi kieleweke.
    Zingatia sana maswali yangu ya hapo juu.
    Kuanzia sasa siitwi MAJITA.Naitwa MAJITA WA-MABOKSI.Napenda wewee!
    Majita aka Wa maboksi.

    ReplyDelete
  15. Wewe anony ulianza kusema MABOX SI MCHEZO,
    kweli si mchezo,but kusema kwamba yamekutoa kweli itakuwa haulali,na nakupa pole kwa kujidanganya na kuwaita watu wa TZ wadanganyika,wewe uko kwa wazungu huko ni kama houseboy,sasa mi nikobongo hapa nina ofisi yangu bomba na sijawahi kuwa houseboy hata siku koma,mna toka huko na degree unabeba box eti nani atanijua,labda kama hapa bongo ulikuwa houseboy,then ukapata zali la kwenda mtoni na kuendelea kuwa house boy hapo sawa,na ni kweli kazi ni kazi but kama una elimu na na unajua utaitumia vipi bongo yaani mbona Bongo maisha mazuri.huko US ama UK nk.hauwezi kujenga,unasema unapata mshahara mzuri,hapo unajidanganya,mshahara inatokana na mazingira na matumizi ya nchi hiyo.mshahara mkubwa matumizi makubwa,na hao wazungu unaowafanyia kazi wakisikia unakandia ulipotoka nao wanakudharau na kukushangaa,kwa kufupi,Kusifia na kujenga sehemu ulipotoka sio unabomoa na kukandia,USIWE MTUMWA USIYE NA AKILI

    ReplyDelete
  16. Nyie mlioko Dar na miji mingineyo mkifanya kazi katika makampuni ya kigeni, kama Shoprite hivi, hambebi maboksi?

    Afadhali mimi nayabeba kwa doli au karti. Nyie mwayabeba mabegani na kichwani!!!!!!!

    Yaani kazi zitutenganishe! Mambo ya utoto haya!

    ReplyDelete
  17. anony 10:15 am unajizungumzia wewe..umeenda kariakoo ukaona watu wanavyosota...wewe kama ulikulia kwenye baba aliyeiba serikalini na umenyonya kutoka kwake basi usizungumze na kudharau kazi.

    Majority ya watu walio nje kinaeleweka kulinganisha na majority ya vijana Bongo hakieleweki nini kitakua kesho. Hao wachache wanaofanya kazi kwa office ndio unaona haleluya!!!!!

    Wewe kaa kimya na pumba zako au unipe email yako nikuforwadie email ninazozipokea kila siku za ma school mates..wanavyoniomba niwatafutie njia ya kuja...don't say a thing....we know everything.

    Ni wangapi wamemaliza mlimani, sokoine, kariuki na muhimbili wameshakimbilia huku tayari?

    We like our country so much no doubt but you will never know the difference if there is nothing to compare.

    Wewe na kaofisi kako umeajiri watu wangapi na unawalipa shilingi ngapi. Na huo mshahara unaowalipa wanayamudu maisha kiasi gani?? na saving yao ni ipi?? Na ni wangapi wataretire salama kwa kiofisi chako.

    Ninachujua ni kuwa wabongo wenye machungu sana rohoni ni wale watoto wa vizito waliofikiria kuwa wao tu ndio watawini tu. Sasa wanaona walalahoi wanakimbia na kutafuta maisha away from them ...wamebakia kutumia computer za baba zao kukandia...wakati wao kila wanachotumia ni cha baba.

    Jiangalie wewe unayekandia watu wanaofanya kazi za mabox...nini unacho chakujivunia ambacho ni chako??? kama sio kila kitu ...gari ya baba...nyumba ya baba...computer ya baba....kula kwa baba ....Unasubiri baba afe uchukue urithi...au ni baba alikufungulia hiyo biashara...wewe ulitoa wapi hela ...kama sio unga au umeiba serikalini ...

    MTAKUNYA SUMU LAKINI WENZENU LIFE INAENDELEA

    ReplyDelete
  18. anony 10:15 HOUSE GIRL/BOY NI KAZI PIA. ILA NYIE WAKOLONI HAMUWALIPI VIZURI...PUMBAFU WEWE..

    ReplyDelete
  19. hahahahah ana endesha forklift au he/she making $7.25 an hr wacha zenu kama kweli ana kazi ya maan mwambie ajioneshe na tunataka kujua ana nondo yenye nguvu gani i mean time pole sana we dont buy that

    ReplyDelete
  20. wewe unayejifanya ana make dollar 7.25 wewe bongo una make ngapi? na nondo wewe unayo yako jionyeshe wewe kwanza na kama umemaliza hiyo nondo nondo yako hela ya nchi waliokusomesha ulirudisha?

    Kwanza wewe ni papa mkubwa uko USA unajifanya siajabu hujasoma hata kidogo...

    Kuonyesha mabox siajabu anawachora tu nyie washamba....kwani hapo mnapopaona siajabu yeye wala hafanyi humo kwenye storage.....tanuatanua tu wakati hamna hata senti mifukoni mwenu....

    ReplyDelete
  21. tehe tehe tehe wabeba mabox bwana ukiwachokoza tu,kwa kupanic hao embu cheki wanavyojitetea duh kazi kweli kweli.eti uyu mwingine anasema marafiki zake kibao wamemaliza mzumbe UD wanamtumia email kibao awafanyie mpango kwa kuja huko,HAO WATAKUWA wamefeli,kama walifaulu vzuri si apply Masters

    ReplyDelete
  22. Jamani mbona watu mnaona mabox mie naona GUYLIAN chocolate ......hizo sio mchezo zinachanganywa na nuts halafu wanazichepu kama vikonokono hivi ama shells ni tamu ......... haloo mdau mfanyakazi naomba nikupatie details zangu uwe unanitumia fresh from the factory .. he he he eh

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...