Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. Give it a rest people, its done and if you really anoyed by this you should start long a go let the girl enjoy her time...

    ReplyDelete
  2. safi sana mambo yanajijibu yenyewe

    ReplyDelete
  3. nilijua tu yani hakya nan wabongo jamani wamemkataa,ai DADA Richa Usife moyo peperusha bendera ya bongo tu bila kujali maneno ya wakosaji

    ReplyDelete
  4. Hebu mwacheni binti wa watu. Ni Mbongo huyo tuacheni ubaguzi jamani maana imekuwa ni AIBU!

    ReplyDelete
  5. MR MICHUZI WEKA KITU KINACHOLEWEKA KUHUSU HIO TVT TUTAONA VIPI NA SITE SEPTIPI?MANAKE LEO NDIO 7SEPTEMBER !!ACHA HAYO MAMBO YANA BOA KILA KUKICHA MISS ;AU NA WEWE VIPI TUKUELEWE HUNA JIPYA?

    ReplyDelete
  6. YAAAP, kumbe wenzetu mlioko nyumbani akili zenu bado ziko kamili,,nilifikiri mmeshalishwa LIMBWATA kutoka Bombay...safi sana, piganieni haki, wamtoe huyo ponjoro au wasirudie TENA huo mchezo wa kitoto.

    ReplyDelete
  7. NDIO MAANA WATANZANIA HAMUENDELEI KAMWE MNAPENDA LALAMIKA BADALA YA KUFIKIRIA KITU NA KUCHANGIA MAMBO YA FUTURE. MNAPENDA KALIA KITU LALAMIKAAAAA WEEEEEEEEEE

    MIE NI MTANZANIA ILA NAONA AIBU, NCHI ZINGINE ZA AFRICA ZIMESHATUMA WATU WA NCHI ZAO ASILI YA KIHINDI ILA MLIONA WEUSI WENZETU WAKILALAMIKA?

    MISS WORLD WANAANGALIA HAYA MAMBO NA HABARI ZIPO KWENYE INTERNET NA MTU AKISUBUTU KUMTOA RICHA BASI MJUE MTAKAYEMTUMA ATAISHIA KWENYE BIN.

    WATANZANIA WANGAPI MMETUMA KWENYE MISS WORLD AU MASHINDANO MENGINE WAKASHINDA.

    SI AFADHALI HATA NACNY ALIJIPATIA U MISS AFRICA ILA HAKUSHINDA KUWA MISS WORLD.

    MNANITIA KINYAA NYIE WABAGUZI.

    ETI MHINDI ATAKUWA KAMA MUHINDI WA INDIA.

    MBONA WAZUNGU HAWAANGALII RANGI WANAPOTUMA WAO KUSEMA KUNA WAZUNGU WENGINE BASI WABADILISHE. NA BADO WANASHINDA

    DESTINY YA MTU NI YA MTU HUYO TU KAMA MKIPELEKA MWINGINE NAE ANAWEZA ASISHINDE

    HATA RICHA AKIENDA ASIPOSHINDA BASI WANGAPI WAMEENDA NA KUSHINDA FROM TANZANIA KUWA MISS WORLD (NONE)

    MNATIA AIBU WATANZANIA WABAGUZI WA RANGI NYIE NA IDDI AMINI MULE SAHANI MOJA.

    MNAKERA SANAAAAAAAAAAAAAAAA

    NDIO MAANA HAMUENDELEI

    AIBU

    ReplyDelete
  8. Braza Michuzi,
    Unajua pamapo ukweli uongo hujitenga! Kama mtu hakubaliki ni hakubaliki na issue hapa si rangi ya huyo Miss wa kihindi, angeweza kuwa mswahili na bado hasingekulika.Hoyce alikuwa amelenga sana ila hamkumwelewa.Vigezo ndio vinamtoa out.Ni miss wa kuchongwa na kina lundenga some months ago.Very Bad

    ReplyDelete
  9. Tatizo sio Uhindi, hana sifa za kushinda Miss TZ. Ni sawa tu na huyo wa last year

    ReplyDelete
  10. 1. HILO NI GAZETI LA UDAKU

    2. ARTICLE ILIYOBEBA UZITO WA JUU NI KWA AJILI YA KUGANGA NJAA, MWENYE GAZETI ANATAKA IWE HIVYO, AKIJUA KUWA WABONGO WANAOPENDA UMBEA, WATANUNUA KWA WINGI.

    NADHANI MCHUZI TUWEKEE MJADALA HAPA TUJADILI KAMA MAGAZETI YA UDAKU YANAFAA KWA MAADILI YA WATOTO NA JAMII YETU AU LA.

    ReplyDelete
  11. bongo bwana kwa kuiga??? Eti the Sun-bongo,aibu......
    kuhusu miss Tz mie naona ni halali yake kwani hakuwa na mpinzani wote wote below standard except miss tzUK.
    Congrats Richa,kelele za wapangaji hazimzuii mwenye nyumba kulala.

    ReplyDelete
  12. JINSI TULIVYOIPIGA CHINI TANZANIA KUINGIA JUMLA JUMLA EAC NA NDIVYO HIVYO TUNAMPIGA VITA HUYO MHINDI ALIYETOKA MUMBAI ARUDI KWAO....SISI TUNAMTAKA QUEEN DAVIDI APEPERUSHE, THE BLU, THE BLACK, THE YELLOW, AND THE GREEN
    kasera,
    kc,ks

    ReplyDelete
  13. hakuna cha nini wala nini, hakuna cha kujifanya ati "miye walinibagua basi na miye nawabagua".. ubaguzi hauna sababu! Ubaguzi asili yake ni hisia ya kujiona bora kuliko mtu mwingine hata kama mtu yule mwingine hajakufanyia wewe jambo lolote lile baya! Angalau mnajitokeza ili tujue kuwa wabaguzi wapo hata wa rangi nyeusi! Na sumu yenu tutaendelea kuipinga kwa nguvu zote. Wabaguzi kama nyinyi ni hatari kabisa kwani hamuishii kwenye kuchukia tu, ubaguzi hauokomi na hasa ukipata nafasi ya kulipiza kisasi! Tunawapinga nyinyi wabaguzi mambo leo, hamna nafasi katika Tanzania na mawazo yenu ni ya hatari kama ukoma! Tutaendelea kuwapinga nyinyi wabaguzi ambao mnataka kutumia ushindi wa Richa kama kichocheo cha itikadi zenu potovu na za kibabe! Tunawapinga nyinyi wabaguzi mambo leo, ambao licha ya kukosa hata sababu moja ya msingi mnataka kumuadhibu binti huyu wa kitanzania kwa vile hafanani nanyi na kwa vile ati "wahindi walininyanyasa!".. Tunawapinga, tunaendelea kuwapinga, na tutazidi kuwapinga hadi pale mtakapotambua kuwa "binadamu wote ni sawa" na kila mtu "ana haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake"!

    Tanzania tutakayoijenga ni Tanzania ile ambapo wana na mabinti wake wote bila ya kujali hali zao za kimaisha, rangi zao, dini zao, au mahali wanakotoka, au asili yao ya kitaifa, watakuwa na haki sawa, na nafasi sawa. Tuliupinga ubaguzi wa mtu mweupe dhidi ya watu weusi, tukaonesha makosa yake, na hatimaye ukaporomoka katika himaya yake ya mwisho kule Afrika ya Kusini, na sasa tumeanza mapambano mapya ya kuupinga ubaguzi wa watu weupe unaofanywa na watu weusi, hadi na wenyewe uporomoke kama vipande vya biskuti na uwe umesagika na kuwa tikitiki kama tikiti maji lililoangushwa kwenye mwamba!

    Fikra zenu na vitendo si za kupuuzwa bali za kubezwa na si za kutweza! Kama vile wabaguzi wa Marekani walipata msemaji wao ndani ya Gavana Wallace, na wale wa Afrika ya kusini kupata msemaji wao kwenye P. W Botha, na nyinyi wa Tanzania inaonekana mmepata msemaji wenu kwenye Hoyce Temu, na waandishi ambao wanajifanya wanatetea usawa kumbe wanashiriki katika kupenyeza sumu yao ya kibaguzi! tunawapinga, tunaendelea kuwapinga na tutazidi kuwapinga!

    Sumu yenu ya kibaguzi huwa haikomi, na hupenya kama mshale wa mwindaji, na kuwadunga wasiokuwa tayari na kuwafanya mateka wa fikra hizo mbovu!! Kwa ngao ya utambuzi wa usawa wa binadamu, tukisimama kidete kama majemedari wale waliopinga ubaguzi kwenye vilima vya Wamatumbi, na wale waliosimama kumwaga damu zao kulinda heshima ya mtu mweusi na haki ya watu weusi kuwa na haki sawa na binadamu mwingine yoyote! Tunawapinga kwa majina ya mababu zetu ambao walipigana kwa nguvu zote kupata nafasi ya kuishi kama binadamu wengine na kutambuliwa kama binadamu wengine na siyo kupigana ili wao wawe juu ya binadamu wengine! Kwa majina ya Mkwawa, na Ihunyo, kwa majina ya Songea na Mirambo! Tunawapinga, tunaendela kuwapinga, na tutaendelea kuwapinga!

    Katika Tanzania hii kila Mtanzania atakuwa na haki sawa na nafasi sawa! Hata wabaguzi wetu na wenyewe wataheshimiwa na kuthaminiwa utu wao licha ya kwamba fikra zao mbovu zitapingwa kwa nguvu zote na hadi kwa masilio ya matone ya damu itiririkayo katika mishipa ya wale wapigania usawa na haki!

    Tunawatangazia kuwa hamna nafasi ya kushinda, hoja zenu ni dhaifu, na mifano yenu ya kibaguzi imeporonyoka kama ndege aliyeruka mtego! Ni ninyi wenyewe mliotega mtego huo na mmnaswa wenyewe!

    ReplyDelete
  14. MICHUZI KWA NINI NA WEWE USIWEKE MAONI YAKO YA KUMPINGA RICHA.
    NDIYO! MAANA YAKE HAKUNA CHOCHOTE UNACHOKITOA KUHUSU RICHA ZAIDI YA NEGATIVITY ILHALI WEWE MWENYEWE UNAWEKA WAKIMBIZI WA KIGANDA HAPO BONGO WASIO NA KIBALI.
    KWANI RICHA AMEKUKOSEA NINI KILA KUKICHA UNAJIFANYA KUENDELEZA LIBENEKE KAMA VILE ULIVYOKUWA UKIFUATILIA MAHANDAKI YA DAR WAKATI UNAJUA FIKA NI KWAMBA JIJI HALIPO MBALI NA OFISI ZENU ZA DAILY NEWS HAPO SALAMANDER.
    RICHA ANASTAHILI KUSHINDA KAMA WALIVYOKUWA WANATARAJIA KUSHINDA WATANZANIA WENGINE.
    KAMA UNALETA MAMBO YAKO YA RANGI, BANDIKA PICHA YA TIMU ZA TAIFA YA TANZANIA YA MPIRA WA RUGBY, GOLF, KRIKETI, HOCKEY NA WATU WOTE WAONE WATANZANIA WANAOILETEA SIFA KWENYE MICHEZO HIYO WANA ASILI YA WAPI!
    HII TABIA YAKO INACHAFUA SANA KWANI WATU WANAPOSHALIA JAMBO LA MUHIMU AMBALO UNALIPINGA, HULITOI HUMU NDANI.
    MBONA HABARI ZA ZITTO KABWE ZIMEKUFA HUMU WAKATI WENGINE WANAENDELEZA LIBENEKE KWA SAAANA VILEVILE. AU NDIYO UNAPIGIA CHAPUO HIYO TIKETI YA USA NA KIKWETE? BE FAIR AND SQUARE. WEWE NI MPIGA PICHA ULIYESOMEA UANDISHI SIYO MPIGA PICHA WA MITAANI.
    HIVYO NI VITU VIWILI TOFAUTI AMBAVYO WEWE TOFAUTI YAKE NADHANI HUJAIFAHAMU. KAMA UNGEKUWA ITS NOT RICHABO UNGEWEZA KUJUA MAADILI YA KAZI YAKO. FUNGA MJADALA NA TUSONGE MBELE SASA. RICHA NI MISS TANZANIA NA ATABAKIA HIVYO HADI MWAKANI. FULL STOP.

    ReplyDelete
  15. Leave the gyal alone! shez fit, clever & Tanzanian, can u just imagine if she was a football playet playin 4 Real Madrid or Man u! wouldnt u cry 4 her 2 play 4 Starz?, dont all accusers b foolish!
    leave her aloneeeeeeee;
    Kwazulu

    ReplyDelete
  16. Gari wamwachie ila Miss World atuwakilishe mshindi wa pili, Hapa tunataka mmbantu mtanzania mmbantu hebu tuwe sensitive na utaifa na tujaribu kutangaza nchi yetu. Haki ya mungu tumechemsha sana. Waandaaji alitakiwa kujua kuwa issue sio miss world bali ni kutangaza na nchi pia. Kama huyu mdosi atatuwakilisha nchi za watu watajua Tanzania ni nchi ya Kidosi. Hivi tuache ubaguzi na nini, India hakuna watu weusi aliochukua uraia huko, Lakini kwa nini hawawakilishi India, wao wanabaki kuwa Raia wa India lakini si wahindi. Na huyu ni raia wa Tanzania lakini si mmbantu.

    Kama issue ni Gari wamwachie hako kagari ila Asituwakilishe miss world Aibu. Vinginevyo Tutayasusa haya mashindano ya Lundenga na wadosi wake

    ReplyDelete
  17. wewe hapo juu unaenda na jina la LOVE nakupa tano,watu wanakera sana na ndiyo maana wa tz hatuendelei,huyu msichana alikuwepo tangu mwanzoni kwa nini hamkuhoji rangi yake?mmesubiri mpaka ameshinda,jamani huyo dada ni mtanzania acheni roho mbaya,kama alijieleza vizuri tatizo liko wapi,tunajua ni freedom speech lakini comment nyingi zimejaa chuki,gadhabu na roho ya kutu,i hope mwl nyrere anatutizama.

    ReplyDelete
  18. Hahahaaaaa inamaana UDAKU bado wanataka kuwadanganya watu?

    Richa yuko gado na anajiandaa na safari ya kwenda China.

    Wanaokereka wale viwembe.

    ReplyDelete
  19. Mamiss Tanzania waliopita bila vilio vya wengi ni Faraja Kota, Nancy Sumari, Hoyce Temu, nk..... These few are the best that we ever had!!! Huyu muhindi wa mwaka huu is a BIG NO!!

    ReplyDelete
  20. Kama kweli walipeleka bakuli nyuma kabla ya mashindano kuisha na kama kweli aliulizwa swali ambalo halikuwapo...lazima hawa watu wasemwe. Kwanza kuwacharge watu $75 halafu waishie kugombania viti hiyo ni adhabu kali sana....halafu kupanga matokeo waht is the point...Hiyo ni aibu hata kama angeshinda muhindi, muarabu au mwingine hiyo si halali.

    ReplyDelete
  21. JAMANI NDUGU WATANZANIA
    NOW IS TOO MUCH....HOW COME ISSUE YA MISS TANZANIA 2007 IMEWAINGIA WATU MOYONI KIASI KWAMBA HATA MASS MEDIA INA COVER THIS TOPIC EVERY DAY(ALMOST A WEEK NOW) VIPI MAMBO YA KUZUNGUMZIA HAYAPO NINI...????????? MTOTO WA WATU MMEMSHIKIA BANGO ETI MHINDI,KWANI INABADILI NINI?? KWA MTANZANIA MWENYE AKILI TIMAMU ASIYE TAHIRA ...KITU MUHIMU NI KWAMBA HUYU DADA AWE BALOZI MZURI KWENYE INTERNATIONAL ARENA SIYO MAMBO YA KWENDA KUJIKANYAGA...HALAFU NAONA MAMBO MENGI WABONGO YANATUPIGA CHENGA .KWA INTERNATIONAL RELATION POLICY YA SIKU HIZI HIYO NI MUHIMU SANA KWA TAIFA KUWA REPRESENTABLE NA MTANZANIA MWENYE ASILI NYINGINE...NDIYO MAANA UNAONA NCHI ZA EUROPE AU NORTH-AMERICA WANAJARIBU KUCHANGAYA WATU WENYE RACE TOFAUTI SIYO KWAMBA WAZUNGU HAWAPO ..NANI ALIFIKIRIA MIAKA HIYO KAMA MTU MWEUSI ANAWEZA KUVAA JEZI YA GERMANY NATIONAL TEAM...ADOLF .H ANGEKUWA ANAFUFUKA LEO...LAKINI THIS THINGS IS NORMAL LEO IJE IWE NCHI KAMA TANZANIA MBAYO TULIKUWA KOLONI ETI TUNABAGUA WATU MBONA AKUNA MJADALA WA KUHUSU MADINI, RUSHWA ,HALI MBAYA YA MAISHA , UKOSEFU WA KAZI, KUPANDISHIWA KODI,BARABARA MBOVU, UKOSEFU WA MATIBABU (WAGONJWA WANALALA CHINI MUHIMBILI),UKOSEFU WA MAJI JIJINI ,WIZI WA MALI YA UMMA HII LIST INAWEZA KUENDELEA MPAKA......WATANZANI HAYO NI BAADHI YA MAMBO YENYE MANUFAA KWA JAMII KULIKONI MISS TANZANIA..MTU ALIYEKO MBINGA AU... HUU MISS NI USIKU WA GIZA ,KITU MUHIMU AKIENDA CLINIC APEWA ASPRIN ATIBU MALARIA BASI
    ANGALIENI MAMBO KWA MAPANA ACHANI MACHUNGU MUDA WAKE UMEPITA.MIE HAKUNA KINACHO NIUMA NINAPO KUJA BONGO ..KAMA KUONA WALALA HOI WANAVYOPIGA MGUU ASUBUHI KUELEKEA MJINI HALAFU WAHINDI NA WAARABU WANAENDESHA RAVA4 NA KUWAPIGIA VUMBI ...IT SO SAD FOR OUR SOCIETY AND SHAME FOR THE COUNTRY...NYIE MMESHUPALIA HUYU DEMU MBONA HAO HAMUWAONGELEI..??????
    kwa Miss wetu congraturation mie nipo mtoni and i will be proud for your success as Tanzanian and dont forget that:
    (is better to be hated for what u are than to be loved for what u are not...)
    Dr. B

    ReplyDelete
  22. WANANCHI WAIJIA JUU KAMATI YA MISS TANZANIA 2007..........
    Hiyo hapo juu ni kichwa cha babari gazeti la (the Bongo sun )
    Inatia huruma sana na ni machonzi makubwa kuona nchi niliyo zaliwa na kukulia (Tanzania )leo iko hivi. kwanza siwezi kuamini kichwa cha habari hapo juu nafikiri hayo ni mawazo ya mkusanya habari hii wala siyo wananchi.
    siwezi kuamini kwamba mambo nyumbani yako swali kiasi kwamba mtanzania wa leo ametosheka na anasumburiwa na vitu vya kupita kama miss Tanzania...
    mtu hana uhakika na mlo wa jioni ,watoto wamefukuzwa shule hawana uniform , mtu ana hela ya nauli kwenda mjini, nyie mnaongelea mambo ya miss......
    kwa wana habari wenzangu mbona masuala ya Rada, uchimbaji wa madini ,Umeme , rushwa n.k mbona sioni heading zake kwenye magazeti lakini suala la huyu msichana mmelipamba sana utafikiri lina ongeza GDP ya nchi(mwana farisafa wa kiengereza na mwandishi wa habari maarufu -alisema journalist ni yule anayeandika habari inayongaa kama kioo kiasi kwamba msomaje akiwa anasoma anaiona sura yake .....) tuna matatizo mengi ambaye yanamgusa kila mtanzania na siyo miss Tanzani...
    Nendeni na wakati....
    kwa mshindi ni mtoto mcheshi, macho mazuri, portable na vigezo kibao and she seems to be kind that is major factor for cute girl.
    Dr. B

    ReplyDelete
  23. MARA KWA MARA NIMEWAHI KUISIKIA TUME YA HAKI ZA BINADAMU IKITOA KAULI PALE MTU/WATU WANAPOKUTWA NA MASAHIBU.
    LEO MISS TANZANIA 2007 RICHA ADHIA ANAANDIKWA VIBAYA MPAKA NA VYOMBO VYA HABARI NA KUWEKA TONE ZA KIBAGUZI.
    CHA AJABU HII TUME KATIKA HILI IMEKAA KIMYA KAMA VILE HAIPO AU YULE MAMA BISIMBA KIJO YUKO LIKIZO?

    RICHA WANAOPIGA KELELE ZA KIBAGUZI NI WACHACHE SASNA HAWAZIDI HATA KUMI, THE REST OF THE TANZANIANS TUPO PAMOJA NAWE!
    WE LOVE YOU, YOU ARE TRULY TANZANIAN GIRL.

    ReplyDelete
  24. Huu ubaguzi wa kijinga uliwaingia watanzania nafikiri ni matunda ya Rev. Mtikila ambaye aliendesha vita zidi ya watanzania wenye asili ya kiasia, haya ndio matunda yake. Baadaye tutaanza kubaguana kwa dini kuwa mwiisilamu/mkristo afai kuwa raisi,balozi, waziri, mkuu wa majeshi, diwani, mkuu wa mkoa, etc.

    Hii sumu ya ubaguzi mnayoifurakia itakuja kuwaumiza hako kataifa kenu vibaya sana. Mimi niko hapa Marekani naona ubaya wa ubaguzi wa rangi, na jinsi gani hawa jamaa zetu weusi walivyopigana nao mpaka hapa walipofika mbapo sasa wewe ukiitwa mbaguzi ni laana kubwa. Ambapo mimi nakula matunda ya mapambano waliyopitia kuleta usawa wa watu hapa. Si jambo la ajabu wanawake weusi hapa amerika wanawakilisha USA katika miss World, miss Universe na kuwa miss USA na washindi ndani ya majimbo hapa USA.

    Sasa nyinyi wabaguzi mnayempinga huyu binti mtazania mnataka aende wapi kuwakilisha.

    I don't agree with Temu, she kinda loser, she had a chance to compete international, did she win? NOOOOOOOOOO, she should shut up and let the winner for 07 represent the country and see how she does it.

    People, if you hate, hate is gonna destroy you.

    To Richa, let your haters be your motivators, just do your thing, everything is gonna be alright, We real Tanzanians are behind you. Don't get depressed by these phony, small minded, ignorants who think by dropping poison we'll think high of'em, Nooo, All I can say to 'em is just go to hell/drop dead/get life, if you don't like her.

    Peace
    Atl USA.

    ReplyDelete
  25. Hao wanaolalamika sasa hivi mimi nawaona ni Wanafiki na wanaendeshwa na ubaguzi usio na maana. Hawakumwona tokea aliposhiriki kwenye vitongoji?
    Huyo Hoyce Temu naye anaendeshwa na ushabiki tu, hana malalamiko yoyote ya msingi. Kama mshabiki kuna mtu alitaka ashinde lakini hakushinda. Afunge mdomo wake na amwache huyo mtoto afanye mambo yake.
    Mtu mwenye madai ya msingi ayafikishe panapohusika. Kama ni rushwa apeleke madai yake PCCB(TAKUKURU)

    ReplyDelete
  26. wewe uliyejiita "love" una maana gani kusema "NDIO MAANA WATANTZANIA HAMUENDELEI"?...this is generalising, it is wrong...allow people to air their views this is a freedom of speech zone...let us DEBATE with facts...na wewe uliyejiita "mwanakijiji"...ni wa kijiji gani!...huvi kweli unaamini "binadamu wote ni sawa"?...mungine anashindia uji wa chumvi yeye na watoto wake, mungine anatupa chakula...kama ni ubaguzi UPO katika maisha yetu ya KILA SIKU hapa nyumbani na huko nje...nyie mnaodai hakuna ubaguzi, come out of that shell and face it...hiki kitu kipo...acheni tutoe madukuduku yetu...kampitisheni huyo richa wenu vijijini mseme "huyu ndio msichana mrembo kuliko wote TZ" muone nani mbaguzi...in fact calling us racists is wrong...we are conservative towards utamaduni wa mtanzania

    ReplyDelete
  27. JAMANI,HEBU MPENI RICHA A BREAK,MAANA KUNA FREEDOM OF SPEECH NA HATE, COMMENTS NYINGI NI HATE COMMENTS, MI NAONA RICHA AMEFANYA VIZURI MISS TANZANIA,NA MISS WORLD ATAPATA NAFASI NZURI, SIJUI AKISHINDA MTASEMAJE? MTAMSIFIA AMEFANYA VIZURI KWA TANZANIA AU?? KESHAKUWA MSHINDI JAMANI MPENI KIDOGO!!!!!!Mimi Dar

    ReplyDelete
  28. Jamani mie naona complaints zimechelewa
    Kati ya wasichana wote, Richa ameprove kuwa she got what it takes. Kajibu maswali yake vizui zaidi ya wote.
    wasichana weusi asilia hawakuonyesha uwezo wao kiakili... IQ
    Urembo ni pamoja na uwezo wako wa kujieleza, sio nguo nzuri, mwendo na smile. Na wale waliotuwakilisha ktk top 10 hakuna hata mmoja ambae angeweza kufanya maajabu miss world. Richa is the best candicate so far and thus i wis u all the best.
    Dont let any one bring u done, u won cause u deserved it... next time wakija wasichana wenye asili ya kitanzania be black, yello or white make sure the IQ is good too.

    ReplyDelete
  29. YAANI WEWE MIBA NDIYO HUNA KITU KICHWANI KABISA, YAANI UMESHINDWA KUJIFUNZA KUTOKA KWA WATU WOTE WALIOCHANGIA HADI SASA HIVI?


    miba said...

    HEBU ANGALIA JINSI UNAVYOJISHUKU
    'wewe uliyejiita "love" una maana gani kusema "NDIO MAANA WATANTZANIA HAMUENDELEI"?...this is generalising,'

    'it is wrong...allow people to air their views this is a freedom of speech zone...let us DEBATE with facts...'

    HIZO FACTS ZAKO ZIKO WAPI? UNAJUA KU-TYPE KWENYE KEYBOARD TU?
    KUMBUKA KUWA HAKUNA UHURU USO NA MIPAKA.
    HAPA UNAITA WACHANGIA WENGINE KANA KWAMBA UNAANDIKA COMMETS ZAKO UKIWA BAR, HEBU ANGALIA ULICHOANDIKA HAPA KINA MANTIKI YEYOTE, UNATUDHALILISHA WATANZANIA WENZIO, HII BLOG HUSOMWA NA WATU WENGI NA WALE WASO WATANZANIA.
    'na wewe uliyejiita "mwanakijiji"...ni wa kijiji gani!...huvi kweli unaamini "binadamu wote ni sawa"?...mungine anashindia uji wa chumvi yeye na watoto wake, mungine anatupa chakula...kama ni ubaguzi UPO katika maisha yetu ya KILA SIKU hapa nyumbani na huko nje...'

    ULICHOANDIKA HAPA NDIYO POINTLESS KABISA, NADHANI HATA UKIRUDIA KUSOMA KAMA UNA AKILI TIMAMU UTAMWOMBA MICHUZI ATUNGUE HUO MTUNDIKO WAKO.
    'nyie mnaodai hakuna ubaguzi, come out of that shell and face it...hiki kitu kipo...acheni tutoe madukuduku yetu...'

    MH SASA HAPA NDIYO KITUKO KABISA, ATI WEWE NI 'conservative towards utamadunni wa mtanzania'
    HIVI KWA UELEWA WAKO WEWE UNAJUA KWAMBA PALE LEADERS CLUB WALIKUWA WANAMTAFUTA MSICHANA MREMBO KULIKO WOTE TANZANIA?
    UMECHELEWA KWELKWELI, NADHANI HATA SISI WANAKIJIJI TUNAKUSHANGAA HASA

    'kampitisheni huyo richa wenu vijijini mseme "huyu ndio msichana mrembo kuliko wote TZ" muone nani mbaguzi...in fact calling us racists is wrong...we are conservative towards utamaduni wa mtanzania'

    MIBA, NINAKUPA USHAURI WA BURE:
    SIKU NYINGINE UKITAKA KUUNDIKA POPOTE PALE HAKIKISHA HAUKO MCHUPA!!!
    September 8, 2007 11:44:00 AM EAT

    ReplyDelete
  30. We unayejiita Sexy acha ushankupe Lilian Abel mbona alijibu vizuri tu, au wewe kiziwi hukusikia? Alaaah!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...