kuna wadau wamekuwa wakiniomba niwaeleze ni wapi watapata pamba za nguvu kutoka marekani wakiwa dar. jibu ni kwamba ukienda millenium tower pale kijitonyama ghorofa ya pili na kutafuta duka la s&b collection utapata vitu kama vilivyo pichani. kwa maelezo zaidi piga +255 748 710 016 ama +255 754 444 188...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Misupu eeh!!Sasa wenye Maziwa makuuuuuubwa kama demu wangu watapata wapi viwalo???.Naona my milk is standing ndo waliopendelewa peke yake,(kwa mujibu wa tangazo lako la biashara).Mmmmh au ndo ubaugzi umeshaanza tiyari.Titaandiaka,titachambua na titasema tu.Miss Patel ovyo.
    Majita

    ReplyDelete
  2. Watuhumiwa 14 wa ujambazi wameuwama mkoani Kilimanjaro

    2007-09-06 21:21:26
    Na Radio One Habari


    Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro limewauwa watuhumiwa 14 wa ujambazi usiku wa kuamkia leo, wanaodaiwa kuwa raia wa |Kenya, ambao walikuwa katika harakati za kuvamia na kupora fedha katika Benki ya Exim, tawi la Moshi.

    Kwa mujibu wa taarifa za kipolisi mkoani Kilimanjaro, jeshi la polisi mkoani humo lilipokea taarifa kutoka kwa wenzao wa Kenya juu ya kundi hilo la majambazi likiwa limepanga safari kutoka Nairobi kwenda Moshi kwa lengo la kufanya uporaji huo.

    Habari zimesema baada ya kupokea taarifa hizo, polisi mjini |Moshi walijiandaa na kujipanga kuanzia eneo la |uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro- KIA, nje kidogo ya mji wa Moshi tayari kukabiliana na watu hao.

    Zimesema hatimaye majambazi hayo yaliwasili majira ya jioni katika maeneo hayo na kuelekea mjini Moshi, lakini yalipofika katika eneo la Maili Sita karibu na mjini majira ya saa mbili usiku jana, yalibaini kuwa yalikuwa yakifuatiliwa na polisi, na ndipo yalipoanza kurushiana risasi na polisi na mapambano makali kuanza na hatimaye polisi kuwazidi nguvu na kuwaua wote.

    Hakuna askari wa jeshi la polisi aliyejeruhiwa katika tukio, lakini majambazi hayo yalilishambulia gari la polisi na kulichakaza kabisa.

    Maiti zote14 za majambazi hayo zimepelekwa katika hospitali ya mkoa ya Mawenzi mjini Moshi na kuvuta mamia ya wakazi wa mji huo waliokuwa na shauku ya kuona miili ya majambazi hayo.

    Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro limesema taarifa kamili, zikiwemo za majina ya majambazi hayo zitatolewa baadaye.

    Du kazi nzuri sana jeshi la polisi moshi hakuna ruksa ya ujambazi nchini kwetu tena

    ReplyDelete
  3. nguo zinaonekana kuwa ni bomba sana , ila duka linaitwaje S & D collection au S & B collection nisije enda nikaanza kung'aa macho

    ReplyDelete
  4. Michuzi usitishe watu wa size zilizoshiba huwezi amini mie harusi yangu ilikuwa tarehe 23 June 2007 nilinunua nguo kwenye hilo duka baada ya kuzunguka sana mjini na kukosa size yangu rafiki yangu akanielekeza millenium tower kwenye hilo duka nikapata wedding dress ya size 20 na nguo ya send off pia nilipata hapo hapo, kweli michuzi unastahili kulifagilia hilo duka sijui ni la mshikaji wako?

    ReplyDelete
  5. Duh, watanzania tumeendelea sasa tutaanza kuagiza nguo kwenye mtandao, sasa mie niko Arusha napiga namba 0754 444188 imezimwa je nitawapataje hao maana natafuta nguo kama hizo kwa kweli ni baaab kubwa , ila tatizo wanaweza nitumia huku AR town na bei zao vipi, Michuzi bwana kwenye hiyo namba hakuna kitu labda wamelala bado

    ReplyDelete
  6. E BWANA FAGILIA GESHI RA PORISHI KWA KUWAMALIZA HAO WASHENZI. UNAJUA KULE KENYA WASHAONA TANZANIA NI SEHEMU YA KUJA NA KUPORA TU KAMA WANAVYOTAKA.

    MAKAMANDA HAO WATU JAMANI MKISIKIA HARUFU YAO TU MIMINIENI RISASI TU, MPAKA WATASHIKA ADABU WENYEWE.

    NYAMBBBAAFFFF ZAO!!!

    ReplyDelete
  7. Nunue hizo nguo kutoka marekani halafu mwenye kwenye blogi hii www.kamerayamwanafunzi.blogspot.com mkasome jinsi ukoloni mambo leo unavyoangamiza nchi hii wakati sie tuko shopping Mall. jamaa katoa mada chungu sana..

    ReplyDelete
  8. Michuzi...Ujambazi na S&B wapi na wapi? Anonymous bwana!hata kufuatilia ka blogu iwe tabu. Ene wey Nafikiri hata kungekuwa na picha za Hoyce Temu(cheka kwa nguvu) Maanake akiideku haita kuwa sawa kwa sababu...niseme hii pia! figa auti

    ReplyDelete
  9. Kudhihirisha ubaguzi wao kila Mhindi sasa atamtumia miss Tanzania kumweka katika matangazo, utadhani zamani hatukuwa na miss Tz!?maana hela zao haziendi kwa mbantu hivihivi.Halafu michu mbona maoni yangu unanibania?

    ReplyDelete
  10. Mbona fesheni kama za miaka ya 70!

    ReplyDelete
  11. Duh inaonekana kuna watu wana madonge na hizi nguo, hivi kweli ni za miaka ya sabini, kama huna hela si kaa kimya, inaonekana wewe umezoea kuvaa mabaibui, teh teh teh

    ReplyDelete
  12. Simu namba ya celtel inafanya kazi mie nimepiga na saturday nilikuwa kwenye duka lao , kwa kweli wanajitahidi sana nguo ni nzuri jamani , mwenzio akifanya kitu kizuri msifieni tusiwe na vijicho pembe watanzania

    ReplyDelete
  13. Mie nilifikiri kanyaboya la catalogue kumbe kweli hizo nguo zipo S & D collection, Mbona huwatangazii mashuka na Duvet covers zimejaa mle ndani hadi nafasi imekuwa finyuuuuuuuuuuuu ya kuchagua magauni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...