jk akiweka sahihi juu ya mpira akiwa na rais wa tff leodgar chilla tenga alipotembelea kambi ya taifa staaz katika hoteli ya golden tulip. jk kawaambia wachezaji kwamba ana matumaini kuwa kesho watashinda na ushindi utakuwa mtamu. alisema yeye atakwenda arusha kwenye kikao na kama akimaliza mapema atarudi kuja kushangilia, na kwamba rais wa zanzibar mh. amani abeid karume atakuwepo kuongoza mashabiki katika ushangiliaji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Kwanini Raisi anatia saini huo mpira? Hiyo ni Hatari sana manake bongo wale wachizi wa salamander hawakawii kutoa copy na kuanza kutumia kama pipi vile. Naomba usalama waangalie hili swala

    ReplyDelete
  2. ebwane bro jk nimekukubali na pamba yako simple sana umetoka sana na unajua sana kupangilia,inafaa sana umekuja na hizo pammba na ningeshangaa unakuja kwenye wanamichezo ungevaa suti!!!unajua sana kupangilia m2 wangu,wasalimie wote wachezaji waambie ni muda wa mazoezi na sio uganga kama zamani pia mpe hi michuzi mwambie nampa nae big up!!ukionana na yule miss mwambie yeye asikonde tunamkubali kwa kuwa anajua mambo ya konozzz msalimie sana mkapa na mwambie angeanza yeye kama hivi leo tungekuwa tunapoigania kuingia world cup na sio mataifa ya africa.

    ReplyDelete
  3. Anon hapo juu. Sisi sasa hata hatukujibu maana watu wengine mnafuka moshi kama sio kuchemka!! Kila kitu usalama, usalamaa weeeee! utadhani hawana shughuli zingine za kufanya.

    ReplyDelete
  4. Kweli JK mambo unayajua maana pamba ulizovunja ni marais wa ulaya tu wanaweza kuvaa kam wewe, hii inaonyesha jinsi gani unakwenda na wakati huyo mtu anayekuchagulia nguo na kukushauri sehemu za kuvaa anajulia. Ingekuwa viongozi wengine masuti tu hata siku moja awaonekani simple hii iwe mfano kwa viongozi wengine mara mojamoja wanatakiwa waonekane simple kama ulivyotokea wewe kwenye kambi ya STARS

    ReplyDelete
  5. ONGELEENI MAMBO YA MAANA SI RAIS KAVAA NINI. ONGEENI RAIS ANAHOJA GANI/ MUULIZENI KUHUSU RUSHWA UMASKINI, MFUKO WA BEI MENGINE MENGI. MBONA HAKUWEKA SAHIHI WATOTO WETU WASIFUKUZWE CHUO KIKUU KWA SABABU YA KARO? JAMBO AMBALO ALISEMA ATAHAKIKISHA HAWAFUKUZI? KUWENI MAKINI. TANZANIA HAIENDELEZWI KWA MIPIRA NA KUVAA.

    ReplyDelete
  6. Kama Rais anapimwa kwa kuvaa vizuri na kuwa na sura nzuri,baasi hapa Rais tumepata.Lakini kama kuna vigezo vingine vya kumpima Rais hapa tumechemka haswaaaaaaa.

    Wewe anon unayemponda Mkapa Koma kabisa.Kwa huo uwanja ulijengwa kwenye uongozi wako??Yani hujui kuwa Mzee Ndoo Langu aliondolewa na Mkapa na ndo tukaanza kuuona Mwanga katika maisha yaliyobora Kisoka.Wewewewewewewewew
    Majita.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...