waziri mkuu mh. el akimpa pole mbunge wa mchinga mh. mudhihiri m. mudhihir hospitali ya muhimbili kwa kukatwa mkono leo. fungua www.tztimes.com kwa habari zaidi na nyinginezo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. wadau wengi inaelekea mmefurahia yaliyomkuta mudhihir,poa tu hiyo ni haki yenu.lakini kumbukeni kwamba wanasiasa wote duniani baba yao mmoja mama yao mmoja na wote ni waongo na wasanii.mpe nchi leo zito kabwe au freeman mbowe atafanya madudu yale yale au even worse,keya mliona madudu ya angloleasing na kibaki baada ya goldenberg ya moi. kikubwa hapa ni kutambua kwamba njia pekee ya kuwadhibiti wanasiasa ni public kuwa vigilant ikiongozwa na media. mudhihir kama mudhihir msameheni tu alikuwa ana behave precisely kama mwana siasa,hivyo kama binadamu anasikia uchungu kama sisi,isitoshe ana baba,mama,watoto,ndugu etc wanaompenda na kumjali,hivyo hata kama tuna usongo na mdhihir basi angalau let us feel pain kwa hao na tuombe mungu ampe nguvu za kustahimili maumivu yake.

    ReplyDelete
  2. michuzi naona uneposti maoni yote bila kuchuja hofu ya buzwagi nini mzee?!!!!!

    ReplyDelete
  3. pole mwanawane, kuna wakati mie kigoma waliniagizia radi, we acha tu!

    ReplyDelete
  4. mh! pamoja na kuwa aliufyatua mtego kabla mheshimiwa waziri hajanasa nikamnunia,kwa hili ni zito sana na nakosa neno la karibu kuelezea hisia zangu hadi nieleweke, nachukua nafsi hii kutoka moyoni kumpa pole kwa yote,kweli nimeamini hujafa hujaumbwa,namshauri awe na subira katika kipindi hiki kigumu kwa sababu hakuna jinsi,inabidi tu maisha yaendelee baada ya hapa. POLE SANA MHESHIMIWA MUDHIHIR M. MUDHIHIR.mdau morogoro

    ReplyDelete
  5. Nyie kama sio watanzania tuacheni watanzania teseme tuliyonayo.Msitulazimishe kumpa pole mtu tusiyempenda mbona Dr.Savimbi alivyouwawa rais wenu hakutuma salaam za rambirambi au majambazi wa Arusha mbona hamkusema au wao ngedere?Na kwanini musimuambie aache kufanya madudu ili wadanganyika tumpende.Angekufa tu hata Watanzannia wanaokufa kwa umasikini anao upromoti yeye nao pia ni watu.

    ReplyDelete
  6. Jamani huyu jamaa msimshambulie sana yeye ni parot, anapewa ,maneno na kuyaweka katika mahadhi ya kimipasho, au hamjui jamaa ni mtunzi wa taarab za mipasho?, hivyo tusimshambulie sana, Japo atakuwa amejifunza kuwa wadanganyika hawawapendi watu wenye tabia ya ukasuku kama yeye. Yeye alijifanya kapata uchungu sana kwa Karamagi kuwa Grilled na Zitto. Sasa yamemkuta watu wanamshambulia badala ya kumuombea Tahafifu.

    Ninacho shukuru ni kuwa amepona na atajifunza kuacha ushabiki kwenye hoja zinazogusa masilahi ya wadanganyika. Mungu Mpe nafuu taratiiibuuuuu ila kwa uhakika na maumivu makali yasiyosikia dawa ili akatutetee wadanganyika turudishe moyo wa imani kwake

    ReplyDelete
  7. I wish you a fast recovery Mheshimiwa.
    Kisha nasema hakuna aliye malaika hapa duniani. Kila mtu lazima ana MABAYA yake na kadhalika MAZURI yake.
    Nikakumbuka katika BIBILIA kuna hadithi moja ambapo Bwana JIZAS aliletewa Mwana Mama aliyefumaniwa katika uzinzi na kwamba kwa kuwa adhabu ya kosa hilo ni kupigwa mawe hadi kufa, basi walimuuliza JIZAS kama wampige mawe huyo mama hadi afe.
    JIZAS alichofanya ni kuchorachora chini, kuinuka na kisha kuwaambia kuwa:- "YOYOTE MIONGONI MWENU AMBAYE HAJAWAHI KUTENDA DHAMBI/KOSA HATA MARA MOJA, AWE WA KWANZA KUMPIGA JIWE HUYO MAMA"
    Nami nawaambia hivyohivyo wale wana bulogi wote wanaomkejeli na/au kumhukumu Mheshimiwa Mudhihir.
    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  8. wadau acheni roho mbaya .kila jambo lapangwa na mungu.huyu ni mmbunge anahaki ya kusema na kutuwakilisha wengine.atapata nafuu kwa uwezo wa mungu siyo wa kabwe wala karamagi..Pole sana mchinga usijali wamachinga wenzio twakuombea usiku na mchana.

    pole mpendwa wetu

    mmachinga wa UK

    ReplyDelete
  9. nyiemnaojifanya midomo mirefu shauri zenu , mjue anapelekewa salamu zote izo, ngojeni akitoka apo kitandani miomo yenu yote itapinda kushoto iyo, ohooooo,

    ReplyDelete
  10. JAMANI!! DINI ZOTE ZINATHIBITISHA KUWA ULOZIOLOGY UPOOO!!, WEWE KAMA UNAJUA KUBWATUKA, KUNAWATU WAENDA KIMYA.
    KAMA UNABISHA MUULIZENI ANAYEJUA KULA CHAPATI, ASIYE NA VUMBI MIGUUNI, ATAKUAMBIENI KILICHOMKUTA HUKO KUTABORA!!.
    "NGO WEYE WACHA"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...