
makocha wa timu za taifa na wachezaji nyota wa zamani. toka shoto in athumani chama, sunday manara, daktari wa timu mwankemwa, rishard adolf, mtemi ramadhani, maximo, mohamed mkweche, isihaka hassan 'chukwu', ahmed amasha, ittamar ambaye ni kocha wa viungo, james kisaka, kocha wa vijana tinocco na kitwana manara

maximo akiwa na james kisaka, juma pondamali mensah na athumani juma chama
TFF KWA KUMINYA CHENJI KIBOKO...
ReplyDeleteTEH TEH TEH TEH TEH. LAKINI MSITUNYIME TIKETI YA MECHI YA MSUMBIJI, TEH TEH TEH TEH TEH.
JUMA CHAMA GWALA LA YANGA ENZI HIZO. KITWANAS' WOTE BADO VIJANA. PONDA NAYE ANAKUMBUKIA NIGERIA 1981. AMASHA ALIKUWA NUKSI KWA SIMBA NA CDA MPAKA AKAMVUNJA MGUU YUSUF AMBWENE.
ReplyDeleteMKWECHE NA ADOLPH ENZI HIZO PAN AFRICAN LAKINI WALIKUWA WABWETE KWA YANGA KILA WALIPOKUTANA NAO.
MTEMI RAMADHAN MSOMI HUYO JAMAA ALIMWACHIA MIKOBA HUSSEIN MARSHA, KISAKA NAYE ALIKUWA KAPU LA MAGOLI KILA ALIOKUWA AKIKAA GOLINI. NILIKUWA SINA IMANI NAYE HUYU JAMAA.
DUH SOKA YA ZAMANI ILIKUWA KIBOKO SIYO SIKU HIZI. HII LONG TIME MISOUP.
Hivi wadau hapa bongo kuna mchezaji ambaye anamkaribia Sunday Manara kwa kabumbu safi alokuwa anaonyesha enzi zake?
ReplyDeleteLalala Gooooh! Hapana! Hapana! Anondosha pale Ahmed Amasha!! Hizo ndio zilikuwa enzi bwana. Kila siku nilikuwa najiuliza hivi jamaa yuko wapi. Safi sana leo Michu umenikumbusha mbali sana maana jamaa alikuwa ka specialize katika kuondoa mipira nyavuni.
ReplyDeleteAthumani Juma Chama "Jogoo" huyu jamaa kama kuna tunzo ya Gwala bora Tanzania basi anastahili. Kwanza likuwa mtemi "Kamuulize Mogella au Zuberi magoha". Harambee Stars wanamuota mpaka kesho. Michuzi ngoja nikukosoe kidogo huyo sio Athumani Idd huyo ni Athumani Juma Chama "Jogoo".
Isihaka Hassan "Chuku"" huyu jamaa hajawahi kukosa penart na alikuwa kipiga huwa anageukia nyuma akimpa mgongo kipa.
Kitwna Manara jamaa alikuwa anuwezo mkubwa wa kumiliki mipira. Alicheza dakika chache CAN 1980 lakini alimake Best African Team. Ah nisije nikajaza kurasa , dah! zamani ilikuwa raha!
Huwa nawaambia watu kuwa katika maisha ya soka Tanzania, kama ujana huwa haujurudii basi na soka haitajirudia tena katika ardhi ya Tanzania....sitasahahu mpira wa enzi hizo, kuna majira hayatanitoka kichwani mwangu mpaka naingia kaburini kama Ahmed Amasha, Athumani China,Said Sued Scad,Salum Kabunda,Idd Pazi,Athuman Chama,Sunday Manara, Mtemi Ramadhani, Mkama Ntare,George Masatu, Zamoyoni Mogella, Keneth Mkapa....eee bwana eh wako kibao msitake nidate bure, soka ya enzi hizo alahaulah haitarudi tena bongo!
ReplyDeleteNikueleze kitu Michuzi? Umenifurahisha sana kwa picha hizi za hafla hii. Ee bwana umenikumbusha mbali sana. Please, tafuta tafuta wachezaji wengine nyota tujue wako wapi ndugu yangu.
ReplyDeleteMichuzi,leo hakuna matusi,kashfa wala longolongo kila mtu ana raha, hawa ndo walikuwa footballers,bongo tulikuwa mbali enzi hizo kisoka.Mungu awarehemu na ambao ni marehemu wa enzi hizo,namkumbuka Lilla Shomari,Said Mwamba"Kizota" na Hamis Thobius Gaga" Gagarino" si mchezo leo umekumbusha mbali sana misoup.
ReplyDeleteHongera Brother Michu,Kwa picha nzuri za kumbukumbu endeleza libeneke
SOKA LA ZAMANI LILIKUWA TAMU BWANA.
ReplyDeleteUZURI WAKE WENGINE TULIOKUWA MIKOANI TULIKUWA TUNAKAA JIRANI NA REDIO (RTD) WATUPELEKE UWANJA WA TAIFA MOJA KWA MOJA KUTOKA PUGU RODI.
NA KAMA ILIKUWA MWANZA BASI SISIEMU KIRUMBA.HAPO UNAKUTANA NA MAREHEMU DOMINIC MWANA WA CHIRAMBO(R.I.P) HAPO UWANJANI WAPO PAMBA YA MWANZA WATOTO WA KAWEKAMO TUPWISA LINDA.
UWANJANI UNAKUTANA NA NTEZE JOHN RUNGU,GEORGE MAGERE MASATU.
BIG UP SANA BRO MISOUP KWELI UMENIKUMBUSHA MBALI.
PIA NAWAPONGEZA WACHEZAJI WA ZAMANI KWA KUAMUA KUTOA USHIRIKIANO KWA KOCHA "MASIKIO MASHIMO"
michu usibane hiyo sijaharibu najitahidi kuosha kinywa
Misupu kwa kweli leo umenifurahisha, yaani duh! hata la kusema sina, maana nikiangalia picha moja na kumuona mchezaji fulani, hapohapo namkumbuka mwingine, kumbe nae yupo kwenye picha inayofuata. Hii imetulia, na hivyo vichwa vikitoa mchango wao na ukasikilizwa, basi si ajabu Stars ikafanya mauaji.
ReplyDeleteMisisi leo umenifurahisha bwana, hizi picha ni balaa! zimenikumbusha miaka ile nikiwa ndo namaliza primary nikiwa najiunga na Secondari ilikuwa balaa, tukiwa na redio moja tu na watangazaji maarufu kama kina mbonde, Jongo na wengineo, ilikuwa balaa. hebu watafute na watangazaji wa Radio TZ waliokuwa wanatangaza wakati huo tujue wako wapi na wanafanya nini!
ReplyDeletepia ningeomba kama inawezekana utupe wasifu wao hawa wachezaji wa zamani tujue wako wapi na wanafanya nini, kama wana biashara tuwe tunawapiga tafu.
Mpenda bol
Misisi leo umenifurahisha bwana, hizi picha ni balaa! zimenikumbusha miaka ile nikiwa ndo namaliza primary nikiwa najiunga na Secondari ilikuwa balaa, tukiwa na redio moja tu na watangazaji maarufu kama kina mbonde, Jongo na wengineo, ilikuwa balaa. hebu watafute na watangazaji wa Radio TZ waliokuwa wanatangaza wakati huo tujue wako wapi na wanafanya nini!
ReplyDeletepia ningeomba kama inawezekana utupe wasifu wao hawa wachezaji wa zamani tujue wako wapi na wanafanya nini, kama wana biashara tuwe tunawapiga tafu.
Mpenda bol
sisi moja wao bila.....tehe tehe tehe
ReplyDeletenadhani tulikwenda nigeria 1980 sio 1981. wakati huo tulikuwa tunasikiliza radio, kulikuwa na mdau abdul masud (nasikia sasa marehemu) jamaa huyu wakati kipindi cha michezo yetu alikuwa,"asalamleikum wakulima nawafanyakazi po pote mlipo huyu ni mtangazaji wenu ABDUL OMARI MASOUD" halafu ilipotokea uvumi wa YANGA BWANGA toka tanga, jamaa alianza kipindi na "lisemwalo liko kama halipo lipo njiani YANGA ajiunga na YANGA ", sisi wengine wanazi wa SIMBA roho zilikuwa zinatutoka, karibu tupate ugonjwa wa moyo. this was the golden age of soccer in TZ, kulikuwa na hamasa sana.
ReplyDelete