ni furaha ilioje kwa tanzania wani wa zamani juma pondamali mensah alipokutana uso kwa uso na tanzania wani wa leo ivo mapunda usiku huu hoteli ya sea cliff

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kaka Ponda mpe mawaidha kijana aache umapepe akiwa mlingotini.

    ReplyDelete
  2. Michuzi umenifurahisha sana na hii picha ya Pondamali ya sasa, nilikuwa natamani sana nimwone anafananaje sasa. Alikuwa anatufurahisha sana na ule mzaha wake wa kudaka mpira kisha kuwakebehi ma-forward wa timu pinzani kwa kuwarushia tena, ati kuthibitisha hafungiki! Lakini siku moja mashabiki almanusra wamtoe nyongo baada ya mzaha wake huo kuleta kizaazaa!

    ReplyDelete
  3. YOTE TISA. KAMA PONDAMALI (MAARUFU MUUZA MKAA) ANGEKUWA ANADAKA SASA HIVI NADHANI ANGEKUWA ANACHEZA ULAYA NA PESA KIBAO.
    NANI ANAKUMBUKA KULE NIGERIA 1981 WAKATI PONDA ALIPOWASHANGAZA WATANGAZAJI, WASHABIKI NA WACHEZAJI WENZAKE ALIPONYKA MKWAJU NA KUFUCHA MPIRA HUKU KILA MTU AKIDHANI UMETINGA WAVUNI?
    NAKUMBUKA SIKU HIYO MTANGAZAJI WA RTD, SALIM MBONDE NA AHMED JONGO WALIVYOPAYUKA NA KUDAI STARS IMELALA WAKATI PONDA ALIFICHA MPIRA KATIKATI YA MIGUU YAKE HUKU MWAMUZI AKIDAI NGOMA IANZE KATI NA MPIRA WALA HUKUTINGA WAVUNI! PONDAMALI NA WENZAKO MLIPASWA MUWE NA HESHIMA KUBWA KAMA SERIKALI YA NYERERE INGEKUWA INATHIMI SOKA.
    SASA KAZI KWA TFF. HAO JAMAA HAWAZIDI HATA HAMSINI (STARS YA ZAMANI). SI VIBAYA WAKAPEWA TIKETI ZA BURE KUANGALIA VIJANA WA LEO WANAVYOJIFANYA WANAJUA SOKA. HESHIMA SIYO KUWAALIKA TU, PIA WAPEWE UZITO KATIKA MAMBO KAMA HAYO ILI KUHAMASISHA VIJANA.
    SIRI KUBWA YA WACHEZAJI WA ZAMANI WALIKUWA WANACHEZA KWA KUJITUMA. HAWANA MAGARI WALA HAWAKULIPWA MAMILIONI KUCHEZEA STARS. HATA KOCHA WAO JOEL BENDERA HAKUTOKA BRAZIL LAKINI WALIFANYA MAAJABU. HIYO NDIYO ILIKUWA SOOOOOKA JAMAANI. AH KWELI WAKATI UKUTA

    ReplyDelete
  4. Huyu jamaa alikuwa mbabe sana. Wakenya hawatamsahau, maana walipoleta vurugu uwanjani alikuwa anapiga ndoo (vichwa) kwa speed ya supersonic!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...