Timu ya Tanzania katika kashindano ya Dunia - Special Olympics imemaliza mashindano leo asubuhi kwa kishindo baada ya kupata medali za:
-Dhahabu kwenye M. 4x100 Wanaume (Emmanuel Mwakyusa, George Njau, Simon Mollel na Kanaeli Palangyo)
- Shaba kwenye M 4x100 Wanawake (Bonifasia Asifiwe, Sekela Mkondya, Blandina Blasi na Kastola Luambano)
Kwa muhtasari Tanzania ina medali kama ifuatavyo:
RIADHA
Dhahabu.............................. 10
Fedha................................ 6
Shaba................................ 8
Jumla................................. 24
MPIRA WA MIGUU (5- A SIDE)
Dhahabu............................ 9
JUMLA KUU MEDALI 33
Kati ya wachezaji 24 walioko hapa ni wawili tu ambao hawakupata medali ya ushindi wa kwanza hadi wa tatu kwenye kundi lake japokuwa kila mmoja alijitahidi sana katika mchezo wake.
Leo ni sharehe za ufungaji kuanzia saa 2.00 usiku za hapa, sawa na saa 9.00 mchana za Tanzania. Angakia CCTV. Kesho tunaondoka hapa kurejea nyumbani ambapo tunatarajia kufika Jumamosi saa 8.30 mchana.
Frank Macha
SHANGHAI
Hizi ni habari njema sana kwa Tanzania. Nawapa pongezi nyingi washiriki wote.
ReplyDeleteSteveD.
dah, wanamichezo wa kimatahira wa kibongo kumbe ni wakali kuliko wanamichezo wenye akili timamu.Inabidi Taifa stars/olimpiki timu iwe inachaguwa matahira kuliko hawa wachezaji wa Simba/Yanga n.k ambao hawajaleta chochote bongo
ReplyDeleteHongera guys
ReplyDeleteAksante sana kwa kutuwakilisha.
ReplyDeleteMungu ibariki Tanzania!
asante sana kwa ujuzi wako.michuzi oyeee
ReplyDelete