
mdau wa kigogo mwisho, Dar, anapenda kutoa Eid Mubarakh kwa wadau wooooooote wa globu hii. ujumbe anasema; kazi na dawa....anapenda salamu zimfikie msela wake wa loooongi alieko majuu ya wapi sijui huko aitwaye nathan chiume. anampa shavu kwa kuanzisha blogu mpya kabisa iitwayo http://tzcommoncents.wordpress.com/
Hivi wewe mzima au mwehu? hii suruali si ungeivalia shingoni tukajua moja?
ReplyDeleteHuyu akijamba shuzi linatokea kifuani -sentimeta chache kutoka mdomoni, na walleti yake iliyo mfuko wa nyuma anaitolea begani...mambo hayo, New York wanavalia magotini, bongo mabegani.
ReplyDeletemh! papaa huyu kiboko, naomba kuuliza...ikibidi masuala ya haja ndogo chapchap INAKUWAJE?...kazi kwelikweli
ReplyDelete@ ndumba
ReplyDeletecomment yako imenivunja mbavu. imagination zako kiboko baba'ke. aminia! hahahahaha
Hahahahahahaha!!!! ka Michu dah..
ReplyDeleteyaani umenichekesha hadi basi.kweli kazi na dawa.
S.
Mmmmmmmh,
ReplyDeleteSasa huyu sijui akienda haja ndogo anafanyaje.Naona mkanda uko kwapani kabisa.Sijui mfuko wake wa nyuma utakuwa sehemu gani.Mmmmh hii kali.Nimecheka ila inabidi sasa nishangae tu.Kinachonifurahisha ni kuwa yeye hana wasiwasi kabisa na amepozi kwa ajili ya picha.Au labda shati lake ndo fupi (Kijasti bikozi) hivyo kaamua kushona suruali ya namna hiyo.
Kaaaazi kwelikweli
.......jamaa alosto inamsumbua,ameishakata tamaa ya maisha.
ReplyDeleteSasa bro MIchu! Huyu Jamaa ni muuza gahawa au spea tairi? Maanake kama anatangaza genero taya???
ReplyDeleteJamani huyu katoka BAra kaambiwa Pwani (Dar) Kuna "mamende" wanaweza mfanza kitu mbaya so ikabidi ajiwahi msimlaumu.
ReplyDeleteHapa jamani inabidi kusaidiana kimawazo. Huyu jamaa ni muuza kahawa na sijui kama kipato chake ni kikubwa kiasi cha kutumia kitambaa cha surali mbili kushona suruali moja. Umasikini wetu unaongezeka pia kwa kutojua matumizi muafaka ya rasilimali zetu. Anyway, kazi njea muuza kahawa.
ReplyDeletewatu wengine bwana, sijui mnawazaga nini jamani, yani ndumba umenichekesha vibaya sana, sio vizuri hivyo jamani. Big up papaa
ReplyDeleteHuyu jamaa bonge la mbunifu
...nimecheka mbavu sina wazee ila not bad not bad at all jamaaa kapendeza na kiatu kapiga kiwi safi na shati jeupe na inaonekana alikuwa anakuwa wa mwisho darasani kama alisoma na kina Nathan,nathan mwokoe mwenzako mpe mtaji si unajua washkaji hawatupani,unajua nikishuka bongo huwa nakunywa na jaamaa zangu waliochoka na kuishia primary ingawaje nina MBA na kazi nzuri tuu unyamwezini....na Nathan big up bro na kazi nzuri ingawaje huko kwako najua wabongo wengi wavivu wa kusoma
ReplyDeleteduuuuu jamaa ananikumbusha zamani enzi za mabolingo "mikono mileki mingi,ndukidi, sekizengi , novele generation"nk uncle J.wa radio one ,joachim wa DOdoma na Mwl.Kunyanja kule ludewa mpo?
ReplyDeleteNathan mshikaji wako wa Primary kakupa shavu I think that is that is so qute
ReplyDeleteah! Nipo hoi katika picha ya comments zilizonivunja mbavu ni hii! Duh! Jamaa kweli mjasiriamali. kwa mtindo huu atauza chai ile mbaya. Michuzi hongera
ReplyDeleteat least ni msafi.
ReplyDeleteNa wanaosema alikuwa wamwisho darasani mnakosea sana.
Bongo unaweza ukawa na akili lakini uwezo mdogo. Opportunity zinakimbia ni watoto wangapi wanafauli kwenda form one nawazazi wao wanashindwa kuwalipia ada na wanaishia mitaani....
Eejama eejama, hizi comments atakufa mtu kwa kuvunjika mbavu na health insuarance siyo wote tunazo, oohooo!!! Kusema ile kweli ya kumwogopa mola, huyu jamaa ni mnyakyusa kabisaaa wa Tukuyu, kiwira-mwankenja, kaenda Dar kwa magari ya mbio za mwenge, na ana uhakika wa kurudi kiwira na magari ya kampeni ya Mbunge mwaka 2010...uwongo Kasyosyombole????
ReplyDelete