SISI WADAU WA SEOUL TUNATOA MKONO WA IDDI KWA WADAU WOTE DUNIANI WA BLOG HII...HAPA SEOUL LEO TUNASHEHEREKEA IDDI EL FITRI.HONGERA KAKA MICHUZI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. WADAU WAISLAM WENZANGU MIMI NINA SWALI MOJA KUHUSU HII SIKUKUU YA EID EL FITR.
    KILA MWAKA HASA SIKU HIZI SIKUKUU HII IMEKUWA IKISHEREHEKEWA SIKU MBILI TOFAUTI; YAANI KUNA WALE WANAOANZA LEO NA WENGINE KAMA WALE WA BONGO WANA SALI LEO (13/10/07).
    KINACHONISHANGAZA NI KWAMBA SIKU YA IDD KUBWA(EID EL HAJJ), WAISLAM KOTE DUNIANI HUJUMUIKA KWA SIKU MOJA NA KUSHEHEREKEA SIKUKUU HIYO BILA KUJALI NANI ALIANZA KULA EID EL FITR.
    NASEMA HIVYO KWA SABABU, KAMA KUNA KUNDI LA WALIOCHELEWA KULA EID EL FIRT, INA MAANA KWAMBA IFIKAPO EID EL HAJJ (MIEZI TATU BAADAYE) LAZIMA WATAKUWA NYUMA SIKU MOJA KWA HIYO WALITAKIWA WAONGEZE SIKU ILI WATIMIZE MWEZI NA KULA HIYO EID KUBWA!
    NDIYO! KWA SABABU HAIWEZEKANI DINI YETU IWE NA MIEZI MIWILI NDANI YA MWEZI MMOJA (MMOJA KUMALIZA SIKU 29 NA MWINGINE 30) WAKATI MWEZI NA JUA TUNAVYOTUMIA NI MOJA. HUWA TUNAPISHANA MASAA.
    KAMA WATU WANAOANZA KUONA JUA NA MWEZI MWEZI HASA WA SAUDIA WANASALI EID EL FITR LEO, KWA NINI WAISLAMU WENGINE WASIUNGANE NA HAO ILI KUEPUSHA HUU MKOROGANYO USIO NA MPANGO?
    NDIYO NI MKOROGANYO KWA SABABU SIJAWAHI KUONA NDGU ZETU WASIO WAISLAMU WAKISHEREHEKEA SIKU YA KUZALIWA KWA ISSA (KRISMAS) AU KUSULUBIWA KWAKE (PASAKA) WAKILA TAREHE AU SIKU TOFAUTI DUNIANI KOTE.
    AU NDIYO MPAKA AJE MTUME MWINGINE ATUELEZE KUWA WAISLAM SASA TUNAKWENDA NA WAKATI NA LAZIMA TUTUMIE JUA NA MWEZI MMOJA KAMA WANAVYOTUMIA WENE WETU WA JERUSALEM.
    TUJARIBU KWENDA NA WAKATI NA KUANGALIA UWEZEKANO WA KUONDOA HIZI HITILAFU ZISIZO NA MPANGO. NAWEZA KUSEMA BONGO WAMEAMUA KULA EID JUMAMOSI ILI KUTAKA KUFIDIA SIKU YA KAZI JUMATATU NA KUWA NA WIKI ENDI NDEFU ITAKAMALIZIKA JUMANNE.
    HAKUNA JINGINE KATIKA HILO KWANI KAMA UGANDA, RWANDA, BURUNDI NA KWENGINEKO KOTE DUNIANI WAMEKULA EID 12/10/07 KWA NINI HUKO KUWE KWINGINEVYO?
    TUMGHUFIRIE MWENYEEZI MUNGU MAMBO MENGINE WAISLAMU TUNAJICHANGANYA WENYEWE NA NDIYO MAANA YTUNAONEKANA ELIMU NDOGO NA WAKOROFI.

    ReplyDelete
  2. TRUE DAT!

    ReplyDelete
  3. UMESEMA KWELI WE ANON WA KWANZA
    ILA KUNA KITU NAWEZA ONGEZA HAPA
    UNAJUA KUWA DUNIANI KOTE DINI
    ZIMEWEKWA NDANI YA MFUKO WA RULERS
    YANI NAKUMBUKA KUNA SIKU MWEZI
    ULIONEKANA TABORA ILA KWA KUWA
    RAIS WA WAKATI(JINA KAPUNI) HUO ALIKUWA AMEPANGA
    KUSAFIRI KESHO YAKE KWENDA MKOA
    MMOJA KUHUDHURIA SHEREHE YA IDD
    RASMI KESHOKUTWA YAKE WALIOUONA
    MWEZI WAKANYAMAZISHWA NA BARAZA
    ILI MHESHIMIWA ASAFIRI.
    ILA NDUGU ZETU WA ANSWAR-SUNA'A
    WAO WAKASWALI KAMA KAWAIDA YAO
    HAPA NAKUONYESHA KUWA UKOROFI HAUPO
    KWA WAISLAM BALI KWA WATAWALA
    WANAOTAKA KILA KITU KIENDE WALIVYOPANGA WAO.MFANO HAPA UTURUKI
    HATA SIKU YA KUANZA HUPANGWA NA
    SERIKALI NA SIKUKUU NDIO HIVYO TENA
    SISI HAPA TUMESHEREHEKEA SIKUKUU
    JANA IJUMAA.
    HALAFU HAKUNA HAJA YA KUSHEREHEKEA
    SIKUKUU KTK SIKU TOFAUTI KWANI
    HAKUNA SEHEM YEYOTE DUNIANI YENYE
    KUTANGULIA SIKU NZIMA.
    KWA HIYO TUNA MAKOSA KAMA TUNA
    TOFAUTI ZETU LAKINI ZIMESABABISHWA
    NA BAADHI YA WATU FULANI ZAIDI NA
    SIO WAISLAM WENYEWE.
    NA WANAOJARIBU KUFUATA MISINGI SAHIHI NDIO HUITWA ''SIASA KALI''
    NA MAJINA MENGI ILA WAKO SAWA ZAIDI
    YETU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...