haidar abeid muchacho akipokea kombe la ubingwa ambalo simba walinyakua mwaka 1975. hivi sasa simba na watani wao wa jadi wameanza kuonekana wa kawaida tu kwenye ligi kuu na wataalamu wa mambo wanabashiri mabadiliko katika soka ambapo hakutokuwa tena na ukiritimba ambao timu hizi mbili zimekuwa zikijivunia miaka nenda miaka rudi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Is it the beginning of the end for mighty Simba and Yanga?

    Nakumbuka vigogo vya jirani wetu Kenya vya AFC Leopalds and Gor Mahia walianza hivi hivi na hatimaye kupotea katika anga la kabumbu nchini Kenya. Gor waliwahi pia kuwa mabingwa wa Kombe la Washindi enzi zile (kama sikosei).Sasa hivi ukiongelea kabumbu Kenya hawa vigogo hawasikiki.

    Je, Simba na Yanga wanaelekea huko huko? Pity them!

    ReplyDelete
  2. anayekabidhidhi kombe hilo ni mheshimiwa nani?

    ReplyDelete
  3. anayekabidhi kombe anafanana na Babu yetu Mhe.Joseph Mungui,mjumbe wa zamani NEC,IRINGA ambye kwa sasa ni waziri wa mambo ya ndani ya nchi.

    ReplyDelete
  4. anayekabidhi kombe ni Mzee Henry Tandau.Hao wazee ndo walikuwa TANU kweli kweli,walipikwa wakaiva,mathalani kama ungemletea dili la Buzwagi kwanza angekupiga katafunua halafu anakuripoti Ikulu kwa mwalimu mara moja.Those were the times when nidhamu ya kazi really meant discipline na uongozi maana yake ilikuwa ni uadilifu kwa kwenda mbele!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  5. Huyu waziri kwenye picha ni Waziri wa Kilimo na chakula enzi hizo, Mungai. Bahati mbaya ama nzuri Mungai huyo huyo bado ni Waziri wa Kilimo na Chakula hadi sasa awamu ya nne.

    ReplyDelete
  6. Anayekabidhi kombe hilo ni Mheshimiwa Joseph James Mungai. Wakati huo alikuwa Waziri wa Kilimo na pia alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT). Huyo ni Simba sana, huoni tabasamu hilo.

    ReplyDelete
  7. Huyo ni Joseph James Mungai, Waziri wa sasa wa mambo ya ndani.

    ReplyDelete
  8. Mbona Kila mtu kwenye hiyo picha kafunga macho?

    ReplyDelete
  9. we ANON wa October 5, 2007 4:14:00 PM EAT

    Angalizo
    kwasasa Mhe .Joseph Mungay ni waziri wa mambo ya ndani,

    waziri wa kilimo,chakula na ushirika ni mhe.stephen wasira a.k.a "tyson".
    ambaye hivi karibuni alipatwa na matatizo ya kuzomewa na wananchi akiwa ziarani huko mbeya

    ReplyDelete
  10. Wewe Jingo upo nchi gani? Huyu Mungai alikuwa Chakula na Kilimo Kabla ya Kupelekwa Mambo ya ndani kwa hiyo Anyo yupo sawa kwa sababu amekuwa waziri wa Kilimo na Chakula wakati wa awamu ya nne

    ReplyDelete
  11. NAMISS MISHIKAKI YA MUCHACHO PALE KARIAKOO,NA UKWAJU,AU CHICKEN TANDOOR,

    ReplyDelete
  12. WAMEFUNGA MACHO TOKANA NA KUAKISIWA KWA MWANGA WA TOKA KWENYE KURUNZI YA KAMERA YA MICHUZI WA WAKTI HUO !

    Mzushi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...