mbio za mwenge bado zinaendelea katika kuhamasisha kampeni mbalimbali za maendeleo ambapo miradi kibao huzinduliwa na pia ujumbe mzito juu ya masuala mbalimbali ya jamii. kilele chake ni oktoba 14, siku ya baba wa taifa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Du Kaka Misupu Hicho Kitochi Bado Kinasumbua Raia???? Mie Naona Kitupwe Tu Kimepitwa Na Wakati Au Kwa Kua Ni Mtaji Kwa Wenyeviti Na Makatibu Wa Wilaya na Vijiji?? Lol Kitambo

    ReplyDelete
  2. UCHEZEAJI WA MALI ZA WANANCHI FANYENI VITU VYA MAANA WACHENI KUTEMBEZA HIKI KIBATARI WATU WANAKUFANYA NJAA WAKATI MRADI HUU UNAKULA HELA SANA

    ReplyDelete
  3. Duuh! haya mambo bado yanaendelea tuu? Mwenge wa uhuru gani?

    ReplyDelete
  4. Hivi mbio za mwenge bado zipo? Zinaeneza sana magonjwa..

    ReplyDelete
  5. Hivi kuna utafiti wowote wa kisayansi ulishafanyika ili kufahamu faida na hasara za mbio za mwenge tangu zianzishwe? Nauliza ili tujue kama kuna haja ya kuendeleza hizi mbio au la.Anony hapo juu anasema zinaeneza magonjwa...kuna masuala mengine?

    ReplyDelete
  6. Madhumuni ya Mwenge wa Uhuru yalikuwa:

    1. Ulete amani pale pasipo amani
    2. Upendo mahali palipojaa chuki
    3. Na heshima ambapo pamejaa dharau

    Nimeimba sana huu wimbo wa "Sisi tumekwisha kuwasha Mwenge, na kuuweka Mlima Kilimanjaro".

    Ni kautamaduni ka kihistoria kukimbiza huu Mwenge lakini je ni kweli haya maudhui ya kuwashwa Mwenge bado yanafuatiliwa? Isije ikawa Mwenge umekuwa fasheni tu.

    ReplyDelete
  7. Sasa hivi inasemekana mbio za Mwenge zinachangia sana kusambaza gonjwa la Kisasa.

    Mafanikio mojawapo ya mwenge ni kuwa na utitiri wa shule, na taasisi nyingine zinazoitwa "Mwenge" tanzania nzima.

    ReplyDelete
  8. Haya mambo ya mwenge yameshapitwa na wakati. MWENGE MWENGE!!!

    kWANZA HIZO HELA ZINAZOKUSANYWA HUWA ZINAENDA WAPI?

    KUPOTEZEANA MUDA TU. %%%*$£""***UUU

    ReplyDelete
  9. MWENGE UKILALA SEHEM FLANI KESHO YAKE MAELFU YA ''MAPUTO'' HUONEKANA NA WATOTO WA SEHEM HIYO HUFURAHI KUYAPULIZA.KAZI KWELI KWELI JAMANI.MAISHA YETU BWANA.HALAFU WATU HUNYANG'ANYWA SANA PESA ZAO KUCHANGIA MWENGE.MWENGE UDUMU,UDUMU ZAIDI
    UKIMWI UENEE,UENEE ZAIDI

    ReplyDelete
  10. Hilo torch haliko "environmental friendly" Angalia huo moshi..kuzungusha moshi kama huo kwa miezi sijui mingapi na mafuta yanayotumika ni kupitwa na wakati..Jamani okoeni mazingira..na hao FFU wanalinda nini huo moto...wamekosa cha kufanya? Majambazi yanaiba yanamaliza nchi ninyi FFU mnalipwa kulinda Tochi...!!! Kuwamulika wenye chuki..wenye chuki ni hao wanaotuibia pesa zetu za Kodi..wakusanyeni kwenye jengo moja...muwafukize huo moshi mpaka wakione kilichomfanya kanga akose manyoya shingoni..Karigabagaho...!!

    ReplyDelete
  11. TANGU MWALIMU JULIAS K NA KIDOGO MZEE MWINYI, SERIKALI KWA UJUMLA HAIJAWEZA KUPATA MTU SHUPAVU WA KUWEZA KULETA MABADILIKO MAKUBWA KATIKA MIFUMO YETU. HASA YA KISIASA LABDA KWA SABABU WALIO WENGI BADO WANANGOJA FIKRA ZA BABA. PENGINE ATHARI YA "ZIDUMU FIKRA ZA ..." BADO HAIJATUTOKA.

    POLE POLE TUNATAKIWA TUBADILIKE TUANGALIE KWA KINA KIPI KINAFAA KUENDELEA NACHO NA KIPI KINAFAA KUACHWA. KWA MFANO ATHARI ZA MBIO ZA ZINGEANGALIWA NA ZIKIDHIHIRIKA MBIO ZIFUTWE - WATU HAWA WAKAFANYE VITU VYA MAANA ZAIDI.

    TAYARI NCHI INA WATU WENGI WANAOLIPWA BILA YA KUFANYA KAZI ZA MAANA. KWA MFANO BUNGE LETU NI KUBWA MNO UKILINGANISHA NA PATO LETU. WAKATI TULIONAO NJIA ZA MAWASILIANO SASA NI BORA ZAIDI. SASA KUNA HAJA GANI YA WATU MIA TATU KUKUTANA ILI KUZUNGUMZA? NDIO MAANA UNAONA HATA WANACHOKIONGEA NA WANAVYOFANYA BAADHI YA "WAHESHIMIWA" HAWA HAVIENDANI KABISA NA NYADHIFA ZAO. NINA DHANI THELUTHI MOJA YA HAO INATOSHA.

    TUTAPUNGUZA VIPI MATUMIZI KAMA TUTAPENDA MIFUMO YENYE KUTAFUNA PESA ZA WANANCHI?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...