huyu ndiye brian mariki wa houston, texas, mdau aliyejishindia zawadi ya $500 baada ya kuibuka kuwa mdau wa milioni 2. nafarijika kuona kwamba hakuna aliyetia neno juu ya ushindi wa brian, ambavyo ndio kusema ni wa halali...
tatizo ni kwamba wadau wengi wa bongo wameweka pingamizi kwamba zawadi isitolewe hadi kieleweke kwa madai kwamba huu ni ushindi wa mezani a.k.a wa upendeleo kwa kile walichodai kwamba wadau wa ughaibuni wana nafasi nzuri ya kushinda shindano kama hili kwa kilichodaiwa kuwa ughaibuni sio tu kuna nyenzo nzuri na zenye spidi ukilinganisha na huku bongo, bali pia muda wa shindano uliwapendelea wa ughaibuni ambako wakati zilipokaribia dakika za lala salama wengi wa huku bongo ambao wanategemea mitandao ya kwenye kefu na sio nyumbani kama wenzao wa ughaibuni, walikuwa wameshapiga mbonji na hata wangekuwa macho nafasi yao kushiriki ilikuwa finyu.
wadau hawa wa bongo wametishia kukata rufaa, hata mahakamani ikibidi, kupinga zawadi hii kwenda ughaibuni.
ukizingatia kwamba poingamizi la wadau wa bongo lina mantiki, najikuta nimewekwa njia panda na sijui nifanyeje wakati bado mkwanja wa $500 ninao mkononi, na mchakato wa kuutuma unakaribia kuhitimishwa.
wadau naomba msaada wa mawazo kwa hili...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 34 mpaka sasa

  1. mimi ninachokataa ni kuwa brian alishasema kwamba ameshinda kabla hata ya shindano kwisha. wape pole wabongo kwanini hawakukataa kabla ya mpambno kwisha wanakataa baada ya kukosa. brian mwnyew bado anasoma mwacheni apate za kumsogeza kidogo

    ReplyDelete
  2. Wabongo ndo maana hatuendelei. Watu walikushauri junsi ya kuendesha jambo hili ukapuuzia. Sheria ni sheria. Kwa nini wakupendelee et kwa sababu huna nyenzo. Kama huna nyenzo basi usishindane na wenye nyenzo. Blogu hii ikitaka kujiosha na jinsi inavyoonekana... "Tabloidish" na kuanza kuwa credible sio mambo ya Kikwete kila siku...lazima imlipe huyu bwana. It is too late to change the rules bro!!!

    ReplyDelete
  3. mpatie bwana Brian kitu yake tu afanyie mambo! Hizo kasoro ndogo ndogo zitarekebishwa wakati wa zawadi ya mdau wa mil 3

    ReplyDelete
  4. nani kawaambia wategemee mitandao ya kwenye cafe!wala hili halina mjadala kwani michuzi hukujua tangu mwanzo, mpe mshikaji chake wala msilete zenu za kuleta.

    ReplyDelete
  5. kama watu mlijua kuwa hili ni shindano mgetafuta internet cafe zenye high speed.
    mpeni huyo zawadi yake...

    ReplyDelete
  6. congratulations brian u deserve the 500 dollars! don take any nonsense anyone says ,tanzanians never agree to any sucess critisizing is our best interset ...enjoy your benjamins

    lynn -uk

    ReplyDelete
  7. KAKA MICHUZI

    MIE UMENISHANGAZA KUWA UNAJIULIZA UFANYEJE. NDIO MAANA MIE NAPENDA MAMBA YA WAZUNGU. WAKISEMA WAMESEMA NA HAKUNA MTU HATAWABADILI MAWAZO KWA SABABU ZA KIUMASIKINI KAMA SINAZOSUMBUA WATANZANIA WENGI.

    KWA KWELI UKIBADILI MAWAZO JUU YA KUWA HUJUI PESA UMPE NANI NAJUA HUTAKI, AU UNA WATU TENA NA KAMA HUTAKI KUMPA BRIAN MIE NI MMOJA WA WATU AMBAO NITAKUDHARAU AS UNAWEKA WEBSITE NA HAUNA MSINGI.

    NI KUWA UTAKUWA UMEONGEA POROJO NA KILA UTAKAPOSEMA UNA MASHINDAO BASI MIE NITAONA UNAONGEA UONGO.

    NIMEKASIRISHWA NA WEWE KUANDIKA KUWA HUJUI UFANYEJE? KWANI WATU WAKIANDIKA HUMU LAZIMA UWASIKILIZE JE ULICHOSEMA MWANZONI MBONA HAWAKUSEMA USIFANYE USHINDI HUO. AU

    KWA IDADI YA WATU WALIOINGIA KATIKA SITE YAKO KUNA ALIYEJUA ITATOKEA HIYO 11 PM. NO HATA MIE NIPO UGHAIBUNI NILIKUWA NIMEJICHOKEA NA KUENDELEA NA MAISHA YANGU NA USINGIZI MNONO.


    NAKUSHAURI FATA ULILOSEMA HUNA HATA HAJA YA KUPROVE NA PICHA ULITAKA E-MAIL ULIPATA TUMA HIYO PESA ASAP KAMA ULIVYOAHIDI

    BRIAN TUAMBIE KAMA UMEPOKEA PESA HIZO.. TUMIA TZNET WEBSITE

    AS MICHUZI ANAWEZA AKAICHIMBIA UJUMBE WAKO.

    NDIO MAANA NAPENDA WATU WALIO WESTERNISED NA SIO KULLIA MALALAMIKO YANAYOFANYA NCHI ISIENDELEE

    MICHUZI LIPA ZAWADI HIYO SIO KESHO USEME ULIENDA NUNUA NYANYA SIJAQLI PESA ZIMETOKA WAPI. WEYE LIPA HIZO PESA ASAP KAMA ULIVYOAHIDI

    LIPA ZAWADI HIYO

    WANAOLALAMIKA WAAMBIE WAINGIE KILA SEKUNDE HADI IFIKIE MILIONI 3 WATABAHATIKA HAPO.....HIYO NI KAMA NI DESTINY YA MUTU

    ReplyDelete
  8. Michuzi,
    Tafadhali mpatie bwana Brian mkwanja wake kuheshimu sheria za shindano. Swala la kusema uko njia panda kwa sasa halitambuliki. Tusubiri wakati ujao wa labda milion 3 ndo tufikirie wadau walalamikaji wa nyumbani tunafanyaje. Kwa sasa imetoka hiyo dola 500 za Brian PERIOD. Tunahitaji kujua kama mkwanja umemfikia Brian.
    Mdau( mmoja wa washindwa!)

    ReplyDelete
  9. The Housemate most deserving the US$100 000 is...

    Richard - to turn his life around
    52.7%


    Maureen - she suffered a lot as a kid
    13.7%


    Ofunneka - for being the mother of the House
    29%


    Tatiana - to boost her modelling career
    4.6%

    unajua kwanini tanzania hakuna vurugu kama somali ama burundi? kwasababu wananchi wanajikubali.. umoja na wana nia kama nimekosea samahani. ila tumejitahidi kwa leo kwa kuendeleza libeneke la kuosha jina la tz. VIVA NYERERE

    ReplyDelete
  10. WEWE ANONY WA KWANZA KABISA USITAKE KULETA HADITHI ZA SUNGURA NA FISI HAPA... WATU WANGAPI HUWA WANAKISIA NA KUJIKUTA WAMEBAHATIKA MAMBO KIBAO? MTU ANAWEZA KUKWAMBIA UKIAMKA KESHO MAMA YAKO MDOGO ATAKUWA HATUNAE NA UKIAMKA UNAKUTA NI KWELI UNATAKA UNIAMBIE ALIMLOGA AMAA HUYO MTU ALIKUWA NA MKATABA NA MUNGU?... ACHA HIZO BWAANA KUNA WATU WAJUKUU WA MTUME WEWEEE!MICHUZI UKIWEZA KUTUBADILISHIA MISS TZ 2007 BASI BADILISHA NA HII ZAWADI YA MSHINDI WA 500DL.

    ReplyDelete
  11. Hivi kwani kuna mtu alipanga hiyo number ifike saa hizo za suiku?

    Ndio maana ya bahati nasibu. Michuzi kama ilikua zawadi itolewe kwa mtu aliyeshika number millioni mbili basi itolewe bila kujali ilikua saa ngapi huyo mshindi alipatikana.

    Mwenzenu alicall sick kujaribu bahati yake.

    Ni bahati yake

    ReplyDelete
  12. Damn,all the complaints so far regarding the results are funny-I mean,if your complaint is "My internet connection isn't as fast as his",then maybe you need to give Africa Online a call or something...Plus,how do you even know if my internet connection is fast at all

    ReplyDelete
  13. Michuzi ,

    Mimi sidhani kama watu wa kulaumiwa ni wadau wa bongo , nadhani kosa ni lako mwenyewe ulitakiwa uconside vitu vyote mpaka time factor .

    Lakini kikubwa ni lazima utimize ahadi yako ...mpe brian wa Htown haki yake .

    ReplyDelete
  14. Hahaha Misupu Acha Janja Ya Nyani Unataka Kumtia Ndani Jelo Lake Dogo...Najua Jelo Kulitoa Bongo Kwenda Marekani Inauma Yaani Unarudisha Nyama Buchani Na Huna Kitoeo. Kazii Kweli Kweli

    ReplyDelete
  15. Michuzi mpatie jamaa mshiko wake kwa kushinda, sheria ilikuwa mtu lazima awe wa million 2 na jamaa andiye wa hiyo milioni 2 sioni sababu ya kuishilia hiyo tunzo yake, yeye ndiye anayeweza ku kushitaki wewe kwa kuleta ubabaishaji baada ya kueeleza ni nani atakuwa mshindi. In short, the man can sue this blog if you keep holding the monies without reasonable doubt.

    Take care y'all, especial our main man mr michuzi. keep up your good works.

    From Atl, the land of braves,hawks and the falcons the dirty birds.

    ReplyDelete
  16. Malalamiko yaliyotolewa na walalamikaji yalitakiwa yaletwe kabla ya shindano. It is too late now, Brian ni mshindi halali wa hili shindano, mpe dogo $500.00 akajirushe.

    ReplyDelete
  17. Michuzi mpe tu chake si ulitaka iwe hivyo, kwanini hukuangalia time lakini, anyway chake ni chake tu mpe atapumzika kubeba mabox kwa muda na kuosha vyombo angalau kwa wiki mmoja! But next time make sure unakuwafair bwana!!

    ReplyDelete
  18. ACHA UZUSHI ISSA. WE UNAKUWA KAMA SIO MPENZI WA MPIRA BWANA. REFA AKISHAAMUA NDIO ITAKAVYOKUWA, HAO WANAOKATA RUFAA NDIO WANATAFUTA USHINDI WA MEZANI.

    KASORO ZOZOTE ZILITAKIWA KUREKEBISHWA KABLA YA KUTANGAZA MSHINDI, SIO SASA HIVI.

    MTUMIE DOGO MSHIKO WAKE FASTA, SIE WENGINE TUSUBIRI DAU LA MTU WA 3,000,000

    ReplyDelete
  19. Michuzi kwa sababu shindano halikuwa na masharti yoyote basi una lazimika kumpatia Bwana Brian zawadi yake.Kwa siku za mbeleni nakushauri uweke japo masharti machache ili kusiwepo na manung'uniko ya aina yoyote.Idumu blogu yetu.

    ReplyDelete
  20. Hehehe ... sijui kama bado inaendelea lakini miaka ya nyuma kule Tanga kila Jumapili asubuhi wadau walikuwa wanakusanyika kwa muuza kahawa barabara ya 13 karibu na sokoni na walibishana mpaka kukaribia kuchapana bakora kuhusu matokeo ya mpira uliochezwa Jumamosi. Hao "wazee wa kahawa" walikuwa "legendary" na walikuwa na kawaida ya kurudia dakika zote 90 za mechi!!

    Mjadala huu wa $500 umenikumbusha enzi hizo ... ninachosema hapa ni kwamba hao "wazee wa kahawa" pamoja na ubishi wao hawakubadili matokeo ya mechi. Kwa hivyo mpe chake Brian na waache "wazee wa kahawa of the Internet" waendelee kubishana!

    ReplyDelete
  21. kwa picha tu dogo anaonekana choka mbaya,mpe tu itamsaidia akanunulie bakuli la uji.

    ReplyDelete
  22. jamani kila dili bongo mbona wanawin wachaga tu?kunani?

    ReplyDelete
  23. Brian Anastaili hiyo zawadi.next time Michuzi weka some law to govern the mashindano.hili Wabongo wasilalame kama ilivyo kawaida yao,
    .Idumu blogu yetu

    ReplyDelete
  24. Kaka Michuzi hebu mpe Brian mshiko wake halafu usovu mambo mengine usitake kukaa nazo mwhisho watu waziibe pls hapa kila mtu anajua BAHATI YA MWENZIO USIILALIE MLANGO WAZI AWE WA UGHAIBUNI WHATERVER THAT IS BAHATI YAKE...WANAOPINGA WASIKATE TAMAA ILA WAJARIBI NEXT TIME.

    ReplyDelete
  25. KWASABABU BONGO NI TAMBARARE, BASI WABONGO NUNUENI MAKOMPUTERS MUWEKE NYUMBANI, UNGANISHENI AFRICA ONLINE, NA PIA HAKIKISHENI MNANUNUA LUKU ZA KUTOSHA, ILI HATA MAJI YAKIISHA MNA-PUMP...LAKINI KUMBUKENI, MSISHINDANE NA UGHAIBUNI, HUKU HAYO YALIKUWA KARNE MBILI ZILIZOPPITA!

    ReplyDelete
  26. UJUMBE KWA MZEE BRIAN, HONGERA KWA USHINDI KWANZA.MIMI BINAFSI NILIJARIBU LAKINI SIKUBAHATIKA NA NILIKUA NIMEPANGA KUIDONATE HIYO $500 KWENYE CHARITY YOYOTE HUKO BONGO.HICHO SI KIASI KIKUBWA LAKINI CHAWEZA SAIDIA KUBORESHA MAISHA YA WATOTO YATIMA HUKO WANAPOISHI.NAKUOMBA SANA ULIFIKIRIE HILO NAWE PIA NA WEWE KUWA HUKO H TOWN NI BAHATI TOSHA, SIDHANI KAMA HAKO KADOLA 500 KATAKULETEA MABADILIKO YOYOTE-AKHSANTE,MUNGU AKUJALIE USHINDE LOTTERY!

    ReplyDelete
  27. HAMNA KITU HAPO MPAKA KIELEWEKE HAKUNA KUPEWA MSHIKO HUO MPAKA IFIKE J3 AMBAPO WADAU WENZANGU WA BONGO WATAKUWA MAKAZINI KWENYE INTERNET LEO NI WEEKEND.
    MICHU HUU NI UPENDELEO MKUBWA KWA WADAU WA UGHAIBUNI MSHIKO HUU KATU HATUKUBALI AKABIDHIWE TUMEWEKA PINGAMIZI HATA MAHAKAMANI TUTAKWENDA KWA HILI TUNANYANYASWA

    ReplyDelete
  28. Acha porojo.Unasema kuna wadau wa bongo wamepinga matokeo.Wamepinga matokeo hayo kwa njia ya simu,e-mail au mmekutana mtaani?Maana sijaona pingamizi lolote hapa kwenye blogu yako.Au unaowaita "wadau wa bongo" ni wewe mwenyewe na wallet yako?Ahadi ni deni,na "ujiko" comes at a price.Mpe mshakiji kilicho chake,usituletee habari za kia za Azim Dewji na Simba (vs ASEC).

    ReplyDelete
  29. kaka michuzi ile sentesi yako ati hata bongo life tambarale naona iliwagusa wengi...inarudiwa rudiwa saaana...

    mdau toka glasgow

    ReplyDelete
  30. "congratulations brian u deserve the 500 dollars! don take any nonsense anyone says ,tanzanians never agree to any sucess critisizing is our best interset ...enjoy your benjamins

    lynn -uk"

    Will do so :D !

    ReplyDelete
  31. OYA MICHUZI KAMA HUYO BRIAN NDO NDO MSHINDI BASI MPE.
    kasera
    kc,ks

    ReplyDelete
  32. Bro Michuzi, kwani hali halisi ya mshindi wetu unaiona. Dogo tangu amefika H-TOWn hajawahi kwenda Barber Shop, tafadhali nakuomba mpe chake kwani Mungu kamjalia kushinda hil jero. Pia najua ilikuwa janja yako kutaka kujua unawadau wanmgapi duniani na ili kuongeza wadau ukatangaza mdau wa Milioni moja atapata jero. Sasa kama umeshajua nakuomba uwaambie wanaodai wadau wako waliokata rufaa waache mambo ya kishamba wasubiri utakapotangaza zawadi nyingine ya mdau wa milioni tatu. mpeeeeeeeeeee chake dogo.

    ReplyDelete
  33. wabongo acheni kuendekezeza njaa, yani vidola 500 vinataka kuwatoa imani.
    Na wewe michuzi acha janja, we mpe mshikaji hizo pesa. kama mahakama ni wewe utashitakiwa kutokana na kutoweka mpangilio mzuri katika hii bahati nasibu mbuzi.

    ReplyDelete
  34. Tutaaminije kama huyo unayemuita Brian ni binadamu hai au changa la macho......anyway...najua hutaitoa hii comment...ila....MESSAGE SENT!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...