Bw. Michuzi,
Nimefurahi sana kuona, katika mtandao wako, umechapisha vitabu vyanguvya *ALFU LELA U LELA* (kitabu cha kwanza, cha pili, na cha tatu),ambavyo vimechapishwa na Mkuki na Nyota Publishers, Dar-es-Salaam.

Hili ni toleo jipya kamilifu litakalokuwa na takariban vitabu kumi. Licha yazile hadithi za zamani zilizopendwa, humo mna hadithi mpya mpya ambazohazijulikani. Na zile zinazojulikana, kama vile hadithi ya *Kamarazanna Badoura,* zilifupishwa.
Mimi, katika toleo hili jipya, nimezitafsiri hadithi zote kikamilifu, na nimeongeza hadithi nyingine nyingi zakusisimua ambazo hapo awali hazikujulikana! Kitabu cha nne, cha tano,na cha sita, vimo mitamboni na vinatazamiwa kutoka mwisho wa mwaka huu.
Kwa wale wanaopenda kuzifaidi hadithi hizi na wanaoviulizia, wanawezakuviagiza vitabu hivyo moja kwa moja kutoka kwa mchapishaji Mkuki naNyota Publishers Dar-es-Salaam, Tanzania.


Shukrani nyingi kwa "kuvipigia debe" vitabu vyangu hivyo!

Hassan Adam
Chuo Kikuu
Cologne,
West Germany

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kaka Hassan Adam, napenda kukujulisha kuwa enzi za "WEST" na "EAST" Germany ziliisha baada ya kuuvunja ukuta wa Berlin. Hivyo usiniangushe ndugu yangu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...