WADAU KUNRADHI, KUULIZA SI UJINGA. NA HILI SI SHINDANO NI SWALI TU LA KAWAIDA AMBALO NAOMBA NISAIDIWE JIBU
KWA UZOEFU WANGU AGHALABU UTAKUTA MDAU ANAONA AIBU KUTAJA YEYE NI WA KABILA GANI, AMA KUNA WADAU AMBAO HUTANIA MAKABILA YA WENZAO KWAMBA YAKO HIVI AMA VILE NA WENGINE HUJISIFU KWA KUWA WA KABILA FULANI KATI YA HAYO TAKRIBAN 120 TULIYONAYO...
SWALI: HAPA BONGO KABILA GANI BORA KULIKO MENGINE NA KWA NINI?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 119 mpaka sasa

  1. Kwa mtazamo wangu sioni kabila bora,kila mtu ana kabila lake na analijua yeye mwenyewe ubora wake uko wapi,hata hivyo baba wa taifa alisema tusiulizane makabila...!! Kwani unataka kutambika?????

    ReplyDelete
  2. Michuzi ulijuaje nilikuwa nasubiri swali kama hili? Kabila bora kuliko yote bwana Wachagga!! sababu:
    1. Watautaji sana tena kwa nyenzo zote ili mradi tu wapate pesa
    2. Ukizunguka mikoa yote ya tanzania hukosi wachagga tena ndo wafanya biashara wakubwa kwenye maeneo hayo.
    3. Hata nchi za jirani na nchi zingine wapo wachagga wamejikita kwenye biashara!
    4. Watu wasiojisikia, wanapenda kujichanganya, hawana hasira za haraka.
    5. Ngono kwao ni zoezi la mwisho yaani pesa mbele ndo ngono badae kama watapata nafasi!

    Hope mmenipata!!
    he he he

    ReplyDelete
  3. Wamakonde na sababu ni kuwa ni mabingwa wa kukata kiuno

    ReplyDelete
  4. Michuzi,
    Kabila bora kuliko yote hapa bongo ni la Mswahili..!! Hope it makes sense...!! Kuna makabila ambayo (sitayataja) wanajiona wamesoma kuliko wenzao, wana pesa kuliko wengine n.k lakini kuwa na vyote hivyo inatokana na economic advantage waiyoipata kutoka kwa system za kikoloni...kwamfano..sehemu ambazo wamissionari wa kizungu walizoingia zilipata faida in the end kwavile walijengewa mashule na kudevelop "elite class" ambayo watoto wao na familia zao zinaendelea kufaidi. Swali ni kuwa ubora wa kabila ni elimu, pesa, akili au ni nini hasa..lazima tuwe na kigezo kabla ya kuamua kuwa kabila gani ni bora...kigezo nilicho nacho ni cha utu..na utu wa mtu si pesa...!! Kila binadamu ana haki ya kuwa treated kwa heshima na kupata huduma zote za jamii "basic needs" hivyo...sisi wote ni waswahili na wadhungu na wahindi na waarabu wote tu bora....kama unendesha Audi...vilevile wote tunakwenda choo..usiku tunalala kitanda kimoja na chumba kimoja..siku ya kufa wote tunakufa tu..kama Mbwa..wala hakuna anayekufa tofauti kwavile ana pesa...Mengi mengi mengi ya kuelezwa..Asante..Je nitashinda dola 500? Asante...!! Mdau wa USA-CA

    ReplyDelete
  5. Hakuna kabila bomba kama WASUKUMA,si wachoyo wa msosi hata kidogo nawala si wakabila,na hatuhusudishi michomo wala utapeli au wizi wa pesa.

    ReplyDelete
  6. Kwanza kabisa naomba nikwambie Bro.Michuzi hapa bongo hakuna kabila bora au zuri kupita mengine. Nasema hivyo kwa sababu nchi haina ukabila kama unavyojua. Lakini kama unataka kusema kabila lipi ni bora basi wewe ambaye umeanzisha mjadala huo utuambie kwa maoni yako wewe Michuzi na kwa uwezo wako wa kuchambua mambo kama mwandishi wa habari wa gazeti la Serikali utuambie ni kabila gani bora.

    ReplyDelete
  7. That's easy, WACHAGA a.k.a MANGI'S. hilo ndilo jibu. Unauliza kwa nini tena? Kwani wewe mwenyewe hujionei kwa macho yako?

    ReplyDelete
  8. Asalaam alyeikum wanablogu,
    kaka Michuzi huko unakoelekea naona ka siko! mada nyeti kidogo! Nachelea kusema kwamba zifuatazo zaweza kuwa dini gani bora,jinsia gani bora n.k
    Well,kila mtu na uhuru wa kutoa maoni yake! (Haki elimuu! Ngwe! ngwe!)

    ReplyDelete
  9. WAGAGAGIGIKOKO...By Bulichekaaa...

    ReplyDelete
  10. Ukisema bora una maana gani, ubora katika kilimo, ngoma, uwindaji au au wa kitu gani? Unatumia kigezo gani kufafanua na kuuelezea ubora?? Ninachoelewa mimi hakuna mtu bora kuliko mwingine, bali kila mtu ana sifa zake tofauti, vilevile na makabila ndivyo huwa hivyohivyo!

    ReplyDelete
  11. WASUKUMA NI BORA...tumesoma sana, tuna maendeleo mazuri sana,(japo viongozi wanakula hela zetu Mwanza hakuendelei, ila Lau Masha kaahidi kupatengeneza pawe kama america), tuna utajiri sana wa asili, ming'ombe, mishamba n.k sitaki kusema mengi, hali inajieleza, WASUKUMA NI BORA FULL STOP.

    ReplyDelete
  12. KAKA MICHUZI,
    Kwanza nianze kwa kukushukuru kuweka mtundiko huu. Nimekuwa nikifuatilia sana na kuona baadhi ya wachangiaji katika blog hii wakiwatania watu fulani kwa kudharau makabila yao. Mfano mzuri, wewe sijui kabila lako, lakini nimeshaona watu wakiudhiwa na kitu fulani cha blog yako, wanakutania kwa kabila lako. Wakijifanya kanakwamba kabila hilo ni dogo sana na lilsilo la maana.

    Kujibu swali lako. Mimi nionavyo, hakuna kabila bora katika Tanzania hata moja. Ni kama kusema baba na mama nani mzazi zaidi ilivyo ngumu kujibu. Ila tu mtu anaweza kusema kabila fulani ni bora zaidi kwa kitu fulani kimoja, viwili, vitatu nk. Lakini hawawezi kuwa mabingwa wa kila kitu.

    Wewe mwenyewe umeona kuna makabila yanadharauliwa, lakini yana mambo mazuri kuzidi yale yanayosifiwa. Wengine utasikia ni watafutaji hela, lakini hapohapo unakuta huo utafutaji unakuwa ni kikwazo kwa jamii miongoni mwao, hasa kama hawatapata hizo hela kihalali.

    Mtu anayesema kabila fulani ni zuri kuliko mengine yote kwa ujumla wake, ni mwongo, na tumwogope. Ila, hatuwezi kumzuia mtu kusema anachotaka, acha tu apayuke maana mdomo ni wake. Utafunga midomo ya watu bwana Michuzi? Wapi na wapi, maana wengine tupo mbali na TZ. Sasa utatusimamia vipi.

    Ili kulinda heshima ya taifa letu na kuacha kujidai wakati ka-nchi ketu bado kanajikongoja na tukabaguana kwa kuona baadhi bora na wengine ovyo, ni kama mtu aliyeona mto akadhani ndio wenye maji mengi kuliko hata bahari, maziwa nk.

    NAWAKILISHA. Kitu kimoja nakusifu, wewe mvumilivu sana, maana kuna watu wanaandika upuuzi na hujawahi kuwatukana au kuwadharau.

    ReplyDelete
  13. ....mchuzi na taaluma yote ya uandishi wa habari na kama ni mtanzania unauliza swali kama hilo?ebu peleka mambo hayo kenya siyo hapa na bahati yako nyerere kafa angefunga hii blogu yako.eti kabila gani bora?we unajua bongo kuna makabila mangapi?hamna kabila bora sisi kama watanzania wote ni bora.

    ReplyDelete
  14. mimi nafikiri wamasai na wamakonde.
    Kwa sababu ya utamaduni wao uko so unique,tabia na namna wanavyoishi, hata muonekano wao uko tofauti,pia wanatambulika hata kimataifa kiurahisi kutokana na sababu nilizotaja hapo juu wamakonde wana sanaa yao ya kuchonga,zile chale zao hata ngoma zao ambazo zinaitambulisha tanzania na utamaduni wetu kwa ujumla . Wamasai wao ni kama symbol ya nchi wakionekana tu ni kivutio kwa watalii,zile dread zao, mavazi, nyimbo zao na namna wanavyocheza ni kivutio kimataifa. Pamoja na hayo makabila haya mawili yana historia ya utani kutokana na tabia zao na namna wanavyoishi kwetu sisi watanzania tunawatambua kwahilo zaidi.

    ReplyDelete
  15. TANZANIA HATUNA NA HATUTAKI KUANZA SASA UKABILA.

    ReplyDelete
  16. Mjadala mzuri sana huu!!!kabila bora kuliko yote ni kabila la utanzania.sababu:lugha ya kabila hili(kiswahili) inaeleweka nchi nzima na kila mtu duniani anaweza kujiunga na kabila hili tofauti na makabila mengine.kuna wasiokubali kuwa kuna kabila la utanzania.jamani naomba tusibaguane sisi wengine kabila pekee tulilokuwa nalo ni utanzania,msitutenge...zemarcopolo.

    ReplyDelete
  17. Swali linaelea mno hewani kwa maana hiyo kuna uwezekano wa kupata majibu mseto. Kungekuwa na vigezo oh! ingekuwa rahisi sana. Kwa mfano nguvu za uchumi, ukarimu, taaluma, utamaduni, siasa n.k, n.k, n.k Basi mkuu kama inawezekana hebu 'litune' swali lako sawasawa tuchangie. Wengine wanaogopa kutaja kabila mara nyingi kutokana na mada inayojadiliwa, kwa mfano kama mnazungumzia habari za kwa... unakuta kabila fulani lipo juu. Ubeki tatu tena unakuta kabila fulani lipo juu, ujambazi tena hivyo hivyo. So pls.be a bit specific.

    Cheers.

    ReplyDelete
  18. miichuzi ,

    Sidhani kama kuna kabila lolote bora na ukomwona mtu anajitamba kuhusu kabila lake then ameishiwa sera. Michuzi are you serious kwamba hayo mambo bado yanaendelea huko nyumbani , mimi nilikuwa nafikiri tumeshapita hiyo level....

    ReplyDelete
  19. Kabila bora ni MAASAI kwa sababu zifuatazo:

    1. Wanaendeleza mila
    2. Walinzi wa mazingira
    3. wametoa viongozi machchari sana Tanzania (Sokoine, Lowassa, Mrema)
    4. Hawana makuu.

    By the way Michuzi kuna jamaa mwingine anabandika picha zako www.lumage.blogspot.com. je, nae ni mdau? Nafikiri blogu yetu hii iko chini ya copyright siyo copyleft

    Mdau Adelaide, Australia

    ReplyDelete
  20. Kabila bora kuliko yote ni Mtanzania sababu 1. Lugha yake inaeleweka kwa jamii zote 2. inaweza kutumika kwa asilimia 60 afrika mashariki bila ya matatizo 3.Inaondoa ubaguzi wa rangi, jinsia na uzawa.

    ReplyDelete
  21. Makabila yote Tanzania ni bora,hakuna lililozidi jingine kwa hili au lile!Wote ni waTanzania halisi.Jingine zuri ni kuwa tofauti na nchi nyingi za Afrika,Tanzania hakuna ukabila na ni vyema kwetu tuendelee hivyo hivyo.

    ReplyDelete
  22. Yaani baada ya kuona kumetulia...Dr. Slaa kajinyamazia, Zitto kajipunzikia, Jk katulia home, hakuna ajali ya kiongozi na mafisaji wanajilia vyao...SASA KILICHOBAKI UMEONA UANZE KUTUCHONGANISHA.......USHINDWE NA ULEGEE

    ReplyDelete
  23. Wazanaki (Nyerere), Wapemba (Mwinyi), Kabila la Mkapa na Wakwere (Kikwete) - They produced presidents.

    ReplyDelete
  24. Sasa hilo nalo swali gani? Ubora wa kitu gani na kwa mtazamo wa nani? Kwa hiyo na sisi Watanzania tumeanza kurudi huko kwenye makabila? Badala ya kuulizana ni kwa nini nchi za Afrika zimeendelea kutia aibu kwa vita, njaa, umaskini, rushwa, maradhi na ujinga karibu miaka 50 baada ya kuwa huru, wewe unauliza kabila?

    ReplyDelete
  25. Mimi nadhani Kabila bora ni huyu mdogo, yaani Joseph Kabila. Baba yake Joseph, Marehemu Laurent Kabila alikuwa dikteta sana na ndo maana nafikiri akajikuta akiuwawa.

    ReplyDelete
  26. Bwana Michuzi, hilo ni swali ama? Mbona majibu yapo wazi? Kabila linalotisha Tanzania na ambalo lipo juu ni WACHAGGA!!! Unafanya mchezo nini? Kila mchagga amefika angalau form six, kila baada ya nyumba kuna shule, hlafu nyumba zetu kule uchaggani ni za nguvu !!! Mambo ya villas tu, full cement, vijijumba vya udongo udongo kwetu hamna.

    Mahoteli ya maana ya kumwaga, na Mungu kwa jinsi anavyolitambua hilo, kuwa wachagga tupo juu, katubariki na Mlima Kilimanjaro, tuzidi kupiga bao.

    Ni hayo tu.

    Shimbonyi Shenu.

    ReplyDelete
  27. KABILA BORA NI LA WABONDEI FROM TA. BWANA WATU HAWA KWA KWELI NI WACHESHI, WAKARIMU, WANAROHO NZURI, WANAUSHIRIKIANO, WAMEELIMIKA KIASI, NK.
    N.S

    ReplyDelete
  28. MICHU KWA KUPENDA KUWATAFUTA WACHAGA MANENO!UNATAKA TU WASEME ILI WALUGALUGA WAANZE KUCHOMBEZA, ANYWAY HAWA JAMAA MIMI KWA KWELI NAWAKUBALI SANA, ILA SIPENDI WANAVYOPENDA KUOANA WENYEWE KWA WENYEWE, YOU HAVE TO MIX WITH OTHERS ILI KUWA TAIFA MOJA KUBWA NA IMARA.BY THE WAY WALIKUWA FAVOURED NA ELIMU KUJA KWAO MAPEMA, ILA NIWAPIGANAJI HATA AMBAO HAWAJASOMA, WACHAGA NOMA, WAPO KILA KONA YA TANZANIA NA SIDHANI KAMA KUNA NCHI HAWAPO HAWA!SHIMBONYI

    ReplyDelete
  29. Nafikiri Utanzania ndo kabila bora.

    Mimi ni Mchagga na ninaona fahari kubwa sana kuwa mchagga ila na kutaja kabila langu kwa yeyote, Ila tu, Uchaga wangu huunifanyi nimuone Mngoni au Msukuma kuwa si bora.

    Kwani kuna mambo mengi hapa kwetu nchini yanafanywa na Watu toka Makabila mbalimbali yaliyobora na kuna mambo mengi mabaya yanafanywa na watu wengi wa kutoka makabila hayo hayo.

    Kwangu mimi nionavyo ni kuwa; Ubora wa mtu sio kabila UBORA wa MTU ni UTU.

    Hayo ni maoni yangu.

    ReplyDelete
  30. You cant be serious,man.What a silly question!?Anyway,labla unataka kusikia kwamba CHINGAZ (including yourself) ndio kabila bora zaidi.

    ReplyDelete
  31. Baba wa taifa akifufuka leo atalia machozi kuona hata kijana wake isa michuzi anazungumzia ukabila.
    ukabila ni mbegu mbaya sana. na inapofikia watu wanazungumzia na kutaja makabila yao basi ujue kuwa harufu hii ya ukabila imeshaanza kujitokeza miongoni mwa watanzania.kuna siku tutazungumzia dini gani ni bora na baada ya hapo tutazungumzia kanda ipi ni bora kati ya ziwa, kaskazini, kusini na kati.
    Eeh Mungu tuepushie hili balaa la ukabila na ubaguzi wa aina wowote ile.
    Kuna yule mwanasayansi mmoja aliwahi kusema hivi majuzi kuwa watu weusi hawana IQ zaidi ya watu waupe eti baada ya kufanya uchunguzi wake.
    kwa kweli huwa najisikia kutapika nikisikia watu wanautukuza ukabila. ilitakiwa iwe aibu hata kuutaja.

    hakuna kabila bora hapa tanzania, yote ni 120 ni bora.
    by mwitongo masanduge.

    ReplyDelete
  32. Hamna kabila bora kuliko yote duniani! Nafkiri kila mwanadamu anaubora nakila kabila lina ubora!
    Tatizo kuna makabila makubwa yanayojiona kwamba wamesoma na wanauwezo kuliko kabila lolote tanzania! Ambapo wenyewe katika makabila yao wanazidiana kwa vijiji na kudharauliana na ninafkiri tabia ya watu si kwakabila zima. Kabila yanayojiona sana nawanadharau sana vikabila vidogovidogo. Mfano nambari one ni no. (01) WAHAYA (02)WACHAGA (03) WASUKUMA (04) WAPARE (05) WANYAKYUSA. Haya makabila ndio wanajiona bora zaidi kuliko wote hapa Tanzania nzima. Wakifatiwa na WAKURYA ni kabila dogo lakini tatizo linakuja juu sana wakorofi na wamesoma hawavumi lakini wapo wao ngumi mkononi. Ila Wahaya na wachaga ni matatizo wengi tabia ya kuwa Mrushi na Mwizi, Taperi wa kutumia nguvu lakini Wahaya ni Mataperi wakutumia Elimu yake na waongo kuanzia kazi mpaka mapenzi na wanapenda sana kesi na ndio maana wahaya wengi ni maloywer, Wasukuma jeuri tu ya hela lakini ujanja hawana na wanajua kutafuta tu nawanapenda utwana kusifiwa kutukuzwa na kuabudiwa ila wako weak sana kwenye mapenzi.

    ReplyDelete
  33. Washambaa, because ushoto is like swedeni, tina matunda ya kizunga, hali ya hewa ni nzui sana savai ni baffalo NY.
    So washambaa nkiboko

    ReplyDelete
  34. Michuzi unalete ukabila sasa, kumbuka maneno ya Hayati Baba wa Taifa unauliza Kabila unataka kufanya Tambiko? Ubora wa Kabila utaupimaje? kwa kipi maendeleo, Culture, elimu, mashauzi or? i don get the logic kaka hapa.
    Binafsi mi Mndamba we are the Best... sasa ulitaka nikwambie we Mwela ndio Bora alaaaa!!!

    ReplyDelete
  35. Karibu "DEMOKRASIA", Sasa kaka Michu umeleta ukabila ndanbi ya haka ka blogi ketu.. Yap!! yatachangwa mawazo na mengi yatazungumzwa, uwe na moyo mkubwa kam autaguswa ama ataguswa (mai waifu wako)!!! Itategmea na mguso wenyewe idadi ya jazba utakayo kuwa nayo.. Yote Kheri... "Na mkianza mambo ya ukabila bai mtamalizana na hakuna atakeyepona..." Mwl J.K Nyerere". Karibu "DEMOKRASIA"... (aKd)

    ReplyDelete
  36. WAZARAMO ! Nyerere alikuta mkoa wa Pwani na maendeleo yake. Akautenganisha na kuunda mkoa mdogo wa Dar . Kisha ukasahau kabisa maendeleo ya eneo hili,

    Utashangaa lami mpaka dodoma au mbeya , lakini alishindwa kujenga hata barabara ya kufika pugu .

    Wazaramo ni wakarimu sana, pamoja na umaskini wao lakini si masikini kuliko wakabila yote.

    Si ajabu ukakuta hata Mmasai anatania wazaramo kuwa hawana maendeleo, wakati watu wa bara wamejazana ktk ardhi ya wazaramo.

    KAMA KWENU KUMEENDELEA MNGEBAKI MAPORINI KWENU TOKA ENZI HIZOO ZA NYERERE, UMEZALIWA DAR KISHA UNATAFUTA CHA KUSEMA . KWENU HATA LIKIZO HUENDI .

    Wenyeji wa Dar na pwani wangekuwa Wahaya ua Wachagga, mngetia akili na kunielewa kirahisi .

    ReplyDelete
  37. kabila bora bongo kuliko yote ni wahaya. kwanza wamesona alfu wana pesa na wapenda maendeleo.

    wangambila stupidi mbele ya maiwaifu.

    ReplyDelete
  38. Hili swali lina lengo la kuturudisha kwenye ukabila ambao tunaupinga kwa nguvu zote hapa Bongo. Kifupi ni kwamba kila kabila lina mila na desturi zake ambazo zinaweza kuonekana mbaya au mzuri kulingana na mazingira ya kabila husika.Hivyo basi hakuna kabila bora zaidi ya lingine kwani kabila linaundwa na watu na mbele ya mungu binadamu wote ni sawa.

    ReplyDelete
  39. HAYA TRIBE

    KAMA MNAVYOJUA EDUCATION NI MUHIMU MAISHANI NA NDIO MAANA BADO NYIE MNASOMA HILI AU LILE.

    MNATANIA WAHAYA NSHOMILE THAT IS VERY COOL ENDELEENI

    NUMBER ONE WAMESOMA TOKA ENZI ZILEEEEEEEEEEEE

    PILI WANAWAKE WA KIHAYA WANANATURAL JUJU MWILINI MNAJUA NASEMAJE

    TATU NDIO WANARINGA WANAJISIKIA ILA WANAFANYA KAZI KUBWA KUJIWEKA KATIKA LEVEL YA KUINGIZA PESA NA WANAFURAHIA MATUNDA YAO

    NNE NDIO U BISHOW UPO HIYO IPO KWENYE DAMU

    KUMBUKENI BUKOBA NI WENYEJI WA UGANDA AS LUGHA, MAJINA MENGI NI SAWA NA HUKO SW UGANDA HIVYO ASILI YA WAHAYA NI WAGANDA

    NI NYERERE ALIYELILIA BUKOBA ALIJUA WATU WA BUKOBA WATASAIDIA KUENDELEZA TANZANIA,I ZA UKOLONI ETC ALIONA WASOMI TANGU ENZNA NDIO AKANG'ANG'ANIA IWE PART YA TANZANIA


    MMMHHH ILA WENGI NYIE MNAPENDA TRADITION YA KIHAYA SEND-OFF PARTIES, HARUSI HUWA MNATAMANI

    SAIDA KALORI MIZIKI YAKE INAWAPA UTAMU HASWA

    HAYA FOREVER

    ReplyDelete
  40. Habari Gani wadau wote humu. Issa Michuzi mie ni mchaga ila naweza kuwasifia Wazaramo japokuwa watu wanasema hawajasoma kusoma sio ndio kuwa na tabia ya roho nzuri, Wazaramo wengi wanatabia nzuri japo wanawake wao ni wambeya na mdomo mwingi Mfano mzuri bila Mangara kwanza ningependa michuzi ungewafahamisha Mangara ni nani< Mangara ndiye aliyemkaribisha bakharesa na kumpa utajiri na Mangara huyohuyo ndio waliokaa wakamwambia nyerere wewe utaongoza nchi Mangara nikatika wazee wa kwanza Dar-es-salaam kuwakaribisha wengine bila chuki na kuwapa maendeleo tizama kina mwinyi na kikwete ni wazaramo ambao hawana chuki wameweza kukaa na makabila bila kujidai bagamoyo-kisarawe-na dar-es-salaam kama ni yao si kama mikoa mengine makabila wanavyoringa nayo jengine wa pemba wanasaidiaana wenyewe watu wa unguja hawajasoma ni wangazija tu unguja ndio wamesoma na niwatu wa comoro na pemba sio wapemba ni watu gani sababu huwezi kusema sie wa moshi ni wachaga. Wachaga hatukusoma sema tunaendeleza nchi Ahsanteni sana Wazaramo kwa kutukaribisha bila chuki na nyie mnakaribishwa kwetu moshi. Wahaya wacheni chuki plzzzzzzzzzzzzzz.

    ReplyDelete
  41. WAZARAMO NA WANDENGEREKO BYFAR ! Ukiamua unaweza kucheka umasikini uliopa Buguruni au chanika, but trust me thats not the worst picture of Tanzania.
    Ukienda Maporini maisha hayaelewiki kabisaa, ila watu wakifika Dar wanajisahau

    ReplyDelete
  42. Kabila bora kabisa ni WAZANZIBARI sababu kubwa ni kwamba ustaarabu ndipo ulipoanzia katika afrika mashariki hii.

    ReplyDelete
  43. Yaani Kaka Misupu Nikama Unapigia Jibu Mstari... WASAMBAA yaani Haina Ubishi

    ReplyDelete
  44. Hujasema bora kielimu au utajiri . Lakini kitu muhimu katika jamii ni upendo na amani .

    Nawapakura Wazaramo na Wandengereko linapokuja suala la ukarimu na upendo , hat ucheshi .

    Ni bora uwe kati ya wazaramo 1,000,000 hautajisikia tofauti na wao. Jaribu kukaaa na Wahaya kumi tu, uone walivyo maprimitive. wataongea kilugha bila kujali hauelewi , majigambo mengi, etc .

    Makabila mengi yanatabia ya kubaguana hata kwa wilaya unayotoka , Uzaramoni hatuna shida hiyo .
    Viwanja vyetu tunaweka mpaka kwa miti tu ya asili. NGOJA AAMIE JIRANI MCHAGGA , KILA SIKU ANASOGEZA MPAKA KUIBA ARDHI YAKO .

    ReplyDelete
  45. wa bena bora !!!! kamwene

    ReplyDelete
  46. Wewe umechanganyikiwa na akili hapa duniani hakuna kabila bora au mtu bora kuliko mwingine.Makabila yote ni sawa.Kama unaona tofauti katika makabila basi wewe ni mbaguzi wa rangi kaa chonjo KICHWA YAKO INAHITAJI MSAADA WA DAKTARI WA MHIMBILI

    ReplyDelete
  47. mithupuu u have started ehhh?
    ngoja waosha vinywa waamkee?waanze kutapikaa mwenyewee utatoa .hiyo ukabilaa siunawajuaaa.......

    ReplyDelete
  48. Acha mambo ya kujadili Makabila kwani tuko RWanda hapa Tanzania tuko watanzania unaulizia makabila unataka kutambika? kutokuwa na amani kunaanzaga hivihivi kiuzembe mambo mengine sio ya kuweka kwenye public kunaleta uadui unapandikiza mbegu ya ukabila kiutaniutani bila kufikiri kwa kina. ndio maana media inaweza ikaleta conflict kwenye jamii kama itapanda mbegu
    kama hizi naomba tuache mambo ya kabila mwisho utauliza dini please tunapenda utulivu.
    Unaweza kupata watakaochangia hawakosekani lakini haijengi ila inabomoa.

    ReplyDelete
  49. I THINK THIS QUESTION PROMOTES UKABILA. NO HUMAN BEING IS BETTER THAN ANOTHER, THE SAME APPLIES TO TRIBES, RACES, ETC.

    ReplyDelete
  50. Mi naona Wabena ndo bora!

    ReplyDelete
  51. Wewe Michuzi kama mwandishi wa habari, hili swali lako ni kijinga. Watu wameuwana huko Rwanda kwa ajili ya mambo kama haya. HAKUNA KABILA BORA. WEWE HUKUMWOMBA MUNGU UZALIWE MMATUMBI. NI UMEJIKUTA TU. KWA HIYO USIANZE KULETA MASWALI AMBAYO HANA KICHWA WALA MIGUU ILA KUCHOCHEA UKABILA. ANGALIA HAPO KENYA JIRANI ZETU WAMEENDEKEZA MAMBO YA UKABILA SASA INAWATAFUNA WENYEWE. HAKUNA KABILA BORA WOTE SISI NI WATANZANIA. NDIO MAANA UNAPOMUULIZA MTU WEWE KABILA GANI HAONI HAJA YA KUKUJIBU NI UPUUZI MTUPU. MIMI MTANZANIA UNATAKA NINI ZAIDI? MWALIMU ALISEMA "DHAMBI YA UKABILA HAISHII HAPO TU, UTAANZA WEWE UNA KICHWA KIKUBWA, WEWE MZENJI WEWE MBARA" ACHA HIZO MICHUZI KUWA KAMA UMEENDA SHULE.

    ReplyDelete
  52. Hivi nyie mnaosema kila kitu NYERERE alisema mna akili kweli???Nyerere Nyerere?Mbona aliponda wanawake na sasa mwanamke ni katibu wa UN??????

    Kabila bora ni WAJITA.Sababu wamekaa kimya muda wote na sasa wamesema na kufunga mjadala hapa kijijini.Na utashangaa watakaoendelea chini yangu wataanza kujenga hoja juu ya mjita huyu.Ndo ubora wenyewe huo.

    ReplyDelete
  53. Kweli michu kuna mdau kasema ngoja waosha vinywa WAAMKE, nadhani anamaanisha waosha vinywa wale wazamiaji kwenye nchi za watu,akimaanisha wabeba maboksi wa amerika na kwingineko ambao sasa hivi wamelala, wale walishaukana utanzania achilia mbali utamaduni, MICHU wamelala ila wakiamka haoooo!sheshe lao kubwa maana wao si ndo huwa wana mijicomputa wakiwa wanapumzika baada ya mijiboksi!TUSUBIRI WAAMKE UTAONA WATAKAVYOKURUPUKA NA HII COMENT YANGU,HAOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!nasikia wengine huwa wanakana ni waafrika, zao ni watsup kwa kwenda mbele, usiwaambie ni mimi nimesema maana duh!wamelala!maboxi boyz and maboks gals, wakiamka hao!heee!

    ReplyDelete
  54. BRO MICHUZI NAONA SASA UNATAKA KUTUGAWA.

    MAKABILA YOTE BONGO POA-KWANI HATUNYIMANI NA TUNACHANGAMANA BILA KUJALI KABILA.

    ReplyDelete
  55. Mambo yote wazaramo. Ukimkuta babu anauza nazi ukataka kuzinunua zote, anakwambia mie zikiisha asubuhi subuhi hii ntafanya kazi gani nyingine, na wenzio watakula nini? Wanawake ili kuonekana familia zao wanakula wali kila siku wanatoka nje na mchele wanapepeta then ndani akirudi anapika ugali. Ule mchele ni wa shoo tuu. Akienda kucheza ngoma basi huyo si wako hata kama ni mkeo, mwache aone sampuli mpya mpya, nawe ruksa mtoto akichzwa jitambulishe waweza chukua. Wanamwaga radhi hadharani. Shughuli huwa pevu pia. Mh, wazaramo is the best,,, hata kazi hawataki, mwanamke ndani asitoke nje awive. Mh siendelei, WAZARAMO nawavulia kofia ingawa mie msukuma-chapa ng'ombe

    ReplyDelete
  56. THE IS ON DEBATE ABOUT THIS,THE BEST TRIBE IN TZ IS HAYAZ,BECAUSE ALL OUR PEOPLE ARE EDUCATED AND WE LEAD WHILE OTHERS FOLLOWS.
    FROM MUSHUMBUSI.

    ReplyDelete
  57. KABILA ZURI NI WAMAKONDE WA KIKE,, WANAKATA KIUNO JAMANI AIII!!!

    ReplyDelete
  58. Kabila bora kuliko lote ni la mafisadi.

    ReplyDelete
  59. Nyerere hakuponda wanawake! Alikuwa mwanasiasa wa kwanza kutambua na kutaka kutokomeza msemo kwamba wakati wa ukoloni mwanamke alikuwa ametawaliwa kwa namna mbili: mkoloni na mwanamme!

    Hatukuwa na mwanamke wakati huo wa kuweza kupata kazi ya UN! Lakini tulikuwa na wakina Bibi Titi na Lucy lameck, na wengineo!

    ReplyDelete
  60. Kabira bora ni WAHAYA

    ReplyDelete
  61. Kabira bora kuliko yote ni wahaya nawakilisha

    ReplyDelete
  62. Big up MIchu. Wacha ningee kikwetu watasema ndio walewale waliokana nyumbani, wengine washatuita waosha vinywa. Michuzi this is da topic big up maaaaaaaaaaaan!! Nafurahi coz umewachangamsha wadau kwa topic hii, pamoja na kuwa inainyesha wengine wamechukia na badla yake wanasema usilete ukabila. this is just a topic guyz u have to get it dat way, u feel w'at i'm sayin'? Tukisema sisi ni watanzania haielezei utamaduni wetu halisi ukitaka kueleza utamaduni wa mtu mmoja mmoja inabidi uelezee kabila lako, hilo ndio chimbuko lako na ndio utamaduni wako ulipo. ambao mnachukia sijui mmetoka kwenye makabila gani, inaelekea hamtaki hata kuyataja makabila yenu. Hii topic haimaanishi kumtenga mtu wala kuendeleza ukabila ni muhimu tukumbuke asili na utamaduni wetu. hakuna utamaduni wa mtanzania kuna utamaduni wa makabila ya watanzania, na ndio maana hata vikundi mbalimbali vinavyojaribu kuendeleza utamaduni vinaeleza kuwa hii ni ngoma ya kabila fulani hawasemi hii ni ngoma ya watanzania. Nyie mnaopinga kuzungumzia makabila mnakataa utamaduni wenu. Nikiendelea kuelezea makabila na kuchagua lipi bora itanichukua muda mrefu sana nafahamu kiundani utamaduni wa makabila 50 na hayo mengine nayafahamu kidogo, katika hayo ninayoyafahamu naweza kusema WAPARE ndio kabila bora kwasababu moja kubwa nayo ni, hilo ndio kabila nililotoka. PAUL. from USA.

    ReplyDelete
  63. Brotha Michuzi, mimi ni mchagga na niko masomoni Marekani. Ninajivunia uchagga wangu lakini kama mkristo siwezi hata siku moja kujiona kwamba mimi ni bora zaidi ya binadamu wenzangu eti kwa sababu mimi ni mchagga. Hii ni kinyume kabisa na maadili na mafundisho ya Kristo. Jamani tuthamini utu wa kila mtu.

    ReplyDelete
  64. KUMBE SASA UMEELEWEKA - WEWE MICHUZI NI MBAGUZI WA HALI YA JUU...SWALI JINGINE UTAKALOOULIZA NI DINI GANI BORA...HALAFU UNAJIITA MWANDISHI WA HABARI?

    BOYCOTT MICHUZI JAMA..WE ARE BETTER THAN THAT...

    THIS GUY HAS A DIFFERENT AGENDA - MICHUZI HAMIA UARABUNI UKATETEE UKABILA WAKO NA UDINI WAKO...

    ReplyDelete
  65. MIMI NAONA WALUGULU,WAPOGOLO NA WANDAMBA

    ReplyDelete
  66. wamasai bwana hua mimi nikishuka tu hivi airport lazima uone picha zao,siku moja nilimuliza dada mwenye gift shop kia,hivi masai mnawalipa mirahaba(Royalties)kwa kutangaza biashara zenu?Akiniambia wamasai ni national pride ni kama twiga,tembo au mlima kilimanjaro,sasa kwenu wadau hawa watu sio muhimu kweli?

    ReplyDelete
  67. Ofcourse its Wabena followed by Wakimbu...

    ReplyDelete
  68. Kaka Michuzi sina nia ya kukutusi, lakini nahisi ukiwa kama mmiliki wablog hii, ulitakiwa usiweke katika blog yako mada kama hii, ambayo kwa kiasi fulani inachochea ukabila na kuleta tofauti miongoni mwa watanzania ambao kwa muda mrefu tumekuwa tukivumilia bila kujihisi mmoja anamzidi mwenzake kwa kabila, dini, koo au alikotoka.Lakini napenda kuchukua fursa hii kumjibu dada Rose na wengine ambao kuhusiana na suala hili wamekuwa wakiwafagilia wachaga au wanakotoka wachaga kwa dalili hii na ile. Nikiwa nimezaliwa mkoani Kilimajaro na kukuliwa huko, namshukuru Mungu kwa kutokuwa mchaga kwani tofauti na wachaga wanavyoonekana nje ya mji wao kuwa ni watu wanaojali maendeleo, wamesoma na ni kabila bora lakini wana utamaduni fulani hivi ambao siwezi kukubalia kuwa kabila hilo limewazidi wengine. Chunguzeni mtajua kuwa wachaga wengi wanaume hawajali wake zao..au wanamdhalilisha mwanamke...mume kwa kutoka kwenda kutafuta maisha mikoa mingine( kama mnavyodai wamejaa kila mahali) huiacha familia yake ambayo mama huwa ndo anahangaika kuwalisha watoto kwa kutegemea ndizi atakazozilima na kuuza kila siku akitoka milimami (mnakodai kuna mavila wakati ni vibanda!)na mpaka mwezi wa disemba kwa msululu wa magari hurejea kula krismass(nyumbani) kunakofuatana na kumwachia mkewe mimba nyingine na kumwacha tena! Nani kasema kuwa wachaga hawajali ngono!Takwimu zinaonyesha karibu asilimia kubwa ya wanawake wa mkoani kilimanjaro wameambukizwa ukimwi na waume zao! ambao wamekuwa wakihangaika kukimbiza shilingi huko na huko pote Tanzania wakiwa pekee bila wakezo...nimezaliwa na kuishi Moshi lakini sijawahi kushuhudia kila baada ya nyumba sita eti kuna shule! kwa moshi mjini pekee kuna shule za msingi zisizozidi ishirini! wachaga wanasifika kwa roho mbaya na ujambazi..(moshi kuchomana visu ni mchezo wa kawaida kwa vijana)...wako tayari kufanya shughuli yoyote hata ya...(tumezee) ili kujipatia pesa.Halikadhalika wanasifika kwa kupenda kutumia nguvu wachilia mbali kupiga wake zao na watoto. Kwa hiyo wadau tabia ya kufagilia makabila fulani bila kujua undani wake tuache..tudumishe utaifa..sote ni watanzania na hilo ndo muhimu..tuvumiliane na tuzingatie kujenga taifa na kujikwamua kutokakatika hali ngumu ya maisha inayotukabili wote..Adios.

    ReplyDelete
  69. Bwana Michuzi, kwa maoni yangu Tanzania hatuna kabila bora kuliko nyingine. Mimi ni Mmasai and I'm proud, siogopi wala sifichi kabila langu. Lakini, nikikutana na Mtanzania sijali wala sifkirii kuuliza kabila lake as long as ni Mtanzania inatosha.

    ReplyDelete
  70. MBONA MANATUTHAHAU NA THITHI JAMANI? NI KINI ICHO? THITHI NDIO BABA DHAO, VUGHAI NA PICHA YA THAMAKI.

    ReplyDelete
  71. mmhhh mzee michu umetafuta balaa la watu kukashifiana tu hamna lolote imehusu nini watu kutajiana kazi zao ,wanabeeba box,wanafanya nini,makhusat,haina haja
    mie naona ufunge tu mjadala wako

    thanx

    ReplyDelete
  72. Nimeshangaa sana watu wanataja kabila linaitwa wachaga. liko wapi hilo? Hakuna kabila la wachaga, bali kuna warombo, wamarangu, wauru, wakibosho, wamachame, wambokomu, nk, na wote wanadharauliana kinyesi! Huo ndio ubora wa kabila? Hebu acheni ujinga huu. Kabila bora ni utanzania, basi!

    ReplyDelete
  73. We Mshombe,
    Vaasu avae nivo ikabila ledi kukela ose..nywi va nyika tumutudima..swi tuvabigie vamasai mpaka vakavona vaahe vaekaa na simba uko he nyika. Iki we uete ukabila aha ni vintu ani ivyo weete wenetuetia Nkondo sa ila ya Iraki yakwe Bush. Kangi ushige kabisaaaa uo mchezo..munzo wetu ni mwe du...Shetani na valao vakwe...!! kakicha tutonga mtaso ombe shauri yako..ambu uneshotwa we....!! Uneshotwa musi wa mwisho..!! Umanje kula vuasu tula sambia na matunda sa he ivunde nicho neti ikabila ledi kukela ose ni la vampare...!! Chakuhera rae hata we...!! Swi twekina MSUYA, YONA, MGONJA na kula Suji MKAPA ekweiye akavona iti kweri vaasu ni vantu si va kawaida...!! Vaasu Vampare avae...!! Mwatuteta iti tula vughai na picha ya samaki..mira kwa ukweri ni keba kukela vala vela vughai na harufu ya viratu...!! nyaaaaaa naherwa..!!
    Kaka Michuzi..unataka translation..tafuta Mpare...Kabila bora ni la Wapare...!!
    MDAU WA USA-CALIFORNIA..!!

    ReplyDelete
  74. KUNA KABILA MOJA MATATA SANA TOKA MBEYA INAITWA WAMALILA.

    AISEE HAWA JAMAA NI KIBOKO NA JAPO HAWASIKIKI SANA (KWA SABABU YAKUTOPENDA MIUJIKO ISIYO NA KICHWA WALA MKIA) MAMBO YAO NI MAKUBWA

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nimeona hapa.wamalila ni kiboko hawana hata uroho'upendeleo'bwana we! Umepatia.

      Delete
  75. MICHUZI ANATUMIWA NA CCM KUTU-DISTRACT NA HAYA MAMBO YA BLOG YAKE KICHAA HII TUJI-KEEP BUSY KUMBE WAO WANACHOTA..MICHUZI NI SHUSHUSHU..MSIDANGANYWE NA MTU..ANATUMIWA KABISAAA...UTAONA HATA ANAWEZA KUI-BLOCK HII POST KWAVILE NIMEMPA VIDONGE VYAKE..HA HA HA...!! UNATUMIWA MICHUZI...MASOUP...!

    ReplyDelete
  76. Baba yangu ni Mjita. Mama yangu ni mchanganyiko wa baba Mnyakyusa na mama Mzaramo.

    Mimi ni wa kabila la Mjita-Mnyakyusa-Mzaramo!

    Na kabila hili ndilo bora sana. Kwani limeua ukabila!

    ReplyDelete
  77. Aroo michuzi unarara hapo hapo?unafanya na makurufundi unafikiri ni shimo ra panya?.....kaeni hapo for tanzania hakuna kabila lililo zaidi si wote ni watanzania ok?

    ReplyDelete
  78. Michuzi mimi ni half cast wa kitanzania manake mimi baba half mchagga half mpare. Mama yangu half mnyamwezi na half kutoka kwa wakwe zako. Nimekua na nimejifunza mila na desturi zote za makabila haya lakini kabila ni lugha tu hamna cha zaidi sikuhizi ukiangalia mila na desturi zote siku hizi ni westernized.

    Mimi naona swali lako ungeuliza Kabila ambalo liko popular. Hata mtu ukitaja hamna anayeuliza hao ni watu wa wapi. Mambo ya kabila bora hapa at this day and age naona yamepitwa na wakati katika nchi yetu. Haya mambo ya utani wa jadi yapo lakini hayarepresent the whole society.
    Wanavyosema Mangi waizi, au wafanya biashara je ni wote? No ....wanavyosema wazaramo wavivu na hawataki shule je ni wote? No...kwa hiyo utu ni bora kuliko kabila....

    ReplyDelete
  79. Hili swali la kijinga kuliko yote ambalo nimeshawahi kusikia maishani mwangu ....2007 watu wanafikiria jinsi gani ya kuendelea as a nation wewe unaturudisha kwenye mambo ya ukabila , Shame on you Michuzi.

    ReplyDelete
  80. ANONY WA UETHIEI CALIFONIA NAKUPATA AVAE, KIMBARE CHAKO NI CHA HATARI!MMH THEKIMANJE ITI HENA VAATHU MHAKA UKO HAKWE BUSH.MIRA MAPAKA KISHUKURI NA MAGHIMBI UKO?MAPERE?VAATHU HOYEEEEEEEEEEEEEE!!!!VAATHU BOMBAAAAAAAAAAAAAA!!

    ReplyDelete
  81. Kwa mtazamo wangu kabila bora ni Tanzania,kila Inchi zinatuonea wivu kwani wanalijua ubora wake uko wapi,hata hivyo Baba wa taifa alilitambua.

    ReplyDelete
  82. Asiwadanganye mtu...kabila bomba ni la Watalii (WAMAKONDE). Tofauti na watu wanavyodhania kuwa wamakonde hawajasoma, hii ni kasumba tu. Wamakonde bwana wamesoma, kisha ni watafutaji sana na huwa hawafanyi biashara za kijinga kama wachagga. Mchagga atauza duka hata kama anapata faida ya shillingi 1 yeye anaona bora liende tu, kisa ana duka na kwao watamuheshimu. Kingine, watalii hawana majivuno, na hawana ukabila. Wao wakishajua tu umetoka sehemu nyingime basi wataongea nawe kiswahili mpaka kwisha. Japo mi ni mrangi lakini tuache utani nimekaa MT, Kilimanjaro, Arusha na Dodoma, sijawahi kuona watu wanaojituma kama watalii. Hongera watalii!

    ReplyDelete
  83. Ehee!!! Nilijua tu Nyerere amefariki hata mwongo mmoja haujaisha mwaanza kuongelea UKABILA.Haya nyie leteni za kuleta.Lakini hata hivyo ni swali zuri la kupema uwezo wa kufikiria na kupambanua wa watu.
    Mimi kwa kuanza ningejibu kutokana na kwamba,Kabila ni jamii inayotambulikana kwa -identity ya lugha moja kama ndivyo basi

    Kiutamaduni(Culture)
    Je ni kabila gani linaziheshimu Culture zake na kuziendeleza -nadhani kwa Tanzania inawezekana Wamasai,ingawaje kuna jamii ya wengine ambao na amini hata asilimia kubwa ya watamzania hawawafahamu:Watindiga,wahdzabe,wamang'ati na wababarbaigi.

    Vilevile ukifuatilia kigezo ch utandawazi -Globolisation amabao ni mchanganyiko wauchumi,elimu,teknolojia na vigezo vinginevyo.
    Hapa unaweza kuja na makabila kama Wahaya,wachaga,wantakyusa na Wapare,ingawaje kufanikiwa kwao kunachangiwa na historia na jiografia ya kimazingira iliyowavutia wamissionari kuwekeza maeneo yao.

    Kati ya hao ni nai anaweza kuishi na mwenzake vizuri,maana ubara ni kuweza kuwa na maisha yenyekuelewana na jamii nyingine isiyo yako tu.Utaona kwa kigezo hicho utawapunguza wengine.


    Mwisho Ubora nadhani unavigezo vyake ingawaje kwa wengi hutanguliza uwezo wa kielimu,uchumi,miundombinu ya majengo nk kutokana na nadharia ya kibepari na Ukoloni mqamboleo.

    Nadhani kabila Bora kuliko lote NiBLOG YA MICHUZI,haina,sera za kidini,kirangi,kikabila,kiutaifa,

    ReplyDelete
  84. .......WASUKUMAAAAA!!! NO DOUBT...

    ReplyDelete
  85. all tribes are great!!! but but but I'M MCHAGA, MACHAME AND IAM PROUD

    ReplyDelete
  86. Bro.Michuzi narudia tena kusema hakuna kabila bora au zuri kushinda lingine nchini TZ. Ningependa utupe orodha ya makabila yote hapa bongo, kwani wachangiaji wote hapo juu ukiwauliza wayataje makabila yaliyoko nchini mwao TZ hawawezi hata kutaja makabila zaidi ya kumi.Anyway kwa ujumla makabila bora kabisa ni: Wamasai, wazanaki, Wairaq, Wamang'ati, wahadzabe, wafyomi, watindiga, wagogo, wamakonde, wandorobo,wakwere,wameru,waluguru, wasambaa,wadigo, wahehe,wasukuma, wachaga,warangi,wazaramo, wakurya.
    Wengine ni wandengereko, wamanyema, wamakua,warangi, na wengine wanafuata. Utataka nimalizie mengine nitafanya hivyo later. Kwa mpangilio huo hayo ndiyo makabila bora.

    ReplyDelete
  87. MICHU WALUGURU NDIO MWISHO WA MATATIZO YOTE DUANIANI HAPA!!! HIVI ULIWAZA NINI MITHUPU NA WEWE UMEISHIWA SERA NINI??!!!!!!!

    ReplyDelete
  88. TENA MKOME KABISA.MSHINDWE NA MLEGEE.KABILA BORA ZA TANZANIA ZIPO
    KANDA YA KATI.DOM,SGD NA TABORA KIASI
    MADEMU WAO WEUPEEE,WANAJUA KUKATIKA
    HAO.WE ACHA TU.KAOE URANGINI,UNYIRAMBANI AU UNYATURUNI
    MAMA MKWE HUMUONI BWANA.WATOTO WANA
    NGOZI NYORORO,NO CHUNUSI WAPO NATURALLY.EBO MKOME NA MSHINDWE WOTE
    MSIOKUBALI MAKABILA HAYA.
    KAKA MICHU UNATUCHOKOZA WAOSHA VINYWA EEE? HALAFU TUAMBIE HELA ZILE BILIONI 10 ZA BOT NANI ALIIBA
    USIBADILI TOPIK HAPA.ACHA KUTUZUGA
    INGAWA NAJUA KYAMA KYA MAPINDOZI
    WANAKUPA MSHIKO PIA.KILA LA HERI

    ReplyDelete
  89. Jamani msihangaike kabila boraa sana ni wayao..haswa wanawake wao kwa "chidimba"" duuh..weee acha tuu

    ReplyDelete
  90. I am proud to be Tanzanian where at least I know I am free. ......weeeeeweeeeeeee........And I won't forget the men who made it TAMBARARE for us..........Cause there ain't no doubt I love this land God Bless Tanzania........hoyeeeeeeeee

    Honesty, I am proud of who I am and I carry my flag up high....I never see a tribal flag before so Michuzi you better just keep your thoughts by yourself sometimes. This is not a good debate question at this time....tomorrow we might wake up and found you ask what is the best religion here....so sometimes keep it tight

    ReplyDelete
  91. Well well well anony 9.08EAT ni half cast jamani jamani this keeps getting better...... sio vibaya kugusa raw nerve za watanzania....... michuzi leta oja nyingine kama hii na lile kabila la mabox limeamka......

    ReplyDelete
  92. The Chagga tribe originated from the Kilimanjaro region, numbering about 900,000 worldwide. They are famous for their adaptability. They were one of the first tribes in the area to become converted to Christianity. Some would say that it gave them access to education and health care.
    They are known as the Jews of Tanzania as many are wealthy, have good businesses, and are in Government. Many have become well educated and now live away from Kilimanjaro but have built their "retirement" home on the mountain. Many would say that the biggest income for Tanzania is the money sent in from abroad by Chaggas who have gained good jobs and honour the family tradition by looking after the "clan". They are wonderful business people. They are also very friendly and welcoming. Their villages around Kilimanjaro are very large because each family have a plot of land called their Shamba. There are no streets of houses as in Europe. Walking around Njaro is like walking though a farm of banana trees and coffee along dirt tracks. The Chagga are wonderful farmers. They can grow five crops together on their shambas. Coffee, bananas, yams, beans and tomatoes. The Chagga are also famous for their "traditional brew" called Mbege. It is made from a special variety of bananas and millet. You will see people drink mbege in all the bars by sharing a calabash. You will be able to visit an Mbege bar in Njaro and watch it being made

    ReplyDelete
  93. WASUKUMA.


    Na Mjadala umefungwa.

    ReplyDelete
  94. SENKYU FERI MACHI BRAZA MICHUSI FOR THIS TOPIC MAN! ACHANA NA HAO WANAOPIGA KELELE ETI LA KIPUUZI, HII NI CHANGAMOTO TU YA KUJUA NANI MWENYE BUSARA YA KUONGEA AU KUJIBU SWALI LOLOTE LINALOKUJA GHAFLA, INABIDI UFIKIRIE NA UJIBU KWA UMAKINI NA SIO KUROPOKA TU NA KUTOA KASHFA! U KNOW WHAT AM SAYING? YEAH MAN HOPE U GOT ME YOO!!
    WACHAGGA NDO KABILA BORA KULIKO YOTE MANAKE WANA UPENDO NA UKARIMU BABA ANGU!! AISEE CHALII YANGU HAWA WAOSHA VINYWA WASIKUBABAISHE KABISA!! BIG UP MAN!! CHAGGA JUU!!!

    ReplyDelete
  95. Wote kwa pamoja pigeni makofi kwa kwa kwa kwaaa!!

    haya wote tena kwa pamoja pigeni vigelegele.. kilililililiiiiiiii!!!

    Wote tena kwa maoja semeni kwa sauti moja kwa furaha na shangwe na vigelegele.......
    WACHAGGA OYEEEEEEE...............OYEEEEEE!!!....
    WACHAGGA JUUUUU......JUUUUUU!!!....

    Aika mbe meku na Mai

    ReplyDelete
  96. MJADALA UNAFUNGWA KWA KUSEMA!!
    KABILA BORA KULIKO YOTE HAPA TANZANIA NI KABILA LA "WATANZANIA" HAKUNA KABILA LINGINE!!

    ASANTE KWA KUTUGOMBANISHA NA KUTUCHONGANISHA KIMAKABILA HUKU MTAANI NI NGUMI TU! WATU WANATUKANANA SAWA MICHUZI TUNASHUKURU LAKINI IPO SIKU TUTAKUTANA USO KWA USO. NDO UTAJUA KUWA KABILA BORA NI "UTANZANIA"

    "TANZANIA OYEEEEEEE"

    ReplyDelete
  97. KABILA BORA NI MTANZANIA
    ASANTE

    BWANA LYIMO TOKA MOSHI

    ReplyDelete
  98. watanzania ni bora kuliko wote

    ReplyDelete
  99. utu wa watanzania unadhihirisha ubora wao

    ReplyDelete
  100. jinsi nilivyozaliwa na wazazi waliochanganyika makabila kibao ya TZ na jinsi huko kwetu tulivyooa na mawifi na mashemeji wa kutoka kila eneo la Tanzania hawa watoto wetu hawana kabila kabisa kwani hawajui hata salam za kabila lolote ni tupo watoto 12 tumeoa na kuolewa sasa MICHuzi KABILA BORA NI MTANZANIA

    ReplyDelete
  101. ZE GOOD KABILA NI UTANZANIA

    ReplyDelete
  102. BAADA YA NDOA YA TANGANYIKA NA ZANZIBAR YULE MTOTO ALIYEZALIWA NDIO KABILA BORA

    NAOMBA MJADALA UFUNGIWE HAPA

    ReplyDelete
  103. Kablia bota ni "Utanzania"

    ReplyDelete
  104. Michuzi toa maksi kwa kabila zilizotajwa na litakalo shinda ndo bora
    funga mjadala

    ReplyDelete
  105. WAO NI WAZANIBARI NA SISI NI WAZANZIBARA:- Hahahaha bwana Michuzi sasa naona umeamua kwachanganya wana kijiji sasa na issue zako za ukabila,,, Tulisema kuhusu RICHA miss Tanzania na we ulikuwa namba moja kupinga issue ya ubaguzi sasa sijui unatuletea maada gani tena humu kwenye kijiji any way tutafika tu kaka lakini kwa namna moja au nyingine naungana na mtoa maoni hapo juu kuwa kabila bora kuliko lingine ni huu UTANZANIA NA AMANI TULIOBAHATIKA KUWA NAYO HAPA NCHINI.... OUT OF DHAT TUTARUDI KWA KINA RICHA ADHIA SASA HIVI KUWA WAO NI WAHINDI MABOHA MABUDHA NA NI BORA KULIKO WENGINE....

    Willy

    ReplyDelete
  106. HAPA BONGO SIJUI KAMA AKINA KABILA WAPO, NINAVYOJUA KABILA ALIONDOKA NA SASA NI RAIS KULE KONGO.
    NADHANI JOSEPH NI BORA KULIKO WENGINE

    ReplyDelete
  107. Habari za kwenu vijana!
    Mimi kwa mtazamo mwangu kabila bora ni maendeleo.Hao wanaosema wao ni wachaga na wameendelea ,sioni kitu ambacho wameendelea ,kuwa na villa na kutokua na nyumba za udongo sio sababu ya kuendelea.
    Mambo ya kuzungumza ni maendeleo na kuweza kuboresha huduma za jamii ili kila mtanzania ajue haki yake ni nini na sio longolongo za ,nani kabila gani.Hiyo haitotusaidia kimaendeleo na wala haitotufikisha mahali.
    Use ur common sense ,let me explain to u, wewe unaejidai kabila lako ni bora ,ulipenda kuzaliwa katika hilo kabila ama ulijikuta tu?Sasa nani kabila bora?
    Aidha to my knowledge ,hili sio swali la msingi ni swali la kijinga ambalo halina kichwa wala miguu.
    Na hao wanaosema wana mlima kilimanjaro kwani mlima kilimanjaro ndio nini?je na wale wenye mlima Everest nao ni kabila bora duniani?
    Sote tumeumba na Mungu ,mbora wetu ni yule mcha Mungu .Asanteni.

    ReplyDelete
  108. i'm of dual heritage origin...half haya and chaga in that order(hayachaga)...so the best tribe are...utanzania daima. love and peace thats all we need...

    ReplyDelete
  109. ebwana huku mashati yanachanika mtaani kwetu. ngumi za usoni nje nje.
    vidole machoni ile mbaya
    ..........................eddy

    ReplyDelete
  110. kwi kwi kwi kwi kwiiiiiiiii!!! etu mutu inakasirika kisa kabila!! Michuzi hajauliza ni uraia upi au utaifa upi bora kauliza kabila lipo bora, nyie mnakazana tu na utanzania, sijui nini, hakuna kabila linaloitwa maendeleo wala utanzania, labda hizo kabila ziko congo... kwi kwi kwi kwiiiii!!!
    WACHAGGA NDO BORA!!
    WACHAGGA OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!!!!!OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!!!!!
    kwi kwi kwi kwiiiiiiiiiiii!!!!!!!!

    ReplyDelete
  111. Halfcast wa kichaga na kinyasa tu ndo bora.Pesa na ngoma huku mtu katia tai shingoni.

    ReplyDelete
  112. Halfcast wa kitaliani na kibondei ndo bora.Vino kwa wingi na bada kwa mchunga halafu unasawazisha na mnazi kazi kwako!!!!!

    ReplyDelete
  113. Kabila la kitanzania ndo bora.Wote twaongea kiswahili.Nakubaliana na anony huko juu.

    ReplyDelete
  114. Na kweli chuzz kabila bora ni la kitanzania angalau hilo kachori za kidosi haziwahusu.

    ReplyDelete
  115. Ni thithi hapa ndio kabila bora ni thithi avaye.

    ReplyDelete
  116. Ingawaje hili swali linaonekana kuchochea ukabila, nafikri kwa namna fulani limesaidia kufahamu kuwa kuna watu wanaoendekeza ukabila, Tanzania ni nchi inayosifika kwa kutokuwa na ukabila. Kwa mtu kujivunia kwa kabila lake si vibaya bali ukabila ni sumu. Epuka ukabila.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...