SPIKA WA ZAMANI MH. PIUS MSEKWA (SHOTO, AKIONGESA NA SPIKA WA SASA MH. SAMWEL SITTA) AMETEULIWA KUWA MAKAMU MWENYEKITI WA CCM KATIKA MKUTANO MKUU WA CHAMA HICHO LEO HUKO CHIMWAGA, DODOMA, AKICHUKUA NAFASI YA MH. JOHN SAMWEL MALECELA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Ni yale yale. Hiyo ni kama mbio za kupokezana vijiti. Mafisadi waliokuwa wanakwenda kasi sasa wana-slow down wanawaachia waendao mwendo wa pole na mabingwa wa kupindisha sheria. Hapo tujiandae MSekwa akiwaombea dua wawasemao mafisadi na CCM, tunaanza eee mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, mungu wa upendo tunakiombea CCM na ufisadi wake kiweze kudumu madakani na kuwaacha wadanganyika wakiwa hoi amin.

    ReplyDelete
  2. hivi kuna tofauti gani kiumri kati ya Malecela na Msekwa?Malecela ana 73,Msekwa ana 72,lakini siku zote Malecela ndiyo anaitwa babu ndani ya CCM.Akigombea,wanamuondoa,tena mapeema!Hawamtaki kwa kisingizio cha uzee,lakini bado wanateua wazee haohao kuongoza chama.Hivi kunani Malecela?why anaogopwa kama njaa??Ilifikia kipindi mpaka Nyerere akataka kutoka CCM kisa Malecela kachukua fomu ya kugombea urais,kwanini hata Nyerere alikuwa anamuhofia sana Malecela na si vingunge wengine wa siku zile kama kina Msuya,Msekwa mwenyewe,Bomani etc????serikali 3,au???Haya tusubiri tuone kama ameridhika safari hii!
    Uteuzi huu Kikwete kakosea step,hawezi kuua makundi.Ona kwa mfano-Sitta ni mtandao,na ndiyo huohuo mtandao ulimwangusha Msekwa kwenye uchaguzi wa u spika.Sasa Msekwa na mtandao unafikiri itakuwaje?
    Kwa maana nyingine Kikwete kajimaliza mwenyewe!!!
    Usibane michu...
    LaLu

    ReplyDelete
  3. Hii,jamaa wewe sa inatuhusu nini? Hao jamaa hawana jipya wameshashindwa kuongoza nchi wamegeuka wao wachuuzi,wawekezaji, kero tupu ahadi hewa tu zimejaa. Usituwekee ishu hizo mbona list of shame hukuweka? Acha unazi au unataka ukuu wa wilaya na wewe?

    ReplyDelete
  4. Kitendo cha Kikwete kumteua Msekwa ni uamuzi mzuri.Naona sasa Kikwete ameamua kuvunja makundi ndani ya chama na mtandao kwa vitendo kwa kumchagua huyu mwenye uwezo mkubwa lakini aliyekuwa nje ya mtandao kwenye nafasi nyeti.Hongera.Ni afya kwa chama na serikali.

    Ni vizuri Raisi aendelee kuchagua watu kutokana uwezo wao badala ya kuangalia nani alimshangilia sana au kumzomea sana kwenye kampeni ya uraisi.Aangalie tu uwezo aachane na nani alifanya nini kizuri au kibaya kwenye kampeni.Mambo ya kampeni ni upepo upitao waweza kuja na mavumbi na takataka usoni lakini ukishapita ni vizuri kuachana na habari zake na kuendelea na business as usual.

    Kwa kumteua Msekwa mimi mheshimiwa Koloboi nampa hongera sana tena sana tu Raisi Kikwete.

    Nami namwahidi kuwa akifanya vizuri nitaendelea kumpongeza na akifanya vibaya nitaendelea kumzomea.

    koloboi@yahoo.com

    ReplyDelete
  5. Braza Michu, hii ndio kitu inayoitwa "MTANDAOZZZZ"... Duh!!! Hawa jamaa hawana aibu!!!

    ReplyDelete
  6. Heeee jamani yani mswekwa hajastaafu tuuu, anasubirii nini?naona listi ya watakao fia bungeni huku bunge linaendelea inazidi kuongezeka.Yani inamaana watu wote waliokuwepo ktk uchaguzi wa mswekwaa...wote ni wazee zaidi ya mswekwaa? au...! Kwanini asitulie nyumbani na kulea wajukuu...? au hana wajukuu?Shame on JK'S GOVERMENT!

    ReplyDelete
  7. Bi Kidude Baraka ana nyimbo yake ya Kuku walala. Maneno yake yasema hivi:

    Kuku lala lala, kipanga anakuja

    Kuwa na mvi si utu uzima
    Kung'oka meno si utu uzima

    Bora mashine iwe nzima

    ReplyDelete
  8. eeeh mungu wa rehema tumekosa nini sisi wadanganyika kwani ni lini utawachukua hawa wazee wako ili hata sisi tupate nafasi ya kuongoza nchi yetu.........ooohps mungu nisamehe wasije wa kaniamina chifupa bure wazee wazima wasio na haya na waliojawa zi sizo busara ok;;;;;;;;;;;nilizaliwa msekwa nimekwenda shule msekwa nimeolewa msekwa ninazaa msekwa na karibu nitakufa bado msekwa tuuuuuuuuuuuuuukwani hakuna watu walioenda shule zaidi ya hiyo mijizi ya nchi inayopokezana vijiti

    ReplyDelete
  9. Siasa sio umri jamani kuna position zinataka wazee wakae, waendelee kuwepo, siasa ni Hekima, busara na majungu wakati mwingine, utaweza hayo?

    ReplyDelete
  10. Ni vizuri chama kimeamua kubadili mfumo wake maana tulidhani itakuwa uongozi wa kudumu. Just one comment huyu jamaa aliyepost maandishi ni mchaga nini??????? Akiongesa or akiongea

    ReplyDelete
  11. Yawwwwwwwwwwwwwn....breaking news doesnt get any more boring than this!

    ReplyDelete
  12. Mimi nashangazwa na hawa viongozi wasioenda mapumzikoni!!!!Si wameshakomba jamani..!!Sasa wawachie wengine wachukue nafasi za uongozi.Kwa mwendo huu nchi yetu inakwenda kulekule.Ni mbio za vijiti wala si uongo!!!Heee utafikiri nchi ni yao peke yao bwana!

    ReplyDelete
  13. Mimi nashangazwa na hawa viongozi wasioenda mapumzikoni!!!!Si wameshakomba jamani..!!Sasa wawachie wengine wachukue nafasi za uongozi.Kwa mwendo huu nchi yetu inakwenda kulekule.Ni mbio za vijiti wala si uongo!!!Heee utafikiri nchi ni yao peke yao bwana!Watoto wao washasoma ng'ambo sasa wana hata wajukuu,inatosha.Maana wengi wao wakiwa madarakani hawakufanya lolote la maana kwa nchi zaidi ya kukomba.

    ReplyDelete
  14. Mh.Msekwa ni kweli kabisa ana historia ya muda mrefu ya uongozi kwenye chama.Lakini mimi sina imani naye kwani sio mshauri mzuri.Akiwa katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu,aliwafanyia roho mbaya watendaji wengi sana ambao walikuwa wachapa kazi kwa ushauri wa majungu aliokuwa akimpa Waziri Mkuu.Hata alipokuwa Spika pia yalitokea malalamiko mengi kwamba hakuwa anawatendea haki baadhi ya wabunge,ndio maana hata hawakutaka kumchagua kuendelea na wadhifa huo.Mimi nadhani CCM wangemchagua mwanachama mwingine kwani Mh.Msekwa atachangia tu kuleta majungu kwenye chama,ukizingatia ndio atakuwa mshauri namba moja wa Mwenyekiti

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...