Home
Unlabelled
BREKING NYUUUUUUUUUUUUUUZZZZ
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Ni yale yale. Hiyo ni kama mbio za kupokezana vijiti. Mafisadi waliokuwa wanakwenda kasi sasa wana-slow down wanawaachia waendao mwendo wa pole na mabingwa wa kupindisha sheria. Hapo tujiandae MSekwa akiwaombea dua wawasemao mafisadi na CCM, tunaanza eee mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, mungu wa upendo tunakiombea CCM na ufisadi wake kiweze kudumu madakani na kuwaacha wadanganyika wakiwa hoi amin.
ReplyDeletehivi kuna tofauti gani kiumri kati ya Malecela na Msekwa?Malecela ana 73,Msekwa ana 72,lakini siku zote Malecela ndiyo anaitwa babu ndani ya CCM.Akigombea,wanamuondoa,tena mapeema!Hawamtaki kwa kisingizio cha uzee,lakini bado wanateua wazee haohao kuongoza chama.Hivi kunani Malecela?why anaogopwa kama njaa??Ilifikia kipindi mpaka Nyerere akataka kutoka CCM kisa Malecela kachukua fomu ya kugombea urais,kwanini hata Nyerere alikuwa anamuhofia sana Malecela na si vingunge wengine wa siku zile kama kina Msuya,Msekwa mwenyewe,Bomani etc????serikali 3,au???Haya tusubiri tuone kama ameridhika safari hii!
ReplyDeleteUteuzi huu Kikwete kakosea step,hawezi kuua makundi.Ona kwa mfano-Sitta ni mtandao,na ndiyo huohuo mtandao ulimwangusha Msekwa kwenye uchaguzi wa u spika.Sasa Msekwa na mtandao unafikiri itakuwaje?
Kwa maana nyingine Kikwete kajimaliza mwenyewe!!!
Usibane michu...
LaLu
Hii,jamaa wewe sa inatuhusu nini? Hao jamaa hawana jipya wameshashindwa kuongoza nchi wamegeuka wao wachuuzi,wawekezaji, kero tupu ahadi hewa tu zimejaa. Usituwekee ishu hizo mbona list of shame hukuweka? Acha unazi au unataka ukuu wa wilaya na wewe?
ReplyDeleteKitendo cha Kikwete kumteua Msekwa ni uamuzi mzuri.Naona sasa Kikwete ameamua kuvunja makundi ndani ya chama na mtandao kwa vitendo kwa kumchagua huyu mwenye uwezo mkubwa lakini aliyekuwa nje ya mtandao kwenye nafasi nyeti.Hongera.Ni afya kwa chama na serikali.
ReplyDeleteNi vizuri Raisi aendelee kuchagua watu kutokana uwezo wao badala ya kuangalia nani alimshangilia sana au kumzomea sana kwenye kampeni ya uraisi.Aangalie tu uwezo aachane na nani alifanya nini kizuri au kibaya kwenye kampeni.Mambo ya kampeni ni upepo upitao waweza kuja na mavumbi na takataka usoni lakini ukishapita ni vizuri kuachana na habari zake na kuendelea na business as usual.
Kwa kumteua Msekwa mimi mheshimiwa Koloboi nampa hongera sana tena sana tu Raisi Kikwete.
Nami namwahidi kuwa akifanya vizuri nitaendelea kumpongeza na akifanya vibaya nitaendelea kumzomea.
koloboi@yahoo.com
Braza Michu, hii ndio kitu inayoitwa "MTANDAOZZZZ"... Duh!!! Hawa jamaa hawana aibu!!!
ReplyDeleteHeeee jamani yani mswekwa hajastaafu tuuu, anasubirii nini?naona listi ya watakao fia bungeni huku bunge linaendelea inazidi kuongezeka.Yani inamaana watu wote waliokuwepo ktk uchaguzi wa mswekwaa...wote ni wazee zaidi ya mswekwaa? au...! Kwanini asitulie nyumbani na kulea wajukuu...? au hana wajukuu?Shame on JK'S GOVERMENT!
ReplyDeleteBi Kidude Baraka ana nyimbo yake ya Kuku walala. Maneno yake yasema hivi:
ReplyDeleteKuku lala lala, kipanga anakuja
Kuwa na mvi si utu uzima
Kung'oka meno si utu uzima
Bora mashine iwe nzima
eeeh mungu wa rehema tumekosa nini sisi wadanganyika kwani ni lini utawachukua hawa wazee wako ili hata sisi tupate nafasi ya kuongoza nchi yetu.........ooohps mungu nisamehe wasije wa kaniamina chifupa bure wazee wazima wasio na haya na waliojawa zi sizo busara ok;;;;;;;;;;;nilizaliwa msekwa nimekwenda shule msekwa nimeolewa msekwa ninazaa msekwa na karibu nitakufa bado msekwa tuuuuuuuuuuuuuukwani hakuna watu walioenda shule zaidi ya hiyo mijizi ya nchi inayopokezana vijiti
ReplyDeleteSiasa sio umri jamani kuna position zinataka wazee wakae, waendelee kuwepo, siasa ni Hekima, busara na majungu wakati mwingine, utaweza hayo?
ReplyDeleteNi vizuri chama kimeamua kubadili mfumo wake maana tulidhani itakuwa uongozi wa kudumu. Just one comment huyu jamaa aliyepost maandishi ni mchaga nini??????? Akiongesa or akiongea
ReplyDeleteYawwwwwwwwwwwwwn....breaking news doesnt get any more boring than this!
ReplyDeleteMimi nashangazwa na hawa viongozi wasioenda mapumzikoni!!!!Si wameshakomba jamani..!!Sasa wawachie wengine wachukue nafasi za uongozi.Kwa mwendo huu nchi yetu inakwenda kulekule.Ni mbio za vijiti wala si uongo!!!Heee utafikiri nchi ni yao peke yao bwana!
ReplyDeleteMimi nashangazwa na hawa viongozi wasioenda mapumzikoni!!!!Si wameshakomba jamani..!!Sasa wawachie wengine wachukue nafasi za uongozi.Kwa mwendo huu nchi yetu inakwenda kulekule.Ni mbio za vijiti wala si uongo!!!Heee utafikiri nchi ni yao peke yao bwana!Watoto wao washasoma ng'ambo sasa wana hata wajukuu,inatosha.Maana wengi wao wakiwa madarakani hawakufanya lolote la maana kwa nchi zaidi ya kukomba.
ReplyDeleteMh.Msekwa ni kweli kabisa ana historia ya muda mrefu ya uongozi kwenye chama.Lakini mimi sina imani naye kwani sio mshauri mzuri.Akiwa katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu,aliwafanyia roho mbaya watendaji wengi sana ambao walikuwa wachapa kazi kwa ushauri wa majungu aliokuwa akimpa Waziri Mkuu.Hata alipokuwa Spika pia yalitokea malalamiko mengi kwamba hakuwa anawatendea haki baadhi ya wabunge,ndio maana hata hawakutaka kumchagua kuendelea na wadhifa huo.Mimi nadhani CCM wangemchagua mwanachama mwingine kwani Mh.Msekwa atachangia tu kuleta majungu kwenye chama,ukizingatia ndio atakuwa mshauri namba moja wa Mwenyekiti
ReplyDelete