habari zisizothibitishwa toka redio mbao zimeingia sasa hivi kwamba bosi wa tanesco aliyetangaza kujiuzulu wadhifa huo amepiga abauti-tani na kwamba hatojiuzulu. juhudi zinafanyika kupata ukweli wa mambo. bakia umejityuni...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. akijiuzulu asijiuzulu yote sawa

    ReplyDelete
  2. NATAKA NA KIKWETE PIA AJIUZULU

    ReplyDelete
  3. Ni kweli kwamba Wakulu wamekataa Barua ya Dr Rashid ya kujiuzulu.Kuna matatizo Tanesco,shirika linaendeshwa kisiasa mno.Haiwezekana kutetea uizi wa Umeme ati kwa sababu kuna upungufu wa Saruji.Kwa mawazo yangu Chairman wa Bodi ya Tanesco Balozi Fulgence Kazaura aachie ngazi,kwani kuwepo kwake hapo ni kikwazo!!!!

    ReplyDelete
  4. Labda watu wanahisa zao huko kampuni ya saruji na haya mahisa yanavyouzwa hapo Dar Exchange! Mwanawane kwa nini watu wasilinde maslahi yao ili gawio lisipungue kwa kununua umeme wa halali.

    Jamani kama kweli tunataka maendeleo ya nchi yetu tuache wizi. Wakubwa kwa wadogo, yaani wenye kuiba umeme wa viwandani na wanaoiba umeme majumbani, hatuwezi kuendelea kwa dizaini hii.

    Sio wizi wa umeme tu tuache na ufisadi mkubwa na mdogo.
    Dini zotee zinakataza wizi na ufisadi huo ufalme wa Mungu tutaona kweli, tunajazana misikitini na makanisani unafiki mtupu.

    Jamani ee kuna watu walilalamikaga huko nyuma kuhusu wafanyabiashara kuingia kwenye siasa haya ndio matokeo yake na bado tutayaona mengi.

    Wewe unayesoma blogu hii umelipia bili yako ya maji na umeme? Umelipa kodi? Una gari unafanya taxi bubu, kazi kupigia kelele wezi wakubwa nao walianzia hivi hivi kidogo kidogo mpaka wakakubuhu.

    Mwizi wa kuku au simu ya mkononi akikatiza mtaani kwenu mnampiga mawe mpaka mnamuua na hawa wezi wa umeme je? Tuwapige na nini? Tissue Paper???
    Mzalendo mwenye uchungu na inji hii.

    ReplyDelete
  5. Tatizo hapo ni Chairman Kazaura yeye ni kikwazo kikubwa sana naomba hii michizi usinibanie kwani nammindi sana pale aliposema friji ni chombo cha anasa hivi kweli michuzi mtu wa dar friji kweli ni kitu cha anasa labda kwao hilo ni mojo kuna pumba nyingi sana katustisha wabongo isitoshe yeye sio mwanasiasa ila anacheza na upambe kwa wanasiasa

    ReplyDelete
  6. Ish!!! mbn kizungumkuti tena...pesa mwanawane!!! kaona wyf wake hatampa unyumba tena, na wala hataenda kwenye kikao Copenhagen tena akaona icwe tabu!!! bongo bwana!!!!

    ReplyDelete
  7. Michuzi naona unanibani kila ninapoweka maoni yangu. Sioni kama yana tofauti na mengine yoyote.

    Nilichotaka kusema ni kuwa kuna anony amesema tatizo ni wafanya biashara kuingia kwenye siasa.
    Ni kweli Karamagi ndio mwenye Vertex securities ambayo ili nadi shares za kampuni ya saruji na sasa ni waziri wa Nishati....UNATEGEMEA NINI??????

    PILI:Kuna Mizee kama Kazaura, bora iondolewe kazini sasa. Wana mawazo ya kizamani,very conservative na wasiopenda ku-train new brain kuleta changes. Tunakubali ni watu wenye experience ya kila engo lakini sasa we look at the reality.

    Mimi binafsi (In my Opinion)sioni tatizo la Kuongeza tariff kwa mwaka na Tanesco irudi on its position;kuliko kujifanya TUNATETEA MASLAHI YA WATU HUKU tukiwaza kupiga dili personal???which is which!!

    There are BRAINS AND WORKERHOLICS in bongo lakin hatuoni.Mfano Huyu Iddris,Peter Ngumbulu, Mr Masawe,Patric Rutabanzibwa to mention few mchango wao umefyonzwa na ufisadi.

    ReplyDelete
  8. Taarifa isiyo rasmi ni ipi? ya kujiuzuru au kutojiuzuru?
    Mzee wa Ph.D hawezi akatoa barua ya kujiuzuru halafu akaifuta kimya kimya hivi hivi bila yale yaliyokuwa yanamfanya ajiuzuru hayajarekebishwa!
    Vinginevyo hiyo Ph.D itakuwa Doctorate of 'Philos'.
    Michu tuleteeni taarifa rasmi na undani wake tukate issues hapa kabla ya kumsagia mzee watu au kumfagilia bila kujua taarifa ya kweli.

    Nyakatakule

    ReplyDelete
  9. Hii kali! Kama ni mtu wa msimamo kwa nini abadilishe uamuzi?Kama ni mtu anayesimama kwenye ukweli mkwa nini akubali uongo?Fisadi ni fisadi tu!

    ReplyDelete
  10. HUYU NI DR KWELI AU NDO SHULE ZA KUIBA VYETI,KAMA KWELI ALITOA TAMKO LA KUJIUZURI KUTOKA NA TATIZO AMBALO LIMEMKERA SANA IWEJE TENA ANA BADILI MAAMUZI YAKE INA MAANA HAJUI ANALOFANYA AU.HAWA NDO RAHISI SANA KURUBUNIWA NA WATU WAJANJA KWANI HANA MSIMAMO WAKE.WAHEZI KUSIMAMAMA KWA MIGUU YAKE HUYO HATUFAI KABISA,KAMA MIMI NI JK NINGEMUONDOA KABISA KTK NAFASI HIYO NA KUMPA MWINGINE.TUTUMIE ELIMU YETU KWA FAIDA YA NCHI HII JAMANI.SI KWA MASLAHI BINAFSI.

    ReplyDelete
  11. Maombi yake yatakuwa yamesikilizwa. Hawa wanasiasa uchwara, balozi nani nani sijui mara waziri wa nishati unawaunganishia washikaji zako umeme kinyemela DR hawezi endekeza vitu kama hivyo.

    Bado issue ya pili RICHMOND ataondoka mtu. Manake inaonekana wanasiasa wanataka ukweli usitolewe na TANESCO sasa babako hapo akubali akasema bora niondoka JK mwenyewe kamhakikishia kuwa endelea na utendaji kila kitu poa hawa wanasiasa wasikutishe. Hapo patamu hii ndio trela movi yenyewe karibia itaanza...ngojeeni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...